Tukiondoa muda ni nini kinabaki?

Tukiondoa muda ni nini kinabaki?

Time exists only into this physical world.

Kiuhalisia hakuna maisha bila muda, na tulipo hapa kila kitu kimeisha, yaan namaanisha maisha haya tunayoyaish leo hii, tupo ktk Past, na roho zetu zilishayapita haya zipo ktk Future, kama nilivyosema muda una exist ktk ulimwengu huu wa mwili, na ktk Roho(unseen world) huko hakuna mpaka wa muda hivyo Roho zinauwezo wa kufanya tendo ambalo kimwil lingefanywa kwa maelfu ya miaka huko rohon likafanyika within the second(japo huko hakuna elimu ya muda hivyo huwez pima tukio kwa muda).

Ushahidi ni kwamba hata ndoto zako zinaproof sometime ukaota jambo fulan ambalo linakuja kukutokea miaka ya mbele, hiyo yote huwa ni taswira za matukio iliyopitia Roho yako na kuyaleta matukio hayo kwa nafsi yako kupitia ndoto ili yaendane na uelewa ama sheria za ulimwengu wa mwili.

Hata hao wanaofuatilia mambo ya time travel wajue kuwa haiwezekan na haitowai kuwezekana, maana dunian ukitaka kutravel in time unatakiwa uwe na mwili usioshikwa ama unaotawaliwa na sheria za muda, zaid unaweza travel in time kiroho tu.

Muda ukisimama basi hata maisha yatasimama.

Na ukitaka uusimamishe muda basi utatakiwa usimamishe saa kuu za dunia zinazotawala muda ambazo ni JUA na MWEZI,

Na ndiomaana huwa tunapinga kuwa hakuna pua ya mtu iliyowai kanyaga mwezini wala hakuna atakayeweza fika mwezini, kwakuwa mwezi ndio main controller wa muda, hivyo basi ukianza kuufuata ni sawa na kusogeza mbele muda wa maisha yako na kufikia limit ya maisha yako hivyo utafika ukiwa maiti mwezin ama ufike ukiwa mzee tofaut na ulivyoondoka dunian.

Muda hauwezi simama mpaka miili yetu ama maisha ya kidunia yatakapo reach point ya end of destination na kufikia ile level ya Roho zetu ziliko ambako hakuna sheria za muda na huko kila kitu kimekwisha.

Niishie hapa nisije wachanganya.
Mm nimeelewa vzr sana
 
Maana yake tumejitengenezea mfumo ambao ni ngumu kuishi nje yake,
Lakini ingewezekana kuishi kama wakale, sindio ?

Wa kale pia walihitaji kufahamu muda/majira kupambana na changamoto zao ,tofauti yao ilikuwa ni njia walizo tumia kufahamu wakati..

Kwa mfano bila ya muda au vipindi flani vya majira inge wezekana vipi kujua wakati sahihi wa kupanda mazao yao !?.
 
Ni athari gani ambazo tunaweza kuzipata tukiondoa utambuzi huo wa muda ikiwa binadam wa mwanzo hawakuweza kuzipata na waliishi pasipo calculations za muda kama sisi tunavyozijua

Athari ni nyingi sana ,na sidhani kama hawakuwa wakitunza muda ila ilikuwa kizamani sana.Binafsi nnakumbuka kwa sababu ya uduni na hali ya umasikini nilikuwa nikitunza muda kwa kuangalia kimvuli cha Jua na wakati mwingine Jua lenyewe.

Nilijua muda upi ni sahihi kuwahi Shule na muda upi ni sahihi kurudi Nyumbani kupambana na Kazi za Nyumbani.Wale Jamaa warina Asali wanao ishi porini ukiwachunguza ni lazima wana namna yao ya kutunza muda.
 
Wakuu naombeni mnifungue akili katika hili limenifikirisha mno, imewezekana vipi. Future iwe ndio hiyohiyo past, future ndio inajijengea past, palipo na future ndipo miguu ya past ilipo hapohapo, na ukiangalia past utaweza kujikuta umejenga future.

Deep down katika kufikiri nauona muonekano halisi wa future unajidhihirisha kwenye past, maana haiwezekani kuiona future ukiwa upo kwenye future mpaka ifikie kuwa past, na ukirudi nyuma kwenye past hiyohiyo, utajiona ulikuwa kwenye future pia kwa nyakati hiyo.

Na inafahamika kuwa hakuna future bila present na hakuna past bila ya present kuhusika katika wakati huo.

