Nilikuwa nasoma Mkwawa, akafika Afisa wa shushushu pale kuwakaribisha wanafunzi wajiunge na TISS. Yaani wanafunzi wote wameitwa kwenye Hall ili huyu mtu awakaribishe kujiunga na TISS.
Akawa anasema,"Watu wengine wanatuita "shushu-shushu", lakini msiogope. Sisi tuna kazi kama watu wengine tu.
Siku hizi ajira sijui inafanyika vipi.
Au nilipoingia JWTZ. Ikatolewa Public Notice: Vijana wote wanaotaka kujiunga na Jeshi,wafike uwanja wa Karume kesho asubuhi. Basi,vibaka wote wa Daressalaam walifika pale.
Yule Kamanda,alikuwa Sajenti,nadhani,akasema:"Sasa,hebu tusikilizane. Nataka mkimbie hapa uwanjani mara nne,duara nne,wale ishirini wa kwanza,watajiunga na Jeshi. Hivyo nilivyoingia Jeshini.