AdvocateFi
JF-Expert Member
- Jan 15, 2012
- 11,492
- 5,050
Mkuu pamoja sana, Pande za Mboka hapa kitaa cha Mwinyi.
Mkuu kwani sasa hivi unaishi wapi?Miaka ya 80's mwanzoni nilipata kuishi Tabora Mjini,baadae nikaja kusoma Tabora Boys miaka ya 90's....leo nimekumbuka maisha ya Tabora,Ujio wa Baba Mtakatifu,enzi za ukuu wa Mkoa Ndugu Gama....Timu ya mpira ya Milambo chini ya akina Job Ayoub "kwasakwasa",Quresh Ufunguo,Dadi Phares,Hamad Mwinyimkuu,Abas Mchemba na Bubu fulani alikuwa na mashuti sana wengine siwakumbuki Matajili wa wakati huo ni matajili wa mbao wakiitwa "Digala",kuna jamaa alikuwa tajili wa mbao mitaa ya Kiyungi karibu na Filter akiitwa Fifi(sijui kama yu hai)...mitaa ya ng'ambo mtaa wa Rehani alikuwepo Mavyombo,Msabaha...!kulikuwa na kina Said Kindamba,Waarabu wa Kwihara na Mrema wa Cheyo!...Miaka hiyo Tabora ilisifika kwa kuwa na Majambazi hatari,wengi wakitokea mitaa ya Ng'ambo..kuna jambazi mmoja walimkata mguu ili aache kuiba akawa anatembea na gongo(nimemsahau jina),Vichaa(wehu) wa kutosha na maarufu kama Athumani Nuna,Super Tall,Aman n.k...Mitaa ya wajanja ilikuwa National na Cheyo!!Misosi kama ugali muhogo,makopa,mawese na ngazi...Vipi nani wa Tabora anipe update za leo?mda sijafika Chemichemi,Gongoni,Bachu,Kanyenye,Kiloleni,Isevya,K'koo,Mwanza Road na Ipuli....Wapi vijana wa enzi hizo wa Mboka Manyema?
Yeap..nakumbuka kuhusu watoto wake..alikuwa anaishi Kiyungi... Unawakumbuka waswezi mkuu? Kuna bibi mmoja pia alikuwa anaishi Kiloleni anaitwa Binti Swedi huyu alikuwa mtaalamu wa kuondoa majini na kuwapa watu uganga. Kiloleni hiyo hiyo kulikuwa na Bibi Paka(hana wengi kama Bibi Nyau) ila yeye kazi yake ilikuwa kutumia kichawi.
Mkuu kwani sasa hivi unaishi wapi?
..nyumbani kwake kuna magari mengii mabovu mabovu,mzee nikifika kona namtuma dogo akamtoe binti enzi hizo hata simu sina ... mitaa ya national kulikuwa na wanangu flani wazee wa ganja sanaaaaaa,afu eti wote saizi ni askari polisi central dsm ..wauza mitumba ndo walikuwa mabitozi. tuliandaa party moja ya washikaji bichi yetu ilikuwa igombe,..
Miaka ya 80's mwanzoni nilipata kuishi Tabora Mjini,baadae nikaja kusoma Tabora Boys miaka ya 90's....leo nimekumbuka maisha ya Tabora,Ujio wa Baba Mtakatifu,enzi za ukuu wa Mkoa Ndugu Gama....Timu ya mpira ya Milambo chini ya akina Job Ayoub "kwasakwasa",Quresh Ufunguo,Dadi Phares,Hamad Mwinyimkuu,Abas Mchemba na Bubu fulani alikuwa na mashuti sana wengine siwakumbuki Matajili wa wakati huo ni matajili wa mbao wakiitwa "Digala",kuna jamaa alikuwa tajili wa mbao mitaa ya Kiyungi karibu na Filter akiitwa Fifi(sijui kama yu hai)...mitaa ya ng'ambo mtaa wa Rehani alikuwepo Mavyombo,Msabaha...!kulikuwa na kina Said Kindamba,Waarabu wa Kwihara na Mrema wa Cheyo!...Miaka hiyo
Tabora ilisifika kwa kuwa na Majambazi hatari,wengi wakitokea mitaa ya Ng'ambo..kuna jambazi mmoja walimkata mguu ili aache kuiba akawa anatembea na gongo(nimemsahau jina),Vichaa(wehu) wa kutosha na maarufu kama Athumani Nuna,Super Tall,Aman n.k...Mitaa ya wajanja ilikuwa National na Cheyo!!Misosi kama ugali muhogo,makopa,mawese na ngazi...Vipi nani wa Tabora anipe update za leo?mda sijafika Chemichemi,Gongoni,Bachu,Kanyenye,Kiloleni,Isevya,K'koo,Mwanza Road na Ipuli....Wapi vijana wa enzi hizo wa Mboka Manyema?
