Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

wakuu kuna anaemkumbuka Adam Gosho na mazingaombwe yake ya uongo na vijana wake wale wa Karate!!?disco la mwanaisungu opp.uhazili.........upinzani wa timu za mpira miaka ile..........timu ya posta na polisi,magereza ya uyui na rhino ya nzega gemu zinapigwa uwanja wa kumbukumbu ya vita pale,watoto wa gongoni na bange zao!kisima cha kilimbika,bwawa la Taliani(kulisemekana kulikua na 'chunusi' kule....lol!)...................wahalifu maarufu aka zile kina Mafuta ya ndege(anakimbia huyo.....hatareeee,Bolt hakamati!),Jackson kuku,sinema za ukumbi wa Diamond miaka ile.

nakumbuka tukio la mabehewa ya petroli kuwaka moto pale stesheni..kilikuwa kipindi cha vita ya ghuba,basi tukajua marekani na saddam wameanza kukinukisha na huku tayari.....lol!

Dah! Rubeye umemtaja jackson kuku nimestuka maana hawa jamaa waliviziaga mzee kasafiri wakaja na kundi lake na mapanga wakavamia nyumba wakabeba vitu vyote ndani kaka yangu mkawa anamjua jackson kuku akasema jackson dah wakampiga upanga kichwani akalazwa kitete week 2 jamaa sijui yupo hai maana alikuwa nooma kweli.
 
Mmesahau uwanja wa Ali Hassan Mwinyi siku game kubwa kubwa Simba na Yanga na Pamba .....mji wote unachangamka na uwanja unajaa...mauza uza uwanjani mvua huwa inanyesha uwanjani tu na Simba wanafungwa....game moja Mackenzie Ramadhani hakuamini...alipigwa 2 pale pale!Milambo ilikuwa ina vipaji sana na motisha sana,ile jeuri ya kwao ikawaponza walipoenda Dar,walijuta na fujo zao!Peter Poka hatasahau!
 
Nahisi tumepishana miaka kati yangu mimi na wewe maana hao uliowataja hata mimi siwajui kama ilvyo wewe humjui Patel, Alikuwepo Uyui sec as head master kama sikosei mpaka early 90s


Mkuu, yule muhindi Patel alikuwepo mkuu wa shule ya Uyui hadi miaka ya 2003 au 2004 hivi kama sikosei!! Alitolewa pale kutokana na malalmiko ya wanafunzi kwa kuwawekea masharti magumu. Nakumbuka kuna wakati ilifikia hadi hatua wanafunzi wakaandamana kuelekea nyumbani kwake ikapelekea FFU kuingilia kati na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.
 
Patel mie namfahamu, na huyu ilibidi akabidhi shule baada ya kushindwa kui manage kutoka na ukorofi wa wanafunzi wa pale na migomo
Nahisi tumepishana miaka kati yangu mimi na wewe maana hao uliowataja hata mimi siwajui kama ilvyo wewe humjui Patel, Alikuwepo Uyui sec as head master kama sikosei mpaka early 90s
 
[QUOTnimepata taarifa humu kuwa mwl.Getaback ni marwhemu mi nimemaliza 1984 lakini hao waalimu wote wamenifundisha waaw kumbe ni mtoto wa mwl Shigela duh pia mwl msha alikuwa mwl.wa siaa mwembamba huyo sijui alinenepa baadae E=blueivvy;6141720]Umenikumbusha mwalimu chiboni ndiye aliyenifundisha English, unaikumbuka ile sala...Our father? Jotter je? mwalimu chiboni ni marehemu, getaback nadhani alirudi kwao ni muiraq wa kule arusha....mwalimu nachenga alikuwa mnoko je unamkumbuka mwalimu balozi na msha? Mwalimu fundi alikuwa mtaalam wa Geography, anaweza kuichambua New York na zile boroughs zake utafikiri amefika, blockln sijui nini? mimi nilimaliza la saba mwaka 1990.... Bila ya kumsahau mama yangu Mwalimu Shigela mwalimu wa darasa la kwanza mungu amzidishie afya njema yupo tabora[/QUOTE]
 
ebwana mi nimesoma cheyo A mwaka 90 darasa la kwanza,nilikuwa nakaa jeshin karibu na nyuki,nilikuwa nikipita cheyo "B" ndio shule ya kwanza kuona wanafunz wanakalia matofali,ila sasa ivi ndo kwa mapedeshee,du!
 
Trust me Mkuu! Mimi nimezaliwa na kukulia huko so napafahamu kwa undani kupita kiasi!Njia ya kwenda Sikonge kuna kijiji kinaitwa tutuo na kama unakwenda urambo kuna kijiji kinaitwa uyumbu huko wamejaa waarabu wakufa mtu ndiyo maana nakwambia waarabu Tabora ni kama wanyamwezi tu kwanza hata hawajisikii kama niliowakuta huku Dar es salaam, yaani wanajichanganya uswazi kama kawa na wengine hadi kinywamwezi kinapanda.
..nakubaliana na wewe kiongozi nilienda mitaa ya ulyankulu nikakuta waarabu kibaooo wanagonga kinyamwezi balaa..
 
