The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Tukubali tukatae, ukiona mtu ana tattoo yoyote ujue ni matokeo ya malezi mabaya.
Tattoo ni ishara ya mtu kutokujijali, kutojali afya wala thamani ya mwili wake na pia kutokutumia akili sawasawa.
Ndio maana China kwa ajili ya kulinda kizazi cha sasa na kizazi cha baadae imepiga marufuku ukengeufu na kuzuia watu kutokuchora tattoo. Sio China tu, nchi nyingi sasa zimeshaanza kuona kwamba tattoo ni mwenendo mbaya kwa jamii hivyo kuanza kuzipiga marufuku.
Ukiangalia, huwezi kukuta familia zinazojielewa na zenye heshima katika jamii kama wanasiasa, wafanya biashara wakubwa, wanasayansi, wasomi nk watoto wao ama wao wenyewe wamechora tattoo. Na hata kama ikitokea alichora kwa bahati mbaya akiwa mdogo, lazima utakuta anaificha sana isionekane katika jamii. Sababu ya kufanya hivyo ni moja tu kwamba tattoo ni ishara ya malezi mabaya ama tabia mbaya.
Huku Afrika hasa Tanzania ambako usimamizi wa maadili na mwenendo mwema katika jamii imeachwa kwa mtu binafsi, vijana wengi huona kuchora tattoo ni ufahahari kua kama Messi ama 50 Cents.
Tulinde kizazi chetu cha sasa na cha baade kutoka kwenye uharibifu huu wa Tattoo, tueleze vijana tattoo sio jambo jema na sio ufahari, ni ujinga.