mkuu umenikumbusha sana simba mwene kulikuwa na makaburi ya saburi mzinga duh!mi pia sijaenda muda lakini kama ulikuwa unajua mbuga ya simbamwene kulikuwa na miembe ya kufa mtu sasa hivi ndio inaitwa ali hassani Mwinyi Yaani mji mpya umekuwa huko
wakuu kuna anaemkumbuka Adam Gosho na mazingaombwe yake ya uongo na vijana wake wale wa Karate!!?disco la mwanaisungu opp.uhazili.........upinzani wa timu za mpira miaka ile..........timu ya posta na polisi,magereza ya uyui na rhino ya nzega gemu zinapigwa uwanja wa kumbukumbu ya vita pale,watoto wa gongoni na bange zao!kisima cha kilimbika,bwawa la Taliani(kulisemekana kulikua na 'chunusi' kule....lol!)...................wahalifu maarufu aka zile kina Mafuta ya ndege(anakimbia huyo.....hatareeee,Bolt hakamati!),Jackson kuku,sinema za ukumbi wa Diamond miaka ile.
nakumbuka tukio la mabehewa ya petroli kuwaka moto pale stesheni..kilikuwa kipindi cha vita ya ghuba,basi tukajua marekani na saddam wameanza kukinukisha na huku tayari.....lol!
Maika ya father malio mgurunde, the late..MBOKA YA MIAKA HIYO HUWEZI ONA MBWA STATION KAMA HAKUNA TREN YA ABILIA, WALIKUWA WANAJUA RATIBA ILI WAPATE MISOSI
Umenikumbusha mwalimu chiboni ndiye aliyenifundisha English, unaikumbuka ile sala...Our father? Jotter je? mwalimu chiboni ni marehemu, getaback nadhani alirudi kwao ni muiraq wa kule arusha....mwalimu nachenga alikuwa mnoko je unamkumbuka mwalimu balozi na msha? Mwalimu fundi alikuwa mtaalam wa Geography, anaweza kuichambua New York na zile boroughs zake utafikiri amefika, blockln sijui nini? mimi nilimaliza la saba mwaka 1990.... Bila ya kumsahau mama yangu Mwalimu Shigela mwalimu wa darasa la kwanza mungu amzidishie afya njema yupo taboraShule nilianzia chemchem duuh ikifika saa nne mbio simbamwene kwenye maembe nilipofika la tatu baba akanihamishia mwenge mazoezi mbona utoro uliisha maana nidhamu, walimu walikuwa wanafundisha vizuri, usafi ole wako uende bila kuoga unaogeshwa Shule, usipovaa soksi fimbo, kulikuwa na mwl chiboni, getaback, makore, dah kama kuna aliyesoma mwenge miaka ya 80_90 atanisaidia ooh chipukizi na skaut ni vitu ambavyo nimevitumikia sana kungekuwa na ajira nadhani ningekuwa na cheo kikubwa sana
Miaka hiyo,mwenye hela kitaa aidha ni mwanajeshi au anafanya kazi tumbaku kule chini-Miemba.Nakumbuka kipindi cha Elnino,mitaa ya chemchem,mihogoni,mabatini na baadhi ya mitaa ya mwanza road vinyumba vilikuwa vinayeyuka vyenyewe kwa maji.
