'Tukio' la Mzee Harry Kitilya limenifikirisha sana. Wenye nafasi za kiuongozi kuweni makini!

Huyo bwana anashtakiwa kwa makosa aliyoyafanya baada ya kustaafu. kimsingi kwa nafasi aliyokuwa nayo TRA, baada ya kustaafu ingelifaa sana Taifa kama angejikita kwenye maswala ya kusaidia jamii. Lakini yeye akajitika kwenye maswala ya wizi.

Alichokifanya kitila ni kitu kibaya sana, kwa umri wake na kwa nafasi aliyokuwa nayo katika Taifa, ukizingatia na hali halisi ya kifedha ya Taifa letu yawezekana alipokuwa TRA alikuwa akijihusisha na maswala ya wizi, ndio maana watu wengi sana chini yake wakawa weziwezi.

amechuma alichokipanda.
 
Kiukweli Mkuu, hueleweki!
Viumbe vyote vilivyolaaniwa hufanya jitihada kusambaratisha Taifa kwa kutumia makabila, itikadi Na imani. Tuwaepuke viumbe hao kwani nia yao ni kuvunja umoja wetu wa Kitaifa ili adui zetu watushinde kwa urahisi.
Tuwaepuke na kuwawekea alama ili watambulike popote waendapo ndani na nje ya nchi kuwa ni sumu usiofaa kuonjwa na walio hai.
 
Mkuu, kwa hiyo watu wasiwe na makabila au imani wala itikadi? au sijaelewa
 
Wakili Petro E. Mselewa nionavyo mwenendo wa kesi hii, niliposoma gazeti la mwananchi juzi, mashaidi waliulizwa kwanini waziri as fedha mustafa mkulo hakyshitakiwa, ? Wakasema hawafahamu walifuata vigezo gani, na masumbuko lamwai aliikumbusha mahakama pesa wanazodaiwa kuziiba ziliishalipwa na bank, hivyo kuona walishitakiwa kwa chuki ya kisiasa tu, wataachiwa huru.
Sasa wakiachiwa huru serikali inawalipa au inafanyaje kufidia muda iliyowapotezea?!
 
Wakiachiwa huru wanaweza kufungua shauri la madai la kushtakiwa kwa hila. Wakishinda shauri hilo la madai waweza kulipwa fidia.
 
Kwanza, nawasalimu waungwana wote wa Jamiiforums. Pili, nakiri kuwa jambo ninalotaka kuliandika hapa limetokea juma linaloisha (Alhamisi). Nimechelewa kuandika hapa kwakuwa nilijipa nafasi ya kutafakari vya kutosha. Nimejifunza jambo kubwa kwenye maisha yangu.

Alhamisi ya tarehe 11 mwezi huu majira ya saa mbili na robo asubuhi nilikuwa kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutekeleza majukumu yangu ya kikazi. Nilikuwa nimeambatana na Profesa mmoja wa UDSM (jina kapuni) ambaye alikuwa mteja wangu na shahidi yangu siku hiyo mahakamani hapo kwenye shauri lililonipeleka.

Mimi na Profesa tukiwa tunaingia mlango wa Mahakama husika (mlango mkuu), gari ndogo ya Magereza ya pickup ilikuwa ikirudi nyuma kutoka Mahakamani hapo. Ndani ya gari hiyo kulikuwa na Washtakiwa/Mahabusu wawili walioketishwa chini kwenye gari hilo kwa nyuma. Mmojawapo alikuwa Mzee Harry Kitilya, Kamishna Jenerali wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aka TRA.

Ilikuwa ni kama tunapishana na gari hilo. Mzee Kitilya alipomuona Profesa anayefahamiana naye (akijitahidi kuchangamka na kusahau kwa muda maswahibu yake) alimwita Profesa kwa jina na kumsalimu. Akajitahidi kumfahamisha na mwenzake kuwa yule ni Profesa na ni rafikiye. Hakujali hata askari wa Magereza waliokuwa wamewasimamia kiulinzi. Kwa bahati njema,dereva alisimama kwa muda 'kuruhusu' salamu hiyo.

Baada ya salamu, Profesa akamwambia Mzee Kitilya: Pole. Akionekana kusawajika, kutamani kuwa nje ya gari ile huru kama mwanzoni na mwenyewe kujiamulia cha kufanya na kusema, Mzee Kitilya akajibu: Asante Profesa, tupo! Gari ikamalizia kona na kuondoka.

Mzee Harry Kitilya alikuwa Mkuu wa TRA iliyokusanya kodi nyingi nchini zilizojenga na kulipia mambo mbalimbali ya kiserikali. Alikuwa Mkuu wa wakusanya mapato ya Serikali na alifanya aliloliweza. Alikuwa akiheshimiwa na wadogo kwa wakubwa wa nchi hii na wakati mwingine kuogopwa. Leo yuko kwenye hali ile.

Ikiwa mti mbichi unatendwa vile, itakuwaje kwa miti mikavu? Nawasihi viongozi mbalimbali waweke akiba ya maneno na matendo yao. Maisha hayana formula!
Kwa hiyo unataka kutuambia kuwa kama ukia mtendaji mkuu wa serikali ukifanya mazuri mengi ndio iwe kinga ya kufanya makosa?" Degree za mansese tabu sana" acha mahakama iamue kama ana kosa au la!
 
