Tujikumbushe sakata la Rada

tusubiri tuone kama watakaofikishwa mahakamani ni dagaa au kambale.. au kama Papa na wenyewe watakuwemo!
 
..damn these mofos it was a forgotten pain lakini again boooom...we have the case here but we dont have names,what a crap!
 
Mimi nasema this is a well planned move.Jk hopped that the Kabwe issue could be covered by Taifa stars if they would have won the fixing match pale Taifa . Ndiyo last kadi ya JK ilibaki maana alijua hawawezi kushinda ili apate nafuu.Kumtumia Mahalu kama ngozi ya kinga ilikuwa ngumu maana alishatumika katika kumtulizia DITTO.

Nasema Hosea ni mnafiki mkubwa na hii ni issue ya Zitto inawala wanatafuta namna ya kuzima madai ya ufisadi serikalini. Sina imani na wewe JK , CCM na hata wewe mpambe Hosea . Hakuna lolote litakalo tokea ila wanatafuta pa kutokea tu.

Natoka naenda Amboni leo narudi kesho kusoma na kujua zaidi .
 
Kama ni kweli kuwa bwana Hosea ametoa kauli hii sitegemei kuwa atakuja na kauli reversed.
Wacha tusubiri, hapo juu tumesoma tu kuwa kunategemewa kufanyika mechi ya KASHFA YA RADAR dhidi ya TAKUKURU. Uhakika wa mpambano huo kufanyika ni jambo la kusubiri.
 
Hosea alishasema PCCB haiwezi kumchunguza Mkapa. Kwa hiyo tutegemee kuona dagaa tu wakishughulikiwa. Haya yatakuwa mazingaombwe ya mwaka natabiri!
 
mh,mie nilifikiri tutaanza na BOT maana ndio kashfa kubwa katika historia ya bongo,.Sina data za kutosha ila nahisi fedha zilizoibiwa BOT zingeweza kununua hata hizo radar 10,naona hii ni danganya toto,upelelezi utafanyika lakini lawana zitakuja kutupia Serikali ya Blair.
 
JF siyo mahala pa kurushia watu matusi.. hapa ni hoja juu ya hoja.. matusi hayastahili JF.. sema kuchukizwa kwako au kebehi ukitaka, lakini mambo ya matusi ya nguoni tunayapinga.
 
Radar partners split up as prosecution beckons

-PCCB expects to file charges through DPP within next three months

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) is finalising a criminal prosecution case against at least one possible suspect in the 28 million pounds sterling (approx. 70bn/-) military radar deal approved in 2002 by the third phase government under former president Benjamin Mkapa.

''We are almost done with investigating this case, and I think we have a case,'' PCCB director general, Edward Hosea, was quoted by Britain's Financial Times newspaper in a newly-filed report from Dar es Salaam.

The highly reputed British defence manufacturer company BAE Systems is understood to be facing fresh pressure over the sale of the radar system to the Tanzanian Government, a deal now under parallel investigations by the UK's Serious Fraud Office and its Tanzanian counterpart, the PCCB.

At the heart of both probes are payments amounting to about 30 per cent of the contract's value, allegedly made by BAE Systems to a Tanzanian agent who helped broker the deal.

Hosea said he expected within the next three months to ask the director of public prosecutions (DPP) to file criminal charges, although according to him, he could not name his targets as the investigation is on-going.

However, people close to the investigation have told the Financial Times that Hosea is not expected to target BAE.


Meanwhile, according to the PCCB boss, the SFO is assisting by finalising the 'natty gritty' of 'tracking the money'.

Investigative interest in the radar deal has been rekindled since the British Government in December ordered the SFO to drop its probe into the 20-year-old al-Yamamah deal for BAE to supply Saudi Arabia with fighter jets. The US Justice Department has since launched its own investigation into whether that deal broke anti-corruption laws.

The SFO is continuing to investigate allegations of bribery by BAE in South Africa, Romania, Chile and the Czech Republic, as well as Tanzania.

SFO assistant director Ms Helen Garlick said both her agency and the PCCB were cooperating to complete investigations into why BAE used a British Virgin Islands company to enter into an agreement with a Panamanian company to provide 'advice and various services' in connection with the Tanzanian radar deal.

Under this agreement, Ms Garlick claimed, BAE made payments in excess of $11m (approx. 14.3bn/-) to one Shailesh Vithlani, who is understood to have been the agent behind the deal through his Dar es Salaam-based company Merlin International.

SFO investigators visited Dar es Salaam, Tanzania's capital, last year and interviewed both Vithlani and Tanil Somaiya, his Merlin International business partner at the time of the deal.