Nakumbuka kuna visamaki fulani hivi vinakaushwa na mawese,ukila hutoi mfupa.Hata sikumbuki vilikuwa vinarokea wapi vile.Kikubwa maembe(dodo&bolibo),ntalali,ntonga,zambarau,ndati...jamani hivi mnavikumbuka hivi!
Ooh.. my Tabora. I miss you so much,baby!
Namkumbuka mzee masoli alikuwa na msichana potable anaitwa mombe...duh mwingine alikuwa anaitwa farida masoli nadhani ni mtangazaji kwa sasa.....pale cheyo kwenye kota za nyuzi kulikuwa kuna kama nyumba nyingi ziko kwenye fensi ina msitu sikumbuki zilikuwa ni za shirika gani karibu na shule ya msingi cheyo A .... MNAWAKUMBUKA kina THOBIAS KOBELLO...watoto wa DR KOBOLLO yule mtaalam wa kuzalisha aliyesoma Hungary nilisoma na thobis sijua ana hali gani maana mara ya mwisho nilisikia amechanganyikiwa kabisakuna dingi moja lilikuwa linaitwa mzee masoli lilikuwa ni meneja wa nyuzi, lilishusha mjengo mmoja mkali sana karibia na relini kama unaelekea inala au kwenye mashamba ya mzee kapela,limekula sana hela za kiwanda cha nyuzi na muhasibu wake nimemsahau jina..
..bila kusahau wauza samaki maarufu(sato) toka mwanza pale benki ya nmb karibu na mihayo sec,wacheza kikapu maarufu mazoezi ndani ya uhazili wakina chaima,kabulola, dani muhina mtoto wa dr muhina,amleki,mbanza,meja(mshikaji alikuwa na ngoma haachi demu). nilipofika tu mboka enzihizo uwanja wa vita karibu na kasu filling station ndo ulikuwa mkubwa kabla mwinyi haujakamilika ndo mechi zilikuwa zinapigwa sana. kwakuwa tulikuwa wapenzi wa movi za kihindi tulikuwa tuna kodisha mikanda ya video pale khaleeji video center na diamond cinema,..Kulikuwa na malori mabovu kayapaka rangi nyekundu!mbele ya nyumba yake kulikuwa kuna uwanja twacheza mpira!ukipita enzi hizo Mzambalaweni unakuta vibanda kibao...biashara ya wajanja kweli ni mitumba,japo ukiwa unafuata Dagaa Mwanza na Kigoma we ndo unaonekana next level...kulikuwa na Binti Swed na Binti Ailala..hawa kukutupia majini hawaoni tabu...
blueivvy nahisi zilikuwa za FRMP,sikumbuki vizuri,thobias kobelo mara ya mwisho nadhani alikuwa na kesi ya kuua kama sikosei na mwingine alifungwa au alikuwa na kesi,watoto walikuwa wanakula unga na bangi vibaya sana. na mchizi wao Mc bob C ndo alikuwa anawaongoza, mdogo wao tu ndo alikuwa ametulia. huyu dr kobello hospitali yake ilikuwa mitaa ya kanyenye karibu na fourways au tanesco..Namkumbuka mzee masoli alikuwa na msichana potable anaitwa mombe...duh mwingine alikuwa anaitwa farida masoli nadhani ni mtangazaji kwa sasa.....pale cheyo kwenye kota za nyuzi kulikuwa kuna kama nyumba nyingi ziko kwenye fensi ina msitu sikumbuki zilikuwa ni za shirika gani karibu na shule ya msingi cheyo A .... MNAWAKUMBUKA kina THOBIAS KOBELLO...watoto wa DR KOBOLLO yule mtaalam wa kuzalisha aliyesoma Hungary nilisoma na thobis sijua ana hali gani maana mara ya mwisho nilisikia amechanganyikiwa kabisa