Tujikumbushe enzi za madaladala maarufu

Tujikumbushe enzi za madaladala maarufu

Iringa-Tanangozi.....Embakassy na Kombora
Songea...Sijui ilikuwa inaelekea wapi kutoka town kupita Bombambili--CHONAPI (hiace hiyo)
kuna maneno ilikua inatoka iringa mjini-kwenda mtera shalawambe sitasahau hili basi lilikosakosa kutubwaga kilimani km kilomita tano kufika mtera,humo ndani ya basi ilikua ni kama kilabu cha ulanzi maana toka tunatoka iringa si dereva,tingo,abiria wote mnakamata ulanzi huku basi linakata mbuga toka asubuhi mtera tumefika saa sita usiku daah!
 
Mwenge Posta- NGW'ANA SHUBERT
Masaki Posta- GOODLUCK,KABIBII na MASAKI ONE POPOZ aka POPO BAWA Double Coaster la Waziri wa enzi hizo Kiula...
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Njia ya Ubungo ndo ilikuwa maarufu kwa usafiri wa mabasi yale..kuna basi lilikuwa linaitwa Simba Ruala, Dege, kuna Dau la Mnyonge, kulikuwa kuna linginelinatwa Jadide kama sijakosea enzi hizo basi ni KAMATA, UDA za hizi gari binafsi ni Binkleb, Yarabi Toba na mengineyo kwa magari ya kusafirisha mizigo yalikuwepo KAURU, KAUDO,KAUMO.....shopping wote tulikuwa tunaenda Sokoni Kariakoo, kumbi za Starehe ni DDC Kariakoo, DDC magomeni Kondoa, DDC keko...Bendi Mashuhuru ni JUWATA Jazz, Bantu Group,Ochesta Safari sound, Mchora Katuni ni Ibra Radi Washokera, gazeti maarufu ni Mfanyakazi na Sani, timu machachari ni Nyota Nyekundu chini ya Keptain Rosta Ndunguru na Sentahafu wa Frank Kasanga Bwaliya, mchezaji aliyekuwa na matege ya ukweli ni Gebo Peter, Mshambuliaji aliyekuwa na mashuti mpaka akapasua mpira alikuwa Juma Mgunda,Mchezaji aliyekuwa anapiga vichwa sana ni abeid Mziba, Timu iliyokuwa inaogopewa ni Wana TP Lindanda Wimbo wa Mpira uliokuwa maarufu ni Yanga kainamaaaaaa Simba ............................
 
Tuliomaliza Jiteute na St. Antony mnakumbuka BOMBASTIK SOUND?

Ngoma tunaiwahi saa 12 kasoro pale mwenge ikielekea posta kuwahi to mbagala kisha ruti zake mbagala posta. Jamaa walikuwa fair sana hakuna mwanafunzi kusimama ktk siti akiwahi na ilikuwa ahsubui inasanya madenti tu! ila nasikitika dada zetu ndo walijipeleka kuwa chambo eti wasilipe nauli.....
 
Mwenge Posta- NGW'ANA SHUBERT
Masaki Posta- GOODLUCK,KABIBII na MASAKI ONE POPOZ aka POPO BAWA Double Coaster la Waziri wa enzi hizo Kiula...
NGW'ANA SCHUBERT mkuu ni jina la kibantu na kijerumani hilo shekhe.
 
UBUNGO-POSTA........"MILANO"
Y
alikuwa magari makubwa automatic gear......dereva wake mmoja akiitwa ukwaju huyu alikuwa mtoto wa aliyekuwa mwenyekiti wa SIMBA S.C.......Kisha dereva mwingine akiitwa ABDALAH MZURI...huyu alikuwa dereva wa VIDETA LINE(motel villa de tanzanie)
 
Mtama kwa watoto; sikumbuki ilikuwa ni wapi

Iringa walikuwa na Kilabu cha kijiji; bedford flani ndani mlikuwa mnakaa mkao wa chai maharage
 
Jamani mbona mmesahau Kitmeer yale ya wahindi au Air Chalinze haya yalitamba sana
All in all hakuna mfano wa mabasi ya Riziki kwa Mungu na Golo kule Temeke madereva na makondakta wake wote walikuwa vichaa kwa mwendo wa kasi
Umenikumbusha mbali ndugu yaani enzi zile za Siri yako, Zafanana, Zainab nk yaliyoku wakienda mikoani
 
msisahau Bijampola, sijui kama ilifanya safari hata moja Dar -Bukoba, ndugu yangu alikata ticket kesho siku ya kusafiri hakukuwa na basi wala nini,
 
Kuna lile lilikuwa linaitwa Scholastika, kuna jamaa yangu alikuwa analizima sana na alikuwa hapandi lingine kama hana haraka mpaka lije scholastika. Nadhani mle ndani kulikuwa na muziki wa kukata na shoka 🙂
 
I hate you!


Kosa langu lipi mbaka uni hate hivyo? mimi nakumbuka nikenda shule enzi zile naona hizo chai maarage sijui daladala , zikipita tuu, nashangaa kibaya kipi kueleza experience yangu. Nakumbuka nilikua namuona Fareed akining'inia mlangoni kwenye zile za Posta - Masaki , ile memory mbaka leo iko kichwani


Hivi Fareed yuko wapi????
 
Zamazamani Bila shaka hapo kwenye Matema Beach unamaanisha Shella Beach ambayo yalikuwa mabasi maarufu Ubungo-Posta, pia kulikuwa na Mtoto wa kaya
 
Tuliomaliza Jiteute na St. Antony mnakumbuka BOMBASTIK SOUND?

Ngoma tunaiwahi saa 12 kasoro pale mwenge ikielekea posta kuwahi to mbagala kisha ruti zake mbagala posta. Jamaa walikuwa fair sana hakuna mwanafunzi kusimama ktk siti akiwahi na ilikuwa ahsubui inasanya madenti tu! ila nasikitika dada zetu ndo walijipeleka kuwa chambo eti wasilipe nauli.....

Hapo kwenye BOMBASTIC SOUND nafikiri/nakumbuka ni BULLET TRAIN. Basi lililokuwa na muziki mzito na mwendo mkali na Dereva kuendesha kwa mbwembwe sana.
 
Nani nalikumbuka "KIWENE"?
Kwa mabinti wa watu walikuwa wenyewe. Always utakuta kabinti kashule kamekaa mbele kwa dereva.
 
Naona mnaisahau njia ya Gongolamboto - Kariakoo, wakati ule kituo kilikuwa mtaa wa kongo ngoma zinaingilia mtaa wa msimbazi!

Kulikuwa na

.Mshua,( hizi zilikuwa mbili, scania basi kubwa)
.NDL
.Kobis (Haka kalikuwa kadogooooooo)
.Six show ( Hizi zilikuwa rossa)

Ilikuwa raha sana kugombania hivi basi aisee
 
Back
Top Bottom