Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Mi nilikuwa nakaa isevya ila nasoma cheyo A. Mmenikumbusha mbali sana! Watoto wa kike wa mzee kagoma walikuwa wazuri sana kwa sababu ya rangi na watoto wa kiume walikuwa watemi sana. Nakumbuka tulikuwa tunacheza mpira (chandimu) mtendeni shule ya msingi, nikampiga kanzu na kisha nikamgeuza kwa tobo mtoto wa mzee kagoma, alikuwa anaitwa Bias nikashangaa akaanza kunipiga ( nilipigwa ngumi na kichwa kwa kumtoa nishai).
Mnakumbuka watoto wa mitaa ya bomba mzinga wakina Mugisha walivyokuwa wakorofi? Kuna kademu katoto ka kwa munene- Jaquiline nilimu approach ila nikasitisha kwa sababu alitaka kwanza apajue home kwetu, nikawa namkwepa kwa sababu kwetu ni choka mbaya!
Nakumbuka tena kuna msichana wa kihindi (Rahma) nilikuwa nampenda cheyo A primary school lakini nilikuwa domo zege, nikawa najiongelesha mambo mengine tofauti kwa muda mwingi ili watu wajue ni mtu wangu! Ha ha ha! Mwl Jacob nae alikuwa anamtaka akahisi labda nakula mzigo, nilikuwa nachezea fimbo za kutosha mpaka nilipokuja kushtuka ndio nikapunguza mazoea na Rahma. Mwl mkuu wetu kipindi hicho alikuwa Mwl Mlekwa.
Dr. Kobelo alikuwa anakaa nyuma ya shule yetu na mke wake alikuwa kutoka Russia.
Kisima cha kilimbika ndio kilikuwa kisima chetu kwa ajili ya kuchota maji.
Mitaa ya isevya, mzee shirima ndio alikuwa tajiri maeneo yale miaka ile na kulikuwa na mtoto wake wa kike Neema shirima alikuwa mzuri sana na anapenda sana masela! Kei na Tito shirima ndio walikuwa agemate wangu!
Nakumbuka mwizi maarufu Shantongo alichomwa moto miaka ya 90's.
Mapadre wa kanisa katoliki ipuli walikuwa wanakula mademu kilaini sana, wale wazungu hawakuwa ma-player.
Nakumbuka tulikuwa tunaenda Tabora hotel kushindana kucheza disco la watoto ili kupata kreti la soda kwa mshindi wa kwanza! Wakubwa walikuwa juu kipindi hicho walikuwa ni Bob wizard na Major. Bob wizard alikuwa mzuri kwa nyimbo za Michael Jackson. Sijajua hawa jamaa wako wapi?
Muungano mess masoja yalikuwa yanatufukuza watoto ikifika saa moja usiku!
Nasikia Tabora panaendelea kwa kasi kwa sasa ila isevya imegoma kuendelea, wachawi ni wengi mno kule!
I miss Tbr since 1995. I miss TZ since 2011.

Ha ha haa... Umenikumbusha mengi na mtaa wangu wa Isevya enzi hizo... Kweli wewe ni kijana wa soweto..
 
I love Tabora
Mnenikumbusha mengiiii saana
Zile sinema ktk uwanja pale soko Kuu
Ngoma ya wa Bisa na Waswezi
Warsaw na Berlin
Tabora Girls......Massawe the beauty and Massawe the Ugly.....Mwambeje na mandazi yake
 
Mkuu ukitaja Warsaw mwili unasisimka,pale chini ya mwembe tulikuwa tunakaa na mademu wa Girls.
Siku ya disco unakumbatia halafu unaishia bafuni tu kwenda kutema mzigo
Nyangara,redo,mbarara na unyuka ndio habari ya mjini
 
Kumbe wewe wa mboka.....nimesoma uyui nlikua best wa major na mansor marjebby
Haaaa mie nilikuwa Mihayo enzi hizo kina mansory ndio mabrother men, na mdogo wake muhsin. Kulikuwa na Juma stuwa pia kalikuwa keupee kale kavulana. Du wakati huo ndio namaliza primary mihayo wao wako uyui. Wakati huo kaka zetu wana endesha baiskeli aina ya phoenix eti ndio watoto wa kishua.. Du kali kweli.
 
