Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,502
- 51,098
Mwaka 2015 aliyekuwa Waziri wa Ujenzi , ambaye leo ni Rais wa Tanzania ndugu Magufuli, alitoa waraka wa mafanikio ya ya serikali ya awamu ya Nne ya ndugu Jakaya Kikwete, katika mafanikio hayo aliorodhesha mamiradi mengi mengi tu yaliyofanywa na serikali ya Mzee Kikwete.
Sasa najiuliza kama Kikwete aliweza kujenga miradi yote hii, huku akiendelea kuboresha mishahara ya watumishi mishahara yao kila mwaka, kuendelea kutoa ajira kwa vijana wetu. Nakumbuka enzi hizo ukinunua magazeti kulikuwa kumejaa matangazo ya ajira tofauti na leo), kupanua demokrsaia nchini, kuweka uhuru mpana wa vyombo vya habari then yeye Magufuli anakwama wapi?
Hii Ripoti ni ya wizara moja tu ya Magufuli, maana yake kila Wizara ikija na ripoti yake ya yaliyotekelezwa maana yake mambo mengi sana yalifanyika mwaka 2005 hadi 2015 lakini tuliona hali za wananchi zikiwa nafuu sana kuliko sasa.
Kwa hiyo ni dhahiri wakati wa utawala wa Kikwete kulikuwa na balance kubwa ya maendeleo ya vitu na watu tofauti na hivi sasa
Hiyo ni baadhi tu ya Screenshot za miradi ya JK, bado kuna miradi mingi mingi sana ambayo ipo kwenye ripoti na miye sijaiweka hapa
Ila ukitaka kujisomea miradi yote iliyokamilika, na iliyokuwa ikiendelea wakati JK anaondoka madarakani basi Soma attachment kwenye huu uzi