Tukiondoa muda ni nini kinabaki?

Tukiondoa muda ni nini kinabaki?

Illusion kwa muktadha gani?

Kila kitu ni illusion, na kama kila kitu illusion, hakuna illusion.

Kwa sababu, ili illusion iwe illusion, inabidi iwe illusion relative to something that is not illusion.
dah hili kweli ni jukwaa la intelijensia!
 
Kinachoratibu muda ni mwezi au jua?
Hata vyote. Kitu chochote kinachoweza kuleta intervals za matukio unaweza kutumia kuratibu muda. Watu wa zamani walikuwa wanajaza maji kwenye chombo halafu wanatoboa tundu dogo, intervals za kupungua kwa maji zilitumika kuratibu muda.
 
dah hili kweli ni jukwaa la intelijensia!
Umeelewa hoja yangu mkuu?

Even nothingness is nothingness with relation to something, you can't have nothingness without something.

Even the very concept of nothingness is something apart from nothingness itself.

Just like the concept of you is something different from you.
 
Time exists only into this physical world.

Kiuhalisia hakuna maisha bila muda, na tulipo hapa kila kitu kimeisha, yaan namaanisha maisha haya tunayoyaish leo hii, tupo ktk Past, na roho zetu zilishayapita haya zipo ktk Future, kama nilivyosema muda una exist ktk ulimwengu huu wa mwili, na ktk Roho(unseen world) huko hakuna mpaka wa muda hivyo Roho zinauwezo wa kufanya tendo ambalo kimwil lingefanywa kwa maelfu ya miaka huko rohon likafanyika within the second(japo huko hakuna elimu ya muda hivyo huwez pima tukio kwa muda).

Ushahidi ni kwamba hata ndoto zako zinaproof sometime ukaota jambo fulan ambalo linakuja kukutokea miaka ya mbele, hiyo yote huwa ni taswira za matukio iliyopitia Roho yako na kuyaleta matukio hayo kwa nafsi yako kupitia ndoto ili yaendane na uelewa ama sheria za ulimwengu wa mwili.

Hata hao wanaofuatilia mambo ya time travel wajue kuwa haiwezekan na haitowai kuwezekana, maana dunian ukitaka kutravel in time unatakiwa uwe na mwili usioshikwa ama unaotawaliwa na sheria za muda, zaid unaweza travel in time kiroho tu.

Muda ukisimama basi hata maisha yatasimama.

Na ukitaka uusimamishe muda basi utatakiwa usimamishe saa kuu za dunia zinazotawala muda ambazo ni JUA na MWEZI,

Na ndiomaana huwa tunapinga kuwa hakuna pua ya mtu iliyowai kanyaga mwezini wala hakuna atakayeweza fika mwezini, kwakuwa mwezi ndio main controller wa muda, hivyo basi ukianza kuufuata ni sawa na kusogeza mbele muda wa maisha yako na kufikia limit ya maisha yako hivyo utafika ukiwa maiti mwezin ama ufike ukiwa mzee tofaut na ulivyoondoka dunian.

Muda hauwezi simama mpaka miili yetu ama maisha ya kidunia yatakapo reach point ya end of destination na kufikia ile level ya Roho zetu ziliko ambako hakuna sheria za muda na huko kila kitu kimekwisha.

Niishie hapa nisije wachanganya.
Bado tu hujapewa ulinzi Chifu ?
 
Katika kitu sijaelewa mnazungumzia muda kwa mantiki ipi yaani huu wa saa au tuna zungumzia wakati yaani mchana na usiku

Kama ni muda yaani huu wa saa nitoe mfano chukulia upo gerezani au sehemu yoyote tu ......... simu inaita ngoja nipokee kwanza nakuja
 
natumia simu napata tabu kutaka kuandika maelezo yangu
 
Umeelewa hoja yangu mkuu?

Even nothingness is nothingness with relation to something, you can't have nothingness without something.

Even the very concept of nothingness is something apart from nothingness itself.

Just like the concept of you is something different from you.
Nakuelewa kwa namna ya uelewa wenyewe
 
Wakuu naombeni mnifungue akili katika hili limenifikirisha mno, imewezekana vipi. Future iwe ndio hiyohiyo past, future ndio inajijengea past, palipo na future ndipo miguu ya past ilipo hapohapo, na ukiangalia past utaweza kujikuta umejenga future.

Deep down katika kufikiri nauona muonekano halisi wa future unajidhihirisha kwenye past, maana haiwezekani kuiona future ukiwa upo kwenye future mpaka ifikie kuwa past, na ukirudi nyuma kwenye past hiyohiyo, utajiona ulikuwa kwenye future pia kwa nyakati hiyo.

