Tuko serious Lowassa awe Rais?

Tuko serious Lowassa awe Rais?

mkuu hawawezi kukuelewa hata kidogo.
Sijui ni nan katuloga watanzania mpaka kuwa wapumbavu kiasi hiki.

Wanadanganywa eti anauchukia umaskin ndio anauchukia kwa familia yake lakn sio kwa watz.

wewe ndo umerogwa ukawa tuko fit
 
Wakuu, Natumaini wote ni wazima wa afya.

Sasa twende kwenye mada. Ndugu yetu Lowassa ni mbunge kwa miaka 25 katika jimbo la Monduli. Na amekuwa akinadiwa kama mchapa kazi na mwenye maamuzi magumu.

Lakini ustawi wa maendeleo katika jimbo la Monduli ni tofauti na kile tunachoambiwa.

Lakini tafiti za UNDP, zinabainisha illiteracy rate au wanaojua kusoma ni wachache mno, ajira ni tatizo kubwa sana monduli... Vijana wengi wamekimbilia Arusha, Namanga, Nairobi, DSM na Zanzibar kama walinzi, wasusi, na wauza shanga.

Hii ni aibu kubwa iliyofunikwa na fedha isionekane, michango kwenye taflija mbali mbali nayo imekuwa kama kisafishio cha aibu hii. Jaribu kufananisha kazi anayo fanya Deo Firikunjombe Ludewa ndani ya muda mchache na kazi ya Lowassa monduli ndani ya miaka 25.

Kinachoonekana kwa jicho la pili ni maandalizi ya muda mrefu ya kutaka urais kwa gharama zozote ikiwa ni pamoja na kuupumbaza umma kwa techniques mbali mbali.

Namaliza kwa kusema, zile milioni Mia 200 anazotoa Lowassa kwenye taflija mbali mbali, zingeweza kutengeneza ajira za wamasai wanao suka dada zetu pale mwenge, Ubungo etc.

Tajiri siku zote hushughulika na matajiri wenzake.

Kaka watu kama wewe ndio taifa linawahitaji. Hongera sana kwa kuona hili na kulielezea hapa. Najua utatukanwa na wanywa viroba lakini message umeshaitoa. Nimesema huko nyuma kwa wenye macho waone, ila taifa letu limekuwa ovyo sana. Ukitaka kuona angalia majibu watakayo toa kuhusu post yako. Halafu si tu Monduli. Hivi Lowasa kafanya nini hasa katika hii nchi..tuwe wakweli. Kasimamia kitu gani na kikafanikiwa mpaka mwisho?
 
Mkuu kiukwel kabisa unaweza sema magufuli msafi ili hali ya kuwa watu washaleta madudu yake hapa jukwaan! (mfano tu yaan wewe mtu kasigina taratibu za kuuza nyumba za serikali, tena kamuuzia ndugu yake ambaye hakuwa hata mwajiriwa by then! ) any way kuwa neutral na kusimamia ukweli pale inapotatikana ni issue sana wanadamu walio wengi! wengi wao mahaba niue huchukua nafasi na ni human nature kwa mtu kuwa na wivu na kile anachokiamini!

Nafikiri neno "ana unafuu" labda linamfaa!

Nimeipata hoja yako. Ni kweli kabisa Magufuli ana upungufu wake kama mgombea yeyote yule. Hatuwezi kupata mgombea malaika.

Labda ni suala la lugha au maneno muafaka ya kutumia. Kati yake na Lowassa, ana nafuu, au afadhali au ni bora. Ni Lugha tu. Huyo mwingine upungufu wake umezidi kipimo kwa vigezo vyovyote vile.
 
Saana tu, nikiona mijitu yenye kichwa yanathubutu kuishabikia ccm. Umezaliwa wapi weye?? Mgombea urais mwenyewe anashangaa inakuwaje mtu aende hospitali mgonjwa, apimwe na Dr. halafu ashauriwe kwenda kununua dawa duka la mtu binafsi. Miaka 54+ baada ya uhuru. Wewe huumwi???? Basi weye ni kichaaaaa
 
Kwa mamlaka aliyonayo rais (kikatiba) bora rais safi kwenye chama kichafu maana ana uwezo wa kufurukuta na kuwanyoosha....nchi hii inataka rais aliye na political will baas...waliopita sidhani kama walishindwa...hawakuwa nayo...nina imani kubwa sana na Magufuli...hata ukimtizama usoni....unaona kabisa jamaa ni mkweli...

Nasubiri kwa hamu kusikiliza vipaumbele vya Lowassa akiwa Rais.

Labda kesho (29/08/2015) atasema wakati anazindua kampeni. Hivi UKAWA wana ilani ya uchaguzi? Ilani inayoweza kubeba zile za CDM, CUF, NCCR and NLD ya Makaidi.

Hadi wakati huu (28/08/2015 - 13:51 PM) sijaelewa nini sera ya Lowassa. Akisema anachukia umaskini watu wanashangalia lakini hajasema umaskini wa nani. Wa kwake na ndugu zake au umaskini wa watanzania wote? Miaka yote ndani ya serikali kafanya nini kupambana na umaskini huo nchini na jimboni kwake?

