Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Simbamwene tulikuwa tunaenda kuangua zambalau na embe boribo juu ya makaburi...vp umekuwa mji?ha ha ha ha ha ha umenikumbusha Mwajuma Ringa?ivi kwanini Mboka Manyema vichaa wengi?...dah Hamis Mambwa aliogopwaje?Diamond near by TMP uwanja wa Chipukizi?ukumbi wa Disco hapo Mwanaisungu geti la kuingia Uhazili...video tunangalizia Maua Bar Opposite na Central Police

Shule nilianzia chemchem duuh ikifika saa nne mbio simbamwene kwenye maembe nilipofika la tatu baba akanihamishia mwenge mazoezi mbona utoro uliisha maana nidhamu, walimu walikuwa wanafundisha vizuri, usafi ole wako uende bila kuoga unaogeshwa Shule, usipovaa soksi fimbo, kulikuwa na mwl chiboni, getaback, makore, dah kama kuna aliyesoma mwenge miaka ya 80_90 atanisaidia ooh chipukizi na skaut ni vitu ambavyo nimevitumikia sana kungekuwa na ajira nadhani ningekuwa na cheo kikubwa sana
 
Nilibahatika kupita huko mwezi wa 11 mwaka jana nikielekea Kahama, Shy. Kwa kweli Tabora ni mkoa uliokwisha, hakuna maendeleo yeyote zaidi ya kuwa na nyoka na vichaa wengi mjini. Mtu ukiiba kibiriti kwa mwarabu dukani basi unatupiwa ukichaa, yaani hakuna cha maana pale. Kila mtu anajifanya alwatani na ukiwa mwarabu unaogopewa kwani wakazi wanakuona wewe ni Mungu mtu.
 
FIFI alikuwa anatuhumiwa kuwaambukiza ukimwi dada zetu kwa makusudi,one day alionekana mitaa ya kwetu na dada mmoja wa pale pale mtaani kwetu anaitwa Tatu Mazegembe........alikuwa na makalio makubwa huyooo wacha.........basi wacha tumtoe nduki na mawe huku tunamwambia yule dada 'unaenda kufa wewe!!!'......aaaaa mboka matata wee.....mji wangu wa utotoni uliokataa kukua!

Mkuu nasikia kuna baadhi ya madada walipokuwa wakisikia hivyo..walikuwa wanaruka kutoka kwenye Pikipiki ya FIFI.
 
Dah,ingawa mimi sio zamani saana,lakini kiukweli umenikumbusha mabali sana...Miaka ya 90 kila mtaa taarab,anaolewa mtu leo baada ya miezi mitatu unasikia taarab kwao anaolewa tena... enzi hizo bendi ya mashujaa inavuma sana.Ndio baadaya maswezi yakaingia na kushika kasi mjini,unaambiwa ukiingia kucheza tu lazima uondoke nao! Nakumbuka ugomvi baina ya Tabora boys na Milambo boys...Nakumbuka wakati huo Wanafunzi wa Uyui wanaonekana mabishoo kuliko shule zote...Wakati huo mimi nasoma Mirambo TPDF ambayo baadaye ilikuja kuwa Unyanyembe..

Enzi zangu ni kipindi cha akina Yahya Akilimali wakati huo kulikuwa na kombe la Mgulunde..dogo alikuwa aknapiga vyenga huyo,wacha kabisa...Timu kali zilikuwa Tabora Boys na Milambo Boyz.Nakumbuka Chuo cha Reli ambacho baadaye kilikuja kufa..

Wakati huo ikisemekana kuwa Tabora ilikuwa miongoni mwa mikoa yenye warembo wakali(lkn sio miss tz!),unakuta mtoto mkali,lakinin fuatilia anapotokea sasa,ndio utashangaa...Wakati huo washua wanatokea Cheyo na National,hapo kabla ya Ally H. Mwinyi na Ipuli.Mitaa kama mwanza road,mabatini,bomba mzinga,matakini,chemchem,minazi mikinda,mbugani,nk. ilikuwa inafahamika kama mitaa ya watu wa hali ya chini!

