Tujifunze Kutoka Libya

Mikakati yao imeshafeli big time,hakuna maandamano na hakutakuwa na maandamano

Jana kuna sehemu nilipita vijana wanafanya mazoezi ya mpira,nje ya uwanja wapo kama wanajeshi 15 au 20

Kwa maana vyombo vya ulinzi na usalama vipo tayar kwa tahadhari

Na kikubwa zaidi wananchi sasa wameshaona madhara ya maandamano
 
Kwamba watu wakitekwa na kuuwawa tukae kimya tu kulinda amani sio?
Ni watu gani huwa wanatekwa? Ni mwananchi au kila anayejifanya Jabari kushindana na dola

Wanaharakati hao wapo nje ya nchi kwa kuhofia uhai wao,wewe unafanya harakati hapa Tanzania unatarajia nini?
 
Way forward kwanza, tuache harakati ambazo zitazidi kutuweka hatarini,maana huku kutekwa unapokuzungumzia tunajua wazi ni kuzungumza dhidi ya dola,kama umechoka kukaa uraiani basi zungumza na ukitekwa usilalamike

Pili, njia ya mazungumzo,serikali haiongozwi na wanyama,ni wanadammu kama sisi,wanasikia na wanajua malalamiko ya wananchi ,tatizo njia tunayo tumia sio rafiki

Ila tukiwa na nia ya kutaka suluhu itapatikana,ndio maana imeundwa tume ya maridhiano,huu ni mchakato mkubwa kuelekea kwenye kuliponya taifa

Tusubiri taarifa yao,kisha tuhoji mbona kuna hili na hili halipo hapa kwenye taarifa yenu? Hapo tayar tunafungua uwanja wa mazungumzo

Kupitia mazungumzo tutarekebisha mengi na kutatua mengi
 
Zile zilikuwa Vurugu au machafuko na sio maandamano .

Hao GEN Z wa Tiktok wao waliratibu vurugu Ila hawakuandamana hata mmoja hii ni research nilioifanya

Zile Account zote before 29/10
Na mpaka sasa zipo zinapost

Sasa the question ikiwa account zote zipo active means hawa Kazi yao ni kuhamasisha vurugu kwa kundi dhaifu

Kundi dhaifu ndo lilikufa 29/10 kwa kuambiwa jeshi litawalinda.

Kundi hili sio wasomi , wala hata hawajui nini wanataka.

Juzi nimemchek Nanauka nikampa mikakati kuwa katika ziara zake alicheki hili kundi

Na naona anafanya hivyo kwa sasa Nanauka ameachana na mambo ya mtandaoni yupo Field.

Kwahiyo VITA hii iliratibiwa na activists, wasomi uchwara wa Tz na mission ikafanywa na laymen wa Tz.

Just imagine MTU unaambiwa hii sheli ya Ridhiwan wewe unapiga moto bila evidence yoyote.

VITA ya Ku- raise awareness kwa young generation sio VITA ndogo hapa JF watu ukileta movement Kama hii ujue unakuwa unahatarisha ugali wao so usitegemee waisapoti kirahisi

Tutashinda.
 
Ikiwa wazungu wanavuna rasilimali zetu si sawa kabisa. Nauliza inakuaje MTZ mwenzako anavuna na wewe hufaidiki vile unavyostahili?

Ndio maana mkaambiwa kabla ya kuhubiri AMANI hakikisheni mnawatendea mema na HAKI, hii Amani itakuja tu.
Mimi na wewe tunajua kwamba hakuna Serikalli ambayo haina ufisadi hapa duniani,na Tanzania ni moja wapo

Kwahiyo cha msingi kupigania amani kwanza kisha mambo mengine yanafuatia,Panapo kuwa na amani ndio watu watakaa na kupigania mambo mengine

Hivi kama yakitokea machafuko,kuna kukaa tena na kuzungumza? Kuna kakaa tena na kutafuta haki?
 
Yote uliyosema ni sahihi kabisa,tuna shida kubwa sana kwakweli

Umemalizia vizuri sana kwamba hii vita ya kuwafungua watu walifungwa kwa propaganda za kihuni ni kazi sana,inahitajia juhudi na kutokatishwa tamaa

Tuendelee kuraise awareness ni swala la muda watakuja kutuelewa

Kwa pamoja tutashinda
 
Hivi kwa nini humwambii mama abdul kutenda haki? Umekazana tu kutuhuburia amani fake.
Wapigania amani wa kwanza kabisa ni sisi Wananchi,sisi tukiwa sawa na kuwa kitu kimoja hapo sasa tunaweza kuwanyooshea viongozi kidole na kuwaambia sisi tunataka amani

Sasa tunaleta vurugu na machafuko,je hao viongozi watakuelewa?
 
