Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Mi nilikuwa nakaa isevya ila nasoma cheyo A. Mmenikumbusha mbali sana! Watoto wa kike wa mzee kagoma walikuwa wazuri sana kwa sababu ya rangi na watoto wa kiume walikuwa watemi sana. Nakumbuka tulikuwa tunacheza mpira (chandimu) mtendeni shule ya msingi, nikampiga kanzu na kisha nikamgeuza kwa tobo mtoto wa mzee kagoma, alikuwa anaitwa Bias nikashangaa akaanza kunipiga ( nilipigwa ngumi na kichwa kwa kumtoa nishai).
Mnakumbuka watoto wa mitaa ya bomba mzinga wakina Mugisha walivyokuwa wakorofi? Kuna kademu katoto ka kwa munene- Jaquiline nilimu approach ila nikasitisha kwa sababu alitaka kwanza apajue home kwetu, nikawa namkwepa kwa sababu kwetu ni choka mbaya!
Nakumbuka tena kuna msichana wa kihindi (Rahma) nilikuwa nampenda cheyo A primary school lakini nilikuwa domo zege, nikawa najiongelesha mambo mengine tofauti kwa muda mwingi ili watu wajue ni mtu wangu! Ha ha ha! Mwl Jacob nae alikuwa anamtaka akahisi labda nakula mzigo, nilikuwa nachezea fimbo za kutosha mpaka nilipokuja kushtuka ndio nikapunguza mazoea na Rahma. Mwl mkuu wetu kipindi hicho alikuwa Mwl Mlekwa.
Dr. Kobelo alikuwa anakaa nyuma ya shule yetu na mke wake alikuwa kutoka Russia.
Kisima cha kilimbika ndio kilikuwa kisima chetu kwa ajili ya kuchota maji.
Mitaa ya isevya, mzee shirima ndio alikuwa tajiri maeneo yale miaka ile na kulikuwa na mtoto wake wa kike Neema shirima alikuwa mzuri sana na anapenda sana masela! Kei na Tito shirima ndio walikuwa agemate wangu!
Nakumbuka mwizi maarufu Shantongo alichomwa moto miaka ya 90's.
Mapadre wa kanisa katoliki ipuli walikuwa wanakula mademu kilaini sana, wale wazungu hawakuwa ma-player.
Nakumbuka tulikuwa tunaenda Tabora hotel kushindana kucheza disco la watoto ili kupata kreti la soda kwa mshindi wa kwanza! Wakubwa walikuwa juu kipindi hicho walikuwa ni Bob wizard na Major. Bob wizard alikuwa mzuri kwa nyimbo za Michael Jackson. Sijajua hawa jamaa wako wapi?
Muungano mess masoja yalikuwa yanatufukuza watoto ikifika saa moja usiku!
Nasikia Tabora panaendelea kwa kasi kwa sasa ila isevya imegoma kuendelea, wachawi ni wengi mno kule!
I miss Tbr since 1995. I miss TZ since 2011.
 
Dahhh Kumbe Steve alifariki!!! R.I.P Bro

Nani anamkumbuka power chuma?
Kuna mtu anaijua REMEMBER MEMBER Uyui sec?
Huyu Sheikh Ilunga alikua mchezaji mzuri wa basket, Kuna mtu anakumbuka?
R.I.P Major.
R.I.P Mzee Kassimu muuza kahawa wa diamond.
R.I.P Issa Kibira.
Nani anamkumbuka Chande mwehu aka Chui. Ukimwita chui umekwisha.
Nani anamkumbuka Profesa? (epaina bisso) anakaa kama unaenda kiloleni alikua mtata saana mwanamke kama ana mimba akipanda basi lake ajue nauli analipa mara mbili yaani yeye na mtoto aliye tumboni haa haaa haaa.
Mnamkumbuka Cast wa mwanaisungu?
Je Patel head master Uyui Sec?
Haya wadau leteni story za mboka....
...ooops Major alifarikii...???? daaaah...!!??
 
...diamond cinema siku za sikukuu, nyomiiiii. siku wakitangaza sinema inamaudhui ya kikubwa yaani inamatukio ya "x" nyomi lake balaaa. kulikuwa na fundi redio pale pembeni mwanae nimesomanae uyui, sovi, khaleej video center tulikuwa member kukodi mikanda ya video kwa siku mia tatu kama sikosei,...
 
DJ Ally Maumba ............ Musa chamwi mkali wa break dance toka magereza
 
Mnamkumbuka epai na bisso? Vipi wale mbuzi Wa albadir? Jambazi sugu akiitwa Jackson kuku? Vipi mwaka ule wajeda walipofanya mauwaji ya majambazi sugu Kiloleni mitaa ya Ghana karibu na klabu cha saanane!
 
