Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

HIVI KWANINI KANISA LA ROMA LIMEDANGANYA MAELFU YA WATU KIASI HIKI?

YAANI WATU TOKA WATOTO WANAMEZESHWA AMRI ZA KATEKISIMU , BADALA AMRI ZA MUNGU KUTOKA KTK BIBLIA

KATIKA KIPENGELE HIKI TUTATUMIA
USHAHIDI WA BIBLIA NA, KITABU
CHA KATEKISIMU NDOGO YA
KANISA KATOLIKI UK 56, ILI
KUTIBITISHA;

A. Amri kumi katika biblia KUTOKA
20:1-17 na Amri kumi katika
katekisimu ndogo ya kanisa katoliki;

I. AMRI YA KWANZA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:1-3
Mimi ni Bwana, Mungu wako,
niliyekutoa katika nchi ya Misri,
katika nyumba ya utumwa.Usiwe na
miungu mingine ila mimi

AMRI YA KWANZA KATIKA
KATEKISIMU
Ndimi Bwana Mungu wako,
usiabudu miungu wengine

II. AMRI YA PILI KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:4-6
Usijifanyie sanamu ya kuchonga,
wala mfano wa kitu cho chote
kilicho juu mbinguni, wala kilicho
chini duniani, wala kilicho majini
chini ya dunia.Usivisujudie wala
kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana,
Mungu wako, ni Mungu mwenye
wivu; nawapatiliza wana maovu ya
baba zao, hata kizazi cha tatu na
cha nne cha wanichukiao, nami
nawarehemu maelfu elfu
wanipendao, na kuzishika amri
zangu

AMRI YA PILI KATIKA KATEKISIMU
Usilitaje bure jina la Mungu wako

III. AMRI YA TATU KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:7
Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu
wako, maana Bwana hatamhesabia
kuwa hana hatia mtu alitajaye jina
lake Bure

AMRI YA TATU KATIKA KATEKISIMU
Shika kitakatifu siku ya Mungu

IV. AMRI YA NNE KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:8-11
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Siku sita fanya kazi, utende mambo
yako yote; lakini siku ya saba ni
Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku
hiyo usifanye kazi yo yote, wewe,
wala mwana wako, wala binti yako,
wala mtumwa wako, wala mjakazi
wako, wala mnyama wako wa
kufuga, wala mgeni aliye ndani ya
malango yako. Maana, kwa siku sita
Bwana alifanya mbingu, na nchi, na
bahari, na vyote vilivyomo,
akastarehe siku ya saba; kwa hiyo
Bwana akaibarikia siku ya Sabato
akaitakasa.

AMRI YA NNE KATIKA KATEKISIMU
Waheshimu Baba na Mama, upate
miaka mingi na heri Duniani

V. AMRI YA TANO KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:12
Waheshimu baba yako na mama
yako; siku zako zipate kuwa nyingi
katika nchi upewayo na Bwana,
Mungu wako.

AMRI YA TANO KATIKA KATEKISIMU-
Usiue

VI. AMRI YA SITA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:13
Usiue.

AMRI YA SITA KATIKA KATEKISIMU
Usizini

VII. AMRI YA SABA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:14
Usizini

AMRI YA SABA KATIKA KATEKISIMU-
Usiibe

VIII. AMRI YA NANE KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:15
Usiibe

AMRI YA NANE KATIKA KATEKISIMU
Usiseme uongo

IX. AMRI YA TISA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:16
Usimshuhudie jirani yako uongo

AMRI YA TISA KATIKA KATEKISIMU
Usitamani mwanamke asiye mke
wako

X. AMRI YA KUMI KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:17
Usiitamani nyumba ya jirani yako,
usimtamani mke wa jirani yako; wala
mtumwa wake, wala mjakazi wake,
wala ng'ombe wake, wala punda
wake, wala cho chote alicho nacho
jirani yako

AMRI YA KUMI KATIKA KATEKISIMU
Usitamani mali ya mtu mwingine
View attachment 901465
HAPO NDIPO HUYU MWANAMKE MWENYE KANISA LAKE LA SABATO ALIPOKOSEA, AMRI YA KWANZA NA YA PILI KWA MUJIBU WA HUYU MWANAMKE AMBAYE ANAONA NI TOFAUTI, NI AMRI MOJA...!