Serikali ni bora ingekuwa inaongozwa na wanyama, these rulers are by far worse than animals, at least wanyama huwa wanaua viumbe wengine ili wawale lakini hawa wanaoua na kufukia miili kusikojulikana calling them animals it's a big insult to all animals.
Tume ya maridhiano ni ujinga na upumbavu na ni matusi na dharau kwa kila mwenye akili timamu, tatizo namba moja la yote haya ni Samia so she has not credible and she has no legitimacy kuunda hicho alichokiita tume. Tume yenyewe siyo inclusive ni ya watu wenye mrengo wa aliye wateua na ambaye kwa macho ya baadhi ya wananchi ndiye mtuhumiwa namba moja, we ain't fools.
Samia wakati anaongea na kilichoitwa wazee wa Dar es Salaam alikiri kwa kusema kuwa kuuawa kwa wale vijana waandamanaji kulikuwa halali nadhani hakukuwa na haja ya tume kuendelea kufuja pesa za walipa kodi wakati mteuzi wa wajumbe wa tume ameshamaliza kwa kukiri order ya shoot to kill na kuitetea kuwa ilikuwa order iliyostahili.
 
Asante kwa maoni yako mazuri, nakubaliana na wewe kuhusu wasiwasi wa tume hiyo na taarifa zake

Tunachokwama wengi wetu ni subira,ukitaka kumpata kobe vizur muache atoe kichwa chake kwenye gamba lake

Hii itume kwasasa ni kama kobe aliyeficha kichwa chake,tusubir wakusanye taarifa kisha watatoa kichwa nje ya gamba

Hapo sasa ndio tuhoji kuna hili na kuna ushahidi wa picha na kimazingira,mbona nyie mmetupa taarifa tofauti?

Je hapo hujafanikiwa kuanika uozo wowote uliofichwa?
 
Let us agree to disagree on the approach of this very sensitive topic.
 
Hizo habar potofu ndio propaganda kubwa zIlizo fanywa dhidi ya Utawala wa Gaddafi

Gaddafi alisema sitamjengea mama yangu nyumba mpaka wananchi wangu wapate makazi,je hilo linasemwa?

Wanandoa kupewa nyumba na pesa ya kuanzia maisha je inasemwa?

Nchi haikuwa na deni hata shilingi,je inasemwa?

Gaddafi kaacha nchi ina reserve ya kitu kama dola million 300,je inasemwa?
 
Acha upotoshaji
 
"Watu ambao walikuwa hawajui kulipa bill za maji au umeme,watu ambao walikuwa wanaingiziwa gawio kwenye account zao kutoka kwenye uchumi wa mafuta,leo hii hawana amani,wengi wanakufa baharini huko katika jitihada za kueleka Ulaya."

Vipi sisi tunafaidika na nini toka kwenye gesi, uranium, tanzanite, dhahabu, makaa ya mawe, almasi, chuma, kilimanjaro, serengeti, bandari salama,tanga na mtwara? Na nyinginezo chungumzima..
Bora hata tungekuwa tunafaidika basi na mali za nchini mwetu, maliasili kibao ila afya mbovu , maji tabu, elimu kipengele, miundombinu jau.. wakati mwingine bora mkae kimya tu.
 
Kijana una shangazi mjinga
 
Kwaiyo wazungu ndo waliwatuma
Kufanya uchaguzi wa ulaghai
Kuteka na kuuwa watu holela
Kubambikia watu kesi za uhaini na ugaidi
Kupora mamlaka ya mahakama na bunge
Tuache maneno, serikali isitafute chaka kusingizia wazungu
 
Kwaiyo wazungu ndo waliwatuma
Kufanya uchaguzi wa ulaghai
Kuteka na kuuwa watu holela
Kubambikia watu kesi za uhaini na ugaidi
Kupora mamlaka ya mahakama na bunge
Tuache maneno, serikali isitafute chaka kusingizia wazungu

Je nchi za Africa unahisi zilikuwa hivi kabla ya ukoloni?
 
Tuchukulie kwamba upo sahihi kwa maelezo yako

Je, kuondoa mfumo huu kandamizi ni kupitia maandamano ya fujo na vurugu?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…