Tukitaka kodi ya SIMcard ifutwe tufanye hivi

Tukitaka kodi ya SIMcard ifutwe tufanye hivi

nimeupenda msimamo wako. Hakika wewe ni mwanamapinduzi halisi, mwanaharakati mwenye ufahamu mkubwa. Yaani point mwanzo hadi mwisho. Nimeshatoa pendekezo, mgomo ufanyike siku 30 baada ya tarehe 20 julai, ambazo zitatosha kujipanga vizuri. Tuwapuuze hao mandumilakuwili ambao wameshatumwa kuja kutukatisha tamaa. Kazi ifanyike. Anza kuwaambia wenzako. Siku 30 baada ya 20 julai zitaangukia tarehe 19 agosti, kuanzia saa 6 usiku wa siku hiyo, na kwa muda wa saa 24, mgomo utaisha saa 6 usiku ya 20 agosti 2013.

Tunaweza!

'that's great...'
 
naunga mkono hoja,organizer wanahitajika ili our enemy awe hurt ipasavyo
 
hii inawezekana kwenye homogeneous society lakini kwa jinsi jamii yetu ya kitanzania ilivyo itakua ngumu sana kuwashawishi watu...ili tukigoma ata sisi wachache ambao tumeelewa nia na madhumuni tunaweza kuwatia hasara ya kutosha sana tu cha muhimu ni ushirikiano....nawasilisha
 
ifike mda nasi wananchi tuwe na sauti, tuanze kulisemea hili.kumbuka katika msafara wa mamba kenge wamo hivyo tusihofie negativities zinazoletwa na wapuuzi wachache.
 
Plan ni nzuri.Binafsi napendekeza wiki moja kabla ya mgomo,tufahamishane kwa sms kwamba 'tarehe flan watanzania woote tunaotumia simu,tuungane kwa pamoja kuzima simu zetu kwa muda wa masaa 48,ili kuishnikiza serikali kuondoa kodi ya sh.1000 kwa kila mwezi.serikali isipotoa majibu ya uhakika basi tuzime simu zetu kwa masaa mengne 48'sambaza ujumbe huu kwa watu zaid ya 15.
Kwanza naona tuna chelewa,harakati hiz zianzie hapahapa kila atakae soma hii thread amjulishe na rfk ake mwenye access ya jf.Na pia ujmbe uanze kusambazwa kuanzia leo usomeke kama huo hapo juu/chn
...'Ndg Mtanzania hasa ww unaetumia simu.Tuungane ktk mgomo wa kuishnikiza serikali kuondoa kodi ya sh.1000 kwa kila line kwa kila mwezi,Mgomo utaanza trh 19 mwezi huu.unachotakiwa kufanya ni kuzima simu yako/zako.mpaka pale tutakapopata jibu la kueleweka kutoka serikalini,na kama hatutapata muafaka tutaendelea na mgomo kwa masaa mengne 60'
Sambaza ujumbe huu kwa waumiaji wa simu zaidi ya 15.

'MKUU MDA UTAKUWA MCHACHE SANA HIVYO TUTASHINDWA KUPATA HALAIKI,MI NADHANI TUFANYE KAMA ALIVYOPENDEKEZA MwanaHaki KUWA SIKU 30 BAADA YA TWENTIETH OF JULY AMBAYO ITAKUWA NI 19 AUGUST MDA UTAKUWA WA KUTOSHA KUWEZA KUPATA WATU WENGI KIASI,NICE'
 
Last edited by a moderator:
naunga mkono hoja,organizer wanahitajika ili our enemy awe hurt ipasavyo

Wewe mwenyewe waweza kuwa organizer. Huu ni mpango wa Watanzania. Hakuna chama wala kikundi wala kamati. Huko ni kupoteza muda. Hapa ni kupashana tu habari. Wewe waarifu wengine, kuhusu huu mgomo... siku 30 baada ya tarehe 20 Julai, ambapo mgomo utaangukia saa 6 usiku, 19 Agosti hadi saa 6 usiku, 20 Agosti 2013, muda wa saa 24, kwa awamu ya kwanza.