Tabora ndo mkoa niliozaliwa na kusomea shule ya msingi! Wazazi wangu wako Ipuli, nachoweza kusema Tabora ndo mkoa wa mwisho kupata uhuru japo umetoa wapigania uhuru wengi sana, Tabora imepata uhuru 2005 baada ya JK kuingia madarakani, ulikuwa ni mkoa usiounganishwa na mkoa mwingine kwa barabara ya maana zaidi ya reli, barabara za lami zimeanza baada ya kikwete, tukawekewa lami barabara ya Tabora-nzega, kwenda kuungana nalami inayotoka singida kuelekea shinyanga, tukajengewa ya kuelekea kigoma kupitia malagalasi, tulajengewa pia lami ya kuelekea itigi na nyingine ya kuelekea Mbeya, Thanks alot JK now we are part of Tanzania
 
Mkuu ukipata mwanya nenda sasa Tabora sio hiyo unayoisema imeendelea saaana.
Baadhi ya mitaa, chemchem iko vile vile, nyumba za miaka ya 90 wakati nikiwa milambo sec. bado ziko vile vile nimetoka december huko
 
Haaaa mie nilikuwa Mihayo enzi hizo kina mansory ndio mabrother men, na mdogo wake muhsin. Kulikuwa na Juma stuwa pia kalikuwa keupee kale kavulana. Du wakati huo ndio namaliza primary mihayo wao wako uyui. Wakati huo kaka zetu wana endesha baiskeli aina ya phoenix eti ndio watoto wa kishua.. Du kali kweli.
Mimi wakt nasoma hapo ndio nlijuana nao cz ya basketball hpo uhazili....wao nlikuta wameshamaliza shule kitambo ma ahmed silencer
 
Kwa kweli JK ndio ameifungua Tabora Kwa kuipa barabara za lami zilizounganusha sehemu nyingine
Kwa sasa ndio Mkoa pekee uliounganishwa na njia za usafiri nyingi
1.Ndege.....Kigoma/Dar
2.Reli.......Kigoma/Rukwa/Mwanza/Dodoma/Morogoro/Dar
3.Barabara ya Nzega.....To Singida/Shinyanga/Mwanza/ArushaMusomaetc
4.Barabara ya Manyoni.....Dodoma//Morogorp /Dar etc
5.Barabaea ya Sikonge......Iringa/Mbeya etc
6.Barabara ya Urambo.......Kigoma/Geita/Kagera
Awamu hii Kwa hakika wataimarisha reli
Na pengine kufikiria Ile Barabara ya Mambali to Kahama

Pia Barabara hizi zimeunganisha Nchi jirani
TABORA mtaitafuta.............Itakuwa ni LULU................WAZO LANGU
I love Tabora...........The weather,ukarimu etc

Uzi huu tutaukumbusha 2020-2025
 
Baadhi ya mitaa, chemchem iko vile vile, nyumba za miaka ya 90 wakati nikiwa milambo sec. bado ziko vile vile nimetoka december huko
Nadhani itakuwa fair kuzungumzia Tabora nzima na sio mtaa mmoja tu. Mi nimetoka huko April mwka huu.
1. Barabara- mitaa mpka ya Kanyenye in abrabara za lami
2. Maduka- Biashara zimechipua sana kuna mtaa ambao ulikuwa na mashine za kusaga ( hamna kwa sasa) bali kuna mashine kubwa sana 2 sa kukoboa mpunga ,tyaa wa Salimini. Sehemu hiyi
Baadhi ya mitaa, chemchem iko vile vile, nyumba za miaka ya 90 wakati nikiwa milambo sec. bado ziko vile vile nimetoka december huko