Unajua muda huu naandika nipo kwenye present, na ndani ya muda huu nipo pia kwenye past ambayo ilikuwa future na kisha future itanigeukia tena kuwa past baada ya muda huu huu kuupita.

Ni kitu cha ajabu sana kwamba hata kabla ya kusukwa kwa mfumo wa muda, binadamu wa kwanza waliweza kujua nyakati walizokuwa wakifanya jambo na baada ya jambo hilo kupita kufanywa, lakini hakukuwa na mtu wala kitu chenye kuwaaminisha kuwa huo ndio muda.

Kama binadamu wa kipindi cha kabla ya kuundwa kwa mfumo wa muda na nyakati, waliweza kuishi kwa namna hii ninayoiona ni ya ajabu kwangu na pengine haikuwa ajabu kwao na haikuwafaidisha wala kupatwa na hasara isiyotokana na kuutambua muda kwa wakati huo.

Ni vipi sisi binadamu wa sasa tukiuondoa huu mfumo tambuzi wa muda tuliojitengenezea? Nini kitatuzuia?

Ni madhara ya aina gani tunaweza kuyapata ikiwa wakale hawakuyapata na haikuwanyima dhima ya kuishi bila kuutambua muda wao?

Ukiishi na jamii kama hazdabe unakuwa umeondoa muda ..
 
Yes! Hapo kwenye hesabu ndipo nilipolenga, ukiangazia hapo awali kuna watu walikuwepo na waliishi vizuri kwa namna wanayoijua wao bila kuutambua muda ili kuendana nao na kabla ya hizo hesabu za kwenda na muda

Suala zito linabakia kwa dunia ya sasa tukiondoa hizi hesabu za muda itatunyima kuishi?
Ukienda tu mahakamani inaitajka ushahidi wa muda wa tukio, kwahyo hivi vitu vilikuja automatically ili kurahisisha baadhi ya mambo.
 
Mkuu
Ebu nikwambie kitu “Huwezi kuuondoa Muda”!!

Lakini nitakujibu kadiri ww unavyomaanisha na kudhani!
Ni ukweli kua ww unadhan muda umetengenezwa…La hasha…hyo si kweli hata kidogo !! Binadamu ametengeneza vifaa vya uhesabia muda na namna ya kuuhesabu hapa tunaongelea saa,simu ,kalenda, na vitu vyote vinavohesabu muda (LAKINI HIVI SI MUDA na wala haviathiri muda wenyewe)

Pia yawezekana wewe umejikita kwene Namna ya uhesabuji wa muda ambao ni universal au hata wa jamii fulani!! mfano siku,week,mwezi,mwaka nk na majina yake jumatatu jumanne…jumapil

KWA MANTIKI HIYO UNAWEZA UKAWA SAHIHI KWAMBA HIVI VINAWEZA VIKAONDOLEWA NA WALA HAVITAATHIRI MUDA.. ingawa vitaathiri uelewa wetu na namna tulivokua tunaitofautisha jana na leo na kesho, saa moja na nyingine, mwaka mmoja na mwingine.Hata hivo hata kama vitatolewa vifaa vya kuhesabia Muda na Mifumo tunayotumia kuutambua bado muda utakuepo na utaendelea kuuyoyoma kama kawaida..na hayo tutayashuhudia katka viumbe vyote vilivo hai ikiwemo sisi binadamu!

Kwan Madhara ya muda yataendelea kuonekana kama kuzaliwa, kukua, kuzeeka, kisha kufa ,kuoza, kupotelea

Kwa maelezo hayo naomba nikurudishe sasa kwene Muda!! Muda hauko kwene vitu,wala hauko kwene watu.Ila unaonekana kupitia matukio,Hivo hata watu wazamani sana waliweza kuhesabu muda kupitia matukio au majira au misimu. Misimu ya mvua,kiangazi,misimu ya joto au ya baridi,

Kifupi uhai uliambatanishwa na Muda!!…Tupo kwa sababu ya Muda lakini Muda haupo kwasababu ya uhai!!
Tuna exist katka certain interval ya muda!!..Muda hausimami wala haujirudii yanayojirudia n matukio
Sure sure umemaliza mkuu.

Sent from my itel A571W using JamiiForums mobile app
 
Kwa mujibu wa Albert Einstein (Relativity Theory) muda ni relative kutokana na frame of refence (hence relativity) na si absolute. Muda ni function ya speed na gravity.

1.Kuuondoa muda kutoka frame yako ya reference inabidi uende kwa spidi ya mwanga katika ombwe
299 792 458 m / s

2. Kitu chochote chenye uzito, hata mdogo kiasi gani, kadiri kinavyozidi kukaribia speed hii, ndivyo uzito wake unavyoongezeka na kukaribia infinity.

