Tuko serious Lowassa awe Rais?

Tuko serious Lowassa awe Rais?

Wakuu, Natumaini wote ni wazima wa afya.

Sasa twende kwenye mada. Ndugu yetu Lowassa ni mbunge kwa miaka 25 katika jimbo la Monduli. Na amekuwa akinadiwa kama mchapa kazi na mwenye maamuzi magumu.

Lakini ustawi wa maendeleo katika jimbo la Monduli ni tofauti na kile tunachoambiwa.

Lakini tafiti za UNDP, zinabainisha illiteracy rate au wanaojua kusoma ni wachache mno, ajira ni tatizo kubwa sana monduli... Vijana wengi wamekimbilia Arusha, Namanga, Nairobi, DSM na Zanzibar kama walinzi, wasusi, na wauza shanga.

Hii ni aibu kubwa iliyofunikwa na fedha isionekane, michango kwenye taflija mbali mbali nayo imekuwa kama kisafishio cha aibu hii. Jaribu kufananisha kazi anayo fanya Deo Firikunjombe Ludewa ndani ya muda mchache na kazi ya Lowassa monduli ndani ya miaka 25.

Kinachoonekana kwa jicho la pili ni maandalizi ya muda mrefu ya kutaka urais kwa gharama zozote ikiwa ni pamoja na kuupumbaza umma kwa techniques mbali mbali.

Namaliza kwa kusema, zile milioni Mia 200 anazotoa Lowassa kwenye taflija mbali mbali, zingeweza kutengeneza ajira za wamasai wanao suka dada zetu pale mwenge, Ubungo etc.

Tajiri siku zote hushughulika na matajiri wenzake.
Hivi sio serikali ya CCM iliyowafukuza wamasai kwao eti ili royal family ya Dubai ipate sehemu ya kuwindia wanyama? Mpaka international media ikaingilia kati.... Nakwambia mwaka huu CCMout!
 
viongozi wote wako hivyo, nenda hata butiama kwa mwalimu ujionee, kwa MKAPA ndio kabisaa kumearibika hata kijiji chao utaamini kama alitoka kule. kwa magufuri je, watu karibu wanakufa kwa kipindupindu kwa kukosa maji safi na salama.
 
Ukawa sawa ikulu,lakini sioni seriousness ya hilo ki 'vision' .jipangeni kwanza msije mkatuletea balaa la uarabuni
Hatutoi nchi na kumuweka amiri jeshi mkuu aliezungukwa na kindi liso dira
 
Kiswahili kibovu rais wako mwenyewe unayemtaka ana kiswahili kibovu balaa,bora huyu ni zile za l na R

Sio rais ninaye mtaka, ni yRais ambaye watanzania wanamtaka. Pia Hana kiSwahili kibovu sanasana ana kiswanglish tu. Pia kushindwa kujua mahali pa kuandika L na R ni tatizo sana. Usijidanganye wala kujipa moyo. Kosea kingereza na sio kiswahili. Kuongea ushindwe na kuandika nako ushinde ulisoma shule gani?
 
Wadau mimi kama mpenda mabadiliko na maendeleo ya nchi yetu nimesikitishwa sana na jinsi mgombea uraisi kwa tiketi ya UKAWA bwana EDWARD LOWASA alivyo tu-disappoint asilimia kubwa ya watanzania wapenda mabadiliko kwa kutuletea hotoba ambayo naiona kama ya kututania watanzania

Naamini watanzania wengi walikuwa na uchu wakutaka kumsikia mheshimiwa mgombea uraisi akitema cheche zenye maana na zakuleta matumaini,lakini badala yake alitoa HOTUBA ambayo hata mtoto wa darasa la 7 anaweza kumshinda,Kwa style kama hii LOWASA ninaweza kumfananisha na MWANAUME anayependwa na WASICHANA WAZURI lakini HAJUI KUTONGOZA hivyo kuishia kuwavunja moyo na mwisho wa siku hukimbia.

Pia kitendo cha kamanda MBOWE (a.k.a DJ) kumtoa Dr SLAA nakumleta huyu jamaa kutoka CCM tena baada ya KUKATWA kitaendelea kuitesa sana CHADEMA na sidhani kwa style kama hii huyu jamaa mheshimiwa kutuongoza kuelekea kwenye MABADILIKO YA KWELI

Mwisho ningeshauri viongozi wa CHADEMA waongee na Dr SLAA aokoe jahazi maana hali ya CHADEMA na UKAWA sio ya kutia matumaini kabisa.

#TANZANIAKWANZA

Ahsanteni sana
 
Kwanza tunakushukuru kwa kutambua lowassa ni rais.... Hapo kweli dozi inaanza kuingia taratibu. waambie na wenzako eeeee!!!!
 
CCM na usanii wake imefika mwisho.hatuitaki.mkulima anayekula mbegu hafai na ni zezeta wa kufa.
 
Back
Top Bottom