Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Salama Mfamao-RIP.
Nimemsahau na Halima Mchuka....yuko wapi huyu dada ???
 
Kawia Saidi....mama na mwana na cheichei siku ya jumamosi saa nne kasorobo asubuhi...huyu mama alimtangulia Deborah Mwenda kutangaza mama na mwana..
 
1.Godfey Mngodo
2. Abissay Stephen
3. Lucas Matipa
4. Idrisa Sadala
5. Nswima Maraso Errrrrrrrnest
6. Tumbo Tamim Risasi
7. Julius Nyaisanga....Club raha leo Show, Misakato
8. Edda Sanga
9. Salim Seif Nkamba " Mjomba"
10. Mohamed Ngombo - RIP
 
Take a break, na tujikumbushe enzi zile za RTD, ambapo kulikuwa hakuna FMs rado kama sasa. Hakika kulikuwa na watangazaji, vipindi bomba na hata nyimbo za kutambulisha vipindi zilikuwa makini sana. Hebu ngoja niwakumbushe baadhi ya watangazaji wa wakati huo.

1. Nassoro Nsekeli- alikuwa na sauti kama ya mafua hivi alikuwa mtaalamu wa kipindi cha Majira- ndiye aliyetangaza kifo cha Nico Zengekala

2. Bujago Izengo wa Kadago- Kibesi chake kilikuwa safi sana

3. David Wakati (DG) - kipindi cha Nipe habari- Kwaherini wote, mungu awalinde na mmbaki salama, mungu akipenda..............

4, Khalid Ponera- Zilipendwa

5. Ahmed Kipozi- taarifa ya habari

6. Hassan Mkumba- matangazo ya vifo

7. Siwatu Luwanda

8. Salama Mfamao
9. Mohamed Amani (Mohamed Dahman)

10. Salim Seif Nkamba

12. CHisunga Steven- kipindi cha Ugua pole duu

13. Bathoromeo KOmbwa (bati Kombwa) - WAkati wa Kazi

14. Ahmed Jongo- Mpira

15. Christina Chokunogela

16. Dominic Chilambo- Mpira

17. Edda Sanga
18. Debora Mwenda- Mama na Mwana
19. Aloycea Maneno- Ombi lako, cheichei Shangazi, mama na mwana

Duu nawamiss sana hawa watu tofauti na watangazaji wa sasa
Teh teh teh,Tido Mhando bwana from catterpilar to butterfly we acha tuu life hii!!!
 
Namkumbuka sana Michael Katembo. Jamaa alifanya watu wakipende kipindi cha ngoma zetu wakati si wengi waliokuwa wakikisikiliza. alikuwa mbunifu sana. Nakumbuka mkwara wake mmoja wakati anaongea anafungulia ngoma moja hivi halafu anajifanya kama kuwafokea wapigaji kuwa ati wameingia studio na kuanza kupiga ngoma zao bila kuruhusiwa!! halafu anawatimua!! kali kuliko yote anaweka sauti ya mbwa anayebweka huku akimuamrisha awafukuze wale wapiga ngoma!!! Jamaa alikuwa ni mbunifu si vidogo!! Nakumbuka miaka fulani ya mwanzoni mwa 80 watu wanasubiri kwa hamu kabisa kipindi chake cha ngoma za kienyeji!!!
 
Teh teh teh,Tido Mhando bwana from catterpilar to butterfly we acha tuu life hii!!!
pia ben kiko,taitas filipo,mikidadi mahamud,sango kipozi,chisunga steven,hawa walikuwa maripota wa uhakika na sauti zao zilikua zinawavuta mno wasikilizaji hasa ben kiko,kutoka taborrra huyyu ni beeeeen kikkko wa rrrrrrrrrrreeeeedio tanzania.hata kisumu kenya kulikuwa na club ya wasikilizaji inaitwa ben kiko salaam klab pia nairobi jinja na maeneo mengine mengi kwa hakika ilikua rtd inasikilizwa kila kona kwa kufata utmu wa watangazaji wanavovutia kwa sautizao na mpangilio mzuri wa vipindi.
 
Sijasikia mkimtaja marehemu Masoud wa kipindi cha michezo, aliyevamiwa na majambazi nyumbani kwake na kumuamuru asali sala za mwisho kisha wakampiga risasi. RIP Masoud... RIP Tumbo Tamimu Risasi...
 
kuna jamaa alikuwa naitwa abdala ngarawa. jackobu tesha bwana alikuwa na XB

yaani extra bass si mchezo. nilikuwa napenda kuwaiga watangazaji enzi hizo nikiwa mtoto namimi najifanya nasoma taarifa ya habari au natangaza vipindi mbalimbali nikiigiza sauti zao
 
duh mewakumbuka watangazaji nikamkumbukaAirini malongo toto ya taarifa ya habari enzi za fm radio pale ITV yuko wapi jamani huyu msichana?
 
Lenny Mambombotela ni Mkenya I think,alikuwa KBC,nakumbuka alikuwa na kipindi cha UHALIFU HAULIPI CHOCHOTE(kama sikosei),pia KBC nao walikuwa wazuri sana enzi hizo,bila kumsahau mtaalamu Freddy Obacho Machoka

Mambomotela alikuwa na kipindi kingine cha Je huu ni ugwana?? dah inakumbusha mbali kweli
 
duh mewakumbuka watangazaji nikamkumbukaAirini malongo toto ya taarifa ya habari enzi za fm radio pale ITV yuko wapi jamani huyu msichana?

Yupo Mbeya kwa sasa ameolewa na anaendesha Restaurant maarufu pale Uwanja wa Sokoine... Duh PIZZA za pale ni kiboko!!!
 
Back
Top Bottom