Mimi nimetoka April 2016. All in all maendeleo haya hayawezo kuwa ya miezi mitano tu . Aidha umetaja mtaa mmoja tu Chemchem. Ili kufanya tarhmini yakutosha ungetembelea mtaa zaidi ya huo mmoja uliotembelea. Sasa kwa wale ambaa mlisoma huko miaka ya nyuma 70s, 80s, 90s, na hata 2000 mkipata mwanya mkajionee wenyewe. tabora imebadilika sana positively:
1. Barabara- nyingi zina lami hata za mitaani- mitaa ya Kanyenye ambauo hata mitaa ya DSM haina lami lakini Tabora kuna mitaa ambayo hungefikiri by now ingekuwa na lami mf. Kanyenye nk.
2. Biashara zimeboom- maduka mbalimbali . Kuna mtaa mmoja nadhani unaitwa Bomani kuna sehemu walikuwa wanakoboa sijui mpunga, ni maduka tu ya nguo. badala yake mtaa huohuo chini zimefinguliwa mashine kubwa 2 za kukoboa mipunga.
3. Nyumba nyingi bora zinmejengwa, na hata zikle za zamani watu wameziorenovate
4. Majengo mengi ya maghorofa yamejengwa ya biashahra
5. Je ulifika mahali panaitwa Freemason ( Jina silipendi lkn wasomaji wanaweza jua kwa nini limeitwa hivyo_- kwanza barabara ya kwenda huko ni znuri sana ( main road) halafu nyumba zilizojengwa huko ni za uhakika sijui kwa DSM nifananishe na wapi ( labda Mbezi Beach) kitu ambacho hata miaka ya 90 ilikuwa ni ndoto. Barabara za kuunganisha na wilaya nyingine na ile barabara sugu kati ya Nzega na Tabora ina lami kwa ujumla kutoka DSM mpaka TBR sasa ni Lami tupu, Usiku kuna mtaa jamani muende wenyewe mkajionee.
6. Walioishi TBr mnapafahamu Kachoma??? ( wasiojua palikuwa panauzwa Pombe za Kienyeji)- pale limefunguliwa soko ni biashara tupu ( Ila manispaa ihakikisha usafi pale)
7. Tabora kulikuwa na sehemu gani decent ya kujipatia chakula labda tabora Hotel ambayo ilikuwa expensive - sasa hivi kuna several places.

Kwa walioishi TBR say 1970- 1990s watanielewa kwani kulikuwa hakuna maendeleo kabisa kama yalikuwepo yalikuwa polepole mnoo.
Mwisho: Ukitaka kuamini chukua taarifa za kibenki kulinganisha kwa wakati ( 5 years, 10 years or so) unaoutaka kwani ni kipimo kimojawapo cha maendeleo!
Kifupi kuna maendeleo makubwa ya muda mfupi! Wenye mitaji yenu muende mkawekeze kwani mpaka Dec. 2016 lami ya kupitia Itigi itakuwa tayari hivyo itarahisisha saana usafiri.
 
Du mboka manyema tabora nimeenda mwaka huu kiukweli tbr imebadilika nimekuta gorofa kubwa nambiwa la NSSF wakati enzi zile hilo eneo ulikuwaga uwanja wa mpira na miembe kibao

Nikaenda stand nikambiwa imehama kwenda ilipo nikashangaa maana kule zamani ikikuwaga majaruba enzi zile tunaenda mzabarauni kununua saa ila leo gorofa

Nikaenda mwana isungu nikambiwa nikashangaa hiyo sehemu bado mziki unapigwa ila jina ndio sio mwana isungu tena

Tabora imetanuka maeneo kama ipuli ilikuwa pirini ila leo eti mjini

Nakumbuka mhindi kanji alikuwa mzamini wa club ya timu ya milambo pia mzazi wa timu ya simba

Nikaenda railway station sikuamini pamepoa kabisa wakati zamani siku ya treni ya dar kwenda mwanza na kigoma panachangamka ilikuwa mishe mishe kama upo zaidi ya kariakoo watu kibao ila leo pamekufa kabisa

Nikauona uwanja wa vita nikamkumbuka jamaa mmoja hivi alikuwa anaitwa matata ebwana alikuwa anarusha mawe uyo siku za mechi watu mkiwa mnachungulia mpira jamaa sijui yupo wapi

Miaka ile kina Steve nyerere, saimon mwapakata Aruna moshi boban almarufu kama babu bado watoto wanasoma shule ya msingi wanakutana katika michezo ya umita shumita shumita viwanja vya chuo cha uwalimu alafu Kuna mzee mmoja hivi mzee tawadadi sijui yupo uyu sijui alikiwaga nani ilikiwaga humkosi katika michezo ya umita shumita shumita