Said Ms Garlick: ''We have nothing but respect for the integrity and persistence of the PCCB. We have been working closely with them and will continue to do so.''

A BAE Systems company spokesman said the company was also cooperating fully with the SFO investigation. ''As this is a continuing criminal investigation, it would be inappropriate for us to comment on the substance of the investigation,'' the spokesman said, adding: ''This cannot of course be taken as any kind of admission.''

Lawyers for Somaiya said he ceased being a shareholder and director of Merlin International on January 8 this year, and added: ''Our client had no prior knowledge and was not aware of the alleged $11m commission payment by BAE to Vithlani at all.''

At the office of Vithcorp Food Packers, another company owned by Vithlani in Dar es Salaam, staff said the businessman - who holds a UK passport - was out of the country. He did not respond to a request for comment.

According to the findings of earlier investigations by THISDAY, Merlin International Limited is a small, low profile local company but with established big business contacts in government circles, whose meteoric rise can be traced back to some 20 years ago in the lakeside city of Mwanza.

It is understood that the company is actually the joint brainchild of both Vithlani and Somaiya, who grew up together as bosom friends in Mwanza.

Records show that Merlin International was originally registered on March 27, 1986, with Vithlani (8,000 shares) and Somaiya (2,000 shares) identified as its two listed shareholders at the time of its formation.

It began operating in Mwanza Region in relative anonymity, dealing in general merchandise and imported goods, and in August 1998 a report was filed with the registrar of companies to indicate that the company had shifted the location of its main offices to Dar es Salaam.

Since then, the company has become inexorably linked with some of the country's biggest defence procurements, including the controversial military radar transaction now under official investigation.

But while Vithlani continues to serve as Merlin International's chairman and managing director, it now appears that Somaiya - a recognized Tanzanian national who also owns other local companies including telecommunications entity Shivacom Limited � has parted ways with the company.
 
Mtuhumiwa kashfa ya rada afikishwa kizimbani Dar
Na Festo Polea

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Takukuru), imekamilisha upelelezi wa tuhuma za rushwa kuhusina na utata wa ununuzi wa rada na mmoja wa watuhumiwa katika kashfa hiyo, Shailesh Pragji Vithlani, amefunguliwa mashitaka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar salaam, ili kujibu tuhuma zinazomkabili.


Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za taasisi hiyo, Mkurugunzi wa Idara ya Elimu kwa Umma wa Takukuru, Mary Mosha, alisema mshitakiwa huyo alibainika kushiriki katika mlolongo wa ununuzi wa rada kutokana na uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo.


Alisema taasisi hiyo imeshafungua kesi namba 1474/2007 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya mtuhumiwa huyo, itakayokuwa chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Sivangilwa Mwangesi.


?Kwa sasa natangaza rasmi kuwa mshitakiwa popote alipo duniani anatafutwa kwa ajili ya kujibu mashitaka yanayomkabili na asipofanya hivyo tutamkamata kwa vile hati ya kumkamata imeshatolewa na mahakama? alisisitiza Mosha


Mosha alisema Mshitakiwa huyo anayetafutwa ana uraia wa Tanzania na Uingereza, hivyo wamewasiliana na Polisi wa Kimataifa (Interpol), ili popote alipo duniani aweze kukamatwa na kujibu tuhuma zinazomkabili.


Hata hivyo Mkurugenzi huyo alipotakiwa kuwataja watuhumiwa wengine waliobainika kuhusika na ununuzi huo wa rada, alikataa kwa madai kuwa taasisi hiyo imeanza kumfungulia mashitaka mtuhumiwa mmoja kwa kufuata taratibu na sheria za Takukuru na kwamba baadaye wataendelea kuwashughulikia wengine.


Source Gazeti Mwananchi
 
Hii habari nayo??
kafikishwa mtuhumiwa mahakamani ama jarada la kesi tu??
Nina wasi wasi hii yaweza kuwa danganya toto, kwani kama atakamatwa vigogo walio husika akiwepo mtukuka wetu mkuu aliye staafu Siasa atakuwemo je hilo litawezekana? ama ndo itaishia hivo mtuhumiwa anatafutwa bado?
 
Jamani, jamani tujaribu kutumia heading za kueleweka. Sasa unaposema mtuhumiwa kafikishwa mahakamani wakati ndani ya habari hiyo inadai kuna Warrant already issued ya kumtafuta huyo mcheza dili watu inatuchanganya kidogo.
 
