KOLOKOLONI
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 2,477
- 2,360
Je unakumbuka mnanda/mchiliku na vituko na matukio yake enzi hizo upo kwenye chati.je umeumis mziki huu wenye radha ya aina yake? Ebu tutajia nyimbo unayoijua
Hawakuiba kioo kweli?
Teh teh nakumbuka jirani yetu pale mitaa ya kongowe kibaha alikuwa na sherehe yake ya harusi mwanzo wa miaka ya 2000 hivi basi usiku pale ilikuwa jirani na home,umeme wamekuja kuchukua home mbali kidogo,basi mwenye shughuli anataka kupiga taarabu na mnanda tu masela wanataka bongo fleva wameshachoka kusubiri mida ya saa 8 usiku hiyo walifanya tumbwili jamaa wakakata waya wa umeme kwa shoka,
Short ilirudi home bahati iliwahi kujizima kidogo tuunguze nyumba, toka siku hiyo hata aje nani home anataka moto hatupeleki ilikuwa fundisho,
Lakini ilikuwa siku hiyo harufu ya bangi mtaa mzima nakumbuka sijui hayo mambo yako mpala leo
Daaaa,kitambo,Namkumbuka jamaa mmoja alikuwa anaitwa kibaka mdudu,alikuwa mcheza mchiriku matata sana,pia marehemu mkama shapu[Afande]alikuwa hakosekani kuangalia usalama watu wasipolwe.....