Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

blueivvy nahisi zilikuwa za FRMP,sikumbuki vizuri,thobias kobelo mara ya mwisho nadhani alikuwa na kesi ya kuua kama sikosei na mwingine alifungwa au alikuwa na kesi,watoto walikuwa wanakula unga na bangi vibaya sana. na mchizi wao Mc bob C ndo alikuwa anawaongoza, mdogo wao tu ndo alikuwa ametulia. huyu dr kobello hospitali yake ilikuwa mitaa ya kanyenye karibu na fourways au tanesco..

Hiyo hosp wewe unazungumzia dr Othman,kobelo hosp.yake ilikuwa bachubachu kule.
 
Enzi za UMISHUMTA pale TTC tabora. Kulikuwa na kikundi flan hv cha drama Toka kazima Sekondari af palikuwa na madem flan hv walikuwa matawi flan Akina Emma Manyanga duhh
 
Hahahhaa hii thread nouma!! inanikumbusha life la Tabora wakuu, maeneo ya Ng'ambo kwenye pilau usiku usiku!! Tukutuku kuchota maji, kwa Sonda kucheki UEFA, hahaha nilikuwapo miaka 10 hadi 12 iliyopita wakuu pale Tabora Boys.

Mzee Sikawa wa DANIDA. Tulikuwa tukienda kuchata maji kwake tunakutana na Nyoso
 
Tabora enzi hizo miaka ya kuna demu alikuwa anaitwa Veronica Mhina alisoma unyanyembe

Student center watu walikuwa wanaenda Ku record ngoma kwa Aziz

National kulikuwa na totoz Kali kama kina magreth

Tatizo Moja kulikuwa hamna makahaba

Nilisoma na kakake akiitwa Gabriel sasa hivi ni Komando jeshini. Veronica kaa mwarabu fulani hivi.
 
Hahaha, sinema diamond, disco Tabora hotel, timu mirambo bwana, Quresh ufunguo, job ayoub, feruz teru!! Kwenye maisha yangu yote sijawahi ona winga ana kipaji kama Feruz Teru! Yaan unaweza mfananisha na J. J. Okocha tu kwa kupiga chenga, sema kitu kilikuwa kinamzuia kucheza ni enka, mabeki ndo ikawa kumkanyaga hapohapo. Mboka.. Mji unaoongoza kwa vichaa Tanzania. Nakumbuka mwalimu Nyerere alikuwa kwa mwaka anakuja ipuli kwa kwa yule mama Asha Maswezi. Waswezi ndo walikuwa wanaenda kumpokea uwanja wa ndege. Sijui alikuwa anaenda kufanya nini kwa yule maza, alikuwa ana mamizimu makali sana ya Maswezi. Mboka kipindi hicho kama huchezi kung-fu hujakamilika. Ushirikina mwingi, kila njia panda nazi zimevunjwa, mavitu kibao. kila kona wanapiga ngoma za kutoa majini, au kupandisha mizimu.

Hahaha hapo kwenye kutoa majini unanikumbusha Binti/Biti Swedi.
 
Mmesahau uwanja wa Ali Hassan Mwinyi siku game kubwa kubwa Simba na Yanga na Pamba .....mji wote unachangamka na uwanja unajaa...mauza uza uwanjani mvua huwa inanyesha uwanjani tu na Simba wanafungwa....game moja Mackenzie Ramadhani hakuamini...alipigwa 2 pale pale!Milambo ilikuwa ina vipaji sana na motisha sana,ile jeuri ya kwao ikawaponza walipoenda Dar,walijuta na fujo zao!Peter Poka hatasahau!

Nakumbuka kipindi hicho tunaenda kuangalia mpira kiingilio 300 (Yosso) tunawaona kina Victor Kilowoko.
 
Enzi za UMISHUMTA pale TTC tabora. Kulikuwa na kikundi flan hv cha drama Toka kazima Sekondari af palikuwa na madem flan hv walikuwa matawi flan Akina Emma Manyanga duhh

Umenikumbusha mbali mkuu.:thumbup::thumbup:😀😀
 
Mi nilikuwa mjini kabisa pale karibu na jamatini ule msikiti wa wahindi, pale NBC opposite na shule ya mihayo secondari. Enzi hizo unaandikiwa wimbo tu wa kizungu ambao uko kwenye chat basi ujumbe umeupata, dah old is gold kwa kweli.

mwasu opposite na Mihayo Secondary ni NMB sio NBC
 
Last edited by a moderator:
Shule ya mwenge mwalimu shigela,chiboni,maduhu,..,shule ya isike msöna, shule ya kitete mlw masaka,fikirini,...
Shengena hoteli pale kitete hospitali washona viatu kina kawawa na kambarage, duka la hassani mkonde pale kwa kina mrua,fundi baiskeli. Ng'ambo kwa juma mzungu, deremsi,mpumuti, kwa gondwe, germano pacha, masendeka, chemchem mwalimu ahamada salum, minazi ya kwa mkonde.
 
Zambarau zilikuwa zinapatikana kwa wingi maeneo ya kwa boga ila inabidi uende kabla ya saa 6 maana mida hiyo majini yanaanza kurudi yanaweza yakakukumba.
 
Nilibahatika kupita huko mwezi wa 11 mwaka jana nikielekea Kahama, Shy. Kwa kweli Tabora ni mkoa uliokwisha, hakuna maendeleo yeyote zaidi ya kuwa na nyoka na vichaa wengi mjini. Mtu ukiiba kibiriti kwa mwarabu dukani basi unatupiwa ukichaa, yaani hakuna cha maana pale. Kila mtu anajifanya alwatani na ukiwa mwarabu unaogopewa kwani wakazi wanakuona wewe ni Mungu mtu.
Mkuu ukipata mwanya nenda sasa Tabora sio hiyo unayoisema imeendelea saaana.
 
Nimeipenda saana thread hii. Nimekumbushwa meengi sana bwana, TBR iko stagnant kiuchumi sijaenda miaka mingi saana,
last time ni 1989.
Tafuta mwanya uende utaipotea. Imeendelea ndani ya miaka 3-5 hivi!
 
Mi nakumbuka wimbo wa shule tu
"Tabora School kichwa cha Tanzania"
"Jinalo kote linatajikaaaaaaaaaaaaaa"
"Hapa alisomeshwaaa,Baba yetu wa Taifa"
Enzi hizo Tabora Boys,tunawaza tu kucheza disco na Tabora Girls....Kulikuwa na demu anasoma sijui Kazima sijui Uyui mzuri sanaaaa,anaitwa Nongwa....Wapi Nongwa wapiiiiii
 
Back
Top Bottom