Nikisema hayo simaanishi CCM ndio malaika.

Uchaguzi wa mwaka huu Taznzania ipo njia panda. Chama sahihi (CDM/UKAWA) wana mgombea asiyefaa. Mgombea sahihi (Magufuli) yupo chama kisichofaa. Najiuliza kipi bora? Mgombea safi kwenye chama kichafu au Mgombea mchafu kwenye chama safi?
 
Wakuu, Natumaini wote ni wazima wa afya.

Sasa twende kwenye mada. Ndugu yetu Lowassa ni mbunge kwa miaka 25 katika jimbo la Monduli. Na amekuwa akinadiwa kama mchapa kazi na mwenye maamuzi magumu.

Lakini ustawi wa maendeleo katika jimbo la Monduli ni tofauti na kile tunachoambiwa.

Lakini tafiti za UNDP, zinabainisha illiteracy rate au wanaojua kusoma ni wachache mno, ajira ni tatizo kubwa sana monduli... Vijana wengi wamekimbilia Arusha, Namanga, Nairobi, DSM na Zanzibar kama walinzi, wasusi, na wauza shanga.

Hii ni aibu kubwa iliyofunikwa na fedha isionekane, michango kwenye taflija mbali mbali nayo imekuwa kama kisafishio cha aibu hii. Jaribu kufananisha kazi anayo fanya Deo Firikunjombe Ludewa ndani ya muda mchache na kazi ya Lowassa monduli ndani ya miaka 25.

Kinachoonekana kwa jicho la pili ni maandalizi ya muda mrefu ya kutaka urais kwa gharama zozote ikiwa ni pamoja na kuupumbaza umma kwa techniques mbali mbali.

Namaliza kwa kusema, zile milioni Mia 200 anazotoa Lowassa kwenye taflija mbali mbali, zingeweza kutengeneza ajira za wamasai wanao suka dada zetu pale mwenge, Ubungo etc.

Tajiri siku zote hushughulika na matajiri wenzake.

embu compare mondoli na wilaya zingine
 
Bwana nani anakudanganya lowasa kuchukua nchi hii,hizo ni ndoto,nsye analijua hilo kakabwa koo hana ujanja[/QUOTE

kwa sababu we rais wa maboya wa fb unadhan kila mtu anaota kama wewe
 
Kweli wamesema; Nyani haoni kundule. Weye unashangaa Monduli kutokuwa na maendeleo, unalinganisha Deo na muda wake mfupi aliokaa bungeni.
Mbona hulinganishi Riziwan na Babake?? Jimbo laa Riz si alikaa babake miaka na hakuleta maendeleo yeyote? Mbona Riz kabla hata ya kuingia mjengoni aliahidi kununua trekta kwa kila kijiji?? Mbona mnakuwa mazuzu? Vijiji hivyo vingelikuwa na trekta angewanunulia nyingine?? Miaka yoote babake amekuwa waziri na sasa ni rais mbona hakupeleka maendeleo huko??
ujinga si lazima ukausomee, Shule ile tulioneshwa kwenye luninga, shule ya msingi, ati juu imeezekwa nyasi, ni wapi ka si jimboni mwake, LETENI HOJA wala si vioja hapa. Ukitaka mapinduzi kamili, mchague Lowasa awe rais wako. Atakuletea maendeleo. Na Chama pekee cha ukombozi kipo UKAWA

WEWE CHAGUA KUNDI LA CHENGE sisi TUNACHAGUA kundi la TINDU LISSU
 
nakumbuka picha iliyoonywesha na kituo cha star tv kuhusu shule ya monduli shule imechoka halafu walikuwa wanaomba msaada huku mbunge wao aliyekuwa akisikika kutoa msaada hakufanya chochote huyu ni msanii hana mpango na maskini ila wezi na matajiri wenzake
 
Magufuli tumeshasikiliza Sera zake ambazo ni zile zile, amekazana kusema anaashangaa tumefikaje hapa kila kitu anashangaa unajiuliza kwani alikua nchi gani? Kesho njooni mmsikilize Sera zake kabla ya kuonga hapa kua hana Sera, pia sidhani kama kuna ukweli wowote kua monduli hakuna maendeleo, au mlitaka awalazimishe wasivae mashuka? Tafuteni hoja za msingi
 
Nasubiri kwa hamu kusikiliza vipaumbele vya Lowassa akiwa Rais.

Labda kesho (29/08/2015) atasema wakati anazindua kampeni. Hivi UKAWA wana ilani ya uchaguzi? Ilani inayoweza kubeba zile za CDM, CUF, NCCR and NLD ya Makaidi.

Hadi wakati huu (28/08/2015 - 13:51 PM) sijaelewa nini sera ya Lowassa. Akisema anachukia umaskini watu wanashangalia lakini hajasema umaskini wa nani. Wa kwake na ndugu zake au umaskini wa watanzania wote? Miaka yote ndani ya serikali kafanya nini kupambana na umaskini huo nchini na jimboni kwake?

