Tukumbushane muziki aina ya mchiliku au mnanda na vituko vyake enzi hizo upo kwenye chati

Wewe ndo umeuuwa wote wliobakia hata kolokoloni hajui mchiriku hao hisani walikuwa noma kuna rafki yangu mmoja alikuw anaimba hilo kundi walimuua way bck, nakumbuka nymbo yao mola na ali mwny...pia kuna nght star ya kkoo.
Dah umenikumbusha night star na kibao chao

🎼. Jumamosi night,jumapili night,alhamis night ijumaa night

Twendeni leoo tuukacheze night

Wako wapi leo tukawaone night 🎼
 
r.i.p omari omari,wapi topaz
dah,siku hizi vinanda having'uli kabisa
Topaaazzziiii

🎧 nakumbuka siku moja siku sitoisahau mama maishani mwangu naliaaa
Yaliyonikuta huko naliaa

Tulitoswa baharini mimi na rafiki zangu mama ooh naliaa 🎧
 
nakumbuka kulikua na makundi maarufu sana, baadhi ni TOPAZ NA BUTI KUBWA
🎧 mwenye nyumba mwenyewe ni mchapa tembo

anaporudi tooka kilabuniii,wapangaji wanasevu mmoja mwingine

Kumbuka hasaa kitu kimoja,mwenye nyumba mwenyewe ni mchapa tembo

Nikilia tabu mieee nikicheka shida maamaaa 🎤
 
Nakumbuka kuna kundi lilitoka maeneo ya mbezi msakuzi nikakutana nao eneo la makabe nika paki gari pembeni ili kuwapisha, dada moja alisogea kwenye mlango akanengua huku amelegeza macho, mpaka nikaona kizunguzungu
Mkuu hukuanguka?
 
Wakuu,

Nautafuta wimbo ''Narudi Chalinze'' by Eleven Star. Naomba kwa yeyote aliyenao wimbo huo.

-Kaveli-
 
Duh! umenirudisha 1995 enzi za Dar Nyota Theatre kundi la CCM.. na nyimbo kama Ally Mwinyi,Shemeji umeulamba Mkopo wa Sukari, Kurumbizi nk. Wakawepo Hisani na nyimbo kama Uko wapi Mama, kuna kipande wanasema"nipe nipe bwana Chidile..." Kuna Atomiki "Meli Ya sumu", Jagwa na ngoma kama Asha,Eleven Stars watoto wa chalinze makazi Tandale na Album lao Narudi Chalinze. Huu muziki una ujumbe sana. Naamini katika mwanamuziki mmoja au bendi za Tanzania nilizopata kuona wakifanya live shows...hawa jamaa wa Jagwa hawana mpinzani. hebu tazama hii...


Mkuu, unao wimbo ''Narudi Chalinze''? nautafuta sana.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom