Tujikumbushe vita vya pili vya dunia. Kumbe wazungu wanaweza kutwangana hivi?

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,648
3,938
VITA VYA PILI VYA DUNIA.

Wakati Ujerumani iliposhambulia Poland, nchi hiyo ilikuwa na mikataba ya kulindana na Uingereza na Ufaransa. Hivyo ilibidi Uingereza na Ufaransa zitangaze hali ya vita dhidi ya Ujerumani. Serikali za Australia, New Zealand, Nepal, Afrika Kusini na Kanada zilishikamana na Uingereza kwa kutangaza vita dhidi ya Ujerumani. Umoja wa Kisovyeti ilikuwa na mkataba wa siri na Ujerumani ikaweza kuchukua nafasi ya kuteka sehemu kubwa za Poland ya Mashariki.

Baada ya uvamizi wa Poland hali kwenye mpaka na Ufaransa ilibaki kimya ingawa vita ilikuwa imeshatangazwa. Uingereza ilipeleka sehemu kubwa ya jeshi lake huko Ufaransa kwa kusudi la kutetea nchi hiyo kama Ujerumani itashambulia.

USIJE UKASIKIA MIAKA MICHACHE IJAYO RAIA MAREKANI WATAFUTA UKIMBIZI NA KUKIMBILIA SOMALIA NA WANAOMBA UNO IWASAIDIE

DUNIA HII UIONE HIVI HIVI. UNAJUA YA JANA LKN YA KESHO HUYAJUI
 
Kitu ambacho hujakijua ni hiki
"TEMBO WANAPOPIGANA KINACHOUMIA CHA KWANZA NI NYASI"

hao wababe wakianza kuzichapa nchi zitakazoanza kuumia ni hizi za afrika na Arabs kwanza kabla hawajaanza kushambuliana kwenye nchi zao.

Marekani au hizo nchi nyingine za Nato zikipigana na Urusi majeshi yao yatakutania Kwenye nchi ambazo sio wanachama wao na huko ndipo parakuwa uwanja wa vita, mfano mzuri ni Ukraine, na hicho kinachoendelea middle East ambapo bado wababe hao hawajaingia kamili japo kuna kila dalili wakaindia
 
Mkuu ,swala la unyasi nila kujitakia tu nadhani limepitwa na wakati

Tuzingatie ukraine -urusi war ngano tumelia sana lakini kuna mashamba yametengwa huko manyara kwajili ya kilimo hicho lakini gvt zetu zimeufyata tu
 
Back
Top Bottom