Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

Tukihoji wanasema ,za Biblia ni za wasabato ,wao wanafata za Vatcan
Mbona ipo wazi hizo sio amri zilizo kwenye biblia na mada sio ya dini kabisa.Mnaleta udini ili muanze kunyooshana vidole wakati wote wakristo na biblia ndo kioo chetu.Haya mambo ndo unakuta wote mnatumia biblia ila madhehebu 6000 na nabii tito ndani ya nyumba,mnaponda nabii tito wakati na yeye kaamua kuelewa anavyotaka.Embu mtu aingie playstore a download bible asreenshot amri za Mungu tuweke hapa msitoe hata nukta...
 
Nimeshaziweka hapo juu kitambo, kaja mmoja anauliza mbona zipo nyingi, au za wasabato.na wafaraga,

Hii inaonesha ni kiasi gan watu wamedanganywa wakadanganyika
 
ISAYA 24

4 Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika.
5 Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.
6 Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu.
tapatalk_1539803124556.jpeg
 
Nimelalamika au nimeweka wazi?

Hebu kasome kutoka 20:1-17 halafu fananisha na hizo za katekisimo za PAPA
Siyo mbaya uliyesoma ukaweka hapa hata wasio na biblia wapate Neno
 
Siyo mbaya uliyesoma ukaweka hapa hata wasio na biblia wapate Neno
Mbona nimeziweka hapa

Labda nizirudie

KUTOKA 20

Kutoka 20

1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
13 Usiue.
14 Usizini.
15 Usiibe.
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
 
2 Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7 Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
13 Usiue.
14 Usizini.
15 Usiibe.
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
 
Nashangaaga sana watu wanasema amri ya 6 ni USIZINI, yaani roma ndio maana BIBLIA INAMUITA MAMA WA MAKAHABA, ambaye amewanyweshwa mataifa mvinyo wa uasherati wake,

Yaani mtu utamkuta ana biblia kubwa jimapili anakaa siti ya mbele, anakwambia AMRI YA 6 USIZINI, hapo ndipo nasemaga ACHA ROMA IITWE ROMA
 
Wewe unaona hapo nimenukuu kutoka kwa wafaraga au wasabato au BIBLIA?

Mbona unataka kuleta udini,hapo nimenukuu kwenye BIBLIA , pingana na biblia ,amin KATEKISIMO YA PAPAView attachment 901471
Kimantik mm naona kitu n kile kile tu
Au niambie amri ambayo ipo katka waroma ambapo haipo katka mwanzo? Au iliekuepo mwanzo na Roma wameitoa
 
Kwanini mkuu ,maana hapa zimetajwa Amri za KATEKISIMO SIO ZA BIBLIA ,kwann isiwe habari nzuri kwa wasabato?

Huon kama jamaa kadanganya kadanhanyika na anaendelea kudanganya maana kamezeshwa hivo toka akiwa mdogo?

Huoni kama Anazidi kupotea na kupoteza watu?
Umewashika pabaya! Naona wana mbwela mbwela tu
 
Kimantik mm naona kitu n kile kile tu
Au niambie amri ambayo ipo katka waroma ambapo haipo katka mwanzo? Au iliekuepo mwanzo na Roma wameitoa
Kweli huoni tofauti kabisa?

Unaweza kunionesha Amri inayokataza kuchonga sanamu kwenye hizo alizoleta mtoa uzi au hizo za katekisimu? Umeiona? Tuanzie hapa kwanza
 
Nimejua amri kumi za Mungu nikiwa mtu mzima, utotoni nilimezeshwa matango kipindi niko kanisa fulani
 
Nashangaaga sana watu wanasema amri ya 6 ni USIZINI, yaani roma ndio maana BIBLIA INAMUITA MAMA WA MAKAHABA, ambaye amewanyweshwa mataifa mvinyo wa uasherati wake,

Yaani mtu utamkuta ana biblia kubwa jimapili anakaa siti ya mbele, anakwambia AMRI YA 6 USIZINI, hapo ndipo nasemaga ACHA ROMA IITWE ROMA
kuna kipindi mzee wangu alimuuliza katekista kuhusu stori ya Nebukadineza kugeuka mnyama,katekista akashangaa maana alikuwa hajui kuwa kuna stori hiyo kwenye Bible
kiufupi Waroma wengi hawasomi Biblia wanasomewa siku ya ibada hadi siku ya ibada nyingine
nimekuwa mroma kwa 18 najua kila kitu
 
Aisee ni hatari
 
Kweli huoni tofauti kabisa?

Unaweza kunionesha Amri inayokataza kuchonga sanamu kwenye hizo alizoleta mtoa uzi au hizo za katekisimu? Umeiona? Tuanzie hapa kwanza
Kuchonga sanam ambapo katka maana usiabudu miungu wengne (miti, ng'ombe, shetan)
Lakn unaweza kujiulza sanam za kanisa katorik zinakuaje sasa? Ule n utamadun tu wa watu wa Israel ambapo kuweka sanamu haimaanisha kwamba maombi yanaenda kwa hzo sanam n mapambo tu ya kikanisa zaid
 
Ishu ni Ukweli ama Usabato? Kwa nini usiandike Amri alizopewa Musa pale mlimani!?
 
Kuchonga sanam ambapo katka maana usiabudu miungu wengne (miti, ng'ombe, shetan)
Lakn unaweza kujiulza sanam za kanisa katorik zinakuaje sasa? Ule n utamadun tu wa watu wa Israel ambapo kuweka sanamu haimaanisha kwamba maombi yanaenda kwa hzo sanam n mapambo tu ya kikanisa zaid
Wewe na wewe acha kutulisha matango pori...waisraeli wa wapi hao unaowazungumzia?
Ambao uchonga sanamu na kuziweka kwenye masinagogi na kuziabudu?

ASANTE
 
Back
Top Bottom