Haya, anza sasa kuwapasha habari wenzako, nao wawapashe habari wengine. Tuma ujumbe kwa kila umjuaye. Kuna nduli hapa wanasema sisi walalahoi hatutaziathiri hizi kampuni kwani kwa suala la mapato yao, makampuni makubwa na watendaji serikalini wanalipia asilimia 80 ya mapato yao, na sisi tunalipia asilimia 20. Kwani haiwezekani kati ya hao watendaji wa hizo kampuni nao kuwa wamezichoka hizi kampuni na wizi wao, nao wakaamua kuingia kwenye mgomo?

Haya, tuone basi hiyo 20% itakavyoshindwa kufikisha ujumbe.

Hahahahahaha!
 
Bila kuwa na viongozi wa kulisema hili wazi kwenye media mgomo huu hautafanikiwa...Naomba Mh Mnyika aje atoe ufafanuzi wa jambo hili jema kwa mstakabali wa wanyonge
 
hii inawezekana kwenye homogeneous society lakini kwa jinsi jamii yetu ya kitanzania ilivyo itakua ngumu sana kuwashawishi watu...ili tukigoma ata sisi wachache ambao tumeelewa nia na madhumuni tunaweza kuwatia hasara ya kutosha sana tu cha muhimu ni ushirikiano....nawasilisha
ngararumo mbona una mawazo finyu namna hiyo? Hebu achana na hizo dhana zilizopitwa na wakati za homogeneous society. Wakati wa ukombozi umewadia kaka. Tumeshanyonywa vya kutosha ndugu! Usikate tamaa, hujachelewa.

Mungu yu nasi. Hii ni vita takatifu. Ina baraka zake zote. Hebu jiulize: Kuna jambo ambalo Mungu anashindwa kulifanya? Atatusimamia, tutafanikiwa. Tuwatie hasara wezi hawa!
 
Last edited by a moderator:
Bila kuwa na viongozi wa kulisema hili wazi kwenye media mgomo huu hautafanikiwa...Naomba Mh Mnyika aje atoe ufafanuzi wa jambo hili jema kwa mstakabali wa wanyonge

Duh! Nakushangaa Kite Munganga! Unadhani kwamba wanasiasa ndio wenye muarobaini wa matatizo yetu? Hili jambo mbona liko wazi? Ni la Watanzania wenyewe na halihitaji kiongozi, kamati ya uongozi WALA chama cha siasa kulisemea.

Mnyika ana ajenda zake za kisiasa. Yeye anakusanya saini kwenye petition yake, kana kwamba jambo hilo litazaa matunda yoyote yale. Hebu fikiria, hata akiwa na saini milioni 20, effectiveness yake itakuwaje? Fikiria kama watu hao milioni 20 wangezima simu zao kwa muda wa saa 24, hasara ambayo wataipata hawa wenye mitandao ya simu, itakuwa kubwa kiasi gani?

Tunataka kuwatia hasara. Kuwanyima mapato. Kuwapiga pale ambapo itauma zaidi, washike adabu!

Kama Mnyika angekuwa na mawazo ya kiharakati, si angekuja na wazo hili?

Hakuna kamati wala kiongozi. Kamati sisi wenyewe. Kwani unadhani watu wa media bado hawajalipata suala hili? JF ni zaidi ya media zote unazozifikiria. Waandishi huanzia kusoma tunachoandika humu ndani kisha kuyapeleka huko waliko. Hili tayari. Timiza wajibu wako. Anza kuwapasha wenzako.
 
Baaaaaaaaasi!!!!
Tarehe iliyopangwana MwanaHaki iwe hiyohiyo.
Julai 20 mpaka 19 agost.kwa masaa 24.
Mungu Ibariki Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
Baaaaaaaaasi!!!!
Tarehe iliyopangwana MwanaHaki iwe hiyohiyo.
Julai 20 mpaka 19 agost.kwa masaa 24.
Mungu Ibariki Tanganyika.

