Ahlan wa sahalan.
Nimekumbuka mbali sana.
Namkumbuka Michael Katembo pale studio 3 na kipindi chake cha Midundo asilia.
Namkumbuka Mzee Angalieni Mpendu idara ya utangazaji biashara.
namkumbuka Edda Sanga wa chumba cha habari.
Nili enjo sana field yangu enzi hizo.
Sitaweza kumsahau Mama Tatu Mbotoni ambaye alikuwa mkuu wa maktaba ya rekodi. Klla tulichofanya au kuhitaji tulipitia kwake.
Sijawasahau wazee etu Mafundi mitambo.
Mzee Edmund Mria (mchaga)
Ali Said Tunku
Noel Namaloe
pamoja na wale engine wa OB.
Nilienjoy sna field angu chini ya wakongwe hawa.
Mimi katika vipindi vya kutuma salam basi alikuwa akikaa Uncle J (Julius Nyaisanga Super Tall) nilikuwa sibanduki pembeni ya redio mpaka kipindi kiishe maana alikuwa anaweka debe nzito sana au akiamua kushuka kwa jirani zetu kule Zaire pia alikuwa anavipanga vitu ambavyo vinakufanya hutaki kuondoka, halafu alikuwa anawajua wanadendi wengi kwa majina na kuanza kuwataja mmoja baada ya mwingine.
Nina swali. Kuna kile kipindi maarufu sana cha usiku nadhani kilikuwa kuanzia saa 4 na robo usiku (baada ya taarifa ya habari) weekdays kiliitwa kijaluba. Hivi wale akina dada waliokuwa wanapiga kelele kuashiria kipindi kile walikuwa wanasema maneno gani? Kuna jamaa aliwahi kutifunga kamba ofisini eti walikuwa wanase mimi yangu nyeupe babu, na mwingine anasema mimi yangu nyeusi babu na mwingine anaitikia mimi yangu nyekundu babu na mwingine anasema mimi yangu bukta nilijaribu sana kusikiliza walikuwa wanasema nini lakini sikupata kitu.
Hahaaaaaaaaa BAK una vituko wewe..Haya maneno hata mimi mpaka leo sijajua yalikuwa ni maneno gani aisee...Hiki ni kipindi nilichokipenda sana enzi hicho,hasa madoido na mikogo ya mtangazaji wake Abdallah Mlawa...Mkuu pia kulikuwa na kipindi cha Ngano za Muziki wakikumbuka hiki???,yaani hapa ilikuwa zakusanywa nyimbo zenye maudhui yanayoendana kisha latengenezwa/launganishwa bonge la stori
Hivi nani alikuwa anaendesha kipindi cha Mikingamo?
Kulikuwa na Karim Besta, Mohamed Kisengo, Jane Nonge, Ananilea Nkya Twende na Wakati, Bakari Msulwa, Idrisa Sadala,
Yuko wapi Bujago Izengo wa Kadago