Tukitaka kodi ya SIMcard ifutwe tufanye hivi

Tukitaka kodi ya SIMcard ifutwe tufanye hivi

Tatizo wabongo tuko kama Waarabu tunasalitiana sana, wazo zuli but usaliti hatutaweza maana hapa tutakimbilia siasa wakati tunaumia wote.
 
Kusema ukweli nilikuwa na line za TTCL 2, VODA 2 na Zantel 3 nimeachana nazo nimebaki na Voda 1 na Zantel 1 na nina uhakika wengi wataachana na line za ziada na baadhi ya kampuni zitaathirika sana.
Hata utumaji wa pesa kwenye simu utampungua, eti natuma 199,000/= nakatwa 600/=. Hapo yeye akienda kutoa anakatwa 3500/=. Wizi mtupu.
 
Jambo la ajabu sana hili, wameshindwa kukusanya kodi kwa kampuni za simu wameamua kuwakamua wananchi wanyonge, hii sawa na kodi ya kichwa, kwa mwaka shilingi 12,000/=. Rwanda nchi ndogo tu inatuzidi kukusanya kodi za simu. Mgomo wa kuzima simu naunga mkono kwa 100% na hata kama nusu ya ya watumiaji watazima simu, mgomo huu utakuwa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani kuna watu wengi ambao watakuwa hawajazima kwa wakati huo lakini hawataweza kuwasiliana na wale waliozima, good plan, bravo.
 
Njia hii itafaa sana lakini ni jinsi gani watanzania wataweza kapata hizo taarifa ili tukubaliane wote pamoja na ili sumu ifike kwenye mifupa na mioyo ya kampuni za simu.

Jana niliongea na mjombawangu kijijini alinipa taarifa kuwa kama tozo la shilingi 1,000/= kwa line litafanyoka basi huenda ikawa ndiyo mwisho wa yeye kumiliki simu. akasema hawezi kulipia shilingi 1,000/ huku hata airtime yenyewe mpaka atumiwe na wajukuu zake, akazidi kusema kuwa kwa kijijini sh 1,000 ni debe la mahindi au mboga ya kula na familia yake. hawezi kuichangia serikali. Nikamuuliza ailaumu serikali na chama chake tawala nikimaanisha CCM kwaani yeye ni mwenyekiti wa kitongoji kupitia CCM. akaniuliza kuwa kwani wao ndiyo wameweka huo ushuru kwenye kodi? nikamwambia ni mapendekezo ya serikali kwenye bajeti ya mwaka huu ambayo ilipishwa na wabunge waliowengi yaani CCM. Akashangaa sana wabunge kupitisha maumivu makubwa kwa wapiga kura wao huku wakijua hali zao. akaniahidi kumuuliza mbunge wake kwa nini alipitisha kodi hii bungeni. baada ya hapo niliongea na mama yangu mdogo akaniambia mwisho wa mwezi simu yake haitakuwa hewani kwa kuwa hawezi kulipa hiyo kodi.
Ndugu, kodi hiyo inakusanywa indirectly. Hapa serikali inahakiki idadi ya wateja ya kampuni husika halafu inaiwekea kiwango cha kuwasilisha kila mwezi kwa hesabu ya 1,000/= kwa kila mteja. Kampuni yenyewe sasa ndo inaparangana kujua itapate hicho kiasi bila kuathiri mapato yake. Hivyo, wanapandisha bei ya vifurushi, utumaji wa pesa n.k. Kwa hiyo mtu wa kawaida hata feel kama amekatwa hiyo elfu. Sasa ni juu ya watumiaji wa kila siku kutegeana kulipa hiyo kodi. Yaani, wewe ukipunguza matumizi yako, mzigo wote wataubeba watakaojipendekeza. Hivyo hivyo na mimi nikipunguza, mzigo wanabeba watakaojipendekeza.
 
u must b out of ua mind....we willl be do and the impacts will be obvious,we gona do it
Mnachekesha kweli nyie.

Mnaijua 80-20 rule?

Kwa taarifa yenu mapato ya kampuni za simu kama Zantel, Airtel na Voda 80% ni kutoka kwa Corporate clients wao na sie wengine akila baba Zabosi ndio tunachangia hiyo 20% sasa hata tukizima sisi simu sitegemei kama mabenki yatazima simu zao, au ofisi za serikali watazima simu zao, wabunge watazima simu zao, makampuni makubwa yatazima simu zao. Na mtu yeyote mwenye shughuli za kumpatia kipato lazima anahitaji mawasiliano hawezi kusima simu yake hata kwa dakika 30.

