Tujikumbushe: Lissu ni Mshindi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,885
TUNDU LISU NI MSHINDI

Na, Robert Heriel

Moja ya sifa ya Mtumishi wa Mungu ni kumshuhudia Mungu kwa Matendo makuu aliyoyafanya. Tumezoea watumishi wa Mungu tuendapo kwenye nyumba za ibada wakituhadithia simulizi za kwenye misahafu kwa habari ya mambo yaliyopita miaka ya kale. Wote 8tumehadithiwa miujiza iliyofanywa na Mungu katika kipindi cha kale. Mathalani, muujiza wa Yona au Yunus kumezwa na samaki pasi na kufa, muujiza wa Daudi kumpiga Goliath au Jaluti, muujiza wa Yesu au Isa kufufuka na visa vingine vilivyomo kwenye Misahafu.

Ukweli ni kuwa visa hivyo hakuna miongoni mwetu aliyeshahidi wa kweli bali tunaviamini kwa vile tunamuamini Mungu kuwa anaweza kutenda jambo lolote.

Mungu atamkumbuka na kumbariki Askofu Mwingira wa Kanisa la EFATHA kwa kuweza kushuhudia ukuu wake kwa Tukio la kimiujiza lililomtokea Bwana Tundu Lissu.

Kama kuna kisa ambacho kingepswa kisimuliwe ndani ya nyumba za ibada kwa dini zote hapa nchini kama reference ya maajabu ya Mungu na uweza wa Mungu basi ni kisa cha Tundu Lissu.

Nampongeza Askofu Mwingira kwa kuweza kuliona hilo na kulisemea ndani ya kanisa lake.

Kwa upande wangu, mimi ni msomi mkubwa wa vitabu vya dini zote bila kujali mafundisho yake. Kwa uzoefu wa mafunzo niliyoyapata huko, ninaungana na Askofu Mwingira Tundu Lisu ni Mshindi.

Watu wote wenye elimu za kiroho, wenye elimu ya dini wataungana na mimi kuwa Mungu yupo upande wa Tundu Lisu.

EMBU FIKIRIA MAMBO HAYA
1. Tundu Lisu kapigwa Risasi kumi na sita (16) lakini kachomoa, Mungu kamponya. Tundu Lisu kashinda Risasi, kashindwa kuangamizwa na Risasi kwa uwezo wa Mungu. Bado usione kuwa Mungu yupo naye. Hata kipofu anaweza kuliona hili. Hata mtoto mdogo anaweza kulitambua hili.

2. Tundu Lisu licha ya kuwekewa vikwazo vya kila namna lakini baso anazidi kupasua anga. Nani asiyejua kuwa Lisu alifukuzwa ubunge, nani asiyejua kuwa Lisu habari zake hazitangazwi kwenye media kubwa, nani asiyejua kuwa Lisu alinusurika kufa kwa kupigwa risasi na waovu.

Lakini licha ya hayo jamaa anazidi kupata kasi, watu hawatangaziwi lakini wanajaa kwa wingi, hujiulizi ni kwa nini, hakuna matangazo, hakuna wasanii, hakuna burudani, miundombinu ya vipaza sauti ni duni lakini watu hawajali wanamfuata, hujiulizi sababu ni nini? Lisu ni mshindi

3. Lissu ni Jasiiri, anatumia kanuni isemayo; Binadamu wote ni sawa mbele za Mungu. Pia usiabudu miungu mingine ila Mungu Peke yake.

Moja ya dalili ya mtu akaaye na roho wa Mungu ni hili. Mtu wa Mungu anawachukulia wanadamu wote ni sawa mbele za Mungu. Hasujudu mtu kwa cheo chake, hasujudu mtu kwa pesa zake, asujudu mtu kwa nguvu zake, ukikosea anakukosoa kwa nguvu zote bila kukuonea haya. Lisu mara kwa mara amesisitiza kuwa Rais ni mtu kama watu wengine. kwa nini asishtakiwe, yeye ni nani wakati ni binadamu kama watu wengine. Lisu mara kwa mara ameonyesha msimamo wake dhidi ya Rais pale amuonapo Rais akikosea.

Lisu anatabia za kinabii, moja ya tabia za kinabii ni kukemea uovu pasipokujali mtenda maovu atafanya nini.

4. Lissu anaogopeka
Mtu yeyote ateteaye haki na akabaki na msimamo huo huo mpaka kufikia kupata madhara na akachomoa, mara zote huogopeka. Kwani watu wote huanza kuhisi kuwa hayupo pekeake, kuna nguvu ya ziada nyuma yake.

Nitatoa mifano,

Daudi alikuwa haogopwi mahali popote pale. Lakini tukio la kumchapa Goliath lilibadilisha taswira nzima ya fikra za watu dhidi ya Daudi. Hata hivyo bado Mfalme Sauli hakumuogopa Daudi. Mpaka siku Mfalme Sauli alipotaka kumuua Daudi kwa kumpiga Mkuki akamkosa, na kama Daudi angetaka kumuua angemuua lakini Daudi aliruka dirishani kutoka ghorofani akasepa. Hapo Mfalme Sauli akaogopa, akajua kuwa sipigani na Daudi bali napigana na Nguvu nyingine ya ziada ambayo baadaye aliijua ni nguvu ya Mungu.

