Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 53,868
- 99,949
The Mwanaisungu honey pot na dj CISCO:thumbup::thumbup:😀😀😀
Mi nilikuwa mjini kabisa pale karibu na jamatini ule msikiti wa wahindi, pale NBC opposite na shule ya mihayo secondari. Enzi hizo unaandikiwa wimbo tu wa kizungu ambao uko kwenye chat basi ujumbe umeupata, dah old is gold kwa kweli.
Tabora enzi hizo miaka ya kuna demu alikuwa anaitwa Veronica Mhina alisoma unyanyembe
Student center watu walikuwa wanaenda Ku record ngoma kwa Aziz
National kulikuwa na totoz Kali kama kina magreth
Tatizo Moja kulikuwa hamna makahaba
Familia ya Dr Kobelo wengi walifariki,akiwepo Dr mwenyewe,mkewe na yule mtoto wao aliyekuwa ana akili sana baadae akawa chizi ,Yule alikuwa anatembea kama amekata centre bolt ya bega la kushoto alikuwa anaitwa Steve. Thobias baadae ya kufungwa alirudi uraiani na mara ya mwisho nilisikia anapiga tempo pale Orion Tabora Hotel, sasa sijui kama bado yupo hapo maana mwaka jana mmiliki wahoteli hiyo Bw POLLE a.k.a Kanyenyela alifariki dunia pia.
Mnaikumbuka ile bustani ya wanyama kule national? Nasikia ilishafungwa siku hizi. Nilikwenda Mboka mwaka juzi sikubaliani na nyie kuwa mji haubadiriki kimaendeleo maana nimeshuhudia majumba ya kufuru Mitaa ya mihogoni kule kama unakwenda kiwanda cha tumbaku Miemba na maeneo ya Ipuli na Cheyo. Kweli maendeleo siyo ya haraka lakini tunajikongoja taratibu.
Umeshau milambo wanaume VS Tabora boys siku moja tabora boys walikimbizwa mpaka mabwenini na Milambo wanaume. Aly mayai alikuwa anasoma Uyui sec, na victor mihayo, kidau na renatus njohore walikuwa tabora boys, pia kuna mtoto wa kiarabu wa tabora boys alikuwa hatari. milambo wanaume kulikuwa na kimti, goliati, mathew, na nk.
Dahhh Kumbe Steve alifariki!!! R.I.P Bro
Nani anamkumbuka power chuma?
Kuna mtu anaijua REMEMBER MEMBER Uyui sec?
Huyu Sheikh Ilunga alikua mchezaji mzuri wa basket, Kuna mtu anakumbuka?
R.I.P Major.
R.I.P Mzee Kassimu muuza kahawa wa diamond.
R.I.P Issa Kibira.
Nani anamkumbuka Chande mwehu aka Chui. Ukimwita chui umekwisha.
Nani anamkumbuka Profesa? (epaina bisso) anakaa kama unaenda kiloleni alikua mtata saana mwanamke kama ana mimba akipanda basi lake ajue nauli analipa mara mbili yaani yeye na mtoto aliye tumboni haa haaa haaa.
Mnamkumbuka Cast wa mwanaisungu?
Je Patel head master Uyui Sec?
Haya wadau leteni story za mboka....