UNAPOAMBIWA USIABUDU MIUNGU MINGINE, NDIO MWENDELEZO HUO KUWA USIJIFANYI SANAMU ZA KUCHONGA N.K

SASA YULE MAMA WA KISABATO KWA VILE ALIKUWA KWENYE SIKU ZAKE, TUMBO LINAMUUMA SAAANA, AKASHINDWA KUONA HATA MKATO, NUKTA..AKAJITENGEA MWENYEWE, AKIJUA KUNA MANYUMBU WATAMFUATA TU....

MMEPOTOKA SANA NYIE WAFUASI WA MWANAMKE MWENYE KANISA LAKE LA SABATO
 
Kumbe amri zimeboleshwa siyo zile za mlima sinai hizi zitakuwa za kwetu kule mbeya makanisa mengi kule
 
Kutoka 20

1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
13 Usiue.
14 Usizini.
15 Usiibe.
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
Kuna tofauti gani kati hizi na alizotela mtoa mada?.
 
Tunajadili zile Amri 10 na sio amri moja Jumuishi
Zile kuu kuu?
Ok acha tujadili km sehemu ya kujifunza mambo zamani yalikuaje,ili tupate kujua walikosea wapi ktk zama za kushika sheria kwa nje,ili tusirudie makosa yao ktk zama hizi za kutakasa mioyo siyo miili
 
Kwanini mkuu ,maana hapa zimetajwa Amri za KATEKISIMO SIO ZA BIBLIA ,kwann isiwe habari nzuri kwa wasabato?

Huon kama jamaa kadanganya kadanhanyika na anaendelea kudanganya maana kamezeshwa hivo toka akiwa mdogo?

Huoni kama Anazidi kupotea na kupoteza watu?

tatizo Wasabato mnasoma Biblia kwa nguvu sana bila kutumia akili. Mimi bwana Mungu wako na usijifanyie sanamu kuna ujumbe gani wa tofauti ndani yake? ujumbe uliopo ni moja kuwa usiwe na miungu mingine. Kwa mantiki hiyo Amri ya kwanza ya Wasabato na amri ya pili ya Wasabato zote ni Mamri moja tu. Ila wao wamezigawa kwa heshima ya Nabii wa Elen G.Whilte. Hawataki kumwangusha huko alipo. hivyo wameamua kuwa watiifu kwake hadi kufa.
 
Hebu tuwianishe
Wasabato:
roho aliwaongoza kutabili mwisho wa dunia,japokuwa Kristo alisema hakuna ajuaye hata mm ila baba,wao wasabato wakasema tunaujua na wakautabiri(huko siyo kumpinga Kristo?)na haukutokea,
Wakatoliki:
Roho mtakatifu aliwaongoza Wameulea Ukristo na kuwazaa madhehebu ya sasa,na kuwafanya watu wamjue Mungu japo wamechoropoka wakaanzisha madhehebu,

Wasabato:
roho aliwaongoza kutaka kwenda ulaya bila visa wala nauli wala chakula wa hawajui hata lugha ya huko wakahubiri injili ya Ellen white,
Wakatoliki:
Roho mtakatifu aliwaongoza kuiunda Biblia ambayo inatumika hata na wasabato kuwatukania wakatoliki,
Walianzisha mashule na hospitali ambazo hata wasabato waliisoma na kutibiwa huko,

Wasabato:
roho aliwaongoza kutabili kuwa Papa Yohane Paulo ndo mkamilisha 666 na ndo mnyama maana hata unabii wa mnyama kupona jerana la mauti umetimia kwake alipopona kuuliwa na risasi,na wakadanganya akina Arlon,papa alikufa na hakuna kilichotokea na kukamilika,

Wakatoliki:
Roho anawaongoza kuanzisha Huduma na miradi ya kimaendeleo inayosaidia jamii hata wasabato pia ni wanufaika,kila siku,

Wasabato:
roho anawatuma kuwakosoa,kuwatukana,kuwakashifu,kuwachukia,kuwazushia kila lililo ovu wakatoliki,na huku wakijisahau wao wenyewe kujikosoa na kutubia udanganyifu wa mama yao,

Wakatoliki:
Roho anawatuma kujichunguza zaidi kuliko kunyooshea wengine vidole,
Kuomba toba kuliko kuwachukia madhehebu,
Kujinyenyekeza kuliko kujiona wakamilifu,
Kukaa kimya kuliko kuwatukana na kurumbana na watoto,
 
Leta ushahidi wa hayo usemayo, wapi waadventista wasabato walitabiri mwisho wa dunia,