Tangu nimekuoa numeona katika mafisadi 10 lazima 6wawe wachaga na ukumbuke wachaga ni kabila dogo tu wangekuwa kama waha au wasukuma nchi hii ingeisha
Sasa hapa issue ya ukabila imetokea wapi...huoni kwamba wewe una changamoto ya ubaguzi...Mungu akusaidie sana....Kama una chuki binafsi na hao watu baki nazo usiziweke hapa kwenye kadamnasi...Watanzania hatukabali tena kugawanywa kwa chuki za kikabila, kikanda na kidini....Mungu akusaidie uachane na hiyo chuki na ubaguzi uliokujaa...
Kongole kwa mtoa mada amejaribu kwa nafasi yake kueleza kinagaubaga kwamba viongozi jamani kuwe makini....madaraka ni dhamana...leo upo kesho haupo...tenda wema nenda zako....kuna msemo wa lugha iliyokuja na meli unasema:.."Be good to people when you go up,they will be good to you when you come down"....Na kamwe tukwepe kukomoana....au kulipiza kisasi....Kisasi ni cha Mungu asema Bwana wa Majeshi.
 
Walikwisha ruka daraja hao wachaga. Kinachofanyika sasa ni kuvunja daraja ili kama watarudi wasivuke. Wachaga wako kilomita nyingi mbele ambazo haziwezi kuzuiwa ndani ya miaka 10 au hata milele.
Sawa meku
 
Kubagua watu kwa misingi ya kabila ni dhambi
Sidhani kama ni sahihi kufikiria namna hii. Ama sivyo hata wanaokumbaatia mambo ya uzalendo wa kitaifa wanakosea pia sababu wanabagua watu wa mataifa mengine.

Maswala ya umoja wa kikabila huwatisha watawala waovu pekee ama sivyo ni mambo ya msingi sana katika jamii, haya ndio yanayojenga umoja wenye nguvu sio wa maneno tupu.
 
Mara ya kwanza wakati mzee Kitilya anaingia mahabusu pale gereza la keko alipokelewa na vijana ambao yeye mwenyewe aliwapeleka gerezani baada ya kuwafungulia mashtaka ya kuiibia TRA

Nilimsikia wakati huo kwa masikio yangu akisema jamaa hao waliokua wakishirikiana na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu wa Mamlaka ya Mapato wameiba kwa njia mbalimbala ikiwemo ya udanganyifu wa kodi mabilioni ya hela na kwamba hawapeleki polisi bali TAKUKURU maana TAKUKURU hawana mchezo!

Wale jamaa kina Robert Mbetwa, Eric Talemwa, Samuel Renjue na wenzao sasa hivi wako nje baada ya kushinda kesi na baada ya kukaa ndani takriban miaka mitano! Hiyo ilikua ni baada kumkaribisha Mzee kwa kumpa godoro la kulalia wote wakiwa watuhumiwa!
Chuki,Visasi na Vinyongo ni sumu kali kushinda ya nyoka.Ole wao wanaoiendekeza.Zamu yao ikifika wakumbuke walikotoka!
 
Mara ya kwanza wakati mzee Kitilya anaingia mahabusu pale gereza la keko alipokelewa na vijana ambao yeye mwenyewe aliwapeleka gerezani baada ya kuwafungulia mashtaka ya kuiibia TRA

Nilimsikia wakati huo kwa masikio yangu akisema jamaa hao waliokua wakishirikiana na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu wa Mamlaka ya Mapato wameiba kwa njia mbalimbala ikiwemo ya udanganyifu wa kodi mabilioni ya hela na kwamba hawapeleki polisi bali TAKUKURU maana TAKUKURU hawana mchezo!

Wale jamaa kina Robert Mbetwa, Eric Talemwa, Samuel Renjue na wenzao sasa hivi wako nje baada ya kushinda kesi na baada ya kukaa ndani takriban miaka mitano! Hiyo ilikua ni baada kumkaribisha Mzee kwa kumpa godoro la kulalia wote wakiwa watuhumiwa!

Alikosea sana kuruhusu Kampuni yake kutumika kama money laundering conduit. Anastahili anachokipitia.
kwa sasa Mungu pekee ndiye anayeweza kumsamehe.

Ama sivyo awe mvumilivu aone kama kujirudi kwa lowasa kunaweza saidia kitu
 
Kwa hiyo unataka kutuambia kuwa kama ukia mtendaji mkuu wa serikali ukifanya mazuri mengi ndio iwe kinga ya kufanya makosa?" Degree za mansese tabu sana" acha mahakama iamue kama ana kosa au la!
Mkuu, your level of thinking and understanding is deteriorating!
 
Anyways, kama alitenda mema na anatendewa haya kwa dhuluma basi atalipwa mara mia, lakini kama anatendewa yaliyo stahili yake, basi mbingu na nchi ni mashuhuda wake
Mniombee kwelikweli
Hizi ni kazi za watu. siyo permanent job
Kama huko ndio kujiandaa kwa hayo mema 100 ya hapa duniani basi ningemuomba Mola asinipe hayo mema. Huenda weye hujawahi hata kuonja mlango wa sero hivyo unaweza kuomba hayo mema yajayo kwa mrengo huo. Ila, yeyote ambaye aliwahi hata kuonja sero ya polisi, hatatamani kuingia humo kwa bei yeyote.
Pili;
Kama kweli kuna tuhuma nzito wala sio kumuonyesha mtu umwamba kwa kulipiza kisasi chochote kile, basi Mhukumuni ajue kuwa yeye ni mfungwa. Kule unyamwezi tuna kamsemo; Justice delayed is justice denayed. Wamfungilie mbali au wamfyekelee mbali ili ijulikane.
 
Back
Top Bottom