SoC04 Tujandae na kuisha matumizi kwa baadhi ya maliasili tulizo nazo

Tanzania Tuitakayo competition threads

SOVIET UNION

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
467
1,312
TUJIANDAE NA KUISHA MATUMIZI KWA BAADHI YA MALI ASILI

Mwisho wa matumizi ya baadhi ya Mali asili uko karibu sana, kama nchi tujiandae na tuchukue hatua sasa.

Mali asili ni moja ya utajiri wa asili kutoka kwa Mungu, ni utajiri ambao upo tangia kuumbwa kwa Dunia hii. Ukisoma historia biashara nyingi zilizo fanyika karine zilizo pita zilihusisha sana mali asili kama Madini, Mimea, Wanyama na kadhalika. Hata sabau ya kutawaliwa kwa Africa ilikuwa ni utafutaji wa utajiri wa mali asili kwa ajiri ya kulisha viwanda wakati wa mapinduzi ya viwanda kule Ulaya.

Tangia hapo mataifa mengi yametumia utajiri wa mali asili kuletea maendeleo kwa wananchi wake, na pia yapo mataifa ambayo pamoja na kuwa na utajiri mkubwa sana wa Mali asili ila imegeuka kuwa ni kama laana. Moja ya mataifa yenye Utajiri mkubwa sana wa mali asili Duniani ni kama vile; Urusi, Marekani, China, Austraia, Brazili, Congo na pia nchi zingine ikiwemo Tanzania.

Kutokana na maendeleo makubwa sana ya Sayansi baadhi ya Mali asili ni kama zinaelekea mwisho wa matumuzi yake, hii ni kutokana na kuwepo kwa mapinduzi makubwa sana ya Sayanzi yanayo pelekea baadhi ya Mali asili kutengenezwa au kuzalishwa Maabara na pia kutengeneza vyombo ambayo havihitaji kutumia malighafi fulani.

Leo hii kuna Almasi inazalishwa maabara na ina ubora sawa sawa na almasi tunayo ichimba pale Mwadui Shinyanga, Kuna Pamba inazalishwa maabara ikiwa na ubora sawa sawa au zaidi ya pamba ya shambani, Hii mipira ya matairi leo hii sio halisi ni mipira inazalishwa maabara ikiwa sawa kabisa kwa ubora na mipira inayo limwa.

Shirika la mafuta la Uingereza yaani BP lilitabiri kwamba ifikapo mwaka 2050 uhitaji wa mafuta uatakuwa umepungua kwa zaidi ya asilimia 80, Bp inaona kabisa mwisho wa matumizi ya mafuta unakuja.

Almasi zinatengenezwa maabara kwa sasa, kila siku watu wanagundua mibadala ya vitu Fulani, tusibweteke na mali asili kabisa.

Hatua ambazo baadhi ya nchi wanachukua
Nchi za kiarabu ni moja ya nchi ambazo zinajiandaa vilivyo na mwisho wa matumuzi ya mafuta, waarabu wanajua fika kwamba mwisho wa matumizi ya mafuta unakaribia na ndio maana leo hii wanawekeza sana kwenye vitu vingine ambavyo vitawasaidia pindi mafuta yakikosa soko. Nchi za Kiarabu leo hii zinawekeza sana kwenye usafiri wa anga zikiwa na mashirika yanayo shindana sawa sawa na mashirika makubwa ya ndege Duniani na mashirika makongwe kabisa, leo hii Dubai ni kituo cha biashara Duniani na wana ndoto ya kuifanya Dubai iwe sawa na New York Marekani, Nchi kama Irani zinawekeza sana kwenye Kilimo na Viwanda pia.

Kule Saudi Arabia wanawekeza sana pia kwenye soka, mbali na kwamba pia na wao wanawekeza kwenye kilimo na viwanda ila pia wanaona soka inaweza kuja kuwasaidia huko mbeleeni.

DP World ni shirika la bandari la Dubai, DP World inajitanua sana Dunuani na wote ni mashahidi hata hapa Tanzania tumewakodishia Bandari.

Rwanda pia hayuko nyuma sana kwenye uwekezaji mbadala na muda sio mrefu uwekezaji wao utawalipa.

Nini kama nchi tufanye sasa?
Muda wa nch kuanza kujiandaa ni sasa hivi yaani ni leo na wala sio kesho, tusingoje kesho tuanze kuajiandaa. Tunaweza jiandaa sasa kwa kuanza kuwekeza kwenye vitu mbalimbali kama vile;

1. Sayansi, bado Taifa hatuipi sayansi kipa umbele kabisa, sayansi ndio mkombozi pekee wa nchi nyingi kwa sasa, tunapaswa kama nchi kuipa kuwekeza mno kwenye sayansi, kwa sababu tuko nyakati za sayasni hivyo tuwekeze hapo, Sayansi itatusaidia kutatua matatizo pindi tukikosa hata soko la malighafi zetu. Tunaweza uza techinlojia nje pia. Juhudi za nchi kuwekeza kwenye sayansi hazipo kwa sasa au ni ndogo sana, Serikali inapaswa san asana kuweka nguvu kubwa sana kwenye Sayansi.