Na hao unaosema walienda bila visa sio.waadventista wasabato ,

Sio kila anayesali jumamos ni.muadventista,

Naomba pia uniambie ni roho gani aliwaongoza kuombea wafu, na kuabudu masanamu
 
tatizo Wasabato mnasoma Biblia kwa nguvu sana bila kutumia akili. Mimi bwana Mungu wako na usijifanyie sanamu kuna ujumbe gani wa tofauti ndani yake? ujumbe uliopo ni moja kuwa usiwe na miungu mingine. Kwa mantiki hiyo Amri ya kwanza ya Wasabato na amri ya pili ya Wasabato zote ni Mamri moja tu. Ila wao wamezigawa kwa heshima ya Nabii wa Elen G.Whilte. Hawataki kumwangusha huko alipo. hivyo wameamua kuwa watiifu kwake hadi kufa.
Wapi zimegawiwa?

Bas zingekuwa kumi.na moja

Roma hamuitaki amri hiyo ISEMAYO.USICHONGE SANAMU ili.muweze kuabudu na kuchonga haya mavinyago
 
Kuna tofauti gani kati hizi na alizotela mtoa mada?.
Wewe unaona sawa ?

Nioneshe amri inayosema IKUMBUKE SIKU YA SABATO NA INAYOSEMA USICHONGE MASANAMU.kwenye hizo za mtoa mada,

Ukinionesha nitaamini huburuzwi kama NYUMBU na mapadri
 
HAPO NDIPO HUYU MWANAMKE MWENYE KANISA LAKE LA SABATO ALIPOKOSEA, AMRI YA KWANZA NA YA PILI KWA MUJIBU WA HUYU MWANAMKE AMBAYE ANAONA NI TOFAUTI, NI AMRI MOJA...!

UNAPOAMBIWA USIABUDU MIUNGU MINGINE, NDIO MWENDELEZO HUO KUWA USIJIFANYI SANAMU ZA KUCHONGA N.K

SASA YULE MAMA WA KISABATO KWA VILE ALIKUWA KWENYE SIKU ZAKE, TUMBO LINAMUUMA SAAANA, AKASHINDWA KUONA HATA MKATO, NUKTA..AKAJITENGEA MWENYEWE, AKIJUA KUNA MANYUMBU WATAMFUATA TU....

MMEPOTOKA SANA NYIE WAFUASI WA MWANAMKE MWENYE KANISA LAKE LA SABATO
Ndio mlivyodanganya?

KANISA LA ROMA LIMEJAA UPAGANI, UKISEMA NI MUENDELEZO ,

KWANINI MNAKUJA KUIGAWA AMRI YA 10 ZIWE MBILI?

KWANINI AMRI YA IKUMBUKE SIKU YA SABATO MMEIONDILEA MBALI?

MNAIONA NI KITUO CHA POLISI

KWANINI INAYOSEMA MSICHONGE SANAMU HAMTAKI HATA KUIONA ILI TU MCHONGE NA MJAZE MISANAMU YENU KANISANI
 
Amri ya kwanza ni 20:1-6 yote ikiwa na maana moja tu usiabudu miungu mingine, sasa wasabato mmegawa katika amri mbili na Amri ya kumi wakatoliki mstari wa 17 wamegawa makundi 2 na wasabato wameweka ktk amri moja. But wote kwa pamoja mnataja amri za Mungu zote.Umefanya vema Aron kuweka mlingayo nimejifunza kitu hapo
Haupo sahihi , waroma hiyo ya kuchonga HAWAITAKI tambua hilo,

Ya Nne ya sabato hawaitaki wameibadili kabisa hata maana

Kwakuwa INAYOKATAZA KUCHONGA MASANAMU WAMEIONDOA , ili kufidia ziwe kumi

Amri ya 10 wakaigawa mara mbili , ( angalia kwa makini)
 
WAABUDU SANAMU ETI WANATAKA MANENO TAKA MANENO LAINI, MIMI.NASEMA HAPANA , MIMI HUWA SIPEPESI , NI NYUNDO YA KICHWA TU....

Katika siku zile za mwisho watu hao ambao ni waasi, ambao hawatataka kuisikia
Sheria ya Mungu, wanaonekana katika mafungu yafuatayo wakizungumza na VIONGOZI wao wa DINI, na kusema,

ISAYA 30:10-11

"Msitoe unabii wa mambo ya haki, TUAMBIENI MANENO LAINI, hubirini maneno YADANGANYAYO; TOKENI KATIKA NJIA, geukeni MTOKE katika MAPITO;
mkomesheni Mtakatifu wa Israeli mbele yetu" (Isaya 30:10,11).