Kaka bado unapotosha. Tarehe ni saa 6 usiku, 19 Agosti hadi saa 6 usiku, 20 Agosti 2013!

Mbona mgumu kuelewa? Au una makusudi wewe?
 
I support the move. Tutaarifiane siku ya kufanya hivyo. hata hivyo ningeshauri vyama vya siasa viingilie kati suala hili. CDM my political party, tafadhari engineer mpango huu ili huwe na ufanisi. Watanzania wanaagamizwa na hawa mabeberu!!
Tukiingiza siasa /kushirikisha vyama vya siasa tutasalitiana mapema. usifikiri wapenda mabadiliko wote tuna iunga mkono CDM binafsi CDM siitaki hata kuisikia ndani ya ngoma ya masikio yangu lakini ni muumini mkubwa wa harakati za kubigania maslahi yangu na wengine ndio maana nikohapa kuunga mkono huu mpango, kwahiyo ukini letea habari za CDM sijui CCM sinta kuelewa zaidi nitakuona unani letea siasa tu. Nashauri vyama vya siasa tusivipe nafasi maana hatutakua wamoja na hatuta shinda vita hii.
 
mbinu nzuri sana, inafaa ifanywe kwa siku maalumu kwa nchi nzima
watu wakubaliane lini, tuandae vipeperushi na matangazo yatolewe kwa nchi nzima
watu watumiane msg za simu, twitter, whattsApp, viber,tangoo nk.
inawezekana kabisa, kwa hili itakuwa fundisho.
 
Bila kuwa na viongozi wa kulisema hili wazi kwenye media mgomo huu hautafanikiwa...Naomba Mh Mnyika aje atoe ufafanuzi wa jambo hili jema kwa mstakabali wa wanyonge
Hizo siasa ndizo zitakazo otesha mbawa mpango huu. kwanini awe Mnyika nasii Nchemba au Kafulila? tusiingize itikadi ktk mpango wetu huu. Minaona/naamini sisi wenyewe raia wa kawaida tunaweza na tutashinda hii vita. Ila hatuta wakataa wanasiasa watakao amua kutuunga mkono ktk hili kwani nawao niwatu pia wanaumizwa na hili lakini sio kukurupuka na kuanza kuwaomba watusaidie huo ni ujinga na kuto jikubali.
 
Mnachekesha kweli nyie.

Mnaijua 80-20 rule?

Kwa taarifa yenu mapato ya kampuni za simu kama Zantel, Airtel na Voda 80% ni kutoka kwa Corporate clients wao na sie wengine akila baba Zabosi ndio tunachangia hiyo 20% sasa hata tukizima sisi simu sitegemei kama mabenki yatazima simu zao, au ofisi za serikali watazima simu zao, wabunge watazima simu zao, makampuni makubwa yatazima simu zao. Na mtu yeyote mwenye shughuli za kumpatia kipato lazima anahitaji mawasiliano hawezi kusima simu yake hata kwa dakika 30.

Sana sana huo mgomo wenu utawaumiza wakina mangi wanauza vocha na kutoa huduma za Tigo/M-pesa

Hofu yako tu!!
 
Njia ya kwanza nimeipenda sana kwani itawagusa moja kwa moja na ni lazima tu tutasikia mayowe yao ya maumivu muda si mrefu pindi tutakapoamua kuitumia mbinu hiyo. Mimi nipo tayari kuizima simu yangu kwa muda wowote ambao tutakubaliana kufanya hivyo. Naunga mkono hoja kwa asilimia zote.
 
Wakuu,

Naona tunatumia muda mwingi kusign hizi petition ambazo hazina athari zinazotakiwa. Nilipokuwa masomoni Marekani, nilifundishwa mbinu moja nzuri ya uanaharakati, lakini nawamegeeni hizi mbili, muweze kuzitumia kufanikisha lengo kuu.


