Tukitaka kodi ya SIMcard ifutwe tufanye hivi

Tukitaka kodi ya SIMcard ifutwe tufanye hivi

Me nashindwa kuamin kwamb humu karibia laki mbil 2nashndwa kuwa specimen kwenye h issue.

Kwa mfano me hapa nilpo nina zaid ya sms 5000, so hata nkitma kwa watu mia ntakuwa nimefanya k2,

Halaf vkwa hawa wanaosema kwamb hatna madhara xana kwenye,makampun basi 2fanye ,hata kama hatuna madhara ,haina shda kwan lengo letu sio kujua kwamb 2namadhara bt tujue kwamb hatutaki kuonewa na wachache(mafisadi)

Pia ndugu MwanaHaki ningependa 2fanya conclution ya ujumbe ambao 2tatumia kuwajulisha jamaa zetu wengne, Huo ujumbe inabdi uwekwe kweny bandiko lako tena pale mwanzon ili kurahsisha kuuna the tuna copy na kuutum kwa wenzetu.


Me binaf nip tayar kwa huu mgomo,iwapo tu utakuw wel organized , hata kweny social media nitaweka kuwashwishi weng,kadri niwezavyo!

by
Walas Ba
Walas Ba, si lazima tuwe na ujumbe mmoja lakini unakaribishwa kutoa maoni yako kuhusu ujumbe usomeke kwa namna gani; kuwa mbunifu. Muhimu tuwe na tarehe moja tu!
 
Last edited by a moderator:
Tatizo siyo kugoma kutumia Sim Card. bali tatizo ni kuwa na wabunge viraza ndani ya ukumbi wa Bunge.

Waziri alipeleka bajeti mbovu bungeni ambayo ina mapendekezo ya kuwepo kwa kodi kandamizi na kuliomba bunge kuzipitisha kodi kandamizi ili iwe sheria na kutumika.

Wabunge wetu viraza na punguani wa akili waliweka maslahi mbele ya vyama badala maslahi yetu tuliowapeleka kule mjengoni kwa kupiga kura ya NDIOOOOOOOOOOOOO!!!!!!

Eti kwa sababu Spika amewaambia kuwa "MKIIKATAA BAJETI, KANUNI ZA BUNGE ZINASEMA RAIS ATALIVUNJA BUNGE....."


-PU-MBAVU ZAO!!!!!!!!

Kwa hiyo wakawa tayari kuipitisha bajeti kandamizi kwetu walalahoi eti ili Rais asilivunje bunge, kwani wao wanajua endapo likivunjwa hapo ina maana wanatakiwa kurudia uchaguzi na ikiwa wao hawana uhakika wa kurudi mjengoni.

Wakaamua kwa kauli moja kusema "NDIOOOOOOOOOO" kumfurahisha Rais na kutuchinjia baharini walalahoi.


Kwa mtazamo wangu hata tufanye nini hiyo imeshapitishwa na kuwa sheria hivyo haiwezi kufutwa kirahisi kama tunavyofikiria.

Tujiandae kwa kauli moja kuweka tofauti zetu za vyama na tuwe kitu kimoja katika kuwaondoa madarakani wabunge wote waliopiga kura ya NDIOOOOOOOOOOO!!!!!!

Hapo tutafanikiwa, vinginevyo.....mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhhhh



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
mizambwa, wabunge wameshindwa kututetea. Hata hiyo hoja ya maandamano inayoletwa na Mnyika ni hoja mfu, kwani itasababisha watu kupigwa virungu na kuumizwa bure. Wabunge na Bunge zima limepitwa na wakati. Kwenye harakati wanasiasa na Serikali yao HUWEKWA PEMBENI! Hebu pevuka kiakili kijana!
 
Last edited by a moderator:
ki uhakika apo umenena mkuu, ila wasiwasi mkubwa ni je watanzania wangapi watakubaliana na njia hii nzuri ya kuikomoa srikali yetu hii dhalimu isiyojali hata wananchi wake.
 