Sana sana huo mgomo wenu utawaumiza wakina mangi wanauza vocha na kutoa huduma za Tigo/M-pesa
 
Watanzania bwana...naona watu hizi harakati za kupinga kodi mpya ya simu kama vile haziwahusu vile...??


Tukumbuke kuwa simcard haina kazi kama huduma za kampuni husika hazipo...Na ieleweke kuwa hakuna huduma yoyote ya bure toka kwenye kampuni ya simu kwa manufaa ya mtumiaji..!
Hii inaonesha kuwa simcard haimnufaishi mtumiaji kama inavyomnufaisha mtoa huduma (kampuni)! Kampuni za simu zinatakiwa kulipa hii kodi kulingana na faida inayotengeneza kwa kila mteja..!
Isitoshe kila mwenye simcard hakuiokota barabarani bali aliuziwa na kampuni na wakati huo VAT ilishakatwa!


Dalili hizi zinanionesha kuwa hapo baadaye tutalazimishwa kulipa kodi ya kumiliki kila kitu hata hivi visimbuzi (ving'amuzi) vya kichina tulivyolazimishiwa! Kama wanafanya hivi kwa simcard seuze kwa umiliki wa saa ya mkononi, viatu, nguo, tv, jiko la mkaa, jiko la gesi, mabegi ya nguo, computers, nk.


Kama hatuwezi kugoma kwa sababu serikali "inatujali na kututendea mengi mazuri" basi tugome kwa sababu haya makampuni ya simu yanatuibia sana na hawalipi kodi serikali ipasavyo!


Inabidi tuamke sasa na kujitetea! "Hakika nawaambia tusipoungana kukemea yale yanayotukera hawa jamaa watawatendea ndugu zetu na watoto wetu makubwa zaidi ya haya tunayotendewa sasa make kazi yao ni kuangalia tumesinzia wapi ili watukandamize zaidi..!"

Wakuu,

Naona tunatumia muda mwingi kusign hizi petition ambazo hazina athari zinazotakiwa. Nilipokuwa masomoni Marekani, nilifundishwa mbinu moja nzuri ya uanaharakati, lakini nawamegeeni hizi mbili, muweze kuzitumia kufanikisha lengo kuu.


Hit your enemy where it hurts the most: his pockets!

Tafsiri yake ni kwamba "Mpige adui yako mahali ambapo ataumia zaidi: kwenye mifuko yake." Tafsiri fupi ni kwamba, kama ana mapato, tafuta njia ya kumnyima mapato, kumtia hasara kubwa, ikiwezekana, mfilisi kabisa. Kwa hili tufanyeje? Badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari na kusign petition, tunachopaswa kufanya ni kuendesha mgomo baridi wa hata saa 24, kwa kuzima simu zetu za mkononi. Matumizi ya simu hizi, kisheria, na kibiashara, ni kwamba, mteja anaponunua line ya simu (SIM card) na kupewa namba ya simu ya mtandao wowote ule, anakuwa na hiari ya kutumia au kutotumia simu yake hiyo, na wala hapangiwi kiasi cha fedha anachopaswa kutumia. Kutumia aku kutotumia ni hiari yake; halazimishwi.

Hebu fikirieni, iwapo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, tena wale ambao wana kipato cha chini ambao ndio wenye matumizi makubwa zaidi, kwani mapato ya hizi kampuni za simu hupatikana zaidi kwenye SMS, na watumiaji hawa ni wengi zaidi kuliko matajiri, waamue kusitisha kutumia simu zao kwa saa 24 hadi 48, hasara watakayoipata wamiliki wa kampuni za simu itakuwa kubwa namna gani? Kampuni hizi zimeingia ubia haramu na Serikali yetu wa kuwanyonya Watanzania ambao wengi wao tayari ni maskini, ambao wengi wao kipato chao hakitoshi hata mlo mmoja wa siku. Ni ajabu walidunduliza MIAKA NGAPI hadi kupata uwezo wa kununua hizo simu zao za mkononi, kisha kununua line, na leo Serikali inakuja na kodi ya kinyemela kuwatoza Shs. 1,000 kwa mwezi? Dharau iliyoje? Basi na sisi (najua nitaitwa mchochezi lakini hizi ni harakati) tuwagomee huduma yao hii, kwa hizo saa 24 hadi 48. Najua wataleta vitisho kwamba kila atakayezima simu yake atafungiwa line yake hiyo, lakini hizo zitakuwa ni nguvu ya soda, kwani hakuna kampuni ya simu hata moja ya kuifungia line yoyote ile iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria, EPOCA, kwani sasa line hiyo ni chanzo cha mapato kwa Serikali.