Ana uraia wa Uingereza na Tanzania? Imekuwaje hapa? Jamaa ana uraia wa nchi mbili, wakati Watanzania Wazawa wakipata uraia wa nchi nyingine wananyimwa magamba ya Tanzania?

Kama wanajua ana uraia wa nchi mbili, mbona hawakumnyang'anya uraia wa Tanzania?

Tunawabana watu wetu huku tunawaachia wageni kutumia faida ya uraia wa nchi mbili.
 
Posted Date::12/10/2007
Watanzania wenye fedha nje waanza kuchunguzwa
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

SERIKALI imeanza kuchunguza sehemu ya fedha za baadhi ya Watanzania ambazo zipo nje kuona kama zimepatikana kwa njia ya rushwa.

Miongoni mwa nchi ambazo ufuatiliaji huo unafanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) chini ya Mikataba ya Kimataifa ni zile ambazo zipo katika mwambao wa Bahari ya Hindi na nyingine za Asia.

Fedha hizo zinachunguzwa chini ya mikataba hiyo ambayo ni pamoja na wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Rushwa, Mkataba wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, ambayo Tanzania imeridhia.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philip Marmo, alilithibitishia gazeti hili ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki iliyopita kuhusu ufutiliaji wa fedha hizo.

Hata hivyo, Marmo alikataa kutaja majina ya mabenki hayo ambayo uchunguzi huo unafanyika kwa ushirikiano na vyombo vya nchi husika.

Lakini alifafanua kwamba, Tanzania imetia saini mikataba hiyo ambayo kwa ushirikiano na nchi nyingine inaiwezesha kuwakamata na kuwarejesha nchini watuhumiwa ambao watakuwa wakichunguzwa kwa kutorosha fedha kwa njia ya rushwa.

Waziri Marmo alisema zipo fedha nyingi ambazo wanazichunguza kuona ukweli wake na watuhumiwa. "Zipo fedha nyingi tu tunazichunguza kuona kama zimetoroshwa na watuhumiwa warushwa," alisema Marmo.

"Tunajua kuna watu wanaweza wakawa wamekimbia, lakini tunachosema chini ya mikataba hiyo watarejeshwa wakibainika," alisema. Alisema chini ya mikataba hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru anaweza kuwasiliana na wa nchi husika na kuonya kwamba watuhumiwa wote watakaobainika watarejeshwa nchini.

Hata hivyo, alifafanua kwamba uchunguzi huo hauhusu watuhumiwa ambao wameweka fedha zao halali nje na kwamba wako huru kufanya hivyo. "Lakini Marmo anaweza kuweka fedha nyingi, bora tu zisiwe fedha haramu zilizopatikana kwa njia ya rushwa," alisema.

Kuhusu biashara ya fedha haramu nchini, Marmo alikiri kuwepo tatizo hilo ambalo alisema Tanzania imekuwa ni moja ya vituo vikuu. Alisema hata uamuzi wa kuanzisha Kitengo cha Kupambana na Fedha Haramu, haikuwa ya kukurupuka bali ilitokana na serikali kubaini hilo.

"Biashara ya Fedha haramu ipo kweli nchini, fedha zinatoka katika baadhi ya nchi kama za Asia, ndiyo maana tulipoanzisha kitengo cha kuzuia fedha hizo, tulijua," alisisitiza Marmo. Waziri Marmo alisema baadhi ya biashara hizo za fedha haramu zilikuwa ni kutoka katika baadhi ya nchi za Asia.
 
.....SERIKALI imeanza kuchunguza sehemu ya fedha za baadhi ya Watanzania ambazo zipo nje kuona kama zimepatikana kwa njia ya rushwa......Miongoni mwa nchi ambazo ufuatiliaji huo unafanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) chini ya Mikataba ya Kimataifa ni zile ambazo zipo katika mwambao wa Bahari ya Hindi na nyingine za Asia....

Hizo ni blah blah za viongozi wetu- nadhani tunasema wanatuyeyusha tu- hakuna jipya na pia sioni sababu kwani wala rushwa wote wanawafahmu vizuri na wengi wao mwezi huu wanapeana rushwa kwa kigezo cha sikukuu!

Je utatafutaji mnyama anayekula kuku wako wakati umefuga vipanga na vicheche kwenye banda lako la uani?

Angekuwa wanataka kufanya kweli wala wasingesema, tungestukia tu vigogo wengi wamewekwa ndani nk.
 
Wacha we.... Watawapata sana, wakianzia na Tangold, Meremeta, Deep Green, Import Support, EPA, etc fedha zote hizo zinjulikana zilikokwenda na wahusika wako wamejaa tele....
 
Back
Top Bottom