Halafu tena vodacom wamepandisha bei za internet bundles toka 20k kwa 5gb hadi 25k na pia toka 30k hadi 40k kwa unlimited internet.
Hili kampuni ni la kina rostam na ccm, kwa hiyo tunapoibiwa, ccm wanafurahi sana maana wanatafuta pesa ya kununulia khanga na kofia ili watanzania waendelee kuumizwa na ufisadi. huu mpango nauunga mkono, tuseme sasa yatosha!
 
Nadhani wana bodi mnakumbuka ilikuwa ipitishwe sheria ambayo kampuni zote za simu zingetakiwa kuuza hisa zao kwa watanzania kupitia soko la hisa la dar. mwenye kufahamu kilichotokea atufahamishe tafadhali. nahisi hapa kuna mbinu chafu dhidi ya watanzania (conspiracy) na serikali ya ccm inahusika moja kwa moja. Serikali corrupt inakula njama dhidi ya watu wake walioiweka madarakani... hii nadhani ni tanzania pekeee, haijawahitokea popote
 
Kwa hili watanzania mmenigusa cha kufanya hizi message wanazotupa pindi umejiunga zitumike (kuwamaliza) kupashana habar mapema . Cha kufanya unaandika ujumbe wa tar ya mgomo then unaanza kuforward sms ukimalizia na neno mtumie na mwenzio ujumbe huu, nataman siku ifike mapema, tukiungana tunaweza!
 
Mini ukweli sitaacha jambo hili lipite bila kusema chochote japo mimi siyo MC. Habari ya kodi hii ya kinyemela ya SimuCard Serikali itake isitake iangalie mpango mwingine mbadala wa kupata mapato yake. Kweli ni wasomi wetu tuliowasomesha kwa kipato chetu kidogo yaani kodi yetu, wameelimika na wamestaarabika ni wataalam wetu sasa tunaowategemea kutoa fikra nzuri juu ya mipango ya maendeleo. Hiki kimesahuriwa na wataalam hao tena wakiwa na maandiko yaliyojaa lugha nzito za kigeni kuonesha kwamba kodi hii ikipita basi Serikali iko vizuri sana katika kutekeleza majukumu yake ya kuwasaidia wananchi wake masikini kufukia maendeleo.

Mpaka hao wasemaji wetu Bungeni kusema ndiyo ipite, mchakato katika wizara husika ulifanyika na wazito hao wa wizara wakasema ama kweli huu ni ufumbuzi wa matatizo katika Serikali yetu, 'haya jamani iwekeni vizuri tuipeleke bungeni ikapitiwe'. Nasema hivi, inawezekana kabisa kupitia tafiti ambazo ninyi mlioende shule mnasema 'Feasibility Study' na baadaye ikafanyika kitu kinaitwa 'Analysis' na hatua nyingine nyingi zinazopelekea kitu kuonekana kweli kina mantiki zilifanyika. Bado Serikali siyo tu ikae chini na kufikiria juu ya jambo hili, bali isitishe kwanza. Hili si jambo la kwanza kusitishwa yapo mengi tena ya muhimu zaidi ya hili.
Upo msemo wa wanajeshi usemao 'Kurudi nyuma siyo kukimbia vita, bali kujiweka sawa ili kupambana vema na adui'. Hii pia ni hatua. tunatambua ni gharama nyingi zimetumika kufikia hali hii, lakini kwa Serikali sikivu na makini, bila shaka huu ni wakati muafaka wa kufanya uamuzi sahihi wa kusitisha kwanza ili kujiweka sawa.

Pengine tujiulize maswali haya:-

  • Hivi katika kuongeza mapato ni kodi hii tu?
  • Ikisitishwa kodi hii Serikali yetu inaelekea kubaya?
  • Hii ni hatua ya mwisho kwa wataalam wetu kifikiri juu ya njia zingine kupata mapato?
  • Inawezekana Serikali kuwasaidia wananchi wake kwa kuchukua walichonacho kidogo ili wasaidie vizuri? Najua wewe pia una maswali mengi yaongeze na tafakari.


