Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

Ndio maana nakwambia unameza vitu bila kuelewa,Kuwa Bwana wa Sabato ni kuwa mkuu wa Sabato, maana yake anaouwezo wa kufanya chochote juu ya Sabato na kila kilichopo kwenye Sabato kipo chini yake,AMKA AROON jifunze maandiko na sio Ubishi wa kidini
KWAHIYO NDIO KARUHUSU MUIBADILISHE IWE DDOMINIKA?

MBONA HAKUNA ANDIKO KAIBADILI AMRI

NIPE HILO ANDIKO, NA WHY KWENYE KATEKISIMU HAIPO?
FB_IMG_1540529857229.jpeg
 
Kama unajua vema, KATOLIKI hakuna siku amabaYo hawaadhimishi Misa Takatifu ,kila siku tunaibada, wewe unaye abudu siku endelea maana mmeshageuza Siku kuwa ndio Mungu wenu.
Wewe bhana acha kukwepa kwepa,

Hata mimi siku zote naabudu, ila kuna moja imetengwa ,

Kama katoliki walivyobadili SABBATH TO DOMINIKA
 
Wewe bhana acha kukwepa kwepa,

Hata mimi siku zote naabudu, ila kuna moja imetengwa ,

Kama katoliki walivyobadili SABBATH TO DOMINIKA
Ha ha ha ha kwajibu lako tu hilo nafsi inakukosoa kutoka lini wasabato mnaibada kila siku? Ninao waona kwa Tanzania angalau ni walutheli pamoja na baadhi ya makanisa ya kipentekoste huwa wanakuwa na ibada katikati ya wiki
 
KWA NINI mtu au dhehebu lolote libadili neno lolote kwenye zile amri kumi za Mungu alizozitamka Mungu mwenyewe pale Sinai? Kwa nini hiyo KATEKISIMU isichukue maneno yote ya Biblia kama yalivyo? Amri kumi za Mungu zipo kwenye Kitabu cha Kutoka (Kut 20:2-7)

Kuhusu kubadilisha neno la Mungu Biblia inasema wazi:-
Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.

Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. (Ufu 22:18-19).

Yesu mwenyewe alisema:-
Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.(Mt 5:18)

SASA NINYI WA KATEKESIMU KWA NINI MNAONDOA MANENO NA NUKTA NA MISTARI ????
 
Ha ha ha ha kwajibu lako tu hilo nafsi inakukosoa kutoka lini wasabato mnaibada kila siku? Ninao waona kwa Tanzania angalau ni walutheli pamoja na baadhi ya makanisa ya kipentekoste huwa wanakuwa na ibada katikati ya wiki
Tuwaulize waanzilishi wa ibada ya DOMINIKA
FB_IMG_1540529670203.jpeg
 
Je! Wale Mitume Waliibadili Sabato?

Yakobo, kiongozi wa kwanza wa kanisa lile la mwanzo, aliandika maneno haya kuhusu zile Amri kumi:

"Anayevunja amri mojawapo ya sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja sheria yote. Maana yule yule aliyesema: "USIZINI, "alisema pia" "USIUE." Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini, lakini umeua, wewe umeivunja sheria" - (Yakobo 2:10, 11).

Luka, tabibu na mwinjilisti katika kanisa lile la kwanza, anatoa taarifa hii.

"Siku ya Sabato tukatoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto, ambapo tulidhani kuwa mahali pa kusali. Tuliketi, tukiongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo" - (Matendo 16:13).

Kitabu cha Matendo cha Agano Jipya kinataja mara 84 ilipotunzwa. Sabato hiyo na wafuasi wa Kristo, zote hizo zilikuwa zikitunzwa zaidi ya miaka 14 baada ya ufufuo wa Yesu: Sabato 2 pale Antiokia (Matendo 13:14,42,44); 1 pale Filipi (Matendo 16:13), 3 pale Thesalonike (Matendo 17:2,3), Sabato 78 pale Korintho (Matendo 18:4,11).

Yohana, wa mwisho kufa miongoni mwa wale mitume kumi na wawili, aliitunza Sabato. Aliandika hivi:
"Siku ya Bwana nilikuwa katika Roho" - (Ufunuo 1:10).

Kulingana na maneno ya Yesu, siku ya Bwana ni Sabato:
"Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato" - (Mathayo 12:8).

Uchunguzi wa ushahidi wa maandiko unaoonyesha wazi kwamba wale mitume hawakufanya jaribio lolote la kuibadili siku ya Mungu ya mapumziko kutoka siku ya saba kwenda ile siku ya kwanza ya juma. Agano jipya, linaitaja siku hiyo ya kwanza ya juma mara nane tu. Katika mifano hiyo yote hakuna ambapo siku ya kwanza ya juma inatajwa kuwa ni takatifu, wala hata kudokezwa kuwa tunapaswa kuitenga kama siku ya ibada
 
Kutoka 20

1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
13 Usiue.
14 Usizini.
15 Usiibe.
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.[/QUOTE

Kuba nyingne hapo naona kama ni maelekezo wala sio Amri Mkuu.
 
KAMA HUJUI AMRI ZA BWANA NA UMEDANGANYWA NA MAPADRI UKAPEWA AMRI ZA KATEKISIMU....

MUNGU ANATOA USHAURI WA BURE WAULIZENI NDEGE WATAWAFUNDISHA....


.yer 8;7 Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui AMRI za Bwana.....

USHAURI ...WA MBINGU.........ayubu 12;7 Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha; Na nyuni wa angani, nao watakuambia;

8 Au nena na nchi, nayo itakufundisha; Nao samaki wa baharini watakutangazia.

USHAURI WA BURE KWA WAROMA,WALUTHER, WALOKOLE, N.K
FB_IMG_1540766958378.jpeg
 
BAADA YA KUMTUMIA PAPA PIUS XI BARUA AKITAKA KUJUA UKWELI WA KUBADILI AMRI YA 4,
BWANA J.L.DAY MKATOLIKI HUYU ALIAMUA KUANZA KUTUNZA SABATO.

NAKALA YA BARUA YAKE NA MAJIBU YA PAPA UNAWEZA KUYAPATA HAPA

THE ROMAN CHURCH'S ADMISSION OF CHANGING THE SABBATH

WAKATOLIKI WA LEO, MNA UJASIRI WA KUULIZA VIONGOZI WENU MASWALI ?

IKIWA HADI PAPA FRANCIS 1 , BENEDICT WAPO TWITER NA MITANDAO MINGINE.
FB_IMG_1540769651368.jpeg
 
Dini ni suala la imani - sio la kimantiki. Kubishana kuhusu usahihi wa biblia au ubora wa dini fulani dhidi ya nyingine kwa kutumia logic ni kupoteza muda.
 
Mungu asingeweza kubadili hata yodi [,] moja wala nukta [.] moja ya Sheria yake takatifu
[Amri Kumi] ili kuafikiana na mwanadamu katika hali yake ya kuanguka; maana jambo hilo lingemfedhehesha sana Mungu kuhusu hekima yake katika kuitoa Sheria hiyo [Amri Kumi] ambayo kwayo anaitawala mbingu na dunia hii.

Lakini Mungu aliweza kumtoa Mwanawe pekee kuwa Badala ya mwanadamu na kuwa Mdhamini wake, kupata adhabu aliyostahili kupata yule mvunja Sheria [Amri Kumi], na kumpa mwanadamu aliyetubu haki yake kamilifu. Kristo akawa Kafara isiyo na dhambi kwa ajili ya wanadamu wenye dhambi, akiwafanya wanadamu kuwa wafungwa wenye matumaini, ili kwa njia ya toba kwa Mungu kwa sababu walikuwa wameivunja Sheria yake takatifu [Amri Kumi], na kwa njia ya imani katika Kristo kama [mmoja aliye] Badala
yao, Mdhamini wao, na Haki yao, wangeweza kurudishwa katika uaminifu wao kwa Mungu na utii wao kwa Sheria yake takatifu [Amri Kumi].
FB_IMG_1540771018853.jpeg
 
Uzuri au Ubaya wa Amri za huyu Mungu ukuzivunja adhabu yake ni moja eti Moto wa milele!,Inakuwaje Mungu hawi fair kiasi hicho?! Yani Mungu hajui uzito wa kuua na Kusema Uongo?au Mzinzi na Muuaji wote adhabu ni ile ile au kamam mimi nakosea kifungu cha adhabu cha hizi amri kinasemaje ikiwa mtu anazivunja au kuvunja amri mojawapo kati ya hizi?
 
MIKA5

13 nami nitakatilia mbali sanamu zako na
nguzo zako, zitoke kati yako; wala
hutaiabudu tena kazi ya mikono yako.
14 Nami nitayang'oa maashera yenu, yasiwe
kati yako; nami nitaiangamiza miji yako.
15 Nami nitajilipiza kisasi katika hasira na
ghadhabu juu ya mataifa wasiosikiliza.
FB_IMG_1540797464209.jpeg
 
Yaani kudhania mambo ya Mungu ni mzaha mzaha kama mnavyofanyaga kwenye kujikumbusha hadithi zenu, lakini hata hadithi zenyewe mnazijulia wapi siku hizi. Nisameheni kwa hilo, mnavyojikumbusha nyimbo za wahuni wanaojiita wasanii wa bongo fleva si sawa katika mambo ya Mungu.

Binafsi nakiona hiki mnachokifanya hapa ni mzaha na ni kushindwa kutofautisha vitu vya kujikumbusha na kuzingatia. Ni nani anakukumbusha jina la baba yako ama mama yako? na majina yao unahitaji kuyakumbuka ama kuyazingatia? Kama mnakosa vya kuleta kujadili huku jf ni nafuu mkakaa kimya ama mkarudi huko fb kwenu, mambo ya Mungu yana namna yake na utaratibu wake.
Nimekuelewa sana mkuu
 
Kuambiwa UMEDANGANYWA NA KUDANGANYIKA NA UNATAKA KUDANGANYA

unasema napaniki?

Ok, ngoja niendelee kukufungua , ila tuwe wanyenyekevu, wala USITOKE NJE YA MADA , wala tusitoe lugha za matusi


AMRI KUMI ZA Mungu alizompa MUSA ZIPO KUMI, NA KANISA LA ROMA KWA KUSHIRIKIANA NA DOLA YA KIRUMI WALIZIBADILISHA hili lilisemwa na NABII DANIELI KUWA LITATOKEA (daniel 7:25)


Nakuleta kwenye hoja yako sasa ,kwanza yale sio maelezo NI AMRI KAMILI

TWENDE KWENYE BIBLE........

AMRI YA PILI KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:4-6
Usijifanyie sanamu ya kuchonga,
wala mfano wa kitu cho chote
kilicho juu mbinguni, wala kilicho
chini duniani, wala kilicho majini
chini ya dunia.Usivisujudie wala
kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana,
Mungu wako, ni Mungu mwenye
wivu; nawapatiliza wana maovu ya
baba zao, hata kizazi cha tatu na
cha nne cha wanichukiao, nami
nawarehemu maelfu elfu
wanipendao, na kuzishika amri
zangu


AMRI YA PILI KATIKA KATEKISIMU

Inasema

"Usilitaje bure jina la Mungu wako"

UMEONA UTOFAUTI TENA MKUBWA?

haya njoo na hoja nyingine....
View attachment 904507
Sizijui amri 10 lakini this makes sense.
 
ZABURI 119;155

WOKOVU U MBALI NA WASIO HAKI KWA MAANA HAWAJIFUNZI AMRI ZAKO


ohoo mimi nimeokoka , nampenda Yesu...NGOJA AJE AWAKANE HAWAJUI....

NI WANGAPI WAKO MBALI NA WOKOVU WA MUNGU?
.
FB_IMG_1540769526812.jpeg
 
Back
Top Bottom