2. Tuwekeze kwenye sanaa, sanaa ni moja ya sekita ambayo haitaathiriwa sana na mapinduzi ya sayansi, tunapswa sana kuwekeza pia kwenye sanaa, bado jitihada ni ndogo sana n asana tumeweka nguvu kwenye mpira wa miguu na kuacha michezo mingine mingi sana ambayo inaweza sana kutusaidia kuingiza pesa, michezo inaweza sana kuja kutuokoa kama nchi endapo tuaweka nguvu huko, Nchi kaa Kenya riadha inawaingiza sana pesa vijana wao. Jack Ma tajiri wa China pia aliwahi zungumzia hili la sanaa, hebu tuipe nguvu sana sanaa.

3. Utalii, Utalii pia utatusaida sana endapo tutajua ni nini hasa kinafanya Nchi kupokea wageni wengi sana, bado hatujajua watu wanataka nini bado tumeweka nguvu sana kwenye utalii wa kuangalia Nyumbu Serengeti na kuacha utalii mwingine. Dubai inapokea watalii wengi sana mamilion ya watalii kwa mwaka. Dubai hupokea watalii hadi million 20 kwa mwaka. Kule wanafuata mambo mengi sana kuanzia Biashara, kupumzika na kadhalika, Nchi kama nchi tuwekeze kwenye vitu vingi vinavyo weza kutufanya tupate watalii wengi, iwe ni kwenye biashara, michezo au kupumzika.

4. Kilimo hasa cha mazao ya Chakula, Ingawa pia kuna baadhi ya vyakula vinaanza kuzalishwa maabara ila kuna furusa kubwa sana bado ya kuweza kuwekeza kwenye kilimo cha mazao ya chakula. Population ya Dunia ni kubwa sana hivyo tutahitaji kuilisha, Hata mataifa yalio mbele kwenye techinolojia bado wanaagiza sana chakula nje ya nchi yao.Hata nchi za kiarabu kwa sasa zinawekeza sana kwenye kilimo, zinabadili jangwa kuwa sehemu ya kilimo wakaijua fika kitawasaidia sana, Nchi kama Nchi bado hatujafanya lolote la maana kwenye kilimo, tunahita kuwa serious kuwekeza kwenye kilimo, bado huko sayansi haijaingia sana.

5.Tutumie mali asili zilizopo kwa ajili ya kuleta maendeleo ya watu kabla hazijatuchachia. Tuna mali asili ndio lakini haziwanufaishi wananchi zaidi ya kusikia taarifa za upotevu wa pesa na rushwa, Mali asili hizi hazina muda mrefu sana endapo zitatumika vyema basi zitatusaidia, kuliko zitumike vibaya na baadae zisiwe na soko na bado wananchi wawe hawajafaidi chochote kile. Nchi kama za Kiarabu zinatumia sana pesa za mafuta kutengeneza hali ya baadae ya raia wao baada ya mafuta kukosa soko.

6. Sekita mbadala, Sekita kama za usafirishaji yaani Bandari, Reli, viwanja vya vya ndege, usafairi wa anga, hivi vikiimarishwa sana vitatusaidia kama nchi, tuimarishe sana hizo sekita ili zije kutusaidia kufanya biashara na wenzetu, au kuja kuwa ndio vitega uchumi vyetu vikuu.Bandari inaweza tusaidia sana mbeleeni, Reli itatusaida pia.

Kama Taifa tunapaswa kujiandaa sasa na hali hii, wenetu walisha anza kujiandaa kitambo sana, ila sisi bado sana.
 
Sayansi, bado Taifa hatuipi sayansi kipa umbele kabisa, sayansi ndio mkombozi pekee wa nchi nyingi kwa sasa, tunapaswa kama nchi kuipa kuwekeza mno kwenye sayansi, kwa sababu tuko nyakati za sayasni hivyo tuwekeze hapo, Sayansi itatusaidia kutatua matatizo pindi tukikosa hata soko la malighafi zetu. Tunaweza uza techinlojia nje pia. Juhudi za nchi kuwekeza kwenye sayansi hazipo kwa sasa au ni ndogo sana, Serikali inapaswa san asana kuweka nguvu kubwa sana kwenye Sayansi.
Sure, tuanze na kuendeleza kutoa kipaumbele kwa akili kubwa zinazofanya mambo makubwa.

Dubai inapokea watalii wengi sana mamilion ya watalii kwa mwaka. Dubai hupokea watalii hadi million 20 kwa mwaka. Kule wanafuata mambo mengi sana kuanzia Biashara, kupumzika na kadhalika, Nchi kama nchi tuwekeze kwenye vitu vingi vinavyo weza kutufanya tupate watalii wengi, iwe ni kwenye biashara, michezo au kupumzika.
Kweli, kila kitu kinaweza kuwa utalii na kivutio mradi tu kukibrandi tu vizuri
 
Back
Top Bottom