Wakati ule daladala za nini,wakati kila mtu anamiliki baskeli?! Mnakumkumbuka TX(kwa sasa ni marehemu) pale stend kuu ya zamani?Kuli alikuwa mkorofi huyo,wacha kabisa.

Dah,Tabora... ingawa nipo mbali lakini nakumis sana,ipo siku nitarudi tu nyumbani..I love You Tabora.
 
Mkuu nasikia kuna baadhi ya madada walipokuwa wakisikia hivyo..walikuwa wanaruka kutoka kwenye Pikipiki ya FIFI.
..ila alikuwa na watoto wazuri sana wa kike,nilibahatika kuwa nae mmoja wao. anyway nakumbuka zaidi vituka vya msimu wa tumbaku,wasukuma a.k.a wasugusu wakisha uza tumbaku cha kwanza ni redio kuubwa cha pili baiskeli. nilikaa mitaa ya kazima kuna mwarabu mmoja alikuwa anaitwa kaserekandis enzihizo ndo alikuwa na mkwanja,kwake ndo kulikuwa na dish kuuubwa,advocate kwikima, na kota za benki na nyuzi ndo watoto masista doo ndo walikuwa wanakaa. disco ngoma ilikuwa isungu wazee wa kurusha chupa na muungano mess ya wanajeshi ukileta fujo tu sijui umegombana na demu wako unachezea kichapo kisha unatolewa nje.
..nilikuwa sikosi wellcome first year ya chuo cha ualimu, girls,uhazili na milambo. mitaa ya cheyo b ndo mji mpya ulikuwa unajengwa,kuna dingi mmoja alikuwa anaitwa chale nasikia amefungua kituo cha redio cg fm kama sikosei, anakaa mitaa karibu na mihayo sec,lilikuwa noma sana kwa videmu. nimekumbuka meengi sana ya tabora na naipenda sana mboka ila tatizo haina maendeleo kabisa,mwaka wa elnino tulitia akili, treni hakuna magari hayaji ndege hazitui uwanja unatereza,sukari ilifika 2000 kwa kilo.tujlijuta...naipenda sana mbokaaa,nilikuwa nazamia kwenye treni daah!
 
Umeshau milambo wanaume VS Tabora boys siku moja tabora boys walikimbizwa mpaka mabwenini na Milambo wanaume. Aly mayai alikuwa anasoma Uyui sec, na victor mihayo, kidau na renatus njohore walikuwa tabora boys, pia kuna mtoto wa kiarabu wa tabora boys alikuwa hatari. milambo wanaume kulikuwa na kimti, goliati, mathew, na nk.

Mkuu,
Umenikumbusha maana nimesoma Mihayo Sec na akina Victor Kilowoko, Mohamed Banka...ilikuwa ni balaa. Nakumbuka mechi ya nusu fainali kati ya Tabora Boys na Mihayo pale uwanja wa Vita (round about-boma road), Mihayo tukiwa na Victor Kilowoko na Medy Banka na Boys wakiwa na Wilfred Kidau na Ren Njohole...Booonge la drama jamani.
Pia pale Milambo alikuwepo mshambuliaji sijapata kuona kwa bongo (namaanisha chenga) akiitwa Feruzi Teru, jamani mboka ni nouma.
Enzi hizo ya miaka ya 90 Mihayo ilikuwa ikiongozwa na 'the late' mwl. Omari mzee wa totoz, yaani enzi hizo kiukweli kulikuwa na mashindano mazuri sana, maana mpaka mwaka 1997 huyu dogo Haruna Moshi 'Boban' akisomea pale Kazima huku akila majani pale miembeni nyuma ya Uyui Sec...jamaa alikuwa na kipaji kizuri saana.
Eneo la Mihogoni kuleee chini kama unaelekea kiwanda cha nyuzi, usiku ilikuwa hukatishi.
Mabasi enzi hizo yalikuwa ni Naamans na Shakila huku NBS akijikongoja, mboka bana ...kule isevya napo duuuuuh!
Halafu kulikuwa na yule muhindi wa Milambo, ndugu yake Kanji (mdhamini wa Milambo), huyu mdosi alikuwa best yangu maana tuliishi nae jirani pamoja na akina Adam Fundikira pale maghorofani jirani na NBC Bank ya sasa, ukiingia sokoni basi unapata matunda yaitwayo ntalali, mantonga, nfulu, makopa etc.
Miss u Mboka Manyema...daaah!
 
Simbamwene tulikuwa tunaenda kuangua zambalau na embe boribo juu ya makaburi...vp umekuwa mji?ha ha ha ha ha ha umenikumbusha Mwajuma Ringa?ivi kwanini Mboka Manyema vichaa wengi?...dah Hamis Mambwa aliogopwaje?Diamond near by TMP uwanja wa Chipukizi?ukumbi wa Disco hapo Mwanaisungu geti la kuingia Uhazili...video tunangalizia Maua Bar Opposite na Central Police

Mwanaisungu ilishagakufa mkuu....
 
Miaka hiyo,mwenye hela kitaa aidha ni mwanajeshi au anafanya kazi tumbaku kule chini-Miemba.Nakumbuka kipindi cha Elnino,mitaa ya chemchem,mihogoni,mabatini na baadhi ya mitaa ya mwanza road vinyumba vilikuwa vinayeyuka vyenyewe kwa maji.

Nakumbuka kuna visamaki fulani hivi vinakaushwa na mawese,ukila hutoi mfupa.Hata sikumbuki vilikuwa vinarokea wapi vile.Kikubwa maembe(dodo&bolibo),ntalali,ntonga,zambarau,ndati...jamani hivi mnavikumbuka hivi!

Ooh.. my Tabora. I miss you so much,baby!
 
Ha ha ha ha Ntalali na Ntonga!pale Tabora Boys alikuwepo Yahaya Akilimali..kafupi lakn kanapiga chenga mpaka balaaa...mwalimu alikuwa Bundala na Brasband ya Kanyaboya....unakutana mtbni na demu bomba ajabu lakin anatoka nyumba ya mbavu za mbwa!jambo la kawaida kukuta mauzauza njia panda..kuku kachinjwa na nazi imebanduliwa!!....watu wanaishi kwa kula vipande vya mihogo vilivyokatwa sokoni.......mtaa wa Marando Ng'ambo unasifika kwa wauza makopa wakiwa na vibatari!FIFI anamiliki pikipiki na ndo Digala....Tabora haiendelei licha ya ukongwe na umaarufu wake!imetoa watu maarufu na imesomesha viongozi pale Tbora Boys!Ngoma ya Waswezi na ushirikina!Wapi Dr.Othman kada wa CUF?U.M.D na NRA ndo ngome zao!1995 Mrema yupo moto..kaja na Makongoro Nyerere uwanja wa Kazima Sec..Nakumbuka Nukuu ya Makongoro "Mfupa uliomshinda Fisi Mbwa ataweza?"...kwamba ye kazaliwa Ikulu na kukulia humo lakn yupo NCCR!Tukamsukuma Mrema mpaka hoteli flani ipo BOMA-Road
 
Ngaliba Dume,mimi mara ya kwanza kumwona Y.Akilimali ilikuwa mechi ka T.Boys na Mihayo.kwnye kombe la Mgulunde(kama sijakosea),ilikuwa inachezwa kwenye kiwanja cha TTC,dogo mfupi ila anawalamba watu vyenga mpaka basi?

Halafu kuna jamaa fulani hivi alikuwa anaitwa Msabaha alikuwa anaishi karibu kwa Sheik Mavumbi,mitaa ya msikiti wa mwanza road;jamaa alikuwa mpole mpole mchana ila usiku alikuwa jambazi la kutupa.Alikuwa ni miongoni mwa Banyamulenge miaka ya 95/96 hivi,sijui kama mnakumbuka.
 
