Tukiondoa muda ni nini kinabaki?

Tukiondoa muda ni nini kinabaki?

SPYnoCODE

Senior Member
Joined
Jun 3, 2022
Posts
151
Reaction score
275
Wakuu naombeni mnifungue akili katika hili limenifikirisha mno, imewezekana vipi. Future iwe ndio hiyohiyo past, future ndio inajijengea past, palipo na future ndipo miguu ya past ilipo hapohapo, na ukiangalia past utaweza kujikuta umejenga future.

Deep down katika kufikiri nauona muonekano halisi wa future unajidhihirisha kwenye past, maana haiwezekani kuiona future ukiwa upo kwenye future mpaka ifikie kuwa past, na ukirudi nyuma kwenye past hiyohiyo, utajiona ulikuwa kwenye future pia kwa nyakati hiyo.

Na inafahamika kuwa hakuna future bila present na hakuna past bila ya present kuhusika katika wakati huo.

Unajua muda huu naandika nipo kwenye present, na ndani ya muda huu nipo pia kwenye past ambayo ilikuwa future na kisha future itanigeukia tena kuwa past baada ya muda huu huu kuupita.

Ni kitu cha ajabu sana kwamba hata kabla ya kusukwa kwa mfumo wa muda, binadamu wa kwanza waliweza kujua nyakati walizokuwa wakifanya jambo na baada ya jambo hilo kupita kufanywa, lakini hakukuwa na mtu wala kitu chenye kuwaaminisha kuwa huo ndio muda.

Kama binadamu wa kipindi cha kabla ya kuundwa kwa mfumo wa muda na nyakati, waliweza kuishi kwa namna hii ninayoiona ni ya ajabu kwangu na pengine haikuwa ajabu kwao na haikuwafaidisha wala kupatwa na hasara isiyotokana na kuutambua muda kwa wakati huo.

Ni vipi sisi binadamu wa sasa tukiuondoa huu mfumo tambuzi wa muda tuliojitengenezea? Nini kitatuzuia?

Ni madhara ya aina gani tunaweza kuyapata ikiwa wakale hawakuyapata na haikuwanyima dhima ya kuishi bila kuutambua muda wao?
 
Hamna mtu alie umfumo wa muda na wakati. kila kitu kipo we ni kujifunza tu. kwa ishu ya past,future na present kuwa at the same time ni kutokama na theory kwamba dunia yetu ni simulation matrix nothing is real just a video game, human we just follow the game rules to survive but all missions are there waiting us.3D is nothing thus why the 4D called the dimension of time where at leat we can talk.
 
Muda ni Kama hela ya kununulia maisha ukitoa muda jua na wewe umekwisha ( wakati wako ).
Kuna vitu Dunia haiwezi vikwepa
1.Muda
2.Mabadiliko.
Hata Biblia iliongelea kuumbwa kwa Nuru ikaitwa mchana na Giza kuitwa usiku ... Utagundua hapa ziliongelewa nyakati na mabadiliko yake.
 
Time exists only into this physical world.

Kiuhalisia hakuna maisha bila muda, na tulipo hapa kila kitu kimeisha, yaan namaanisha maisha haya tunayoyaish leo hii, tupo ktk Past, na roho zetu zilishayapita haya zipo ktk Future, kama nilivyosema muda una exist ktk ulimwengu huu wa mwili, na ktk Roho(unseen world) huko hakuna mpaka wa muda hivyo Roho zinauwezo wa kufanya tendo ambalo kimwil lingefanywa kwa maelfu ya miaka huko rohon likafanyika within the second(japo huko hakuna elimu ya muda hivyo huwez pima tukio kwa muda).

Ushahidi ni kwamba hata ndoto zako zinaproof sometime ukaota jambo fulan ambalo linakuja kukutokea miaka ya mbele, hiyo yote huwa ni taswira za matukio iliyopitia Roho yako na kuyaleta matukio hayo kwa nafsi yako kupitia ndoto ili yaendane na uelewa ama sheria za ulimwengu wa mwili.

