Tujikumbushe: Waziri Magufuli alipotoa waraka wa mafanikio ya Rais Kikwete kwenye mambo ya ujenzi kuanzia mwaka 2005 hadi 2015

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,447
2,000
Mwaka 2015 aliyekuwa Waziri wa Ujenzi , ambaye leo ni Rais wa Tanzania ndugu Magufuli, alitoa waraka wa mafanikio ya ya serikali ya awamu ya Nne ya ndugu Jakaya Kikwete, katika mafanikio hayo aliorodhesha mamiradi mengi mengi tu yaliyofanywa na serikali ya Mzee Kikwete.

Sasa najiuliza kama Kikwete aliweza kujenga miradi yote hii, huku akiendelea kuboresha mishahara ya watumishi mishahara yao kila mwaka, kuendelea kutoa ajira kwa vijana wetu. Nakumbuka enzi hizo ukinunua magazeti kulikuwa kumejaa matangazo ya ajira tofauti na leo), kupanua demokrsaia nchini, kuweka uhuru mpana wa vyombo vya habari then yeye Magufuli anakwama wapi?

Hii Ripoti ni ya wizara moja tu ya Magufuli, maana yake kila Wizara ikija na ripoti yake ya yaliyotekelezwa maana yake mambo mengi sana yalifanyika mwaka 2005 hadi 2015 lakini tuliona hali za wananchi zikiwa nafuu sana kuliko sasa.

Kwa hiyo ni dhahiri wakati wa utawala wa Kikwete kulikuwa na balance kubwa ya maendeleo ya vitu na watu tofauti na hivi sasa

1601978268804.png


1601978366006.png


1601978473351.png1601978563250.png


1601978612677.png1601978719079.png1601978785429.png


1601978829103.png1601978897638.png1601978955976.pngHiyo ni baadhi tu ya Screenshot za miradi ya JK, bado kuna miradi mingi mingi sana ambayo ipo kwenye ripoti na miye sijaiweka hapa
Ila ukitaka kujisomea miradi yote iliyokamilika, na iliyokuwa ikiendelea wakati JK anaondoka madarakani basi Soma attachment kwenye huu uzi
 

Attachments

  • File size
    971.3 KB
    Views
    12

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
5,537
2,000
Sasa mbona amekua na kawaida ya kuwaponda hao watangulizi wake hadharani kwa kutofanya chochote na pia kutuaminisha ya kwamba asipokuwepo yeye, basi hakuna kitakachofanyika nchini!

Kwenye hiyo ishu ya mishahara ma ajira, huenda kuna watu wachache wanafaidika zaidi awamu hii huku wengi tukiumizwa. Nina wasiwasi ile mijitu yenye miraba minne inayomlinda kila mahali na mibunduki ya kutisha, inalipwa salary kubwa sana.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,447
2,000
Ukisoma hiyo ripoti kumbe hata ujenzi wa barabara kubwa ya Dar-Chalinze (Expressway) na Interchange Tano, kumbe Mjomba JK alishaiweka kwenye plan na tayari alishaitengea bajeti ya upembuzi yakinifu shilingi bilion 7.72

Halafu leo tunakuja kudanganyana eti utawala uliopita haukufanya kitu. Duh!

1601980253168.png
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
5,537
2,000
Kikwete alijenga Flyover ngapi ? Alinunua ndege ngapi ? Hii nchi ilichezewa sana ...

Hizo flyovers na ndege zimegharimu shilingi ngapi kiasi cha kusababisha Wafanyakazi Wazalendo wa Nchi hii wadhulumiwe stahiki zao kwa miaka yote hii mitano?

Na wakati Nchi inachezewa, Magufuli alikua wapi? Unataka utuaminishe kwa sasa haichezewi? Au tumembadili tu huyo mchezeaji?
 

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
2,540
2,000
Hizo flyovers na ndege zimegharimu shilingi ngapi kiasi cha kusababisha Wafanyakazi Wazalendo wa Nchi hii wadhulumiwe stahiki zao kwa miaka yote hii mitano?
Zimegharimu hela nyingi, bado amejenga hospitali za rufaa 10, zahanati 1198, vituo vya afya 487 na Hospitali za Wilaya 99 na pia ameajiri watumishi wa afya wanazoidi 14, 000. Kuna bomba la mafuta la Hoima, Stiegler's Gorge, Serikali imehamishiwa Dodoma, Mshahara hata yeye Magufuli haumtoshi lakini ndio ameamua, kuleta maendeleo ni bora kuliko kujiongezea mishahara.
 

Elythrobacter

Member
Sep 29, 2020
48
125
Zu
Zimegharimu hela nyingi, bado amejenga hospitali za rufaa 10, zahanati 1198, vituo vya afya 487 na Hospitali za Wilaya 99 na pia ameajiri watumishi wa afya wanazoidi 14, 000. Kuna bomba la mafuta la Hoima, Stiegler's Gorge, Serikali imehamishiwa Dodoma, Mshahara hata yeye Magufuli haumtoshi lakini ndio ameamua, kuleta maendeleo ni bora kuliko kujiongezea mishahara.
Zungumza utopolo mwingine unoona unafaa ila ajira iache kabisa na usioongee mkuu.
 