3. Hivyo, hakuna kitu chenye uzito, hata mdogo vipi, kinachoweza kufikia spidi ya mwanga katika ombwe 299 792 458 m / s

4. Hivyo, hakuna kitu ambacho kina uzito ambacho kitaweza kuuondoa muda.

5. Kutokea kwa mtazamo wa muale wa mwanga na photon ambayo inakwenda kwa spidi ya mwanga 299 792 458 m / s, muda haupo. Mwanga una experience ulimwengu ambao hauna past wala future, hivyo hauna muda.

Hapa nimeangalia muda kwa relation na speed tu, sijaingia kwenye gravity kubwa kama karibu na black holes.
Tukisema Mungu mwenye nguvu zote mmiliki wa hii dunia na ulimwengu wote alitumia muda wa siku saba kuumba hii dunia na ulimwengu wote tunakuwa tunakosea? Au wakati wa uumbaji hakukuwa na muda?
 
Maana yake tumejitengenezea mfumo ambao ni ngumu kuishi nje yake,
Lakini ingewezekana kuishi kama wakale, sindio ?
Wewe una hakika gani ya kuwa wakale hawakuwa na mifumo yao kuangalia muda? Wewe kwako muda unatafsiri kwa sababu kuna saa,simu,kalenda, na majina ya siku,week,mwezi,miaka. Sasa em tuondoe ivyo vitu tuone wakale walitumia nini kujua Muda.
Kwa mufano kabla ya Yesu muda uliesabiwa kurudi nyuma. Mf mfalme fulan alitawala kuanzia mwaka 570 hadi 538 ..je siku zilikuwa zinarudi nyuma? Walitumia nini kujua muda kwa wakati wao? Kwa hiyo huwezi kuondoa Muda maana ndiyo maisha halisi. Ukiondoa muda manake hakuna maisha tena.
 
Mkuu
Ebu nikwambie kitu “Huwezi kuuondoa Muda”!!

Lakini nitakujibu kadiri ww unavyomaanisha na kudhani!
Ni ukweli kua ww unadhan muda umetengenezwa…La hasha…hyo si kweli hata kidogo !! Binadamu ametengeneza vifaa vya uhesabia muda na namna ya kuuhesabu hapa tunaongelea saa,simu ,kalenda, na vitu vyote vinavohesabu muda (LAKINI HIVI SI MUDA na wala haviathiri muda wenyewe)

Pia yawezekana wewe umejikita kwene Namna ya uhesabuji wa muda ambao ni universal au hata wa jamii fulani!! mfano siku,week,mwezi,mwaka nk na majina yake jumatatu jumanne…jumapil

KWA MANTIKI HIYO UNAWEZA UKAWA SAHIHI KWAMBA HIVI VINAWEZA VIKAONDOLEWA NA WALA HAVITAATHIRI MUDA.. ingawa vitaathiri uelewa wetu na namna tulivokua tunaitofautisha jana na leo na kesho, saa moja na nyingine, mwaka mmoja na mwingine.Hata hivo hata kama vitatolewa vifaa vya kuhesabia Muda na Mifumo tunayotumia kuutambua bado muda utakuepo na utaendelea kuuyoyoma kama kawaida..na hayo tutayashuhudia katka viumbe vyote vilivo hai ikiwemo sisi binadamu!

Kwan Madhara ya muda yataendelea kuonekana kama kuzaliwa, kukua, kuzeeka, kisha kufa ,kuoza, kupotelea

Kwa maelezo hayo naomba nikurudishe sasa kwene Muda!! Muda hauko kwene vitu,wala hauko kwene watu.Ila unaonekana kupitia matukio,Hivo hata watu wazamani sana waliweza kuhesabu muda kupitia matukio au majira au misimu. Misimu ya mvua,kiangazi,misimu ya joto au ya baridi,

Kifupi uhai uliambatanishwa na Muda!!…Tupo kwa sababu ya Muda lakini Muda haupo kwasababu ya uhai!!
Tuna exist katka certain interval ya muda!!..Muda hausimami wala haujirudii yanayojirudia n matukio
Wewe mutoa mada soma komenti ya huyu mwamba.
 
