My people,
15 - February -2011
Benghazi, Libya
Ghasia zilianza rasmi baada ya Utawala wa Muammar Gaddafi kumkamata mwanasheria anayejulikana kwa jina la Fathi Terbil ambaye alikuwa mtetezi wa haki za binadamu
Baada ya wananchi kujua hilo tukio walikasirishwa sana,na hapo ndipo Maandamano rasmi yalianza viunga vyote vya Libya
Baadae Serikali ilitumia nguvu kubwa kwa kuwapiga risasi waandamanaji,baadae wandamanaji nao wakapora silaha na kuunda vikundi wa uasi dhidi ya Serikali
Kutoka maandamano ikaja kuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe, nchi yote ikachafuka hatimaye NATO ikaingilia kati na kufunga anga na kuanza kuwapiga au kuwashambulia askari au wanajeshi wa jeshi la libya,mwisho wa siku Utawala wa Gaddafi ukaanguka
Kilichofuatia baadae nchi haikutawalika tena,uasi ukawa mwingi na machafuko ikawa sehemu ya maisha ya kila siku ya Libya
Watu ambao walikuwa hawajui kulipa bill za maji au umeme,watu ambao walikuwa wanaingiziwa gawio kwenye account zao kutoka kwenye uchumi wa mafuta,leo hii hawana amani,wengi wanakufa baharini huko katika jitihada za kueleka Ulaya.
Wananchi jua kwamba nasi ikifikia hatua hiyo ya machafuko,wazungu wataingilia kati ,si kwakuwa wanatupenda ila kwa ajili ya Kuja kuvuna rasilimali za Tanzania
Ndio maana baadhi yetu tunapoamua kuwa mabalozi wa amani tunajua nini maana ya kukosa amani,tunajua si ushujaa kuwa wakimbizi
Kwahiyo tujue kwamba AMANI NI TUNU YETU BASI TUILINDE KWA WIVU MKUBWA
Tunashukuru na kufurahi kuona kwamba kuna members wengi wanatuunga mkono kwenye hii kampeni itakayodumu hadi 31 Dec 2025
Tanzania ni yetu basi tudumishe amani ya nchi yetu
Ni hayo tu!