'Tukio' la Mzee Harry Kitilya limenifikirisha sana. Wenye nafasi za kiuongozi kuweni makini!

Kwanza, nawasalimu waungwana wote wa Jamiiforums. Pili, nakiri kuwa jambo ninalotaka kuliandika hapa limetokea juma linaloisha (Alhamisi). Nimechelewa kuandika hapa kwakuwa nilijipa nafasi ya kutafakari vya kutosha. Nimejifunza jambo kubwa kwenye maisha yangu.

Alhamisi ya tarehe 11 mwezi huu majira ya saa mbili na robo asubuhi nilikuwa kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutekeleza majukumu yangu ya kikazi. Nilikuwa nimeambatana na Profesa mmoja wa UDSM (jina kapuni) ambaye alikuwa mteja wangu na shahidi yangu siku hiyo mahakamani hapo kwenye shauri lililonipeleka.

Mimi na Profesa tukiwa tunaingia mlango wa Mahakama husika (mlango mkuu), gari ndogo ya Magereza ya pickup ilikuwa ikirudi nyuma kutoka Mahakamani hapo. Ndani ya gari hiyo kulikuwa na Washtakiwa/Mahabusu wawili walioketishwa chini kwenye gari hilo kwa nyuma. Mmojawapo alikuwa Mzee Harry Kitilya, Kamishna Jenerali wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aka TRA.

Ilikuwa ni kama tunapishana na gari hilo. Mzee Kitilya alipomuona Profesa anayefahamiana naye (akijitahidi kuchangamka na kusahau kwa muda maswahibu yake) alimwita Profesa kwa jina na kumsalimu. Akajitahidi kumfahamisha na mwenzake kuwa yule ni Profesa na ni rafikiye. Hakujali hata askari wa Magereza waliokuwa wamewasimamia kiulinzi. Kwa bahati njema,dereva alisimama kwa muda 'kuruhusu' salamu hiyo.

Baada ya salamu, Profesa akamwambia Mzee Kitilya: Pole. Akionekana kusawajika, kutamani kuwa nje ya gari ile huru kama mwanzoni na mwenyewe kujiamulia cha kufanya na kusema, Mzee Kitilya akajibu: Asante Profesa, tupo! Gari ikamalizia kona na kuondoka.

Mzee Harry Kitilya alikuwa Mkuu wa TRA iliyokusanya kodi nyingi nchini zilizojenga na kulipia mambo mbalimbali ya kiserikali. Alikuwa Mkuu wa wakusanya mapato ya Serikali na alifanya aliloliweza. Alikuwa akiheshimiwa na wadogo kwa wakubwa wa nchi hii na wakati mwingine kuogopwa. Leo yuko kwenye hali ile.

Ikiwa mti mbichi unatendwa vile, itakuwaje kwa miti mikavu? Nawasihi viongozi mbalimbali waweke akiba ya maneno na matendo yao. Maisha hayana formula!
Kama ukijiheshimu utaheshimiwa.TRA ni janga la taifa letu,na sina wasi wasi wowote kwamba Kitilya naye alikuwa janga.Naamini angekuwa msafi asingepata madhila haya.Anastahili na wala hastahili huruma.
 
Tangu nimekuoa numeona katika mafisadi 10 lazima 6wawe wachaga na ukumbuke wachaga ni kabila dogo tu wangekuwa kama waha au wasukuma nchi hii ingeisha

Utakutwaje na makosa kama una elimu ya kufanya kazi fulani
Ingekua kuna mamlaka za kuangalia makosa ya wachawi ... labda ingekua kwenye hilo kundi.. Maana kama 8:10 ya ukoo ni wa wachawi likely watakutwa na makosa ya kichawi au kibaka
Lakini kama 8/10 ya ukoo ni wa wasomi basi watakutana na makosa yanayoendana na kazi zao
 
Kwanza, nawasalimu waungwana wote wa Jamiiforums. Pili, nakiri kuwa jambo ninalotaka kuliandika hapa limetokea juma linaloisha (Alhamisi). Nimechelewa kuandika hapa kwakuwa nilijipa nafasi ya kutafakari vya kutosha. Nimejifunza jambo kubwa kwenye maisha yangu.

Alhamisi ya tarehe 11 mwezi huu majira ya saa mbili na robo asubuhi nilikuwa kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutekeleza majukumu yangu ya kikazi. Nilikuwa nimeambatana na Profesa mmoja wa UDSM (jina kapuni) ambaye alikuwa mteja wangu na shahidi yangu siku hiyo mahakamani hapo kwenye shauri lililonipeleka.

Mimi na Profesa tukiwa tunaingia mlango wa Mahakama husika (mlango mkuu), gari ndogo ya Magereza ya pickup ilikuwa ikirudi nyuma kutoka Mahakamani hapo. Ndani ya gari hiyo kulikuwa na Washtakiwa/Mahabusu wawili walioketishwa chini kwenye gari hilo kwa nyuma. Mmojawapo alikuwa Mzee Harry Kitilya, Kamishna Jenerali wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aka TRA.

