Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,890
Titus Kaguo, London
HabariLeo; Monday,February 19, 2007 @00:06
Ataka ichunguze kama kuna kigogo alihusika
RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Taasisi ya Kuzuia Rushwa Tanzania (PCB),
kuchunguza kama kuna kiongozi wa Tanzania alihusika kupokea rushwa wakati
wa ununuzi wa rada inayodaiwa iliongezwa bei ya mauzo kwa zaidi ya nusu ya
bei halali.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizungumza jijini London na Watanzania
wanaoishi Uingereza, ambao aliwapa uwanja wa kuuliza maswali kuanzia
dakika ya kwanza ya kukutana nao. Kauli hiyo ilitokana na kauli ya Aman
Kagugila, aliyedai rushwa imegeuka ni kazi za watu kujiajiri ambayo pia
aliihusisha na suala la ununuzi wa rada kuwa lilikuwa na rushwa, lakini
Serikali haijatoa msimamo zaidi ya Uingereza kusaka wahusika.
Rais Kikwete alisema mjadala uliopo hivi sasa hapa Uingereza ni nani
waliokula fedha hizo ambapo alisema Maofisa wa Ofisi ya Uchunguzi (SFO)
walifika Dar es Salaam kuomba wazungumze na wakala, Serikali yake ikatoa
kibali na hata wakitaka kurudia basi watapewa kibali.
Lakini Rais Kikwete alisema kwa upande wa Tanzania, amewapa jukumu PCB
kuchunguza akina nani inawezekana walikula fedha hiyo. Nimewaagiza PCB
waangalie hawakupata fedha huku? Na mpaka sasa tunaendelea kuchunguzana
kwa upande wetu na nadhani tuliachie hapa sipendi kutoa maoni yangu,
tuiachie taasisi, alisema.
Sakata la rada limekuwa likiwagusa Watanzania wengi hata nje ya nchi, kwa
kile kinachoelezwa kuwa iliuzwa kwa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 40, bei
inayodaiwa kuongezwa kwa nusu ya bei ya halali na maofisa wa Euro Space,
Kampuni ya Serikali ya Uingereza.
Akizungumzia mikataba ya madini, Rais Kikwete alisema pia ameagiza
mikataba ya masuala ya uchimbaji wa gesi na utafutaji mafuta yote
iangaliwe upya ili yasije kujitokeza ya migodi ya dhahabu.
Akifafanua zaidi, alisema mfumo wa mapato kwenye dhahabu haukuwa na makosa
kwani unaeleza waziwazi kuwa watalipa asilimia tatu ya mrabaha na asilimia
30 ya kodi, lakini tatizo lilikuwa kwenye kifungu kinachosema ulipaji wa
asilimia 30 utafanywa baada ya kampuni kupata faida.
Alisema kutokana na hilo, aliona kabisa wachimbaji wa madini wanaweza
wakaondoka bila kulipa kodi hiyo kwani kutokana na mitaji mikubwa ya
kwenye uchimbaji urudishwaji wa faida kamili unaweza kuwa mgumu hivyo
madini yakaisha bila wao kulipa kodi ya asimilia 30.