Kampuni hizo haziwezi kukiuka mkataba wake na Serikali; tuzitie adabu, tuzitie hasara. Adabu isipotosha, mgomo huo (boycott) unarudiwa, mpaka Serikali na wabia wake haramu washike adabu, na waiondoe kodi hiyo haramu. Kwani wamiliki halali wa nchi hii ni nani kama sio sisi Watanzania, tena wanyonge, masikini, tulio wengi? Kwani viongozi wetu wanaolilia kututawala huja kuomba kura kwa nani wakati wa uchaguzi, kama sio kwetu sisi, ambao ndio tunaowapa dhamana hiyo ya kutwaa madaraka? Sasa cha kuogopa ni nini? Tukijipanga vizuri, tutafanikiwa. Hakuna kuogopa, zama hizo zimepitwa na wakati. Hata hivyo, kususia kutumia huduma hii ya simu SIO KOSA LA JINAI! NI HIARI! Tujipange! Inawezekana!



Put his dirty laundry out in the open!
Tafsiri ya mbinu hii ya pili ni "Anika nguo zake chafu hadharani!" Tafsiri fupi ni "anika siri zake za uhalifu/ufisadi hadharani". Kwa lugha ya Kiingereza, "dirty laundry" ina maana ya "uhalifu/ufisadi". Tukubali ukweli. Hakuna asiye na siri. Kampuni hizi za mawasiliano ya mkononi zimekuwa zikiwaibia (pasi na kuwa na ushahidi wa jinsi wanavyoibiwa) wateja wake kuwa miaka lukuki. Waajiriwa kwenye kampuni hizo, ambao ni Watanzania wenzetu, wamekuwa (kutokana na njaa zao) wakirubuniwa kushiriki kwenye wizi huu, pasi na kujua kwamba huu ni unyonyaji mkubwa kwa Watanzania, wengi wao ambao ni maskini.

Watanzania wengi wamekuwa wakilalamika jinsi pesa zao zinavyokatwa kinyemela pasi na kuwa na maelezo kwa sababu gani mambo haya yanafanyika. Kwa bahati mbaya, baadhi ya watendaji katika vyombo husika vya kusimamia sheria husika nao wameingizwa mtegoni, kwa kupewa ruzuku lukuki (bahasha za khaki), ambapo, kwa mfano, wanaposafiri nje ya nchi, hupangiwa masurufu makubwa ambayo kampuni hizi huhesabu kuwa "gharama ya uendeshaji kampuni ya ziada", au "overhead"/ Hapa tunahitaji kuwabembeleza Watanzania wenzetu wanaofanya kazi kwenye kampuni hizi kuwa wazalendo zaidi, na kutufunulia uchafu wote unaofanywa na kampuni hizi, kama ilivyofanyika kwa kampuni ambayo imekuwa ikiliibia taifa kwenye mapato ya matumizi ya umeme kwenye minara yake ya kurushia mawimbi, zaidi ya 1,700, na kusababisha hasara ya zaidi ya Bilioni 119 KWA MWEZI! Sasa harakati na ziendelee.

Tuanike nguo zao chafu hadharani, kila mtu azione: Tuifanye thamani ya kampuni zao iwe ndogo kabisa, kiasi kwamba wezi hawa washitakiwe kwa mujibu wa sheria, ikishindikana, wauze kampuni zao kwa wafanyabiashara wengine ambao wataogopa kutuibia, kwani watatambua kwamba, kwanza, wamenunua kampuni hizo kwa bei ya "kutupa", lakini pili, watatuheshimu Watanzania na kuogopa kurudia makosa ya wenzao.


Mbinu hizi mbili zinatosha. Acheni kuhangaika na hizo petition. Hazisaidii chochote. Mkitaka ushauri wa jinsi ya kuratibu harakati hizi, nitawapa, lakini msiniPM. Sitapokea PM ya mtu yeyote kuhusu hili, kwani najua miongoni mwetu humu wamo mandumilakuwili wengi tu. Siko tayari kumwamini mtu yeyote nisiyemjua kuhusu hili. Nitaweka mambo hadharani.

Kila la heri.

A luta continua!

