Tukitaka kodi ya SIMcard ifutwe tufanye hivi

Tukitaka kodi ya SIMcard ifutwe tufanye hivi

hata tukifanya wiki ni wakati umefika wajue sisi ndio tuna say ya mwisho kuhusu matumizi ya simu wanashindwa kuwatoza kodi halafu wanafikiria kutunyonya
 
Well written. Mimi nina karibu mwezi situmii simu ya mtandao mmojawapo. Nimeizima.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

mimi simcard zote zinazoniambia nikasajili wakati nilisajili nazitupa kule..
 
Nizime simu nikose hela nyie hamjui simu zinavyotuingizia hela nini buku kulipia kwa mwezi hamuoni aibu yani mwezi mzima kukatwa buku inakuwa shida tena unakatwa kidogokidogo na si mara moja kha nyie watu wa porini ama mi sitazima simu hata watoze buku kwa dakika simu yangu itakuwa on fully charged
 
Wakuu,

Naona tunatumia muda mwingi kusign hizi petition ambazo hazina athari zinazotakiwa. Nilipokuwa masomoni Marekani, nilifundishwa mbinu moja nzuri ya uanaharakati, lakini nawamegeeni hizi mbili, muweze kuzitumia kufanikisha lengo kuu.


Hit your enemy where it hurts the most: his pockets!

Tafsiri yake ni kwamba "Mpige adui yako mahali ambapo ataumia zaidi: kwenye mifuko yake." Tafsiri fupi ni kwamba, kama ana mapato, tafuta njia ya kumnyima mapato, kumtia hasara kubwa, ikiwezekana, mfilisi kabisa. Kwa hili tufanyeje? Badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari na kusign petition, tunachopaswa kufanya ni kuendesha mgomo baridi wa hata saa 24, kwa kuzima simu zetu za mkononi. Matumizi ya simu hizi, kisheria, na kibiashara, ni kwamba, mteja anaponunua line ya simu (SIM card) na kupewa namba ya simu ya mtandao wowote ule, anakuwa na hiari ya kutumia au kutotumia simu yake hiyo, na wala hapangiwi kiasi cha fedha anachopaswa kutumia. Kutumia aku kutotumia ni hiari yake; halazimishwi.

Hebu fikirieni, iwapo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, tena wale ambao wana kipato cha chini ambao ndio wenye matumizi makubwa zaidi, kwani mapato ya hizi kampuni za simu hupatikana zaidi kwenye SMS, na watumiaji hawa ni wengi zaidi kuliko matajiri, waamue kusitisha kutumia simu zao kwa saa 24 hadi 48, hasara watakayoipata wamiliki wa kampuni za simu itakuwa kubwa namna gani? Kampuni hizi zimeingia ubia haramu na Serikali yetu wa kuwanyonya Watanzania ambao wengi wao tayari ni maskini, ambao wengi wao kipato chao hakitoshi hata mlo mmoja wa siku. Ni ajabu walidunduliza MIAKA NGAPI hadi kupata uwezo wa kununua hizo simu zao za mkononi, kisha kununua line, na leo Serikali inakuja na kodi ya kinyemela kuwatoza Shs. 1,000 kwa mwezi? Dharau iliyoje? Basi na sisi (najua nitaitwa mchochezi lakini hizi ni harakati) tuwagomee huduma yao hii, kwa hizo saa 24 hadi 48. Najua wataleta vitisho kwamba kila atakayezima simu yake atafungiwa line yake hiyo, lakini hizo zitakuwa ni nguvu ya soda, kwani hakuna kampuni ya simu hata moja ya kuifungia line yoyote ile iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria, EPOCA, kwani sasa line hiyo ni chanzo cha mapato kwa Serikali.

Kampuni hizo haziwezi kukiuka mkataba wake na Serikali; tuzitie adabu, tuzitie hasara. Adabu isipotosha, mgomo huo (boycott) unarudiwa, mpaka Serikali na wabia wake haramu washike adabu, na waiondoe kodi hiyo haramu. Kwani wamiliki halali wa nchi hii ni nani kama sio sisi Watanzania, tena wanyonge, masikini, tulio wengi? Kwani viongozi wetu wanaolilia kututawala huja kuomba kura kwa nani wakati wa uchaguzi, kama sio kwetu sisi, ambao ndio tunaowapa dhamana hiyo ya kutwaa madaraka? Sasa cha kuogopa ni nini? Tukijipanga vizuri, tutafanikiwa. Hakuna kuogopa, zama hizo zimepitwa na wakati. Hata hivyo, kususia kutumia huduma hii ya simu SIO KOSA LA JINAI! NI HIARI! Tujipange! Inawezekana!



Put his dirty laundry out in the open!
Tafsiri ya mbinu hii ya pili ni "Anika nguo zake chafu hadharani!" Tafsiri fupi ni "anika siri zake za uhalifu/ufisadi hadharani". Kwa lugha ya Kiingereza, "dirty laundry" ina maana ya "uhalifu/ufisadi". Tukubali ukweli. Hakuna asiye na siri. Kampuni hizi za mawasiliano ya mkononi zimekuwa zikiwaibia (pasi na kuwa na ushahidi wa jinsi wanavyoibiwa) wateja wake kuwa miaka lukuki. Waajiriwa kwenye kampuni hizo, ambao ni Watanzania wenzetu, wamekuwa (kutokana na njaa zao) wakirubuniwa kushiriki kwenye wizi huu, pasi na kujua kwamba huu ni unyonyaji mkubwa kwa Watanzania, wengi wao ambao ni maskini.

Watanzania wengi wamekuwa wakilalamika jinsi pesa zao zinavyokatwa kinyemela pasi na kuwa na maelezo kwa sababu gani mambo haya yanafanyika. Kwa bahati mbaya, baadhi ya watendaji katika vyombo husika vya kusimamia sheria husika nao wameingizwa mtegoni, kwa kupewa ruzuku lukuki (bahasha za khaki), ambapo, kwa mfano, wanaposafiri nje ya nchi, hupangiwa masurufu makubwa ambayo kampuni hizi huhesabu kuwa "gharama ya uendeshaji kampuni ya ziada", au "overhead"/ Hapa tunahitaji kuwabembeleza Watanzania wenzetu wanaofanya kazi kwenye kampuni hizi kuwa wazalendo zaidi, na kutufunulia uchafu wote unaofanywa na kampuni hizi, kama ilivyofanyika kwa kampuni ambayo imekuwa ikiliibia taifa kwenye mapato ya matumizi ya umeme kwenye minara yake ya kurushia mawimbi, zaidi ya 1,700, na kusababisha hasara ya zaidi ya Bilioni 119 KWA MWEZI! Sasa harakati na ziendelee.

Tuanike nguo zao chafu hadharani, kila mtu azione: Tuifanye thamani ya kampuni zao iwe ndogo kabisa, kiasi kwamba wezi hawa washitakiwe kwa mujibu wa sheria, ikishindikana, wauze kampuni zao kwa wafanyabiashara wengine ambao wataogopa kutuibia, kwani watatambua kwamba, kwanza, wamenunua kampuni hizo kwa bei ya "kutupa", lakini pili, watatuheshimu Watanzania na kuogopa kurudia makosa ya wenzao.


Mbinu hizi mbili zinatosha. Acheni kuhangaika na hizo petition. Hazisaidii chochote. Mkitaka ushauri wa jinsi ya kuratibu harakati hizi, nitawapa, lakini msiniPM. Sitapokea PM ya mtu yeyote kuhusu hili, kwani najua miongoni mwetu humu wamo mandumilakuwili wengi tu. Siko tayari kumwamini mtu yeyote nisiyemjua kuhusu hili. Nitaweka mambo hadharani.

Kila la heri.

A luta continua!

P.S.: Moderators, nalazimika kuirudia post hii kwenye uzi wake, baada ya kuiweka chini ya post nyingine, kwa kuwa naona hata hao walioanzisha post hiyo ya kukusanya saini kupitia petition wameichoka. Nadhani wameelewa kwamba wanachokifanya hakina tija kwao.


Ujumbe mzuri MwanaHaki. Unaweza kunisaidia vitabu nyenye ujumbe wa namna hii 'Hit your enemy where it hurts the most: his pockets!' ili nivitafute na kuvisoma vinasaidia kuelimisha watu.
 
Wakuu,

Niliandika hivi kwenye post yangu.

Mbinu hizi mbili zinatosha. Acheni kuhangaika na hizo petition. Hazisaidii chochote. Mkitaka ushauri wa jinsi ya kuratibu harakati hizi, nitawapa, lakini msiniPM. Sitapokea PM ya mtu yeyote kuhusu hili, kwani najua miongoni mwetu humu wamo mandumilakuwili wengi tu. Siko tayari kumwamini mtu yeyote nisiyemjua kuhusu hili. Nitaweka mambo hadharani.

Sasa wewe nduki mbona unaniPM? Simwamini mtu yeyote humu ndani, zaidi ya marafiki wangu wachache. Wengine wenu mnaweza kuwa Usalama wa Taifa, mkitaka kunichunguza. Kama kuna mtu anataka ushauri, aweke post yake hapa, nitamjibu. Siamini katika hizi PM, kwani wapo waliojifanya marafiki zangu, wakaniPM, kumbe walikuwa wanafiki wakubwa!

Hizi ni harakati za ukombozi. Mtaniwia radhi, lakini ukweli ni kwamba wasaliti na ndumilakuwili wapo wengi miongoni mwetu! Kwa HILI, tafadhali sana msiniPM!
nduki, baadaye nitakuweka kwenye Ignore List. Umekiuka masharti yangu ya harakati hizi. Hutaweza tena kuniPM! Wala siwajibiki kuomba radhi, kwani naijua serikali yetu. Kwani ninyi hamjaona walichofanyiwa Ulimboka na Kibanda?

Ushauri wangu kwako nduki na wengine, kama ninyi ni wanaharakati wa kweli, kwa nini ujumbe utumwe kwa watu 15? Ujumbe utumwe kwa KILA MTU anayeweza kufikiwa. Kwa nini mnaweka idadi ya watu? Lengo ni kutaka WATANZANIA WOTE wajue habari hizi.
 
Last edited by a moderator:
Ujumbe mzuri MwanaHaki. Unaweza kunisaidia vitabu nyenye ujumbe wa namna hii 'Hit your enemy where it hurts the most: his pockets!' ili nivitafute na kuvisoma vinasaidia kuelimisha watu.

Mbinu hizi nilifundishwa tu. Sijui kama kuna vitabu. Lakini jaribu Google.
 
Nizime simu nikose hela nyie hamjui simu zinavyotuingizia hela nini buku kulipia kwa mwezi hamuoni aibu yani mwezi mzima kukatwa buku inakuwa shida tena unakatwa kidogokidogo na si mara moja kha nyie watu wa porini ama mi sitazima simu hata watoze buku kwa dakika simu yangu itakuwa on fully charged
mopaozi hujaelewa maana halisi ya harakati hizi. Mimi bila simu yangu ni sawa na kukata mikono yangu. Kukosa mawasiliano kunanipa hasara, kwani nakosa kuwasiliana na wateja wangu, n.k. Nimejiajiri mwenyewe. Nikikosa saa 1 tu ni hasara, sembuse saa 24?

Kinachozungumziwa hapa ni kuukata ufisadi tunaofanyiwa na hizi kampuni za simu, kwani, kwanza, wanatuibia kwenye makato wakati tunapopiga simu (hatuna uwezo wa kuthibitisha iwapo wametukata gharama wanazotangaza wao); na pili, kodi hii ya SIMcard si halali, haikupitishwa na wabunge wetu. Wabunge wa CCM walipitisha Bajeti ya Serikali Kuu ili kulinda maslahi yao, si yetu. Spika Makinda aliwapa mkwara mzito, na kuwaambia, kwa mujibu wa sheria, kama wasingepitisha bajeti hiyo Rais angelivunja Bunge. Walitetea matumbo yao, wakaipitisha. Wabunge wa CHADEMA walikuwa msibani Arusha, kwa wiki moja, hawakuipitisha bajetii hiyo.

Nadhani sasa umeelewa MSINGI wa harakati hizi. Huu ni mwanzo tu. Bado harakati nyingine zitakuja. Kama wewe wajiona bora zaidi kuliko sisi, KAA KIMYA, si lazima uandike upuuzi wako humu. Endelea na usaliti wako, lakini usije kulalamika siku watakapokuja kukudai kodi ya kumiliki TV, kisambuzi, DVD player, na hata hiyo simu yako ya mkononi, unayoiona muhimu sana kwako. Wakiweza kufanikiwa na kodi hii ya kidhalimu, nani wa kuwazuia kuanzisha kodi nyingine?
 
Last edited by a moderator:
MwanaHaki, Maundumula na wengineo nisaidieni kwani vocha za simu hazina kodi (VAT)?.

Kila bidhaa inayonunuliwa, Kyaiyembe, inalipiwa VAT, haijalishi suala hilo limewekwa VAT au la. Ila, kwa mujibu wa sheria, baadhi ya huduma, kama vile vyuo vya kitaaluma vimesamehewa kulipia VAT, kwa hiyo hata ada za vyuo hivyo hazitozwi VAT.

Vocha ni bidhaa kama soda, sigara, bia, n.k.
 
Last edited by a moderator:
Kila bidhaa inayonunuliwa, Kyaiyembe, inalipiwa VAT, haijalishi suala hilo limewekwa VAT au la. Ila, kwa mujibu wa sheria, baadhi ya huduma, kama vile vyuo vya kitaaluma vimesamehewa kulipia VAT, kwa hiyo hata ada za vyuo hivyo hazitozwi VAT.

Vocha ni bidhaa kama soda, sigara, bia, n.k.
Nashukuru mkuu MwanaHaki kwa taarifa majibu.
Ngoja niumize kichwa ili nijue sababu za kuweka kodi ya SIM Card, nisubirie kuanzishwa kwa kodi ya ATM CARD!.
 
Last edited by a moderator:
Kila bidhaa inayonunuliwa, Kyaiyembe, inalipiwa VAT, haijalishi suala hilo limewekwa VAT au la. Ila, kwa mujibu wa sheria, baadhi ya huduma, kama vile vyuo vya kitaaluma vimesamehewa kulipia VAT, kwa hiyo hata ada za vyuo hivyo hazitozwi VAT.

Vocha ni bidhaa kama soda, sigara, bia, n.k.
Nashukuru kwa majibu mkuu!.
Ngoja nitulizane nisubirie kuanzishwa kwa Kodi ya umiliki wa ATM CARD
 
Me nashindwa kuamin kwamb humu karibia laki mbil 2nashndwa kuwa specimen kwenye h issue.

Kwa mfano me hapa nilpo nina zaid ya sms 5000, so hata nkitma kwa watu mia ntakuwa nimefanya k2,

Halaf vkwa hawa wanaosema kwamb hatna madhara xana kwenye,makampun basi 2fanye ,hata kama hatuna madhara ,haina shda kwan lengo letu sio kujua kwamb 2namadhara bt tujue kwamb hatutaki kuonewa na wachache(mafisadi)

Pia ndugu MwanaHaki ningependa 2fanya conclution ya ujumbe ambao 2tatumia kuwajulisha jamaa zetu wengne, Huo ujumbe inabdi uwekwe kweny bandiko lako tena pale mwanzon ili kurahsisha kuuna the tuna copy na kuutum kwa wenzetu.


Me binaf nip tayar kwa huu mgomo,iwapo tu utakuw wel organized , hata kweny social media nitaweka kuwashwishi weng,kadri niwezavyo!

by
Walas Ba
 
Last edited by a moderator:
kodi hiyo ya 1000/= kwa mwezi ni kwa makampuni yote ya cm au TTCL wako pembeni?
 
Tupate wanaharakati watuongoze tuifanye hiyo no moja.

Tatizo siyo kugoma kutumia Sim Card. bali tatizo ni kuwa na wabunge viraza ndani ya ukumbi wa Bunge.

Waziri alipeleka bajeti mbovu bungeni ambayo ina mapendekezo ya kuwepo kwa kodi kandamizi na kuliomba bunge kuzipitisha kodi kandamizi ili iwe sheria na kutumika.

Wabunge wetu viraza na punguani wa akili waliweka maslahi mbele ya vyama badala maslahi yetu tuliowapeleka kule mjengoni kwa kupiga kura ya NDIOOOOOOOOOOOOO!!!!!!

Eti kwa sababu Spika amewaambia kuwa "MKIIKATAA BAJETI, KANUNI ZA BUNGE ZINASEMA RAIS ATALIVUNJA BUNGE....."


-PU-MBAVU ZAO!!!!!!!!

Kwa hiyo wakawa tayari kuipitisha bajeti kandamizi kwetu walalahoi eti ili Rais asilivunje bunge, kwani wao wanajua endapo likivunjwa hapo ina maana wanatakiwa kurudia uchaguzi na ikiwa wao hawana uhakika wa kurudi mjengoni.

Wakaamua kwa kauli moja kusema "NDIOOOOOOOOOO" kumfurahisha Rais na kutuchinjia baharini walalahoi.


Kwa mtazamo wangu hata tufanye nini hiyo imeshapitishwa na kuwa sheria hivyo haiwezi kufutwa kirahisi kama tunavyofikiria.

Tujiandae kwa kauli moja kuweka tofauti zetu za vyama na tuwe kitu kimoja katika kuwaondoa madarakani wabunge wote waliopiga kura ya NDIOOOOOOOOOOO!!!!!!

Hapo tutafanikiwa, vinginevyo.....mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhhhh



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Nizime simu nikose hela nyie hamjui simu zinavyotuingizia hela nini buku kulipia kwa mwezi hamuoni aibu yani mwezi mzima kukatwa buku inakuwa shida tena unakatwa kidogokidogo na si mara moja kha nyie watu wa porini ama mi sitazima simu hata watoze buku kwa dakika simu yangu itakuwa on fully charged
mapinduzi hayahitaji watu wote lazima wengine muwe nyuma, wewe unaweza vip wale wa kijijn???
 
ni wazo zuri, Nashauri siku ya kuzima iwe tarehe 08.08.2013

tuhusishe Na vyombo vya Habari Na wana harakati wapenda haki Na wadau wengine wanaochukizwa Na kodi za kiholela

Itafanikiwa zaidi kampeni zisiwe tu za mtandaoni
 
Nashukuru mkuu MwanaHaki kwa taarifa majibu.
Ngoja niumize kichwa ili nijue sababu za kuweka kodi ya SIM Card, nisubirie kuanzishwa kwa kodi ya ATM CARD!.

Hiyo ya ATM Card iko njiani yaja! Hata ya National ID Card pia, pindi watakapokupa!
 
Agreed.

Nimeupenda msimamo wako. Hakika wewe ni mwanamapinduzi halisi, mwanaharakati mwenye ufahamu mkubwa. Yaani point mwanzo hadi mwisho. Nimeshatoa pendekezo, mgomo ufanyike siku 30 baada ya tarehe 20 Julai, ambazo zitatosha kujipanga vizuri. Tuwapuuze hao mandumilakuwili ambao wameshatumwa kuja kutukatisha tamaa. Kazi ifanyike. Anza kuwaambia wenzako. Siku 30 baada ya 20 Julai zitaangukia tarehe 19 Agosti, kuanzia saa 6 usiku wa siku hiyo, na kwa muda wa saa 24, mgomo utaisha saa 6 usiku ya 20 Agosti 2013.

TUNAWEZA!
 
Back
Top Bottom