Nikisema hayo simaanishi CCM ndio malaika.

Uchaguzi wa mwaka huu Taznzania ipo njia panda. Chama sahihi (CDM/UKAWA) wana mgombea asiyefaa. Mgombea sahihi (Magufuli) yupo chama kisichofaa. Najiuliza kipi bora? Mgombea safi kwenye chama kichafu au Mgombea mchafu kwenye chama safi?
Mkuu sibonike, hapo kwenye red tunahitaji elimu ya kutosha kuhusu uchaguzi wa mwaka huu. Maana hata mimi nimeungana na Dr. Slaa kupumzika, ila nimepoteza dira ya kura yangu niipeleke wapi? JF ebu wekeni hoja hapa ili nifanye maamuzi sahahi.
 
Kipi ni rahisi kusahihisha? Mgombea safi kwenye chama kichafu au chama kisafi chenye mgombea mchafu?

Kwa lugha nyingine, kipi ni rahisi zaidi - chama kisafi kumuweka sawa mgombea wao mchafu wakishinda uchaguzi au mgombea safi kuwaweka sawa watu wa chama chake akipata uongozi?

Kwa kutumia maneno ya Nape - kipi nafuu? Kuweka Oil safi kwenye gari chakavu au kuweka Oil chafu kwenye gari mpya?

Nahisi kila mtu atakuwa na jibu lake hapa.
 
kwanza kabisa una kiswahli kibovu kama cha mwanafunzi wa darasa la 3, SIO TAFLIJA NI TAFRIJA. Michango katika tafrija ni jambo la kawaida sana.
pili Mbunge anasimamia Sera na Ahadi alizowaahidi wananchi wake, hicho ndicho cha kumhoji na ikiwezekana kumwajiabisha nacho, Mila na tamaduni za watu wa Monduli vinahusika sana hapa. WAADZABE walichinjiwa Punda na serikali ili wakubali shule.
Tatu wewe sio Mkazi wa Monduli hujui katika sera zake aliwaahidi kitu gani na kitu gani hajatekeleza kama mbunge wao..

Mwishokitendo cha kumsaidia mtu kwa kumpa Pesa haimaanishi familia YAKO imejitosheleza sana, Uzoefu unaonyesha viongozi wenye nyadhifa wa CCM huwa hawapaswi kua wana upendeleo kwenye majimbo yao tu, wanapaswa kuitumikia nchi yote kwa ujumla.
Bila kusahahu ukweli kua CCM ime tafuna mabilioni ya shilingi bila hata kutoa msaada popote, mfano mmoja wapo ni bilioni 200 kwenye katiba mbovu iliyokwama, TANESCROW,EPA etc. How about that huh?
TUKO SERIOUS

Kiswahili kibovu rais wako mwenyewe unayemtaka ana kiswahili kibovu balaa,bora huyu ni zile za l na R
 
Magufuli ni Rais wa awamu ya tano tumwamini ataweza kukutumikia vema watanzania kunyoosha mafisadi.

Anyooshe mafisadi wakati yeye mwenyewa BONGE LA FISADI . Kumbuka 10 percent ya kwenye mabarabara yanayoharibika ndani ya mwaka, majengo ya umma, kumbuka hesabu za CAG
 
Wakuu, Natumaini wote ni wazima wa afya.

Sasa twende kwenye mada. Ndugu yetu Lowassa ni mbunge kwa miaka 25 katika jimbo la Monduli. Na amekuwa akinadiwa kama mchapa kazi na mwenye maamuzi magumu.

Lakini ustawi wa maendeleo katika jimbo la Monduli ni tofauti na kile tunachoambiwa.

Lakini tafiti za UNDP, zinabainisha illiteracy rate au wanaojua kusoma ni wachache mno, ajira ni tatizo kubwa sana monduli... Vijana wengi wamekimbilia Arusha, Namanga, Nairobi, DSM na Zanzibar kama walinzi, wasusi, na wauza shanga.

Hii ni aibu kubwa iliyofunikwa na fedha isionekane, michango kwenye taflija mbali mbali nayo imekuwa kama kisafishio cha aibu hii. Jaribu kufananisha kazi anayo fanya Deo Firikunjombe Ludewa ndani ya muda mchache na kazi ya Lowassa monduli ndani ya miaka 25.

Kinachoonekana kwa jicho la pili ni maandalizi ya muda mrefu ya kutaka urais kwa gharama zozote ikiwa ni pamoja na kuupumbaza umma kwa techniques mbali mbali.

Namaliza kwa kusema, zile milioni Mia 200 anazotoa Lowassa kwenye taflija mbali mbali, zingeweza kutengeneza ajira za wamasai wanao suka dada zetu pale mwenge, Ubungo etc.

Tajiri siku zote hushughulika na matajiri wenzake.

tupo serious ccm kuendelea kututawala?
 
Back
Top Bottom