Tujiulize kuhusu usalama wa vyakula Tanzania

wazanaki

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
1,092
804
wakuu, leo mtujikite kwenye mada ya vyakula, katika dunia ya sasa 90% ya vyakula tunavyokula ni industrial processed ni sehemu chache sana zilizobaki hasa vijijini ambapo unapata chakula pure, ambacho hakina preservative, ila mostly vyakula tunavokula vinatoka kwenye industries na makampuni binafsi, mfano, unga, soda, bia, bites, mafuta ya kupikia, maji.

Lakini je kuna umakini kiasi gani katika vitengo vya kuchunguza vitu tunavokula ni salama, najua kuna vitengo vinahusika na hivi vitu, lakini hii mambo ni nyeti sana kuliko sector yoyote unayopifikilia, maana sector ya usalama wa chakula ikishindwa kufanya kazi yake kwa umakini, taifa linaweza angamia kama vifo vya kumbi kumbi, au tunaweza zalisha watoto wengi wenye ulemavu.

Sumu si kitu poa, unapoamini sector fulani serikalini kwenye usalama wa chakula cha mwananchi, unakua ni kama umempa roho za wananchi milioni 60. Kwa maana ya kwamba either kimakusudi au kwa bahati mbaya anaweza akaruhusu mazingira hatarishi ya chakula. cha msingi hapa nilichotaka kuuliza je serikali inaangalia swala hili kwa jicho la tatu, au inachukulia poa.

Ukichunguza taifa kama ujerumani, lina udhibiti mkali sana wa vyakula, kuanzia viwandani hadi kwa consumer, kwa maana wanakagua kwa umakini bidhaaa zinazoingia kwenye nchi, hotel, restaurant, quality ya chakula, upimaji wa quality ya maji, kiwango cha dawa za sumu za mashambani. wanakagua klila angle, hawana masihala katika hii kitu.

Je, kwa Tanzania nchi yetu, Watanzania wenzangu, je haya mambo yapo, nilitaka kujua tu, wote ni watanzania lazima tujue, kama ukaguzi unafanyika vizuri ni swala la heri, lakini kama unamapungufu, tuelezane. toa maoni kama una mawazo.
 
Good point ,Swala la vyakula ni sawa na utunzaji wa dawa aina ya DDA kwani madhara ni makubwa mno kama hakuna mpango mkakati wa utunzaji wa vyakula vyetu ni kweli kabisa kuna vyakula vingi ni shida mitaani huku watu tunafakamia tu ,Hili swala watumishi wa Afya lazima walione hilo
 
mkuu, point nzuri sana, ila kwann watanzania hutawaona kwenye mada kama hii ndo kitu kinachoogopesha, ni kama reality horror movie
 
Good point ,Swala la vyakula ni sawa na utunzaji wa dawa aina ya DDA kwani madhara ni makubwa mno kama hakuna mpango mkakati wa utunzaji wa vyakula vyetu ni kweli kabisa kuna vyakula vingi ni shida mitaani huku watu tunafakamia tu ,Hili swala watumishi wa Afya lazima walione hilo
pia hili ni swali ambalo ilitakiwa aulize mbunge wa jimboni kwako, lakini cha kushangaza tunauliza watu wa jamii forum huku wabunge wakiongelea mada………...
 
usalama wa chakula ni usalama wa taifa.

ila huku kwetu usalama wa taifa wamekariri ni kuvaa miwani nyeusi na kuvaa suti kama ile ya Musiba.
 
Back
Top Bottom