Hata hao wanaofuatilia mambo ya time travel wajue kuwa haiwezekan na haitowai kuwezekana, maana dunian ukitaka kutravel in time unatakiwa uwe na mwili usioshikwa ama unaotawaliwa na sheria za muda, zaid unaweza travel in time kiroho tu.

Muda ukisimama basi hata maisha yatasimama.

Na ukitaka uusimamishe muda basi utatakiwa usimamishe saa kuu za dunia zinazotawala muda ambazo ni JUA na MWEZI,

Na ndiomaana huwa tunapinga kuwa hakuna pua ya mtu iliyowai kanyaga mwezini wala hakuna atakayeweza fika mwezini, kwakuwa mwezi ndio main controller wa muda, hivyo basi ukianza kuufuata ni sawa na kusogeza mbele muda wa maisha yako na kufikia limit ya maisha yako hivyo utafika ukiwa maiti mwezin ama ufike ukiwa mzee tofaut na ulivyoondoka dunian.

Muda hauwezi simama mpaka miili yetu ama maisha ya kidunia yatakapo reach point ya end of destination na kufikia ile level ya Roho zetu ziliko ambako hakuna sheria za muda na huko kila kitu kimekwisha.

Niishie hapa nisije wachanganya.
 
Makala yako imejaa ufahamu muhimu sana. Ingawawengi wa Watanzania hukwepa kujadili mada kama hizi ambazo ninanukia imposibility.

Wanadamu sisi ndo tuliweka hesabu za muda. Ingawa Nature yaani Muumbaji alituwekea kitu kinachoitwa MAJIRA au NYAKATI ambapo kila hesabu ya muda inafit humo.

Hebu tujiulize kuhusu siku za mzunguko wa mwezi yaani month. Mwezi February umekuwaje mfupi kuliko miezi yote? Zile siku 31 au 30 za miezi mingine zilipimwaje?

Nawaza kwamba tunaweza kugundua kitu kwenye hii mada yako lakini inahitaji tafakuri deep
 
Yes! Hapo kwenye hesabu ndipo nilipolenga, ukiangazia hapo awali kuna watu walikuwepo na waliishi vizuri kwa namna wanayoijua wao bila kuutambua muda ili kuendana nao na kabla ya hizo hesabu za kwenda na muda

Suala zito linabakia kwa dunia ya sasa tukiondoa hizi hesabu za muda itatunyima kuishi?
 
Kijana chukua hii kuhusu muda.
1. Muda ni kiumbe.
2. Kila sehemu(space) yenye nafasi kuna muda.
3. Tuuondoe kwanza hup muda tuone kitatokea nini.
Labda utuelezee kwa faida ya wote,
1.ulishawahi kukiona kiumbe muda na kinafaniaje
2.kinaishi wapi ?
 
Muda kama tunavyoufahamu ni kiinimacho tu (an illusion). Upo kama haupo. Wakati uliopita, uliopo na ujao vyote ni maono ya binadamu tu ili aweze kuuelewa uwepo wake. Yupo kama hayupo!

Uwepo wa muda unategemea na spidi yako unayosafiri. Ukisafiri kwa kasi sana kukaribia spidi ya mwanga (haiwezekani kwa kitu chenye mass kuifikia kasi ya mwanga) muda unadorora na unakwenda polepole mno kiasi kwamba baada ya muda hutaweza kutofautisha kati ya wakati uliomo, uliopita na ujao. Na ukiwa na bahati mbaya ukavuka event horizon na kudumbukia kwenye black hole basi huko hakuna muda. Ni uwepo tu! Ni milele! Muda haupo!

Mambo haya ni mazito sana na ukiyafikiria kwa kina kichwa kinaweza kupata moto. Hebu jaribu kufikiria. Muda ulianza lini? Nani aliuanzisha? Na kabla ya muda kulikuwa na nini? Muda ni nini?

Ngoja nijipikilishe kiugali hapa nitarudi.
 
Time exists only into this physical world.