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
2,540
2,000
Zu

Zungumza utopolo mwingine unoona unafaa ila ajira iache kabisa na usioongee mkuu
Walimu wapya zaidi ya elfu 12 wameajiriwa na ajira mpya zingine zimeshatangwa, walimu zaidi ya 120,000 wa elimu ya awali na I hadi la IV wamepatiwa mafunzo ya ufundishaji na ujifunzaji. Uimarishaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu wataalamu elimu 13,350 wamepewa mafunzo
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,131
2,000
Kikwete alijenga Flyover ngapi ? Alinunua ndege ngapi ? Hii nchi ilichezewa sana ...
Flyovers ZOTE ni miradi ambayo JPM amekutwa taratibu zote zimefanyika na pesa zilishapatikana!!

Role ya JPM kwenye flyovers ni ile ile kama alivyokuwa Waziri wa Ujenzi... Nyapara Hodari!!

Ubungo1.png

TAZARA.png


Ubungo 2.png

Kwa maana nyingine, role aliyo-play JPM kwenye Flyovers ni sawa na ile aliyo-play akiwa Waziri wa Ujenzi! Ni kama anayo-play sasa kwenye ujenzi wa Mwendokasi! Ni kama anayo-play kwenye uboreshaji barabara za jiji la Dar es salaam!

Miradi yote hiyo kakuta mchakato umeshakamilika, na pesa zimepatikana!!

Lakini akina Pascal Mayalla wanataka tukigusa tu pale Ubungo Interchange, tuseme "ASANTE MAGUFULI"

Pascal, kwenye ule uzi wako nilikuuliza ikiwa hali yenyewe ndo hii, hiyo "Asante Magufuli" unayotaka tuwe tunasema ni kwa sababu ipi?!

Hata hivyo, hukujibu, unaonaje basi ukinijibu tuseme Asante Magufuli kwa lipi wakati yeyote ambae angeingia madarakani angeweza kujenga hata kama angekuwa Hasheem Rungwe?!
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
5,537
2,000
Zimegharimu hela nyingi, bado amejenga hospitali za rufaa 10, zahanati 1198, vituo vya afya 487 na Hospitali za Wilaya 99 na pia ameajiri watumishi wa afya wanazoidi 14, 000. Kuna bomba la mafuta la Hoima, Stiegler's Gorge, Serikali imehamishiwa Dodoma, Mshahara hata yeye Magufuli haumtoshi lakini ndio ameamua, kuleta maendeleo ni bora kuliko kujiongezea mishahara.

All in all, Watanzania walio wengi hawamtaki. Na ashukuru Tume ya Uchaguzi na Polisi ni mali yake.

Kinyume na hapo, angeelewa vizuri kupitia sanduku la kura Watanzania tunahitaji nini! Ndege au maisha bora.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,447
2,000
Kikwete alijenga Flyover ngapi ? Alinunua ndege ngapi ? Hii nchi ilichezewa sana ...

Hujui kuwa mradi wa flyover ya TAZARA ulikwekwa saini ya ujenzi wake na serikali ya JK?

Tatizo mmelishwa propaganda za TBC mnadhani kwamba JPM ndo kila kitu!. No, ndiyo kwanza anatembelea nyota za wenzie!
 

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
2,540
2,000
All in all, Watanzania walio wengi hawamtaki. Na ashukuru Tume ya Uchaguzi na Polisi ni mali yake.

Kinyume na hapo, angeelewa vizuri kupitia sanduku la kura Watanzania tunahitaji nini! Ndege au maisha bora.
Mafisadi na mabeberu ndio mnamchukia
 

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
2,540
2,000
Hujui kuwa mradi wa flyover ya TAZARA ulikwekwa saini ya ujenzi wake na serikali ya JK?

Tatizo mmelishwa propaganda za TBC mnadhani kwamba JPM ndo kila kitu!. No, ndiyo kwanza anatembelea nyota za wenzie!
Yeye ndio ametekeleza maono na ndoto za Chama Cha Mapinduzi
 

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
2,540
2,000
Kuna mwenye wazo na mtekelezaji wa wazo, kila mmoja ameleta mabadiliko na kila mmoja ametoka Chama Cha Mapinduzi, Chagua Chama Cha Mapinduzi mpate mabadiliko ya kweli na maendeleo ya kweli. Usidanganywe na vibaraka wa kisiasa.
 

Securelens

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
313
1,000
Takwimu hizo zinaonesha kuwa Mheshimiwa Kikwete kwa miaka 10 alijenga KM 5568 za barabara kwa kiwango cha lami. Yeye Mheshimiwa Rais Magufuli katika kipindi cha miaka 5 tu tayari amekamilisha kujenga KM 3500 za barabara na KM zingine 2500 ujenzi wake unaendelea. Zote ni kwa kiwango cha lami.

