Mohammed wa 5
JF-Expert Member
- Jun 20, 2022
- 1,215
- 2,992
Hope ni wazima wana JF,
Je, uliwahi kufanya tukio gani la hatari kipindi unakua?
Sitosahau siku moja ilikuwa ni likizo ya Pasaka siku ya Ijumaa tukiwa group la watoto kama 6 hivi, mmoja alikuwa wa kike Jesca, tulienda porini sio mbali sana na maeneo tunayoishi.
Baada ya kutembea tembea kidogo kuna sehemu tulikuta mzinga wa nyuki mkubwa, kwa akili za kitoto, tukaanza kurusha mawe kwenye mzinga, wale nyuki muda mfupi tu walisambaa eneo lote, ile siku tuliumwa na nyuki balaa.
Tukaanza kulia huku tukipiga kelele za maumivu, tusaidieni tunakufa, baada ya muda tulikuja kuokolewa na wakata miti waliopo eneo lile. Nakumbuka Jesca na Isam walikuwa na hali mbaya walishambuliwa sana na nyuki. Jesca na Isam walilazwa ICU maana hali yao ilikuwa taabani.
Ikabidi tukimbizwe hospital kwa matibabu, tunamshukuru Mungu wote tulipona, nakumbuka ilikuwa story kubwa mtaani.
Naomba kuwasilishaa 🙏