Tukubali mvinyo kwa wachache au maji kwa wengi?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,866
TUKUBALI MVINYO KWA WACHACHE AU MAJI KWA WENGI!?

Leo 14:40hrs 20/08/2022

Wanachama wenzangu wa CCM na wadogo zangu wa Uvccm tukiwa busy kupongeza muda wote kwa kufanya matukio ya hamasa huku mitaani kuna kizazi kilichopevuka kinachohoji mambo ya msingi ambayo sisi hatuyaoni au tunayaletea mzaha lakini yanagusa moja kwa moja wananchi,"well informed and analytical minded generation ipo mtaani" huko mitaani wao hawana muda wa kupongeza bali kupata majibu ya kila changamoto kuhusu na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambayo ndio perfomance appraisal yetu tulipojinadi nayo kwenye uchaguzi wa 2020,

Tukumbuke kila mwaka vijana laki sita wanamaliza vyuo vikuu,na pengine Hayati Rais John Magufuli aliwaamsha zaidi kwa kuwaambia nchi hii ni tajiri,na akawathibitishia kuwa nchi hii kweli ni tajiri,sasa wanapoona ubunifu wa tozo zinazowaumiza halafu waziri mwenye dhamana anawaambia kama hawataki waende burundi.

Hii inawafanya vijana hao kuanza kuwa wanafalsafa na kuhoji hoji kila kitu hadi sasa hata ujugu anaandika toka timu ya singida irudi tozo inapanda sana,wengine wanahoji kwa nini burundi na sio Zambia kwa Rais Haikainde Hichilema au Malawi kwa Rais Lazarus Chakwera!? au kwa nini asiende yeye kwanza uko burundi,naamini hiyo haikuwa kauli nzuri kwa Watanzania.

Ilikuwa ni kawaida ya kila baada ya wiki mbili kutoa mrejesho juu tozo "press", tuliambiwa kila senti itaenda kunakostahili na wakasema kuwa kila baada ya wiki mbili watakuwa wanatupa mrejesho wa mapato na matumizi ya tozo za miamala ya simu,sijui kama inafanyika,kiuchumi tozo kwenye miamala ya simu ilileta athari kwenye mifumo ya fedha ambapo miamala ilipungua kwa zaidi ya 53% lakini pia kulikuwa na upotevu wa ajira kutokana na kufungwa kwa vibanda vya kutolea huduma.

Athari hii itapelekea atahari nyingine kwa mapato ya Serikali kupitia VAT na service charge na hata corporate tax kushuka,kwa haraka haraka tozo kwenye simu zimeleta athari kwenye makampuni ya simu maana watu waliacha kuweka pesa kama walivyozoea,watu walizoea kuweka hadi mamilioni kwenye simu zao baada ya kuona tozo,watu wakakimbilia benki lakini hivi leo imewekwa tena tozo kwenye miamala ya benki,je nini tutarajie!?

Wananchi wameamua kunyamaza kuhusu hizi tozo maana hata waseme vipi self evaluation kwa wengi hamna na hata wakiwa nayo wanaambiwa waende burundi,watu wanasema heri bunge liongekuwa na wabunge wapinzani.

Wabunge wa upinzani ndani ya bunge walikua namchango mkubwa sana kwa Taifa leo hawapo tena tuendelee kuunga juhudi hata kama tunaumia hakuna namna,lakini mimi niseme maoni yangu,kuwepo kwa wabunge wengi na niseme karibia wote toka CCM ingeweza kuwa afya kwetu kama chama kingejikita katika kusimamia na kuwatetea wananchi.

Hayati Rais Magufuli aliweza kuongea lugha moja na wananchi,walipopata shida hakuwaambia waende burundi,alisimamisha msafara na kutatua tatizo lao hapo hapo na kujizolea imani kubwa toka kwa wananchi,kwa namna hiyo CCM ingeweza kushika dola kwa miaka mingi zaidi kama bunge lingesimama kutetea wananchi.

Lakini kwa wabunge kusemekana kupitisha hizi tozo zote na kuwa kimya na kushindwa kupaza sauti ni kujitoa kwenye uhakika wa kutawala dola kwa muda mrefu mfano ni hili la tozo palitakiwa pawe na pande mbili ndani ya bunge lakini wengine waligusiagusia tuu tena kwa hofu yakuwa pwekee mfano mbunge mmoja tu ndio alisemea madhara ya tozo katika kukua kwa uchumi unaotegemea watu wa kipato kidogo kidogo.

Niwakumbushe wanachama wenzangu wa CCM,Makada na makomredi tukitaka tusifanye kampeni 2025 basi tufanye Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi husika,tusianze biashara ya kuwakubali viongozi binafsi badala ya kukubali Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM chini yao,tumezoea Viongozi wa kitaifa kuwambia Viongozi wa Chama na Serikali kuwa kumtukuza,kumsifia na kumpongeza na kumpamba Mwenyekiti hata kama hakuna chochote kinachofanyika ni moja ya "Key performance indicators ya wateuliwa kwa Mteuzi ndio maana kwenye hotuba za viongozi mbalimbali katika dakika tano wanazopewa dakika nne wanatumia kwa ajili ya mteuzi dakika moja kwa ajili ya kuomba miradi wakati huo huo CCM yenye Ilani yake ya Uchaguzi iliyo kwenye utekelezaji haitajwi popote.