Hit your enemy where it hurts the most: his pockets!

Tafsiri yake ni kwamba "Mpige adui yako mahali ambapo ataumia zaidi: kwenye mifuko yake." Tafsiri fupi ni kwamba, kama ana mapato, tafuta njia ya kumnyima mapato, kumtia hasara kubwa, ikiwezekana, mfilisi kabisa. Kwa hili tufanyeje? Badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari na kusign petition, tunachopaswa kufanya ni kuendesha mgomo baridi wa hata saa 24, kwa kuzima simu zetu za mkononi. Matumizi ya simu hizi, kisheria, na kibiashara, ni kwamba, mteja anaponunua line ya simu (SIM card) na kupewa namba ya simu ya mtandao wowote ule, anakuwa na hiari ya kutumia au kutotumia simu yake hiyo, na wala hapangiwi kiasi cha fedha anachopaswa kutumia. Kutumia aku kutotumia ni hiari yake; halazimishwi.

Hebu fikirieni, iwapo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, tena wale ambao wana kipato cha chini ambao ndio wenye matumizi makubwa zaidi, kwani mapato ya hizi kampuni za simu hupatikana zaidi kwenye SMS, na watumiaji hawa ni wengi zaidi kuliko matajiri, waamue kusitisha kutumia simu zao kwa saa 24 hadi 48, hasara watakayoipata wamiliki wa kampuni za simu itakuwa kubwa namna gani? Kampuni hizi zimeingia ubia haramu na Serikali yetu wa kuwanyonya Watanzania ambao wengi wao tayari ni maskini, ambao wengi wao kipato chao hakitoshi hata mlo mmoja wa siku. Ni ajabu walidunduliza MIAKA NGAPI hadi kupata uwezo wa kununua hizo simu zao za mkononi, kisha kununua line, na leo Serikali inakuja na kodi ya kinyemela kuwatoza Shs. 1,000 kwa mwezi? Dharau iliyoje? Basi na sisi (najua nitaitwa mchochezi lakini hizi ni harakati) tuwagomee huduma yao hii, kwa hizo saa 24 hadi 48. Najua wataleta vitisho kwamba kila atakayezima simu yake atafungiwa line yake hiyo, lakini hizo zitakuwa ni nguvu ya soda, kwani hakuna kampuni ya simu hata moja ya kuifungia line yoyote ile iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria, EPOCA, kwani sasa line hiyo ni chanzo cha mapato kwa Serikali.

Kampuni hizo haziwezi kukiuka mkataba wake na Serikali; tuzitie adabu, tuzitie hasara. Adabu isipotosha, mgomo huo (boycott) unarudiwa, mpaka Serikali na wabia wake haramu washike adabu, na waiondoe kodi hiyo haramu. Kwani wamiliki halali wa nchi hii ni nani kama sio sisi Watanzania, tena wanyonge, masikini, tulio wengi? Kwani viongozi wetu wanaolilia kututawala huja kuomba kura kwa nani wakati wa uchaguzi, kama sio kwetu sisi, ambao ndio tunaowapa dhamana hiyo ya kutwaa madaraka? Sasa cha kuogopa ni nini? Tukijipanga vizuri, tutafanikiwa. Hakuna kuogopa, zama hizo zimepitwa na wakati. Hata hivyo, kususia kutumia huduma hii ya simu SIO KOSA LA JINAI! NI HIARI! Tujipange! Inawezekana!



Put his dirty laundry out in the open!
Tafsiri ya mbinu hii ya pili ni "Anika nguo zake chafu hadharani!" Tafsiri fupi ni "anika siri zake za uhalifu/ufisadi hadharani". Kwa lugha ya Kiingereza, "dirty laundry" ina maana ya "uhalifu/ufisadi". Tukubali ukweli. Hakuna asiye na siri. Kampuni hizi za mawasiliano ya mkononi zimekuwa zikiwaibia (pasi na kuwa na ushahidi wa jinsi wanavyoibiwa) wateja wake kuwa miaka lukuki. Waajiriwa kwenye kampuni hizo, ambao ni Watanzania wenzetu, wamekuwa (kutokana na njaa zao) wakirubuniwa kushiriki kwenye wizi huu, pasi na kujua kwamba huu ni unyonyaji mkubwa kwa Watanzania, wengi wao ambao ni maskini.

