Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

DHAMBI AMBAYO MUNGU ANAICHUKIA,KUFANANISHWA NA SANAMU,

Isaya 2

8 Tena nchi yao imejaa sanamu; huabudu
kazi ya mikono yao, vitu vilivyofanywa kwa
vidole vyao wenyewe.

9 Mtu mnyonge (MUUMINI) huinama, na mtu mkubwa(PAPA/ASKOFU/PADRI)
hujidhili; kwa hiyo usiwasamehe.
FB_IMG_1540840391863.jpeg
 
Mbona nimeziweka hapa

Labda nizirudie

KUTOKA 20

Kutoka 20

1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
13 Usiue.
14 Usizini.
15 Usiibe.
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
Sasa mbona naona zimefka 17
 
Je! Wale Mitume Waliibadili Sabato?

Yakobo, kiongozi wa kwanza wa kanisa lile la mwanzo, aliandika maneno haya kuhusu zile Amri kumi:

"Anayevunja amri mojawapo ya sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja sheria yote. Maana yule yule aliyesema: "USIZINI, "alisema pia" "USIUE." Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini, lakini umeua, wewe umeivunja sheria" - (Yakobo 2:10, 11).

Luka, tabibu na mwinjilisti katika kanisa lile la kwanza, anatoa taarifa hii.

"Siku ya Sabato tukatoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto, ambapo tulidhani kuwa mahali pa kusali. Tuliketi, tukiongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo" - (Matendo 16:13).

Kitabu cha Matendo cha Agano Jipya kinataja mara 84 ilipotunzwa. Sabato hiyo na wafuasi wa Kristo, zote hizo zilikuwa zikitunzwa zaidi ya miaka 14 baada ya ufufuo wa Yesu: Sabato 2 pale Antiokia (Matendo 13:14,42,44); 1 pale Filipi (Matendo 16:13), 3 pale Thesalonike (Matendo 17:2,3), Sabato 78 pale Korintho (Matendo 18:4,11).

Yohana, wa mwisho kufa miongoni mwa wale mitume kumi na wawili, aliitunza Sabato. Aliandika hivi:
"Siku ya Bwana nilikuwa katika Roho" - (Ufunuo 1:10).

Kulingana na maneno ya Yesu, siku ya Bwana ni Sabato:
"Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato" - (Mathayo 12:8).

Uchunguzi wa ushahidi wa maandiko unaoonyesha wazi kwamba wale mitume hawakufanya jaribio lolote la kuibadili siku ya Mungu ya mapumziko kutoka siku ya saba kwenda ile siku ya kwanza ya juma. Agano jipya, linaitaja siku hiyo ya kwanza ya juma mara nane tu. Katika mifano hiyo yote hakuna ambapo siku ya kwanza ya juma inatajwa kuwa ni takatifu, wala hata kudokezwa kuwa tunapaswa kuitenga kama siku ya ibada
Hivi Paulo aliposema mtu asikuhukumu kwa ajili ya siku,mwandamo wa mwezi wala sabato mambo hayo ni kivuli cha yajayo alimaanisha nini
Naomba fafanuzi tafadhari
 
Hizi ni Amri zilizochakachuliwa na kanisa la ROMA ,

Watu maelfu mmemezeshwa amri zilizochakachuliwa na kuwekwa kwenye katekisimo, Zile Amri kumi ORIGINAL alizopewa musa pale SINAI, zipo kwenye biblia hata hamtaki kuzifatilia ,mfananishe na hizo za PAPA
Hata ulizonazo wewe zilitunzwa na kanisa Katoliki,
 
Sabato imeanzia EDENI,

Roma imetokea ndani ya ROMA YA KIPAGANI, ulishajiuliza why, kanisani kwenu kumejaa masanamu tu,
Eti nini?
Sabato imeanzia Eden,
Inamaana Amri kumi alipewa adamu na siyo Mose
Km ilianzia Eden kwa nini mnapoambiwa ninyi siyo Wakristo huwa mnakataa maana sote tunajua Ukristo ulianzia kwa nani,
Ukisema ulianzia Eden ni km kutaka kutudanganya kuwa Ellen na akina Miller na ninyi ni dini moja na mayahudi ambao mpaka sasa wanafuata taratibu za awali
 
Hizi ni Amri zilizochakachuliwa na kanisa la ROMA ,

Watu maelfu mmemezeshwa amri zilizochakachuliwa na kuwekwa kwenye katekisimo, Zile Amri kumi ORIGINAL alizopewa musa pale SINAI, zipo kwenye biblia hata hamtaki kuzifatilia ,mfananishe na hizo za PAPA
Zitaje tuzione sio unalalamika kama mtoto
 
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako
MAANA YAKE
Ewe ndugu yangu na kaka yangu shavu kibonyeo angalia yanayokupata kwa kuivunja hii Amri kuu.Nini haswa kilichokusukuma mpaka ukaenda kuionja ya mama yake Mouthplate ata mpaka ukawa unataka yeye mzee baba akuite wewe baba na wewe ukawa unamuita ni mwanao.Dah Dunia ni tambara Bovu mzee shavu kibonyeo
 
Katika tamaduni na mila za mashariki ya kati mwanamke alipewa nafasi mdogo sana ktk jamii. Nazo amri hizi walitungiwa wanaume. Kunahitajika uandikaji mpya wa biblia kwenda na wakati.
 
Hizi amri kum za mungu ni za kitambo sana vp hazija editiwa bado mpaka leo? Maana papa hachelewi
 
Hizi amri kum za mungu ni za kitambo sana vp hazija editiwa bado mpaka leo? Maana papa hachelewi
 
Hizi ni Amri zilizochakachuliwa na kanisa la ROMA ,

Watu maelfu mmemezeshwa amri zilizochakachuliwa na kuwekwa kwenye katekisimo, Zile Amri kumi ORIGINAL alizopewa musa pale SINAI, zipo kwenye biblia hata hamtaki kuzifatilia ,mfananishe na hizo za PAPA
Wasabato utawajua tu, hasa jaluo, wapare,vijita vya ziwani kure kijijini kure, vibishi ivo hatare, heeeeee

hasa huyu AROOON Yuko USA bila passport sijui atarudi!
 
1.Usiabudu miungu wengine.
2. Usiape bure kwa jina la Mungu wako.
3. Shika Kitakatifu Siku ya Mungu wako
4. Waheshimu Baba na Mama, upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue
6. Usizini
7. Usiibe
8. Usiseme uongo
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya watu.
Hizi amri sio za kwenye bible mkuu
 
Ninayoweza kutekeleza mbili tu
4. Waheshimu baba na mama
5. Usiue
 
Hizi amri sio za kwenye bible mkuu
Za kwenye bible ni zip?. Soma biblia yako vizur uelewe..na siyo kusoma kama pambo au kupiga makelele ili uonekane umesoma biblia...
..
"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" asema Bwana
 
1.Usiabudu miungu wengine.
2. Usiape bure kwa jina la Mungu wako.
3. Shika Kitakatifu Siku ya Mungu wako
4. Waheshimu Baba na Mama, upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue
6. Usizini
7. Usiibe
8. Usiseme uongo
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya watu.
Rafiki ahsante . ila hizi siyo! Kasome kutoka 20:1 na kuendelea. Hiyo ya pili siyo , ni habari kuchonga sanamu!!!!. Na ya mwisho ni habari ya kutamani. Kutamani hakugawanyiki Mali na make! Ukishasoma umetulia ziandike vizuri sasa. Barikiwa
 
Back
Top Bottom