Mfano wa Pili,
Kina Shadrack, meshack na Abednego, hawakuwa chochote mbele za watu lakini walikuwa ni watu wazito mbele ya Mungu. Watu walikuwa wanawachukulia poa, lakini baada ya kukataa kusujudia sanamu ya Mfalme Nebukadreza, huku wakiwa na ujasiri kuwa hata Mungu asipotusaidia mbele ya Moto wa Tanuru bado hawatasujudia sanamu. Walitupwa kwenye tanuru, na hapo hapo muujiza ukatokea, hawakuungua. Wakaambiwa watoke nje ya Tanuru. Walitupwa wakiwawanazomewa lakini wakatolewa kwa kunyenyekewa. Kuogopwa.

Mifano ipo Mingi, ipo mifano ya Daniel, Paulo na Sila, Mtume Muhamad.

Kitu kimoja kikubwa watu wasichokijua ni kuwa, mtu yeyote anayepingana na udhalimu kwa ngazi ya kitaifa au kimataifa huyo ni Mtume wa Mungu.

Tundu Lisu ni Mshindi kwa sababu yupo na Mungu.

5. Kukimbia uhamishoni
Mashujaa wengi karibu wote walikimbilia uhamishoni kwa sababu mbalimbalio. Nitaanzia kwenye Biblia, Nabii Musa alikimbia Kutoka Misri kwenda nchi ya Midian, kisa na mkasa alikimbia mkono wa Farao baada ya kumuua mmisri akiwa anamtetea muisrael mwenzake. Baadaye alirudi kuwakomboa waisrael.

Nabii Eliya alimkimbia Malikia Yezebeli ambaye alitaka kumuua kisa na mkasa alikuwa mkosoaji mkubwa wa ufalme wake, na hakutaka kuungana naye. Baadaye Eliya alirudi akawaangamiza majeshi ya manabii bandia wa Yezebeli

Nabii Daudi alikimbia Yerusalemu akimkimbia Mwanaye Absalomu ambaye alitaka kumpindua. Baadaye Daudi alirejea na kuikomboa nchi yake.

Yesu wa Nazareth, alitoroshwa na kukimbizwa uhamishoni huko Misri akitokea Uyahudini akimkimbia Mfalme Herode aliyetaka kumuua. Yesu alirejeshwa na wazazi wake kutoka Misri uhamishoni na kurudi Uyahudini baada ya Mfalme Herode Kufariki.

Mifano ni Mingi.

Tundu Lisu naye anaingia kwenye Rekodi ya kupelekwa uhamishoni baada ya kupigwa Risasi 16 na kuponeshwa na Mungu.

Wanaosema Lisu ni Mbeligiji na kibaraka wa wabeligiji wasilaumiwe. Bali waonewe huruma kwa sababu hata zamani walikuwepo waliosema;

Yesu ni Mmisri kisa na mkasa alikimbizwa huko Misiri kwa kuogopa kuuawa na Mfalme Herode
Pia walisema Musa ni Mmidiani kisa na Mkasa alikimbia mkono wa Farao na kulowea umidiani mpaka akapata mke huko

Kumbuka: Yesu alikaa uhamishoni zaidi ya miaka 10
Musa alikaa uhamishoni zaidi ya miaka 20 alirudi akiwa na miaka 40
Musa alikaa uhamishoni kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Tundu Lisu amekaa uhamishoni kwa miaka mitatu.

Kitu kimoja cha kuzingatia ni kuwa watu wote waliopambana na watu Kama Tundu Lisu walikuwa wanajua wanapambana na Mungu. kutokana na miujiza iliyokuwa inatokea.

Hata sasa wanaopambana na Lisu wanafahamu kuwa wanapambana na Mungu. Huwezi mpiga mtu Risasi 16 alafu akawa hai alafu bado usielewe upo kwenye vita na nani. Labda uwe kichaa.

Mara nyingi wanaoendelea kupambana na watu wa Mungu huishia kuangamia. Huwezi pambana na mshindi ukabaki salama. Kitendo cha Mungu kukuonyesha uwezo wake bila kukuathiri wewe ni dalili tosha kuwa unapewa WARNING, na yeyote ashupazaye shingo yake itavunjika.

Nashukurru sana Askofu Mwingira wa Kanisa la EFATHA kwa ujumbe wako. Mwenye kusikia na asikiye, asiyetaka kusikia azidishe kiburi na jeuri.

Mshindi hatishiwi na jeshi
Mshindi hatishiwi na silaha
Mshindi hatishiwi na jela
Mshindi hatishiwi na maneno ya kipuuzi
Mshindi hatishiwi na matokeo ya kutetea haki

Nami haya nimeyashuhudia kwa macho yangu, Ole wangu nisipompa Mungu utukufu kwa yale niliyoyaona kwa macho yangu.

Mwisho: Mche Mungu na uzishike amri zake, kwa maana muda tulionao ni mchache wala asitokee wa kutulaghai.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro
0693322300
 
Back
Top Bottom