Mimi ninachoamini uhalisia wa future unaonekana na kujidhihirisha kwenye past, yaani baada ya kuisha muda wake ndio utaouona...so
Kulingana na wewe naweza kukubali na pia kukataa
--------------------------------

Kuna jina moja limenitoka, ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Albert eistein,
Yeye alikuja na 4 dimension yake kuipinga ile ya 3 dimension ya eistein kuwa

"matukio ya past na future yote ni ya kweli sawa.
Kwa sababu ya hili, hakuna wakati maalum unaoitwa "sasa"/present.

"There's no moment that is happening now".

Mtu anaweza kusema kuwa nothing is "happening" and there's nothing "becoming".
Hii ikiwa na mantiki ya kuwa Kila kitu, kutoka kwa vitu hadi matukio, kipo tu.
Na akamalizia kwa kusema
Our definition ya "sasa"/Now haipo katika Eternalist universe
-----------------------------
Huyo Mr.aliniacha na maswali mengi sana maana past na future vyote ni sawa kama alivyoelezea.
Ila kifikra zangu naona kabisa huwezi kuiona future bila kuanza na present/now, kisha present inageuka kuwa past hapo ndio ndomana nilisema kuwa sura iliyokuwa ya future ndio sura itakayoonekana kwenye past.

Sasa kwanini present isihusike hapo..?
Hakuna present kwa sababu kila kitokeacho tayari ni past. Huyo jamaa alikuwa sahihi kimtindo. Kuhusu future hiyo illusion tu haina maana kwamba inaweza kutokea.
 
Tukisema Mungu mwenye nguvu zote mmiliki wa hii dunia na ulimwengu wote alitumia muda wa siku saba kuumba hii dunia na ulimwengu wote tunakuwa tunakosea? Au wakati wa uumbaji hakukuwa na muda?
Kwanza inabidi uthibitishe huyo Mungu yupo na si zao la fikra zako tu.
 
Mungu yupo. Wewe dhibitisha kuwa hayupo.
Kwanza hujui tofauti ya dhibitisha na thibitisha.

Pili hujui kati ya anayesema Mungu yupo na anayebisha, nani ana "burden of proof" kuthibitisha.

Hujui mambo ya msingi kabisa katika kanuni za mijadala hii.

Hujathibitisha Mungu yupo.
 
Time exists only into this physical world.

Kiuhalisia hakuna maisha bila muda, na tulipo hapa kila kitu kimeisha, yaan namaanisha maisha haya tunayoyaish leo hii, tupo ktk Past, na roho zetu zilishayapita haya zipo ktk Future, kama nilivyosema muda una exist ktk ulimwengu huu wa mwili, na ktk Roho(unseen world) huko hakuna mpaka wa muda hivyo Roho zinauwezo wa kufanya tendo ambalo kimwil lingefanywa kwa maelfu ya miaka huko rohon likafanyika within the second(japo huko hakuna elimu ya muda hivyo huwez pima tukio kwa muda).

Ushahidi ni kwamba hata ndoto zako zinaproof sometime ukaota jambo fulan ambalo linakuja kukutokea miaka ya mbele, hiyo yote huwa ni taswira za matukio iliyopitia Roho yako na kuyaleta matukio hayo kwa nafsi yako kupitia ndoto ili yaendane na uelewa ama sheria za ulimwengu wa mwili.

Hata hao wanaofuatilia mambo ya time travel wajue kuwa haiwezekan na haitowai kuwezekana, maana dunian ukitaka kutravel in time unatakiwa uwe na mwili usioshikwa ama unaotawaliwa na sheria za muda, zaid unaweza travel in time kiroho tu.

Muda ukisimama basi hata maisha yatasimama.

Na ukitaka uusimamishe muda basi utatakiwa usimamishe saa kuu za dunia zinazotawala muda ambazo ni JUA na MWEZI,

Na ndiomaana huwa tunapinga kuwa hakuna pua ya mtu iliyowai kanyaga mwezini wala hakuna atakayeweza fika mwezini, kwakuwa mwezi ndio main controller wa muda, hivyo basi ukianza kuufuata ni sawa na kusogeza mbele muda wa maisha yako na kufikia limit ya maisha yako hivyo utafika ukiwa maiti mwezin ama ufike ukiwa mzee tofaut na ulivyoondoka dunian.

Muda hauwezi simama mpaka miili yetu ama maisha ya kidunia yatakapo reach point ya end of destination na kufikia ile level ya Roho zetu ziliko ambako hakuna sheria za muda na huko kila kitu kimekwisha.

Niishie hapa nisije wachanganya.
...Umeishatuchanganya! Mimi nlidhani JUA, na Sio MWEZI, ndio Mhimili Mkuu wa Muda??
 
Back
Top Bottom