Tukumbushane muziki aina ya mchiliku au mnanda na vituko vyake enzi hizo upo kwenye chati

Duh! umenirudisha 1995 enzi za Dar Nyota Theatre kundi la CCM.. na nyimbo kama Ally Mwinyi,Shemeji umeulamba Mkopo wa Sukari, Kurumbizi nk. Wakawepo Hisani na nyimbo kama Uko wapi Mama, kuna kipande wanasema"nipe nipe bwana Chidile..." Kuna Atomiki "Meli Ya sumu", Jagwa na ngoma kama Asha,Eleven Stars watoto wa chalinze makazi Tandale na Album lao Narudi Chalinze. Huu muziki una ujumbe sana. Naamini katika mwanamuziki mmoja au bendi za Tanzania nilizopata kuona wakifanya live shows...hawa jamaa wa Jagwa hawana mpinzani. hebu tazama hii... http://m.youtube.com/watch?v=wf7hWQ4FWDc
 
Mchiriku una mashairi fulani yanayowakikisha maisha ya uswahilini vizuri sana.
 
Duh! umenirudisha 1995 enzi za Dar Nyota Theatre kundi la CCM.. na nyimbo kama Ally Mwinyi,Shemeji umeulamba Mkopo wa Sukari, Kurumbizi nk. Wakawepo Hisani na nyimbo kama Uko wapi Mama, kuna kipande wanasema"nipe nipe bwana Chidile..." Kuna Atomiki "Meli Ya sumu", Jagwa na ngoma kama Asha,Eleven Stars watoto wa chalinze makazi Tandale na Album lao Narudi Chalinze. Huu muziki una ujumbe sana. Naamini katika mwanamuziki mmoja au bendi za Tanzania nilizopata kuona wakifanya live shows...hawa jamaa wa Jagwa hawana mpinzani. hebu tazama hii... http://m.youtube.com/watch?v=wf7hWQ4FWDc

Clips zinahusika. Machizi wamewarusha watasha na "Baba Dulla" mpaka itabidi watasha wajiulize Baba Dulla ni nini.

Shukurani.

Hii hapa nyingine wapo kitaa Bagamoyo ghetto red hot, kuna mchizi anacheza huku kashikilia viatu halafu mikono juu.

https://www.youtube.com/watch?v=vnAPPXVCQQg

Halafu hapa kuna "Mwana wa Kitwana"

https://www.youtube.com/watch?v=-8CMmK-IbtU

Videos zimenikumbusha bongo sana, kuna machizi walikuwa wanapiga mchiriku hiki kipande cha "Kwa Mfuga Mbwa" kuanzia Argentina mpaka Mahakama ya Ndizi, halafu wengine kipange cha Buguruni kuanzia Malapa mpaka CCM huku.
 
Huu mziki wa mchiriku ni mzuri sana kuusikiliza kwani unaelimisha na kuburudisha. Tatizo lake ni kwenye LIVE SHOW zao tu, kama wewe ni mtoto wa kishua hata kusogea hautaweza.Utakutana na sura ambazo huwezi amini kama zipo kwenye sayari hii.Halafu pombe ya gongo na bangi ndio kiburudisho chao.
 
Duh! umenirudisha 1995 enzi za Dar Nyota Theatre kundi la CCM.. na nyimbo kama Ally Mwinyi,Shemeji umeulamba Mkopo wa Sukari, Kurumbizi nk. Wakawepo Hisani na nyimbo kama Uko wapi Mama, kuna kipande wanasema"nipe nipe bwana Chidile..." Kuna Atomiki "Meli Ya sumu", Jagwa na ngoma kama Asha,Eleven Stars watoto wa chalinze makazi Tandale na Album lao Narudi Chalinze. Huu muziki una ujumbe sana. Naamini katika mwanamuziki mmoja au bendi za Tanzania nilizopata kuona wakifanya live shows...hawa jamaa wa Jagwa hawana mpinzani. hebu tazama hii... http://m.youtube.com/watch?v=wf7hWQ4FWDc
Wewe ndo umeuuwa wote wliobakia hata kolokoloni hajui mchiriku hao hisani walikuwa noma kuna rafki yangu mmoja alikuw anaimba hilo kundi walimuua way bck, nakumbuka nymbo yao mola na ali mwny...pia kuna nght star ya kkoo.
 
Kiukweli hata mimi naukubali tatizo mashabiki wake walikuwa hatari sana yaani hawakosi bisibisi,kisu,kipanga au wembe.
 