Hivyo utaona kuwa Rais Magufuli amejenga barabara mara mbili zaidi ya zile zilizojengwa na Mhe Kikwete. Mpe kura yako Oktoba 28 aendelee kufanya maajabu katika ujenzi wa barabara nchini.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,131
2,000
Kuna mwenye wazo na mtekelezaji wa wazo, kila mmoja ameleta mabadiliko na kila mmoja ametoka Chama Cha Mapinduzi, Chagua Chama Cha Mapinduzi mpate mabadiliko ya kweli na maendeleo ya kweli. Usidanganywe na vibaraka wa kisiasa.
Hivi hujiulizi kwanini sikutaja SGR?!

SGR na yenyewe Magu kakuta mchakato wote umekamilika na funding imepatikana! Hata hivyo nahesabu kama mradi wa JPM kwa sababu alipoingia ile funding ya mwanzo alipiga chini na akaleta funding ya kwake na akafanya baadhi ya mabadiliko!

Kinyume chake, kakuta Flyovers kila kitu kimeshafanyika na pesa imepatikana! Kwahiyo alichokuta JPM sio WAZI bali ni fully funded project waiting to take off!!

Huwezi kumsifia rubani kwa ubora wa ndege za Boeing kwa sababu tu yeye ndie anazirusha!!!

Kwamba eti tuchague CCM kupata mabadiliko ya kweli hicho ni kiroja!!! Kama nchi ingekuwa ni shati, ina maana tunatakiwa kufanya mabadiliko ya shati kwavile limechakaa!!

The question is: Nani kachakaza hilo shati?! Yaani zaidi ya miaka 50 ya uhuru mnaishia kuiba tu leo watu wanashituka ndo mnatuambia "tuchagueni" tulete mabadiliko!!!

Tuwachague tulete mabadiliko au tuwachague muendelee kuangamiza taifa?! Leo hii simulizi za flyovers eti ndo zina-trend... flyovers?! Are we serious?!
 

Securelens

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
313
1,000
Hivi hujiulizi kwanini sikutaja SGR?!

SGR na yenyewe Magu kakuta mchakato wote umekamilika na funding imepatikana! Hata hivyo nahesabu kama mradi wa JPM kwa sababu alipoingia ile funding ya mwanzo alipiga chini na akaleta funding ya kwake na akafanya baadhi ya mabadiliko!..
Siyo kweli Flyover ya Ubungo mkopo wake ulisainiwa tarehe 20 March 2017 . Ni Rais Magufuli aliyesimamia majadiliano yake na hatimaye mkopo kutolewa. Angalia hapa chini


DAR ES SALAAM, March 16, 2017 —The World Bank Group President, Dr. Jim Yong Kim, will visit Tanzania from March 19-21, 2017.

During his visit, Dr. Kim will meet with President John Pombe Magufuli, to discuss key engagements of the strategic partnership between the Republic of Tanzania and the World Bank Group. Dr. Kim will also spotlight World Bank Group-supported investments in transformational infrastructure, and highlight the need for continued investments in human development, especially education quality and investing in the early years.

PROGRAM OF VISIT

Laying of foundation stone for Ubungo overpass, together with H. E. Dr John Magufuli
When:
Monday, March 20, 2017
Where: Ubungo
Participants: Senior Government of Tanzania Officials; World Bank Group Officials, Media, General Public

Visit to Zanaki primary school
When:
Monday, March 20, 2017
Where: Upanga, Dar es Salaam
Participants: Hon. Dr. Joyce Ndalichako, the Minister for Education, Science and Technology and Senior Government of Tanzania Officials; World Bank Group Officials; Media

This will be Dr. Kim’s first visit to Tanzania. The partnership between the World Bank Group and the Government of Tanzania began in June 1960 when the International Finance Corporation, the World Bank Group’s private sector arm, invested $2.8 million in the Kilombero Sugar Company. In 1962, the World Bank provided $4.6 million to then Tanganyika for the School Construction Equipment Project, followed by $5 million for the 1965 Agriculture Credit project.

The World Bank is currently financing 23 national projects amounting to $3.6 billion, in addition to seven regional operations through which Tanzania accesses $551 million in financing, reaching a total commitment of $4.3 billion. The bulk of this support (22 percent) focuses on the transportation sector, followed by urban development (20 percent).

A physician and anthropologist, Dr. Kim has dedicated his career to international development. For more than two decades, he helped under-served populations by improving healthcare in countries around the world. Dr. Kim became the 12th President of the World Bank Group on July 1, 2012, after serving as President of Dartmouth College, a pre-eminent center of higher education in the United States. Dr. Kim is a co-founder of Partners In Health (PIH) and a former director of the HIV/AIDS Department at the World Health Organization (WHO).
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom