Tujikumbushe enzi za madaladala maarufu

''VIBES'' hiki kiford almaarufu hiace kwa bongo kilikuwa kinapiga ruti pale moshi mjini to kioriloni, ilikuwa na mziki wa kufa mtu,was a first hiace in town kuwa na sound kali namna ile na ilikuwa imerembwa sana maana ilikuwa ni super custom short roof. Si mchenzo 98 hiyo.
 
Akachube!
Yes ngoma nzito!
Skolastika!
Ecarus ( uda)!

mkuu hiyo 'Akachube'
mmiliki wa gari hilo alimaanisha ' I got you baby' wimbo maarafu wa wanamziki wa London- UB40. Naikumbuka sana 'Computer Love'
 
Haya mnakumbuka moody punk, Scaba Scuba, Chisu Papino...zilianza na route na Dar - Moro enzi hizo stendi ilikuwa magomeni mapipa na palikuwa na hoteli maarufu sana ikiitwa michuzi mikali....namkumbuka rafiki yangu catoonist wa aina yake John Kaduma ( RIP)..
 
big up mkuu, umenikumbusha mbali! Enzi hizo tukipanda magari ya UDA, nikitoka M/Chai kwenda Azania sec. tukitelemkia pale fire.
Nilitamani sana kupanda yale mabasi marefu-ekarusi 'kumbakumba'.
Nawashangaa wale wa waliopanda mabasi ya 'embakkasi' kule Songea; Bijampola (bukoba). Issue hapa ni 'daladala'.

umenikumbusha mbali, baadhi ya uda zilikuwa zinaiba route na kugeuzia hapo magomeni m/chai, ilikuwa ni vurugu tupu kupanda gari asubuhi kama unavyoona vurugu za mbagala wakati wa jioni na asubuhi. kipindi hicho morogoro road ni single lane. nilikuwa bado bwa'mdogo miaka hiyo ya 80's na ndio naanza shule ya msingi, toka m/chai kuja shule posta na bi mkubwa. nashukuru Mungu nilibahatika kupanda hayo ma'ekarus, nakumbuka nauli ya mwanafunzi ilikuwa ni senti 50 (thumni!! -naamini wengine hawakuwahi kutumia hizo hela mpaka sasa).

Kulikuwa kuna kitu cha Sea Never Dry, Sponsors, Shella Beach, UDA, Bombastick, City Train, na Vi-bus fulani hivi vina injini ya isuzu - vilikuwa na box body (nadhani ziliundwa hapa hapa bongo).
 
kabombe tours, kkoo - muhimbili, mazee tulikuwa tunakaa seat ya kibench nyuma ya driver ni noma, ila jamaa walikuwa peace. Ila muda mwingi ni kutembea kutoka kkoo mpaka tambaza. Jioni kulikuwa na mabasi ya mashirika yanabeba wanafunzi
 
mbeya kulikua na mwailubi,urassa,sokolo,mbembela,double coaster ya kwanza mbeya nzima el_kibo,karanja ilikua inapiga tripu tukuyu-mbeya mjini,wengine wataongezea.
Bouble coster za kwanza ni BlackBelt,Kyupi Trans wewe!!1990 sema jingine wewe!!:A S 465:
 
Si mchezo mazee,umenikumbusha mbali sana.(tky-kiwira apange bus service) (tandika-s/uhuru bob futo,patan)(tmk/kilwa road-s/uhuru kitmeer ngamia,nyati nk) y/vituka-s/uhuru above the rim"kumba kumba"ukitoa sh50 unamwambia konda kata naul wanafunzi wote.
 
UBUNGO-POSTA........"MILANO"
Y
alikuwa magari makubwa automatic gear......dereva wake mmoja akiitwa ukwaju huyu alikuwa mtoto wa aliyekuwa mwenyekiti wa SIMBA S.C.......Kisha dereva mwingine akiitwa ABDALAH MZURI...huyu alikuwa dereva wa VIDETA LINE(motel villa de tanzanie)

Halafu kulikuwa na tetesi kuwa yalikuwa ya mchungaji mmoja wa kanisa !
 
Sio Matema Beach ni Shella Beach (mziki mkubwa), usisahau Ole wao wafuatao nyayo za simba - Ubungo-Posta

Matema Beach ndio baadaye iliitwa Shella Beach na Baadaye tena Miami Beach. Lkn hayo yote ni majina ya baadaye hapo mwanzo hizo ngoma ziliitwa JADIDE. Lingine la kampuni hiyo ni RIYAMI

Mengineyo Ubungo - Posta

Kokomorwo, Safari, Ndaro, Jay Shankar, Mokasini, Padova, Sai Baba
(miaka ya 85-95)

M'nyamala Posta: Labda Baadae, Chagua Bega na Toto Safaris
 
Umenikumbusha mbali sanaaaaaa.......... Ubungo posta, kulikuwa na dege, simbachawene, simba mawala, toto kanko
 
mbeya kulikua na mwailubi,urassa,sokolo,mbembela,double coaster ya kwanza mbeya nzima el_kibo,karanja ilikua inapiga tripu tukuyu-mbeya mjini,wengine wataongezea.
Mulilege, Mwasalemba! Martin ngulo! ukufuma Ku-mbeje -Kutukuju- kungonde Kyela
 
Back
Top Bottom