Nimeipenda saana thread hii. Nimekumbushwa meengi sana bwana, TBR iko stagnant kiuchumi sijaenda miaka mingi saana,
last time ni 1989.
 
Ndipo nilipoishi mkuu!japo mi si mwenyeji wa Tabora!japo Isukamahela,Mtakuja,Igombe,Kaliua,Ulyankulu nimefika

Mkuu Ngaliba Dume mimi nimezaliwa Tabora kijiji cha Kakulungu karibu na yule mtusi mfugaji wa ng'ombe wengiiii. Alikuwa anatenda ya kuiuzia maziwa Tabora Hotel (wakati ule). Ndo nilikozaliwa zamani sana maana la saba nilimaliza mwaka 1985.
Ila mkuu naomba kujua maana ya Mboka Manyema. Pamoja na kuzaliwa Tabora neno hili nimelisikia humu JF. Hebu nifafanulie mkuu maana elimu haina mwisho, waweza jua hili na wengine wakajua lile. Nisaidie tafadhali.....
 
Hivi kuna mtu anavikumbuka vitabu vya lugha ya kinyamwezi vilivyokuwa vinauzwa pale TMP Tabora? Nimevikumbuka sana wakuu vitabu kama vile "Salala Yabukila Kumbasa" yaani mkosi ulionzia na shoka ikimweleza jamaa mmoja alikuwa na na mkosi kiasi kwamba kila hatua aliyopitia ilimletea balaa. Mfano kuna mnyama mharibifu wa mazao alimtega shambani kwake akamnasa lakini alipokwenda kumwambia mkewe waende kubeba nyama ya mnyama huyo wakakuta mnyama amebadilika na kuwa mama mkwe wake yaani mama wa mkewe!!!!
Kitabu kingine kinaitwa "Myanda Mpina Na Shigani Shinge" yaani Kijana Maskini na hadithi Zingine hadithi inayomwelezea kijana mmoja masikini alivyostruggle na maisha.
Nakumbuka vitabu hivi vilikuwa vinatungwa na Padri mmoja wa kanisa katoliki hapo Tabora jina nimelisahau wakuu.
Naombeni mnikumbushe wakuu......
 
Dah enzi hizo maeneo ya maua bar ndo kama sinza!

ebwana hii sehemu sijui ina nini mpaka sasa ukifika pako vile vile pamechangamka mwaka jana mwenyeji wangu anasema twnde uku pamechangamka mda huu kufika naona kituo cha polisi, na njia panda nikasema hapa si maua bar akasema hapana panaitwa zero, jmaa mmoja akadakia akasema ndiyo penyewe mkuu jina limebadilika tu sasa.
 
Miaka ya 80 nilikua primary shy likizo kwa bibi tabora babu alikua polisi tulikaa lainipolisi no.02 jirani na maua bar weekend tabora jaz ilikua ndo inaelekea kufa inaburudisha maua watoto haturuhusiwi usiku unakula mziki kwenye varanda la kota za polisi.vipi faraji katalambula na hadithi za simu ya kifo.
 
wakuu kuna aliesoma isevya primary kabla ya '93 humu!??

samahani lakini!
 
Mabadiliko yapo mengi sana, mfano miaka hiyo eneo ambalo leo linaitwa Mwinyi kulikuwa na majaruba ya Mpunga na pori la miembe, nyuma ya Tabora Boys pia kulikuwa na pori kubwa ambako tulikuwa tukifuata Ndati leo hii kuna kitongoji kikubwa cha Kariakoo hali kadhalika nyuma ya tukutuku kuna mji mpya wa Lwanzari mabadiliko ni mengi sana wehu wote uliowataja wengi wameshatangulia mbele ya haki, TABORA YA SASA SI KAMA ILE YA ZAMANI
 
Mabadiliko yapo mengi sana, mfano miaka hiyo eneo ambalo leo linaitwa Mwinyi kulikuwa na majaruba ya Mpunga na pori la miembe, nyuma ya Tabora Boys pia kulikuwa na pori kubwa ambako tulikuwa tukifuata Ndati leo hii kuna kitongoji kikubwa cha Kariakoo hali kadhalika nyuma ya tukutuku kuna mji mpya wa Lwanzari mabadiliko ni mengi sana wehu wote uliowataja wengi wameshatangulia mbele ya haki, TABORA YA SASA SI KAMA ILE YA ZAMANI

Naitafuta mihayo form four wa 1990
 
Tbr jamani imebadilika...tena sana,nilisoma Tabora school enzi.za Mwalimu Mrisho,Masele,Karunguyeye,Sagenge na Kanyaboya...nimeenda juzi kati...kuna maendeleo sana
 
Back
Top Bottom