ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,529
- 21,530
- Thread starter
- #161
Mr. KalamuNataka nijibu swali lako kitulivu kabisa, na kama kweli unayo nia ya kuelewa jibu hutajifanya hujui jibu.
Ni hivi: Unaamini au huamini kuwa Samia Suluhu Hassan anajuwa kuwa huo mfumo upo, au hajui?
Kama Samia anajuwa mfumo huo upo, amefanya juhudi zipi za kuurekebisha/kuuondoa ili Tanzania anayoiongoza iwe nchi ya utulivu; na yeye atawale kwa AMANI kabisa? Umemweleza nini huyo Samia kuhusu hili, mkuu Ertugrul? Kwani nawe hutaki Samia atawale nchi hii wakati wananchi wake wote wakiwa na maelewano mazuri, bila ya kugawanyika kimakundi kama kulivyo sasa hivi?
Hivi kweli hujui "maandamano ya fujo na vurugu" yanasababishwa na nani, hujui kweli au unajifanya tu kutojuwa?
Fujo na vurugu vinasababishwa na ukandamizaji; unyimwaji wa haki; bila ya hivyo usingeona fujo na vurugu. WaTanzania ni watu wapole sana; tena wapenda AMANI. Ni nyinyi, mnaopigania huo mfumo na huyo Samia na Kikwete ndio mnaosababisha yote haya.
Kuhusu kuuondoa mfumo kwa njia za fujo na vurugu; hilo hata wewe huna jibu; nijuavyo mimi, bila Samia Suluhu Hassan kuondokana na dhana ya kudhani anaweza kutawala taifa hili kwa nguvu za mitutu ya bunduki; hili hata yeye anacheza kamali tu!
Kwa bahati mbaya sana huu mchezo wake umesababisha waTanzania kupoteza maisha; na inawezekana bado wengine wataendelea kupoteza maisha; na kupoteza muda wa kuliendeleza taifa hili. Lakini na yeye, pamoja na Genge lake lote, hawatatoka salama
Haya ya kutumia fujo na vurugu kudai haki ambayo mnaitaka sio njia sahihi kwa sasa,madhara yameonekana tayar tena makubwa
Na umekiri tena kwamba huenda kukawa na uwezekano wa watu tena kufa kwa kutimia njia hizo hizo
Je, bado mnataka kuwatumia vijana wasiojielewa na kufuata kila mnacho waambia kuandamana kwa fujo na vurugu ili mfikie lengo lenu hata kama watapoteza uhai wao?
Hapo mnakuwa na tofauti gani na Uongozi wa sasa?