Ndio Askofu Mario Mgulunde!kombe lake lilikuwa linaleta raha sana mjini!Akilimali alikuwa balaaaa,kafupi na chenga za kufa mtu!ulikuwa ni wakati wa raha mechi yetu Tabora Boys na Milambo lazma defender ya FFU ifike....Msabaha jamczi Sugu..hakuna mtu aliyeishi Mboka miaka hiyo asimjue!Tbora kwa ugumu wa maisha iliongoza kwa vibaka na majambazi!wanawake akikukamata hutoki!mana vijimama vya mboka ushirikina kwa sana
 
Halfu huu mgogoro wa T.B na M.B sijua ulianziaga wapi.Mimi nimekuwa nikaukuta,nikauacha sijui kama bado unaendelea.Nakumbuka kipindi fulani waliumizana sana baada ya Walambo kuwavamia T.B kule kwao majira ya jioni/usiku.

Asikuambie mtu,Tabora ina historia yake bwana.Kama hujakulia kule huwezi kujua raha ya maisha yakule..
 
Umeshau milambo wanaume VS Tabora boys siku moja tabora boys walikimbizwa mpaka mabwenini na Milambo wanaume. Aly mayai alikuwa anasoma Uyui sec, na victor mihayo, kidau na renatus njohore walikuwa tabora boys, pia kuna mtoto wa kiarabu wa tabora boys alikuwa hatari. milambo wanaume kulikuwa na kimti, goliati, mathew, na nk.

Eeeh bwana eeh. Nilikuwepo hiyo siku, tulichapa BOYS na GIRLS. Tabora girls walikuwa wanawashangilia sana BOYS. Ndipo milambo wakachukia na kuanza kutembeza bakora. Unawajua WARSAW? Walikuwa wanatuita sisi wa MILAMBO eti NATO (NO ACTIO TALKS ONLY)
 
Halfu huu mgogoro wa T.B na M.B sijua ulianziaga wapi.Mimi nimekuwa nikaukuta,nikauacha sijui kama bado unaendelea.Nakumbuka kipindi fulani waliumizana sana baada ya Walambo kuwavamia T.B kule kwao majira ya jioni/usiku.

Asikuambie mtu,Tabora ina historia yake bwana.Kama hujakulia kule huwezi kujua raha ya maisha yakule..

Historia ya ugomvi wa T.B na M.B ni wasichana wa T.Girls...na uhasama wa kimasomo!T.B wamekuwa wakifanya vizuri ktk masomo na kuwabeza M.B!Mara nyingi T.B wanajiita "vipaji"(sijui ni kweli?) wakati wanawaona M.B kama "vilaza"....lakin zaidi ile hali ya kuwa shule ya Jeshi wakati huo ilifanya T.B wajiamini zaidi ya M.B
 
..ila alikuwa na watoto wazuri sana wa kike,nilibahatika kuwa nae mmoja wao. anyway nakumbuka zaidi vituka vya msimu wa tumbaku,wasukuma a.k.a wasugusu wakisha uza tumbaku cha kwanza ni redio kuubwa cha pili baiskeli. nilikaa mitaa ya kazima kuna mwarabu mmoja alikuwa anaitwa kaserekandis enzihizo ndo alikuwa na mkwanja,kwake ndo kulikuwa na dish kuuubwa,advocate kwikima, na kota za benki na nyuzi ndo watoto masista doo ndo walikuwa wanakaa. disco ngoma ilikuwa isungu wazee wa kurusha chupa na muungano mess ya wanajeshi ukileta fujo tu sijui umegombana na demu wako unachezea kichapo kisha unatolewa nje.