Kiuhalisia hakuna maisha bila muda, na tulipo hapa kila kitu kimeisha, yaan namaanisha maisha haya tunayoyaish leo hii, tupo ktk Past, na roho zetu zilishayapita haya zipo ktk Future, kama nilivyosema muda una exist ktk ulimwengu huu wa mwili, na ktk Roho(unseen world) huko hakuna mpaka wa muda hivyo Roho zinauwezo wa kufanya tendo ambalo kimwil lingefanywa kwa maelfu ya miaka huko rohon likafanyika within the second(japo huko hakuna elimu ya muda hivyo huwez pima tukio kwa muda).

Ushahidi ni kwamba hata ndoto zako zinaproof sometime ukaota jambo fulan ambalo linakuja kukutokea miaka ya mbele, hiyo yote huwa ni taswira za matukio iliyopitia Roho yako na kuyaleta matukio hayo kwa nafsi yako kupitia ndoto ili yaendane na uelewa ama sheria za ulimwengu wa mwili.

Hata hao wanaofuatilia mambo ya time travel wajue kuwa haiwezekan na haitowai kuwezekana, maana dunian ukitaka kutravel in time unatakiwa uwe na mwili usioshikwa ama unaotawaliwa na sheria za muda, zaid unaweza travel in time kiroho tu.

Muda ukisimama basi hata maisha yatasimama.

Na ukitaka uusimamishe muda basi utatakiwa usimamishe saa kuu za dunia zinazotawala muda ambazo ni JUA na MWEZI,

Na ndiomaana huwa tunapinga kuwa hakuna pua ya mtu iliyowai kanyaga mwezini wala hakuna atakayeweza fika mwezini, kwakuwa mwezi ndio main controller wa muda, hivyo basi ukianza kuufuata ni sawa na kusogeza mbele muda wa maisha yako na kufikia limit ya maisha yako hivyo utafika ukiwa maiti mwezin ama ufike ukiwa mzee tofaut na ulivyoondoka dunian.

Muda hauwezi simama mpaka miili yetu ama maisha ya kidunia yatakapo reach point ya end of destination na kufikia ile level ya Roho zetu ziliko ambako hakuna sheria za muda na huko kila kitu kimekwisha.

Niishie hapa nisije wachanganya
Mkuu shukrani sana.

Moja kwa moja hilo la kwenda mwezini limenikuna kichwa kwakweli

Tukirudi kwenye namna ya kuundoa muda si suala la wanadam wote kukubaliana kwa siku moja , ni kitu ambacho kitachukua muda sana na ndani ya muda huo huo tutakuwa tuna toa kitu kimoja kimoja kwenye dhana ya muda mwisho tufikie uhalisi wa maisha wa wakati ule katika wakti huu.....sijui km umeipanta point yangu vizuri mkuu.

(Mf. Huwezi kubomoa ofisi ya ghorofa lililo kwenye makazi ya watu kwa kulianzia chini, bali utaanzia juu kushuka chini kwa kubomoa tofali moja moja.
 
Wakuu naombeni mnifungue akili katika hili limenifikirisha mno , imewezekana vipi....;
future iwe ndio hiyohiyo past , future ndio inajijengea past ,palipo na future ndipo miguu ya past ilipo hapohapo, na ukiangalia past utaweza kujikuta umejenga future.

deep down katika kufikiri nauona muonekano halisi wa future unajidhihirisha kwenye past,
maana haiwezekani kuiona future ukiwa upo kwenye future mpaka ifikie kuwa past,
na ukirudi nyuma kwenye past hiyohiyo, utajiona ulikuwa kwenye future pia kwa nyakati hiyo.

Na inafahamika kuwa hakuna future bila present na hakuna past bila ya present kuhusika katika wakati huo .....

unajua Muda huu naandika nipo kwenye present, na ndani ya muda huu nipo pia kwenye past ambayo ilikuwa future na kisha future itanigeukia tena kuwa past baada ya muda huu huu kuupita ....