Dah! hii nyuzi imenikumbusha mbalii sana....Vitu kama master wetu Tabora Adam gosho aka ninja,alichezea kichapo cha maana kwa demu kutoka zambia,Jamaa ametutembeza sana mitaani na maigizo yetu ya kininja ninja,Tukiwa skauti na chipukizi pandisha sana matofali ya ujenzi uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,Uwanja wa vita kuangalia mechi ni mwendo wa kuruka ukuta au kusukuma baiskeli ya mlemavu kula sana Zambalau katika mapori ya kiwanda Cha nyuzi,matunda ndatiii utamu wake cjapata ona na wala sijawahi kutana nayo tena toka nimeondoka mboka,bint Swedi mtaalamu wa Maswezi,Kuzamia misosi ya kambi za Jeshi ndioo dah full ujanja halafuu maafande full amani unajipigia wali maharage utakavyo,mitaa maaarufu ya fujo fujo,Cheyo,sukuma street,gongoni,isevya,kiloleni,movie diamonds,indoors games zote pande za Rufita Club........Chizi fresh Makamba Jeki na kama umesoma Tabora chimbo maarufu la kusoma vitabu na hadithi za kiajemi ilikuwa ni pande za Maktaba kuu Tabora....Dah masiku kweliii yanakimbia
 
Umenikumbusha maktaba ya mkoa Tabora karibu na TMP daa....kipindi nasoma mihayo shule ya msingi kabla haijawa sekondari...ndo ilifanya mpka leo hii niwe na ugonjwa wa kupenda kusoma novo...hususani za kiswahili
 
Mkuu mimi ni mgonjwa hasa wa kusoma vitabu na nahakika kabisa mambukizi ya ugonjwa huu niliyapata katika maktaba ile ya Tabora.
 
Mkuu mimi ni mgonjwa hasa wa kusoma vitabu na nahakika kabisa mambukizi ya ugonjwa huu niliyapata katika maktaba ile ya Tabora.
Pale jirani kuna uwanja wa chipukizi nadhan upo mpaka leo kipindi hicho ulikua umezungushiwa fenci hkuna mtu kukatiza...baada ya kuondoka padre mmoja mzungu miaka hiyo ...uwanja ukaharibika na nadhan hv sasa hautamaniki...km kawaida yetu waswahili kutokua na utamaduni wa kutunza vitu
 
Mi nakumbuka tu kazima sec, mzee alikua anafundisha pale kazima early 90's wakati huo tunaishi maeneo ya sido mie bado kinder sana, mshua alikua mtata sana kwa mwanafunzi wakorofi kitu ambayo ilipelekea baadhi ya mwanafunzi kuanza kumuwinda usku. Baadae aliona isiwe sheedah akaachana na ualimu na tukahama tabora.
Nachokumbuka tulkua tukiwaona wale wabibi wabibi wamejitanda manguo meusi tulkua tunajua ni majini hivyo tunawakimbia, wakati ule ushirikina ulikuwa mwingi sana Tbr, wapi kitete shule yangu niliposomea vidudu. Dah hakika nikirud TBR nitapotea
 
Nilikuwepo Tabora miaka sabini mwishoni na themanini mwanzoni. Wakati timu ya vijana ya chipukizi chini ya Brother pale mission ikiwika baadaye ilitoa wachezaji ambao walikuja kuwa tishio katika timu mbalimbali tz kama Rajabu Risasi. Hamisi Limonga. Dickson Kanumba. Aidha Nakumbuka KAMISETA ya wakati ule ya kina Ahmed Amasha, Ally Mazunzu, zito kiaratu. Dakota n.k.
 
Duh Nakumbuka jumba la simema diamond talks. Wakati huo timu ya TAT ukiwa na wachezaji hatari kina gadaf. Ismaili. Hassan Morocco , Nakumbuka vitongoji maarufu kama Isevya. Gongoni. Ng,ambo n.k
 
Daaah wakuu mmetiririka sana kuhusu Tabora a.k.a Mboka Manyema
Mkuu umemikumbusha uwanja wa Chipukizi,jirani yake kulikuwa na shule ya viziwi na mabubu
Yaani Misa ya watoto pale kanisa katoliki jioni ikiongozwa na Padre Tengi au Padre Dino
Wale mabubh walikuwa tunawaogopa sana dadeki,nao wakawa wanatutandika mbaya tukiwacheka
Pale Maktaba karibu na TMP ndio palinifanya niwe mpenzi wa kusoma Novels mpaka leo,na nimejifunza kumbe utamadunu wa kujisomea vitabu unatengenezwa,ninafanya hivyo kwa wanangu ili wawe na huo utamaduni baadae
Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mnaingia wakati wa "fungulia Mbwa" au unaingia na mlemavu
Kuokoata mpira mpaka uwe na sare za scout au chipukizi
Daaaaah wapi watu wa Mboka Manyemaaaaaaaaa back 1990's
 
Mkuu#camber mbona kama tumesoma wote cheyo A....kama ulianza std one 92 tulikuwa darasa moja
 
Back
Top Bottom