Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Samahani kama nitakuwa nimemsingizia
Bujaga Izengo Kadago (RIP)?
.
Umemsingizia, Bujaga Izengo Kadago yuko hai, anapiga mzigo pale SUA TV-Morogoro.

Unaweza ukawa umemchanganya na Karim Besta (RIP).

Bujaga, Besta, Betty Mkwasa na Ahmed Kipozi, walitimka RTD, 1995 wakajiunga DTV. Kipozi na Mkwasa wakahamia ITV wakati Bujaga na Besta walienda ATV ya Morogoro ambapo Bujaga akaishia SUA TV, na Besta akabaki Abood hadi mauti yalipomkuta mwaka juzi.
 
Jamani hivi Jacob Tesha yuko wapi? ukitaka kusikia "bass" ya kufurahisha basi ulikuwa unatakiwa usikilize taarifa za habari.
Baada ya kumaliza na ngwe ya Sumaye kama Press Sec.wake, alirudishwa Maelezo briefly, then amepelekwa wizara ya Habari, nadhari kusubiri kustaafu kwa heshima.
 
Jacob Tesha nakumbuka ni afisa habari katika wizara moja hapa nchini! yuko wapi Chisunga Steven wa kanda ya kati, vipi mnamkumbuka Ben Kikomeko ( Ben kiko-kanda ya kaskazini), yuko wapi Ahmed Jongo, mnamkumbuka marehemu Masakilija- wa Mwanza. Kile kipindi cha Club Raha leo mnakikumbuka?
 
Halima Kihemba -
Anko J - Nyaisanga - Sauti yake bomba sana hasa akisoma Taarifa ya Habari.
 
I used to enjoy listerning soccer Comentators Kama Charkes Hilary, Swedi Mwinyi Ahmed Jongo, Most recently Juma Nkamia! Sweet and Fond Memories!
 
1. Dunstan Tido Mhando.

2. Suleiman Kumchaya.

3. Ben Kiko (Benedict Kikoloma - Homeboy) - Wakati wa vita ya nduli Amin.

4. Leonard Mambombotela???

5. Idd Rashid Mchata - Mchatta (kulikuwa na KM Chadema/Mtangazaji na Refa (nimekumbushwa).

6. (Abdul Masoud)inasemekana aliuawa kwa utapeli 80's. Wamenikumbusha.
7. Mzee Kijaruba Abdallah Mlawa.

8. Mikidadi Mahmoud. (http://www.bongocelebrity.com/2009/03/12/tanzania-rhythm-rtdmikidadi-mahmoud/).

9. Julius Nyaisanga.

10. Sango Kipozi.

11. Charles Hilary.

12. Mshindo Mkeyenge.......

safi sana Mkuu - memory nzuri - tumewakumbuka wengi sababu wakati huo Radio ilikuwa moja tu - mi nilipenda kipindi cha michezo - mbili kasoro robo na majira saa tatu na jambo asubuhi----

Sikonge kuna wimbo huu nafikiri utaukumbuka

--- kumekuchaa jamaa kumekuchaaa ----majogoo vijijini wanawikaa----wananchi amkeni tufanye kazi sasaaa......tusonge mbeleee - tosonge mbeleee

Nikisikia unapigwa basi najua tayari kumekucha kweli - kujiandaa kwenda shule....Hapa nakumbuka ujamaa ujamaa vile duh.
 
Kuna kipindi cha weekend kilikuwa kinaitwa club raha leo show mwakikumbuka watu si makelele na magitaa yanachapwa si mchezo na je kwa wale wa Arusha mwamkumbuka Leonard Mambo Mbotela wa KBC na jw huu ni uungwana? BTW mie bado nasikiliza TBC taifa radio yenye watangazaji makini, vipindi makini na wamemaintain kama miaka hiyo si mibitoz na micheck sistaz ya leo inazikilira redio ya malimbukeni wenye shuleless wa CLOUDSSSSSS
 
Hivi ni kwanini Sued Mwinyi siku hasikiki na hasa kwenye mpira? Yule bwana anaweza sana kutangaza football bana
 
Nakumbuka enzi hizo kipindi cha mama na mwana cha Debora Mwenda watoto tulikuwa hatukosi. nakumbuka Jumamosi mchana wakati kipindi kipo hewani watoto mmejikusanya wenyewe kwenye radio mbao yenu kunasa hadithi (ua jekundu) ili jumatatu ukaisimulie darasani.
Watoto wa siku hizi sijui hata kama huwa wanasimuliana hadithi huko mashuleni jamani.
 
Back
Top Bottom