Nchoji sijakubali kuahirisha agenda hii. Nitaendelea kusema kila nipatapo wasaa wa kunena katika mtandao na popote pale mpaka Serikali itakapositisha KODI hii ambayo ni maumivu ya wazi.
 
ki uhakika apo umenena mkuu, ila wasiwasi mkubwa ni je watanzania wangapi watakubaliana na njia hii nzuri ya kuikomoa srikali yetu hii dhalimu isiyojali hata wananchi wake.
kilaboy, kwenye harakati za ukombozi wasaliti na ndumilakuwili ni wengi. Achana nao. Hata kwenye mapinduzi ya Iran yaliyompeleka kiongozi wao Shah uhamishoni (exile), wanamapinduzi hao hawakuaminiana wao kwa wao, na walichinjana kwa mamia na maelfu ya mamia. Kulikuwa na ukatili wa aina yake; watu waliuwawa bila nafasi ya kujitetea, kwa "kushukiwa tu" kuwa wasaliti, chini ya mwamvuli wa kile kilichoitwa Mapinduzi ya Kiislam.

Hivi ni wapi kwenye Uislam ambapo imeamrishwa kuutoa uhai wa mwanadamu mwingine?

Kwa hiyo kilaboy, usiwajali hao watakaotusaliti, wewe jali kile unachoweza kufanya, kama kweli wewe ni mwanaharakati. Pilipili usoila yakuwashiani?
 
Last edited by a moderator:
Nchoji, kodi hii ni mwanzo tu wa kodi zitakazofuata, iwapo tutashindwa kuidhibiti Serikali. Ngoja nikupe orodha ya kodi unazopaswa kujiandaa nazo.


  1. Kodi ya kumiliki kilongalonga chako
  2. Kodi ya kuwa na ATM Card
  3. Kodi ya Kitambulisho cha Taifa (na kwa kuwa hii ni lazima kuwanayo, na kwa mujibu wa NIDA ni kwamba hata makazi yako yatakuwa wazi kupitia Kitambulisho cha Taifa, hutaweza kuikwepa)
  4. Kodi ya kumiliki luninga na redio pamoja na DVD player kama unayo
  5. Kodi ya kumiliki kisambuzi chako (king'amuzi)
  6. Kodi ya kuzaa watoto wengi (wameiga kutoka China ambako ni marufuku kuzaa zaidi ya mtoto mmoja!)

... na nyinginezo.

Chagua moja. Unaingia moja kwa moja kwenye harakati au haupo. Hkuna mjadala, lakini naona unaunga mkono hoja.
 
Last edited by a moderator:
Ni wazo zuri sana! Tanzania ina vichwa jamani,Itangazwe siku hiyo ili tuzime tu,wanachotufanyia sasa ni usenge!!!!!
 
Well written. Mimi nina karibu mwezi situmii simu ya mtandao mmojawapo. Nimeizima.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

safi, hapa umetumia mbinu ya kwanza vyema, ya pili tumeshauriwa kuwaanika, Hebu Sema, ni mtandao gani huo umewatema?
 
Binafsi sikubaliani na kodi ya simu, lakni tuseme ukwel, kati ya watz mil 45 wanaolipa kodi ni chini ya mil 3, huko marekani income tax ni 27%, bado kod zingine, lakni watz tumefundishwa ku- accept the situation, no way we cn hit the enemy where it hurts, hata ku-air their dirty laundry wl nt help, Watz wana vichwa vgumu sana mkuu, huwez amini kuna maeneo nchi hii kama ulienda mwaka '89 na ukienda leo yako vile vile, Bado wa2 wanavaa nguo zenye viraka.. zaid zaid mitaa hiyo hiyo unakuta mtu amekuwa mbunge or whatsoever kwa miaka 35.... sis kulalama tu ndio ze2 mkuu, hata wale tunaodhani wanasimama il kuwatetea wanyonge ndio wasalit wakubwa...... kama ni nyama hi ni ya ngoz mkuu, imezoea fimbo.
 
Well written. Mimi nina karibu mwezi situmii simu ya mtandao mmojawapo. Nimeizima.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Watakufungia mi line 2 zipo on ila siweki salio napokea tu.
 
Back
Top Bottom