P.S.: Moderators, nalazimika kuirudia post hii kwenye uzi wake, baada ya kuiweka chini ya post nyingine, kwa kuwa naona hata hao walioanzisha post hiyo ya kukusanya saini kupitia petition wameichoka. Nadhani wameelewa kwamba wanachokifanya hakina tija kwao.
 
Mkuu nimekusoma (kukuelewa) vizuri sana hizo mbinu ni takatifu kama shambulio basi hili naliita KISU CHASHINGO yani hapa adui humpi nafasi hata ya kuomba maji. Ila hizi plane kwa hapa bongo bado ni ngumu ukilinga nisha na mataifa mengine, nakinacho ipa ugumu plani hizi ni unafiki na kutokua wazalendo myoyoni mwetu. Tukubali tukatae plane namba moja ni nzuri kama tusinge kuwa wanafiki, nina uhakika pindi tutakapo kubaliana kuzima simu zetu wapo watakao tusaliti nakuendelea na matumizi yao kama kawa
 
Maundumula na Wengine hebu kuweni Wazalendo wa Kweli kwa Kumhurumia Mtanzania wa Chini - Mwenye Kipato Kidogo! Lengo Kuu la Kulalamika/Mgomo ni Kufikisha Ujumbe kwa Wausika Kuwa Kodi hii Hatyitaki!!
 
Lukosi unaona wasomi wa ukweli na mawazo ya kuokoa sio wewe mbeba maboksi
 
Hiyo safi!Ktk uchafu wa makampuni ya simu kwa sasa yameajiri wahindi wengi kuliko watanzania na pia baadhi ya operations wamehamishia india na hivyo ma engineer wetu kupoteza ajira

Mkuu una data, anza kuzimwaga. Usizikalie. Ni saa ya kuwalipua nduli hawa!
 
Watanzania tumekuwa waoga sana wa kutekeleza maamuzi yetu wengi wetu ni watu wa porojo nyingi kutekeleza inakuwa ngumu.
 
Ingawa na mimi kipato changu kinategemea kampuni za simu lakini kwa hili lazima niunge mkono.
 
Zantel, Airtel na Tigo nimeshazima...wikendi hii nazima Voda vile vile.

Mkuu umeeleweka vizuri. Nakuunga mkono kwa 100%. Tuanze kwa kuyasusia haya makampuni ya simu. Wakiona wanaingia hasara ni lazima wataitafuta serikali na kuwabana ili hii kodi iondoshwe!

Kaka nakusifu lakini unaharibu. Tujipange ili athari iwe kubwa zaidi. Inabidi tuwatangazie Watanzania wenzetu tarehe ambayo itawawezesha kujipanga vizuri, kwani tukiweka, kwa mfano, muda wa siku 30 kabla ya tarehe husika, idadi ya washiriki katika mgomo baridi huu itakuwa kubwa zaidi. Utaona jinsi tutakavyobembelezwa tusisusie kutumia simu zetu; watatishia hata kutufungia, lakini zitakuwa ni danganyatoto!

Tujipange. Mimi napendekeza siku 30 baada ya tarehe 20 Julai, ambayo itaangukia tarehe 19 Agosti 2013. Mgomo huo uanze saa 6 usiku wa 19 Agosti na kukamilika 20 Agosti 2013. Hii itakuwa kwa MITANDAO YOTE!

Kazi ni kwenu!
 
Tatizo wabongo tuko kama Waarabu tunasalitiana sana, wazo zuli but usaliti hatutaweza maana hapa tutakimbilia siasa wakati tunaumia wote.

Kaka kuwa na imani; hata tukifanikiwa kwa kiwango cha asilimia 20, bado tutakuwa tumefanikiwa. Ndio, Wabongo tunategeana, lakini wenzetu walio waoga wakiona tumefanikiwa kiasi, tutakaporudia mgomo idadi itaongezeka. Kuwa na imani!
 
u must b out of ua mind....we willl be do and the impacts will be obvious,we gona do it
Maundumula

Kwenye harakati za ukombozi kuna watakaopata athari hasi. Acha hao akina Mangi wauza vocha waumie, ili nao waone wanavyoshirikiana na wanyonyaji hao wanaojidai, eti, ni wawekezaji! Kama sisi wa 20% tusingekuwa na umuhimu kwa hizo kampuni za simu, wasingekuwa wanatumia fedha nyingi kutangaza bando lukuki, kwenye redio na luninga, kutushawishi kutumia huduma zao. Tutaona hiyo 20% itakavyofanya kazi, kwani ni 20% ya wateja wangapi?
 