Ni kitu cha ajabu sana kwamba hata kabla ya kusukwa kwa mfumo wa muda, binadamu wa kwanza waliweza kujua nyakati walizokuwa wakifanya jambo na baada ya jambo hilo kupita kufanywa, lakini hakukuwa na mtu wala kitu chenye kuwaaminisha kuwa huo ndio muda

Kama binadamu wa kipindi cha kabla ya kuundwa kwa mfumo wa muda na nyakati, waliweza kuishi kwa namna hii ninayoiona ni ya ajabu kwangu na pengine haikuwa ajabu kwao na haikuwafaidisha wala kupatwa na hasara isiyotokana na kuutambua muda kwa wakati huo...

Ni vipi sisi binadam wa sasa tukiuondoa huu mfumo tambuzi wa muda tuliojitengenezea ? Nini kitatuzuia ?
Ni madhara ya aina gani tunaweza kuyapata ikiwa wakale hawakuyapata na haikuwanyima dhima ya kuishi bila kuutambua Muda wao !!?

Mkuu
Ebu nikwambie kitu “Huwezi kuuondoa Muda”!!

Lakini nitakujibu kadiri ww unavyomaanisha na kudhani!
Ni ukweli kua ww unadhan muda umetengenezwa…La hasha…hyo si kweli hata kidogo !! Binadamu ametengeneza vifaa vya uhesabia muda na namna ya kuuhesabu hapa tunaongelea saa,simu ,kalenda, na vitu vyote vinavohesabu muda (LAKINI HIVI SI MUDA na wala haviathiri muda wenyewe)

Pia yawezekana wewe umejikita kwene Namna ya uhesabuji wa muda ambao ni universal au hata wa jamii fulani!! mfano siku,week,mwezi,mwaka nk na majina yake jumatatu jumanne…jumapil

KWA MANTIKI HIYO UNAWEZA UKAWA SAHIHI KWAMBA HIVI VINAWEZA VIKAONDOLEWA NA WALA HAVITAATHIRI MUDA.. ingawa vitaathiri uelewa wetu na namna tulivokua tunaitofautisha jana na leo na kesho, saa moja na nyingine, mwaka mmoja na mwingine.Hata hivo hata kama vitatolewa vifaa vya kuhesabia Muda na Mifumo tunayotumia kuutambua bado muda utakuepo na utaendelea kuuyoyoma kama kawaida..na hayo tutayashuhudia katka viumbe vyote vilivo hai ikiwemo sisi binadamu!

Kwan Madhara ya muda yataendelea kuonekana kama kuzaliwa, kukua, kuzeeka, kisha kufa ,kuoza, kupotelea

Kwa maelezo hayo naomba nikurudishe sasa kwene Muda!! Muda hauko kwene vitu,wala hauko kwene watu.Ila unaonekana kupitia matukio,Hivo hata watu wazamani sana waliweza kuhesabu muda kupitia matukio au majira au misimu. Misimu ya mvua,kiangazi,misimu ya joto au ya baridi,

Kifupi uhai uliambatanishwa na Muda!!…Tupo kwa sababu ya Muda lakini Muda haupo kwasababu ya uhai!!
Tuna exist katka certain interval ya muda!!..Muda hausimami wala haujirudii yanayojirudia n matukio
 
Kwanini
Muda kama tunavyoufahamu ni kiinimacho tu (an illusion). Upo kama haupo. Wakati uliopita, uliopo na ujao vyote ni maono ya binadamu tu ili aweze kuuelewa uwepo wake. Yupo kama hayupo!

Uwepo wa muda unategemea na spidi yako unayosafiri. Ukisafiri kwa kasi sana kukaribia spidi ya mwanga (haiwezekani kwa kitu chenye mass kuifikia kasi ya mwanga) muda unadorora na unakwenda polepole mno kiasi kwamba baada ya muda hutaweza kutofautisha kati ya wakati uliomo, uliopita na ujao. Na ukiwa na bahati mbaya ukavuka event horizon na kudumbukia kwenye black hole basi huko hakuna muda. Ni uwepo tu! Ni milele! Hakuna muda!

Mambo haya ni mazito sana na ukiyafikiria kwa kina kichwa kinaweza kupata moto. Hebu jaribu kufikiria. Muda ulianza lini? Nani aliuanzisha. Na kabla ya muda kulikuwa na nini? Muda ni nini?