Hapa ni unabii ambao haiwezekani kukosa kuuelewa. Unatabiri dhahiri ya kwamba
katika siku zile zilizo karibu sana na kuja mara ya pili kwa Kristo, yaani,
"siku za mwisho," kutakuwako na kundi la watu wanaokiri KUMTUMIKIA BWANA, lakini
ambao ni WAASI kuhusiana na suala la SHERIA, wanaokataa katakata kuyasikia au
kuyatii mafundisho ya Sheria. Watawaambia wachungaji wao waziwazi kwamba
HAWATAKI UKWELI ULIO DHAHIRI, bali wanataka wahubiriwe kutoka kwenye mimbara "MANENO LAINI." Wanawataka viongozi wao wa dini 'wageuke na KUTOKA katikaMAPITO,' na KUTOKA katika NJIA," ili wapate kuhubiri "MANENO YADANGANYAYO."

MIMI HAPANA ,MIMI NI NYUNDO TU, NA SIPANGIWI NIMETUMWA NA BWANA
 
Yaani kudhania mambo ya Mungu ni mzaha mzaha kama mnavyofanyaga kwenye kujikumbusha hadithi zenu, lakini hata hadithi zenyewe mnazijulia wapi siku hizi. Nisameheni kwa hilo, mnavyojikumbusha nyimbo za wahuni wanaojiita wasanii wa bongo fleva si sawa katika mambo ya Mungu.

Binafsi nakiona hiki mnachokifanya hapa ni mzaha na ni kushindwa kutofautisha vitu vya kujikumbusha na kuzingatia. Ni nani anakukumbusha jina la baba yako ama mama yako? na majina yao unahitaji kuyakumbuka ama kuyazingatia? Kama mnakosa vya kuleta kujadili huku jf ni nafuu mkakaa kimya ama mkarudi huko fb kwenu, mambo ya Mungu yana namna yake na utaratibu wake.
 
Haupo sahihi , waroma hiyo ya kuchonga HAWAITAKI tambua hilo,

Ya Nne ya sabato hawaitaki wameibadili kabisa hata maana

Kwakuwa INAYOKATAZA KUCHONGA MASANAMU WAMEIONDOA , ili kufidia ziwe kumi

Amri ya 10 wakaigawa mara mbili , ( angalia kwa makini)

View attachment 911088
Hujielewi,soma biblia kwa faida yako na sio kwa faida ya kanisa lako
 
Wewe unaona hapo nimenukuu kutoka kwa wafaraga au wasabato au BIBLIA?

Mbona unataka kuleta udini,hapo nimenukuu kwenye BIBLIA , pingana na biblia ,amin KATEKISIMO YA PAPAView attachment 901471
Yaani inaonyesha wewe unaenda kanisani kwaajili yakutafuta vifungu vyakubishana na sio kumjua Mungu.ndugu yangy labda nikuulize swali moja. ulishawahi kuwaona watu wazima wamebeba katekisimu wanaingia nazo kwenye ibada. swali La Pili. je? katika dhehebu lako wewe hakuna vitabu kwaajili ya watoto na je ? hakuna vitabu vingine zaidi ya biblia mnavyovisoma.ila nataka nikuambie kitu kimoja kama ungeutambua ukuu wa Mungu usingeingia katika mabishano yakidini na kidhehebu.Yawezekana Mimi najua tofauti labda.lkn Mungu ninaemjua Mimi ni Mungu Wa wote haangalii mabishano yetu wala majivuni yetu anaangalia matendo yetu.
 
Kwanini mkuu ,maana hapa zimetajwa Amri za KATEKISIMO SIO ZA BIBLIA ,kwann isiwe habari nzuri kwa wasabato?

Huon kama jamaa kadanganya kadanhanyika na anaendelea kudanganya maana kamezeshwa hivo toka akiwa mdogo?

Huoni kama Anazidi kupotea na kupoteza watu?
hakuna alichopotosha hapo.kwa mfano unapoambiwa usiue .huu ni msamiati mrefu sana .haimaanishi kuua tu .ata kutoa mimba nikuua pia.kuwaza pia inaesabika
 
Back
Top Bottom