Watanzania wengi wamekuwa wakilalamika jinsi pesa zao zinavyokatwa kinyemela pasi na kuwa na maelezo kwa sababu gani mambo haya yanafanyika. Kwa bahati mbaya, baadhi ya watendaji katika vyombo husika vya kusimamia sheria husika nao wameingizwa mtegoni, kwa kupewa ruzuku lukuki (bahasha za khaki), ambapo, kwa mfano, wanaposafiri nje ya nchi, hupangiwa masurufu makubwa ambayo kampuni hizi huhesabu kuwa "gharama ya uendeshaji kampuni ya ziada", au "overhead"/ Hapa tunahitaji kuwabembeleza Watanzania wenzetu wanaofanya kazi kwenye kampuni hizi kuwa wazalendo zaidi, na kutufunulia uchafu wote unaofanywa na kampuni hizi, kama ilivyofanyika kwa kampuni ambayo imekuwa ikiliibia taifa kwenye mapato ya matumizi ya umeme kwenye minara yake ya kurushia mawimbi, zaidi ya 1,700, na kusababisha hasara ya zaidi ya Bilioni 119 KWA MWEZI! Sasa harakati na ziendelee.

Tuanike nguo zao chafu hadharani, kila mtu azione: Tuifanye thamani ya kampuni zao iwe ndogo kabisa, kiasi kwamba wezi hawa washitakiwe kwa mujibu wa sheria, ikishindikana, wauze kampuni zao kwa wafanyabiashara wengine ambao wataogopa kutuibia, kwani watatambua kwamba, kwanza, wamenunua kampuni hizo kwa bei ya "kutupa", lakini pili, watatuheshimu Watanzania na kuogopa kurudia makosa ya wenzao.


Mbinu hizi mbili zinatosha. Acheni kuhangaika na hizo petition. Hazisaidii chochote. Mkitaka ushauri wa jinsi ya kuratibu harakati hizi, nitawapa, lakini msiniPM. Sitapokea PM ya mtu yeyote kuhusu hili, kwani najua miongoni mwetu humu wamo mandumilakuwili wengi tu. Siko tayari kumwamini mtu yeyote nisiyemjua kuhusu hili. Nitaweka mambo hadharani.

Kila la heri.

A luta continua!

P.S.: Moderators, nalazimika kuirudia post hii kwenye uzi wake, baada ya kuiweka chini ya post nyingine, kwa kuwa naona hata hao walioanzisha post hiyo ya kukusanya saini kupitia petition wameichoka. Nadhani wameelewa kwamba wanachokifanya hakina tija kwao.

Kwanzankabisa nikupongeze na pia wanajamvi wote kuitikia wito huo. Najua wapo wanaobeza pengine haitakuwa na nguvu, lahasha itafanikiwa sana, na ikubalike kuwa litakuwa ni zoezi endelevu kila wiki siku fulani(ndani ya wiki) wananchi wanazima simu zao kupinga toza la kodi. hakika haitachuku hata miezi miwili itaondolewa, na pia mwamko huo utatupelekea hata kugomea nauli, bei ya sukari, mafuta n.k
Angalizo:
Mashaka yangu ni njinsi ya kusambaza habari hizi nje ya wingo huu wa internet na kuwafikia watu wengi sana ingawa naona wengi wataunga mkono.
Nani atatoa tamko na kuonekana kuwa amesikika? njia gani tutatumia, NGOs, vyama vya wafanyakazi na vyama vya ushirika?
SP
Hivi hatuna chama cha walaji Tanzania?
 
Back
Top Bottom