Ngoja nijipikilishe kiugali hapa nitarudi.

Misungwi hoyee!!!
Kwanini tunajipa nguvu kwa kuamini kuwa kwenye roho hakuna muda

ni vipi km upo na pengine kuna hesabu zao za kuendana nao.

Fikra zangu zinaniambia ni km vile muda una relate uungu. (Kuna uungu ndani ya muda) kwa maana upo ulikuwepo na utaendelea kuwepo.

Ila suala la kuendelea kuwepo liko juu ya akili zetu za ubinadam sababu hatujafika katika uhalisia na katika roho muda upo pia kwa namna yake.
 
Kwanini

Kwanini tunajipa nguvu kwa kuamini kuwa kwenye roho hakuna muda,
ni vipi km upo na pengine kuna hesabu zao za kuendana nao...
Fikra zangu zinaniambia ni km vile muda una relate uungu. (Kuna uungu ndani ya muda) kwa maana upo ulikuwepo na utaendelea kuwepo
Ila suala la kuendelea kuwepo liko juu ya akili zetu za ubinadam sababu hatujafika katika uhalisia na katika roho muda upo pia kwa namna yake...
Mimi sijagusia mambo ya kiroho. Na ukiingiza mambo ya kiroho na Mungu mjadala utaharibika maana hayo hayathibitiki!
 
Mkuu
Ebu nikwambie kitu “Huwezi kuuondoa Muda”!!

Lakini nitakujibu kadiri ww unavyomaanisha na kudhani!
Ni ukweli kua ww unadhan muda umetengenezwa…La hasha…hyo si kweli hata kidogo !! Binadamu ametengeneza vifaa vya uhesabia muda na namna ya kuuhesabu hapa tunaongelea saa,simu ,kalenda, na vitu vyote vinavohesabu muda (LAKINI HIVI SI MUDA na wala haviathiri muda wenyewe)

Pia yawezekana wewe umejikita kwene Namna ya uhesabuji wa muda ambao ni universal au hata wa jamii fulani!! mfano siku,week,mwezi,mwaka nk na majina yake jumatatu jumanne…jumapil

KWA MANTIKI HIYO UNAWEZA UKAWA SAHIHI KWAMBA HIVI VINAWEZA VIKAONDOLEWA NA WALA HAVITAATHIRI MUDA.. ingawa vitaathiri uelewa wetu na namna tulivokua tunaitofautisha jana na leo na kesho, saa moja na nyingine, mwaka mmoja na mwingine.Hata hivo hata kama vitatolewa vifaa vya kuhesabia Muda na Mifumo tunayotumia kuutambua bado muda utakuepo na utaendelea kuuyoyoma kama kawaida..na hayo tutayashuhudia katka viumbe vyote vilivo hai ikiwemo sisi binadamu!

Kwan Madhara ya muda yataendelea kuonekana kama kuzaliwa, kukua, kuzeeka, kisha kufa ,kuoza, kupotelea

Kwa maelezo hayo naomba nikurudishe sasa kwene Muda!! Muda hauko kwene vitu,wala hauko kwene watu.Ila unaonekana kupitia matukio,Hivo hata watu wazamani sana waliweza kuhesabu muda kupitia matukio au majira au misimu. Misimu ya mvua,kiangazi,misimu ya joto au ya baridi,

Kifupi uhai uliambatanishwa na Muda!!…Tupo kwa sababu ya Muda lakini Muda haupo kwasababu ya uhai!!
Tuna exist katka certain interval ya muda!!..Muda hausimami wala haujirudii yanayojirudia n matukio
Mkuu, maelezo yako ndyo itakuwa back up yangu, ngoja niingie chimbo panapo majaliwa ntarudi lakn ntaanzia hapo

Ila kwa sasa chukua Like yangu kwanza.
 
1. Ushawahi kuiona njaa ?
2. Popote penye nafasi muda upo na unaishi.

Mkuu
Ebu nikwambie kitu “Huwezi kuuondoa Muda”!!