Last edited by a moderator:
Maundumula

Kwenye harakati za ukombozi kuna watakaopata athari hasi. Acha hao akina Mangi wauza vocha waumie, ili nao waone wanavyoshirikiana na wanyonyaji hao wanaojidai, eti, ni wawekezaji! Kama sisi wa 20% tusingekuwa na umuhimu kwa hizo kampuni za simu, wasingekuwa wanatumia fedha nyingi kutangaza bando lukuki, kwenye redio na luninga, kutushawishi kutumia huduma zao. Tutaona hiyo 20% itakavyofanya kazi, kwani ni 20% ya wateja wangapi?

Haya kila la kheri mi simu yangu itakuwa ON
 
Plan ni nzuri.Binafsi napendekeza wiki moja kabla ya mgomo,tufahamishane kwa sms kwamba 'tarehe flan watanzania woote tunaotumia simu,tuungane kwa pamoja kuzima simu zetu kwa muda wa masaa 48,ili kuishnikiza serikali kuondoa kodi ya sh.1000 kwa kila mwezi.serikali isipotoa majibu ya uhakika basi tuzime simu zetu kwa masaa mengne 48'sambaza ujumbe huu kwa watu zaid ya 15.
Kwanza naona tuna chelewa,harakati hiz zianzie hapahapa kila atakae soma hii thread amjulishe na rfk ake mwenye access ya jf.Na pia ujmbe uanze kusambazwa kuanzia leo usomeke kama huo hapo juu/chn
...'Ndg Mtanzania hasa ww unaetumia simu.Tuungane ktk mgomo wa kuishnikiza serikali kuondoa kodi ya sh.1000 kwa kila line kwa kila mwezi,Mgomo utaanza trh 20 julai .unachotakiwa kufanya ni kuzima simu yako/zako.mpaka pale tutakapopata jibu la kueleweka kutoka serikalini'
Sambaza ujumbe huu kwa waumiaji wa simu zaidi ya 15.
 
Watanzania bwana...naona watu hizi harakati za kupinga kodi mpya ya simu kama vile haziwahusu vile...??


Tukumbuke kuwa simcard haina kazi kama huduma za kampuni husika hazipo...Na ieleweke kuwa hakuna huduma yoyote ya bure toka kwenye kampuni ya simu kwa manufaa ya mtumiaji..!
Hii inaonesha kuwa simcard haimnufaishi mtumiaji kama inavyomnufaisha mtoa huduma (kampuni)! Kampuni za simu zinatakiwa kulipa hii kodi kulingana na faida inayotengeneza kwa kila mteja..!
Isitoshe kila mwenye simcard hakuiokota barabarani bali aliuziwa na kampuni na wakati huo VAT ilishakatwa!


Dalili hizi zinanionesha kuwa hapo baadaye tutalazimishwa kulipa kodi ya kumiliki kila kitu hata hivi visimbuzi (ving'amuzi) vya kichina tulivyolazimishiwa! Kama wanafanya hivi kwa simcard seuze kwa umiliki wa saa ya mkononi, viatu, nguo, tv, jiko la mkaa, jiko la gesi, mabegi ya nguo, computers, nk.


Kama hatuwezi kugoma kwa sababu serikali "inatujali na kututendea mengi mazuri" basi tugome kwa sababu haya makampuni ya simu yanatuibia sana na hawalipi kodi serikali ipasavyo!


Inabidi tuamke sasa na kujitetea! "Hakika nawaambia tusipoungana kukemea yale yanayotukera hawa jamaa watawatendea ndugu zetu na watoto wetu makubwa zaidi ya haya tunayotendewa sasa make kazi yao ni kuangalia tumesinzia wapi ili watukandamize zaidi..!
"

Nimeupenda msimamo wako. Hakika wewe ni mwanamapinduzi halisi, mwanaharakati mwenye ufahamu mkubwa. Yaani point mwanzo hadi mwisho. Nimeshatoa pendekezo, mgomo ufanyike siku 30 baada ya tarehe 20 Julai, ambazo zitatosha kujipanga vizuri. Tuwapuuze hao mandumilakuwili ambao wameshatumwa kuja kutukatisha tamaa. Kazi ifanyike. Anza kuwaambia wenzako. Siku 30 baada ya 20 Julai zitaangukia tarehe 19 Agosti, kuanzia saa 6 usiku wa siku hiyo, na kwa muda wa saa 24, mgomo utaisha saa 6 usiku ya 20 Agosti 2013.

TUNAWEZA!
 
Back
Top Bottom