Hata Viongozi wote wa Chama na Serikali kila wakiongea wanamtukuza tu mteuzi yaani wanatumia muda mwingi kumtukuza kiongozi tu hata pasipostahili,utasikia tu namshukuru sana Mwenyekiti kwa kuupiga mwingi, namshukuru sana Mwenyekiti kwa baridi sasa hivi makambako, njombe ni kama Urusi.

Ndugu zangu tulipiga sana kampeni kali kuelimisha juu ya umuhimu wa tozo ya miamala kuwa ingejenga miundombinu mbalimbali nchini ili kuboresha huduma kwa wananchi, baada ya wananchi kupiga kelele juu ya utitiri wa kodi au tozo mbalimbali jambo lililofanya serikali kujitokeza na kutolea ufafanuzi juu ya tija itakayopatikana kwenye tozo hizo.

Am very open to the idea, binafsi nimepunguza miamala kupitia simu maana duu inauma bana,juzi kati nilituma hela kwa ndugu yangu kijijini na kama kawa ikakatwa(tozo) akaniuliza serikali inaonea watu imekata hela nyingi vipi kwa wagonjwa wanaotumiwa ili wakatibiwe? nikamjibu serikali inakusanya hela hizo ili zijenge nchi, akaniuliza mbona hatusikii taarifa za tozo kama ile kampeni?Ndugu zangu viongozi mliopewa dhamana hatuihitaji hadi msimu wa bunge ndio utoe taarifa za tozo bungeni.

Toeni taarifa za mapato kila mwezi through mass media na tujue zimetumika wapi na wapi hivyo ndio kujenga nchi na imani kwa wananchi kwa yale mnayoyasema,tozo zinauma bana lakini tukijua zimeenda wapi kufanya nini angalau machungu yanapungua.

Wakati wa Hayati Rais Magufuli watu walikatwa kodi kubwa lakini walivyojua inaenda kujenga madaraja,kununua ndege,kujenga rada katika viwanja vya ndege,kujenga stand kila mkoa na wilaya, kujenga masoko kila mkoa na wilaya,kukarabati shule kongwe zote nchini watu walikubali na kuridhia kodi ziendelee,nashauri tutoe taarifa ili wananchi wajue,Je, hili nalo linamwitaji Rais ndio afanye?

Wasaidizi wa Rais mpo wapi katika hili? Fedha inaweza ikajenga au ikabomoa uongozi bora.

Nimalize kwa tafakari jadidi kuhusu rasilimali zetu ambazo tungezitumia vyema basi kusingekuwa na ulazima wa hizi tozo,niseme tu "hakuna manufactured and finished goods za Tanzania zinazokwenda Kenya wala China"tunazo rasilimali nyingi sana lakini Tanzania badala ya kuzalisha na kuuza nje,tumekuwa shamba la "rasilimali madini malighafi" za mashambani mifugo hai kama ng'ombe mbuzi kondoo.

Kwa ufupi mfano jirani zetu Wakenya wanapata kila kitu kutoka Tanzania wanachofanya ni kufanya kufanya processing kwenye viwanda vyao, packaging kisha wanaandika "Made in Kenya" na kuuza kokote duniani,Hivyo Tanzania haiwezi kuwa kwenye Top 10 list sababu ipo wazi kokote kuwa sisi ni Watizedi kama wanavyotuita ni shamba la bibi la Kenya.

Ukiona magari yanapeleka bidhaa Kenya ni mazao na Malighafi kwa ajili ya viwanda vyao,Hakuna Manufactured and Finished Products za Tanzania zinazoenda Kenya,

Wakenya hasa Vijana wamejaa hadi Ubaruku Mbarali , Namanyere Rukwa walifanya Business and Economy Intelligence, Watanzania tuko busy na Iyena Iyena hamasa na kusifia Viongozi wa kisiasa,tusiwe shamba la Wakenya, Warwanda, Wachina, Waarab, Wazungu kwa mazao,madini mifugo na malighafi mbalimbali kwa ajili ya viwanda vyao halafu warudi tena watufanye soko lao la kuuza bidhaa kutoka viwandani kwao wakati malighafi wametoa huku huku Tanzania bara.

Exportation ya Kenya inategemea zaidi malighafi kutoka Tanzania bara hivyo Uongozi wowote imara upande wa Tanzania bara lazima kunakuwa na uadui mkubwa na Wakenya,Pia the most productive flight route ya Kenya Airways ni za kuja Tanzania hasa Dar es Salaam na Kilimanjaro ndizo zinaifanya JKIA kuwa busiest aviation HUB ya East Africa hivyo kuanzishwa upya kwa ATCL ni Business threat kwao na wako radhi ndege zote za Watanzania zife ziuzwe au zitaifishwe ili kulinda biashara ya ndege zao.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam,
0755078854


-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Mimi naamini tunaelekea sasa kwenye nchi ya ahadi. Kuna siku tutaongea tu lugha moja kama Taifa. Maana haya mateso ya tozo yatawaamsha wengi waliolala.

Enzi zile watumishi wa umma ndiyo walikuwa nivtarget namba 1 ya unynyasaji! Sasa wamehamia mpaka kwa wale wenzangu na mimi waliounga mkono kila aina ya ujinga!
 
Back
Top Bottom