Ilikuwa ni kama tunapishana na gari hilo. Mzee Kitilya alipomuona Profesa anayefahamiana naye (akijitahidi kuchangamka na kusahau kwa muda maswahibu yake) alimwita Profesa kwa jina na kumsalimu. Akajitahidi kumfahamisha na mwenzake kuwa yule ni Profesa na ni rafikiye. Hakujali hata askari wa Magereza waliokuwa wamewasimamia kiulinzi. Kwa bahati njema,dereva alisimama kwa muda 'kuruhusu' salamu hiyo.

Baada ya salamu, Profesa akamwambia Mzee Kitilya: Pole. Akionekana kusawajika, kutamani kuwa nje ya gari ile huru kama mwanzoni na mwenyewe kujiamulia cha kufanya na kusema, Mzee Kitilya akajibu: Asante Profesa, tupo! Gari ikamalizia kona na kuondoka.

Mzee Harry Kitilya alikuwa Mkuu wa TRA iliyokusanya kodi nyingi nchini zilizojenga na kulipia mambo mbalimbali ya kiserikali. Alikuwa Mkuu wa wakusanya mapato ya Serikali na alifanya aliloliweza. Alikuwa akiheshimiwa na wadogo kwa wakubwa wa nchi hii na wakati mwingine kuogopwa. Leo yuko kwenye hali ile.

Ikiwa mti mbichi unatendwa vile, itakuwaje kwa miti mikavu? Nawasihi viongozi mbalimbali waweke akiba ya maneno na matendo yao. Maisha hayana formula!
Huyu atashinda kesi na uraiani atarudi,.come jan 2026 maombi ya watanzania yatajibiwa vilivyo. Ataanza na Dotto James atueleze ndege mjomba alizonunua nani aliidhinisha hizo pesa.Huyu lazima anyookee lupango
 
Tangu nimekuoa numeona katika mafisadi 10 lazima 6wawe wachaga na ukumbuke wachaga ni kabila dogo tu wangekuwa kama waha au wasukuma nchi hii ingeisha
angalia matoke ya Nacte ndio utajua wachagga na akina nani ,mtateseka saaana kujaribu kuchafuabtaswira ya walionitambua na hamatafanikiwa kamwe,wadogonzetu wameendeleza utamaduni wa hili kabila,natamani saana na wale waliopo pale Muhimbili madaktari wa fani mbali mbali nao pia watimuliwe ,ingependeza saaana.
 
Tangu nimekuoa numeona katika mafisadi 10 lazima 6wawe wachaga na ukumbuke wachaga ni kabila dogo tu wangekuwa kama waha au wasukuma nchi hii ingeisha

Rudi shule ukajifunze kuandika kwanza, na uzuri sasa hivi elimu ni bure hivyo gharama yako itakuwa ni sare na daftari tu.
 
Mleta mada hueleweki pamoja na kujiita wakili.Si inasemwa wazi kuwa hakuna aliye juu ya sheria na kuwa watu wote Ni sawa mbele ya sheria uliitakaje Ya Kitilya sheria isizingatiwe au? Wakili hufai wewe unamwaga Siri za wateja mitandaoni
 
Bora hata huyo Profesa kaongea naye Mzee Kitilya.

Kuna watu wakikuona una matatizo hivyo wanakukaushia kama hawakujui, wanaogopa hata kuongea nawe wataonekana wana urafiki nawe na wao wanaweza kuchunguzwa.

Nilishuhudia kaka wawili wa familia moja wanabishana. Baba yao alikuwa na urafiki fulani na Mzee Rugemalira. Baba akasema Mzee Rugemalira anapata tabu sana gerezani, kwa kuwa ni mtu aliyewahi kumfahamu katika biashara zake awali, angependa kwenda kumuona mahabusu na kumfariji.

Wale vijana wawili wakawa wanabishana. Mmoja akisema kwamba kumtembelea Rugemalira italeta picha mbaya na Baba yao anaweza kusakamwa na serikali, kijana mwingine akasema serikali haina haki ya kumsakama Baba yao kwa kuwa hana hatia, na kama anataka kwenda kumtembelea Rugemalira, hilo ni jambo la ridhaa kwake.

Nimesahau kumuuliza yule Mzee kama alimtembelea Rigemalila mahabusu au hakumtembelea.

Sio hilo tu, sasa hivi hata mwanaccm kumtembelea mpinzani mwenye matatizo ni kosa kwa mungu wa Tanzania.
 
..Pasikuwepo na mabadiriko ya katiba ambayo haiwaondoi (exonerated )kwenye lawama wote watoa maamuzi kuanzia kwenye Executive tutaendelea kumuvika paka kengere kuwa watu wa kabila fulani ndio wezi,mafisadi huku tukijuwa kuwa waliotoa maamuzi hayo ya ufisadi wako pembeni hawawezi kuguswa na sheria.Tuepukane na tribal sentiments mambo haya yanasababisha chuki ,kukomoana nakusambaratisha utaifa wetu.
 
Back
Top Bottom