Nawasikiliza bendi moja ya Indie Rock, jamaa ni Ivy League (Columbia) preppy boys kutoka NYC , lakini wamepiga kwa kuchukua vionjo fulani vya kiafrika, kuna vinanda fulani katika "California English" utadhani umerudishwa "Kwa Mfuga Mbwa".

Vampire Weekend - California English
http://youtu.be/vTYDSWqAeNc
 
Duh! umenirudisha 1995 enzi za Dar Nyota Theatre kundi la CCM.. na nyimbo kama Ally Mwinyi,Shemeji umeulamba Mkopo wa Sukari, Kurumbizi nk. Wakawepo Hisani na nyimbo kama Uko wapi Mama, kuna kipande wanasema"nipe nipe bwana Chidile..." Kuna Atomiki "Meli Ya sumu", Jagwa na ngoma kama Asha,Eleven Stars watoto wa chalinze makazi Tandale na Album lao Narudi Chalinze. Huu muziki una ujumbe sana. Naamini katika mwanamuziki mmoja au bendi za Tanzania nilizopata kuona wakifanya live shows...hawa jamaa wa Jagwa hawana mpinzani. hebu tazama hii... http://m.youtube.com/watch?v=wf7hWQ4FWDc

daaah mkuu cd zao zinapatikana wapi!?? au kama vp nitumie kwa email nijue
 
ehh mie namkumbuka Jamaa alikuwa anaitwa Kunguru wa Mizoga alimuimbia jamaa Mmoja anaitwa Shua mtemi wa Kiboko Msheli maeneo ya Magomeni Makuti
 
Dah,long time kitambo Mkuu,enzi hizo Maskani Kuu ya Mchiriku ilikuwa Mwembe Yanga Famagusta kwenda mpaka kwa Mpogo. Vibao vya enzi zile kama vile Kinyago Msela,Saidi Kipaka/Masikani Famagusta nk vilikuwa balaa,hapo ni moshi wa msuba kama vile mpo Jamaica. Kwa upande wa sasa Vijana wanajitahidi sana kuuendeleza huu Mziki but cha kusikitisha haupewi kipaumbele kwenye Media karibu zote kama inavyopewa taarabu na wakati huu Mziki una mafundisho makubwa sana kwa hali ya sasa na vile vile ni rahisi sana kuwafikia wahusika wakuu ambao ni Vijana. Embu sikiliza wimbo kama Usije Mjini Kaka,una mafundisho makubwa sana kwa wale Vijana wakijijini wenye mawazo kuwa Mjini ndio kila kitu,jamaa anawaambia kuwa huku Mjini ajira kubwa ni kuokota makopo na scrapers.

Na upande wa pili wakusikitisha kwenye huu mziki ni kuondokewa na waimbaji/watunzi wake mahiri kama vile Omary Omary,Juma Mpogo,General Lupozi n.k R.I.P.

mkuu hivi hawa jamaa cd zao zinapatikana wapi nazitafuta sana... muda huu kuna wimbo unaitwa kuruthumu ndio nilikuwa nausikiliza umenikimbusha mbali sana.
 
Zamani pale Msasani zilipo ofisi za Zantel na New Msasani Club kulikuwa kunapigwa mnanda kila weekend...

Palikuwa na eneo la wazi basi wale Wamakonde wa kwa Mussa Hassan (Msasani), Wazaramo na wenyeji wengine wa maeneo ya karibu walikuwa wanajazana hapo...

Kuna jamaa zetu fulani wanaitwa Chikokoti na Said Makacholi ulikuwa huwakosi hapo kwenye disco vumbi hilo...

Nakumbuka hizi nyimbo kama Nipeleke nipeleke, Mama nataka uji au Mama nipe Panadol naumwa gono mimi...

hii thread imefanya siku yangu kuwa nzuri sana.
 
Yallah mbavu zangu yaani nalia kwa kicheko maana umenikumbusha enzi yake wakiitwa kuja piga sehemu wanapanga foleni halafu wanajidai kuingilia mlango wa uwani wanatokea mlango wa mbele wakifika sebuleni (sitting room) wanajidai macho juu macho juu mwenyeji naye anaangalia juu mzunguko ukiisha sebuleni hakuna kitu ni kweupe vimekombwa vyote vya kabatini hadi vitambaa ktk viti kinachoachwa ni kisichobebeka kiurahisi, mwizi hajulikani. mkuu hongera kuleta mada hii ila nyimbo sikumbuki hata moja.
 
haha ya hivyo mimi sikupata ishuhudia
 
Back
Top Bottom