..nilikuwa sikosi wellcome first year ya chuo cha ualimu, girls,uhazili na milambo. mitaa ya cheyo b ndo mji mpya ulikuwa unajengwa,kuna dingi mmoja alikuwa anaitwa chale nasikia amefungua kituo cha redio cg fm kama sikosei, anakaa mitaa karibu na mihayo sec,lilikuwa noma sana kwa videmu. nimekumbuka meengi sana ya tabora na naipenda sana mboka ila tatizo haina maendeleo kabisa,mwaka wa elnino tulitia akili, treni hakuna magari hayaji ndege hazitui uwanja unatereza,sukari ilifika 2000 kwa kilo.tujlijuta...naipenda sana mbokaaa,nilikuwa nazamia kwenye treni daah!

Yeap..nakumbuka kuhusu watoto wake..alikuwa anaishi Kiyungi... Unawakumbuka waswezi mkuu? Kuna bibi mmoja pia alikuwa anaishi Kiloleni anaitwa Binti Swedi huyu alikuwa mtaalamu wa kuondoa majini na kuwapa watu uganga. Kiloleni hiyo hiyo kulikuwa na Bibi Paka(hana wengi kama Bibi Nyau) ila yeye kazi yake ilikuwa kutumia kichawi.
 
Halfu huu mgogoro wa T.B na M.B sijua ulianziaga wapi.Mimi nimekuwa nikaukuta,nikauacha sijui kama bado unaendelea.Nakumbuka kipindi fulani waliumizana sana baada ya Walambo kuwavamia T.B kule kwao majira ya jioni/usiku.

Asikuambie mtu,Tabora ina historia yake bwana.Kama hujakulia kule huwezi kujua raha ya maisha yakule..

Eeeh bwana eeh. Nilikuwepo hiyo siku, tulichapa BOYS na GIRLS. Tabora girls walikuwa wanawashangilia sana BOYS. Ndipo milambo wakachukia na kuanza kutembeza bakora. Unawajua WARSAW? Walikuwa wanatuita sisi wa MILAMBO eti NATO (NO ACTIO TALKS ONLY)

Nani alikuwepo pia siku tuliyokwenda kwa mkuu wa shule kufanya fujo kilichotokea kwa kuku wake aliofuga bandani11? na tulivyokwenda kumwaga ki..esi T.G?

GO EAST,GO WEST,MILAMBO IS THE BEST...haya maandishi unayakuta juu ya ubao darasani..
 
mihayo ya HOKOLOLO, tulikuwa na kpa mmoja matata sana MGOMVI KAMBI mdogo wake SAHAU...jamaa alikuwa mzuri sana golini, he died though...enzi za FIRST & LAST pale kanyenye kwa refa mzee msonga na wanae kibao...
 
Kweli mimi mwenyeji pale lakini wewe nakupa salute, kuna watu umenitajia mwenyewe nimechoka mfano Adam gosho,Makamba jeki haa haaa haaaa...katika wachezaji usimsahau wastara bari bari. kuna mtu alikua anaitwa albanda wiii kwa kula huyu jamaa hata makamba jeki anasubiri. Ahh Uyui Sec nakumbuka Remember Member sijui kuna mtu anaijua hii humu? anyway Mnamkumbuka Amani mwehu, Roshi, Jetha haa haa haaa
Chiku kaspoti haa haaa haaaa

daaaaah!noooma mukuu!amani mwehu....hahahahahahahahah................wastara baribari,feruz telu
quresh ufunguo,jobe ayubu na wenzao wengi walinunuliwa simba wote kipindi ile bana.........wakawapisha kina alyy mayay na kina kidau na kina rena njohole waliokuwa shule pale!

nawakumbuka watoto wa mzee mmoja maarufu pale anaitwa mzee kagoma........warembo ila ''wanachapisha'' hao.....hataree!
 
Mkuu nasikia kuna baadhi ya madada walipokuwa wakisikia hivyo..walikuwa wanaruka kutoka kwenye Pikipiki ya FIFI.

huyu tatu mazegembe ninaemsema hapa alivunji,ka mguu kwa kuruka aisee!
 
Back
Top Bottom