Lakini nitakujibu kadiri ww unavyomaanisha na kudhani!
Ni ukweli kua ww unadhan muda umetengenezwa…La hasha…hyo si kweli hata kidogo !! Binadamu ametengeneza vifaa vya uhesabia muda na namna ya kuuhesabu hapa tunaongelea saa,simu ,kalenda, na vitu vyote vinavohesabu muda (LAKINI HIVI SI MUDA na wala haviathiri muda wenyewe)

Pia yawezekana wewe umejikita kwene Namna ya uhesabuji wa muda ambao ni universal au hata wa jamii fulani!! mfano siku,week,mwezi,mwaka nk na majina yake jumatatu jumanne…jumapil

KWA MANTIKI HIYO UNAWEZA UKAWA SAHIHI KWAMBA HIVI VINAWEZA VIKAONDOLEWA NA WALA HAVITAATHIRI MUDA.. ingawa vitaathiri uelewa wetu na namna tulivokua tunaitofautisha jana na leo na kesho, saa moja na nyingine, mwaka mmoja na mwingine.Hata hivo hata kama vitatolewa vifaa vya kuhesabia Muda na Mifumo tunayotumia kuutambua bado muda utakuepo na utaendelea kuuyoyoma kama kawaida..na hayo tutayashuhudia katka viumbe vyote vilivo hai ikiwemo sisi binadamu!

Kwan Madhara ya muda yataendelea kuonekana kama kuzaliwa, kukua, kuzeeka, kisha kufa ,kuoza, kupotelea

Kwa maelezo hayo naomba nikurudishe sasa kwene Muda!! Muda hauko kwene vitu,wala hauko kwene watu.Ila unaonekana kupitia matukio,Hivo hata watu wazamani sana waliweza kuhesabu muda kupitia matukio au majira au misimu. Misimu ya mvua,kiangazi,misimu ya joto au ya baridi,

Kifupi uhai uliambatanishwa na Muda!!…Tupo kwa sababu ya Muda lakini Muda haupo kwasababu ya uhai!!
Tuna exist katka certain interval ya muda!!..Muda hausimami wala haujirudii yanayojirudia n matukio
Yes nakuelewa sana
 
Muda kama tunavyoufahamu ni kiinimacho tu (an illusion). Upo kama haupo. Wakati uliopita, uliopo na ujao vyote ni maono ya binadamu tu ili aweze kuuelewa uwepo wake. Yupo kama hayupo!

Uwepo wa muda unategemea na spidi yako unayosafiri. Ukisafiri kwa kasi sana kukaribia spidi ya mwanga (haiwezekani kwa kitu chenye mass kuifikia kasi ya mwanga) muda unadorora na unakwenda polepole mno kiasi kwamba baada ya muda hutaweza kutofautisha kati ya wakati uliomo, uliopita na ujao. Na ukiwa na bahati mbaya ukavuka event horizon na kudumbukia kwenye black hole basi huko hakuna muda. Ni uwepo tu! Ni milele! Muda haupo!

Mambo haya ni mazito sana na ukiyafikiria kwa kina kichwa kinaweza kupata moto. Hebu jaribu kufikiria. Muda ulianza lini? Nani aliuanzisha? Na kabla ya muda kulikuwa na nini? Muda ni nini?

Ngoja nijipikilishe kiugali hapa nitarudi.
Vipi kama mwengine akisema muda ni matukio?

Mchana ni tukio, usiku ni tukio na tunaona haya matukio yakipishana. Matukio yakamfanya binadamu aunde nadharia kwa kulingana na matukio husika. Binadamu akaunda muda.

Tu-assume kama ingelikuwa ni mchana tu pasipo usiku au ni usiku tu pasipo mchana pengine tungehesabu kuwa tuna muda?

Kwa maana hiyo kama hakuna matukio-hakuna muda! Ikiwa mleta Uzi anauliza ukiondoa muda kutabakiwa na nini? Kitakachobaki ni umilele kwa hali ileile iliyokuwa.
 
Back
Top Bottom