Na inafahamika kuwa hakuna future bila present na hakuna past bila ya present kuhusika katika wakati huo.

Unajua muda huu naandika nipo kwenye present, na ndani ya muda huu nipo pia kwenye past ambayo ilikuwa future na kisha future itanigeukia tena kuwa past baada ya muda huu huu kuupita.

Ni kitu cha ajabu sana kwamba hata kabla ya kusukwa kwa mfumo wa muda, binadamu wa kwanza waliweza kujua nyakati walizokuwa wakifanya jambo na baada ya jambo hilo kupita kufanywa, lakini hakukuwa na mtu wala kitu chenye kuwaaminisha kuwa huo ndio muda.

Kama binadamu wa kipindi cha kabla ya kuundwa kwa mfumo wa muda na nyakati, waliweza kuishi kwa namna hii ninayoiona ni ya ajabu kwangu na pengine haikuwa ajabu kwao na haikuwafaidisha wala kupatwa na hasara isiyotokana na kuutambua muda kwa wakati huo.

Ni vipi sisi binadamu wa sasa tukiuondoa huu mfumo tambuzi wa muda tuliojitengenezea? Nini kitatuzuia?

Ni madhara ya aina gani tunaweza kuyapata ikiwa wakale hawakuyapata na haikuwanyima dhima ya kuishi bila kuutambua muda wao?
"The advantage of having time is so that not all things occurs at the same time"
 
Muda kama tunavyoufahamu ni kiinimacho tu (an illusion). Upo kama haupo. Wakati uliopita, uliopo na ujao vyote ni maono ya binadamu tu ili aweze kuuelewa uwepo wake. Yupo kama hayupo!

Uwepo wa muda unategemea na spidi yako unayosafiri. Ukisafiri kwa kasi sana kukaribia spidi ya mwanga (haiwezekani kwa kitu chenye mass kuifikia kasi ya mwanga) muda unadorora na unakwenda polepole mno kiasi kwamba baada ya muda hutaweza kutofautisha kati ya wakati uliomo, uliopita na ujao. Na ukiwa na bahati mbaya ukavuka event horizon na kudumbukia kwenye black hole basi huko hakuna muda. Ni uwepo tu! Ni milele! Muda haupo!

Mambo haya ni mazito sana na ukiyafikiria kwa kina kichwa kinaweza kupata moto. Hebu jaribu kufikiria. Muda ulianza lini? Nani aliuanzisha? Na kabla ya muda kulikuwa na nini? Muda ni nini?

Ngoja nijipikilishe kiugali hapa nitarudi.
Mwanga husafiri kwa particle iitwayo photon nayo inaweza kupimwa mass yake ndio maana wazungu wanajaribu kuunda space ship yenye spidi ya mwanga.
 
Hebu mkuu nieleweshe ukisafiri wka kasi kwenda wapi? Utashindwa kutofautisha kwa sababu uko speed sana au vipi?

Black hole iko wapi? Kuna mtu amewah kudumbukia huko?

Hizi mambo naonaga kwnye movies za avengers.. hebu nieleweshe tafadhali
Hata mimi nimejiuliza,kwa mfano ukisafiri kwa spidi ya mwanga kwenda adromeda alpha centauri utatumia miaka minne ya mwanga sasa huo sio muda ?
 
hakuna kitu kina itwa future , future ni illusion tu , mambo wakati sahihi ni sasa , ukishasema nitanunua gari tayari umetengeneza illusion kwenye kichwa chako sio reality , ninanunua gari ndio jambo la kwel fture nikuudanganya ubongo wako tu .
Kwahiyo rais ajaye baada ya samia tayari anatawala au atakuja kutawala baade baada ya samia
 
nu sawa kabsa una vyozungumza ila future ina baki kuwa jambo ambalo sio reality ni dhana tu
Ni dhana lakini baade itafika itakua reality kama unavyosubiri kifo chako
 
Athari zitakazo tokea ni kwenye utendaji wa kila cku wa maisha ya binadam mfano. Hautajua kam imebaki lisaa moja giza liingie. Kwa wanafunzi hautajua sas ni wakat wa kwenda nyumbn
Inshort ile time frame ya kufany kazi au majukum flan itatushinda ku control titarud kweny analogue kam zaman yan mtu unfanya jambo kwa approxmataion bila kuwa na uhakika
Kwahiyo muda utakuwepo ila tu itakua ngumu kuucalculate
 
Hata mimi nimejiuliza,kwa mfano ukisafiri kwa spidi ya mwanga kwenda adromeda alpha centauri utatumia miaka minne ya mwanga sasa huo sio muda ?
Hapo muda utakuwa umefreeze kwa hiyo speed mkuu
 
Back
Top Bottom