Miaka ile timu za mpira za miguu Daraja la tatu Kuna timu ya Posta kina amani mwenda Kuna timu ya police kina sharifu Kuna timu ya watoto wa mjini gongoni, timu ya rufita pia ilikiwepo timu ya watoto wa uswahili kiloleni hiyo timu ya maji maji timu ilikuwa na vijana Wana uwezo hii sema watoto wakiswahili wao

Du tabora enzi zile
 
Akina juma mnene na bob rich walisumbua sana kwenye breakdance mitaa ya isevya. Enzi hizo kama hujui kucheza hutakiwi kuingia kwenye stage aisee!
 
Akina juma mnene na bob rich walisumbua sana kwenye breakdance mitaa ya isevya. Enzi hizo kama hujui kucheza hutakiwi kuingia kwenye stage aisee!

Kaka nahisi tunajuana, hao watu walikuwa ni marafiki zangu, sijui wako wapi sasa! Bob rich bado yuko mboka ila juma mnene sijui yupo Dar au wapi!?
 
Nami ngoja nichangie kidogo huu uzi, maana nimeishi mboka manyema kwa takribani miaka 12, kuna mambo nayakumbuka kidogo na si vibaya kuyashea na wana, mimi mboka niliishi maeneo manne tofauti, kwanza kabisa bachu, then kanyenye, then mitaa ya karibu na SIDO na mwisho kabisa Cheyo. Tabora enzi zetu kulikuwa na vipaji sana vya mpira wa miguu na mpira wa kikapu, baadhi ya vijana waliokuwa wanapiga kandanda safi ni pamoja na kina Modu Banka, Kilowoko, Mayai, Iddi Moshi, Mrisho Moshi (Boban kipindi hicho bado kinda kabisa, akiwa pamoja na kina Nuru Mchemba, Meddy Azam, Petty Simbila na wengineo)
Kwenye kikapu enzi hizo ndio court la Uhazili limebamba kinoma, kila jumapili kulikuwa na game ya East and West, ilikuwa ni soo, mpaka mziki mkubwa ulikuwa unafungwa, umeme unavutwa kutokea zile nyumba nyeupe za walimu wa TTC ambazo zipo jirani kabisa na court la basketball la Uhazili, zimetenganishwa na fensi ya nyavu tu. Father Adam ndio alikuwa mhamasishaji, Kocha mchezaji kipindi hicho, kutoka East walikuwa watoto wa kuanzia Uhazili kurudi National hadi Cheyo huko, kina Mecco, Lubisha. Kutoka West kulikuwa na kina Marehemu Major, Dick wa Kanyenye etc. Jumapili wajanja wote lazima waishie hapo Uhazili.
 
Mkuu nimekubali,
Hata mimi unanijua!!!
 
#Mboka Manyema kama nimekutaja basi jua nakujua, maana niliowataja humo wote nawajua, n wengine wengi tu ila nimewasahau majina yao maaana ni kitambo sana, ila huwa ninapata amani sana ninapo ona madogo wa Mboka wakizidi kushine hadi sasa kwenye kikapu, mfano ni Salim Mchemba, namuona anafanya vizuri sana kwenye kikapu, pia alikuwepo jamaa mmoja hivi anaitwa James Kilongozi, siku hizi sijui yupo wapi, alikuwa naye fresh kwenye kikapu.
 
Mi nakumbuka wimbo wa shule tu
"Tabora School kichwa cha Tanzania"
"Jinalo kote linatajikaaaaaaaaaaaaaa"
"Hapa alisomeshwaaa,Baba yetu wa Taifa"
Enzi hizo Tabora Boys,tunawaza tu kucheza disco na Tabora Girls....Kulikuwa na demu anasoma sijui Kazima sijui Uyui mzuri sanaaaa,anaitwa Nongwa....Wapi Nongwa wapiiiiii

Hahahaha alisoma Kazima, nimesoma nae. She was a definition of beauty.
 
Back
Top Bottom