Tujadiliane hapa videos ambazo hazipo Youtube ila Watanzania wanapenda ziwepo wadau tupige views na pesa

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Nadhani kila moja jukwaa hili anajua youtube wanalipa pesa kwa videos zako unazokubali kuwawekea matangazo yao.

Hakuna kipimo kimoja ama kilichokuwa fixed kujua malipo ni kiasi gani kwa views kadhaa ila ukweli ni kwamba pesa ipo.

Sasa naombeni wadau tupeane idea za niche gani ambayo wabongo wanapenda sana iwepo youtube ila mpaka sasa hakuna mdau mwenye channel ya hayo maudhui.

Kwa haraka haraka mimi nimeona mtu akianzisha kufundisha masomo ya sekondari au vyuoni kupitia youtube anaweza kupiga views kibao sana tu hasa kipindi cha mitihani.

Na kwa nyie je mnaona wapi goli lipo wazi

Project yangu ya Upwork naona kitumbua kimeingia mchanga nimetumia tokens (connects) zote nlizonunua kwa takribani elf 20, nimeomba kazi bila mafanikio kwa sasa nataka kujaribu huku youtube.. GLOBAL CITIZEN Nafaka
 
Duh pole sana kuna jamaa humu humu yeye aliingia freelancer akapata mchina kila week anakula zake dollar 60 ni virtual assistant na yuko chuo anafurahi mwenyewe.

Wabongo hata sijui wanataka nini
 
Kuna mdau aliwahi kusema kuhusu Pranks. Tanzania hakuna pranks na zinapendwa, wengi wamejazana kwenye channels za kenya na UG zenye pranks. Do public pranks utakuwa game changer in TZ. Tena ukiifanya vizuri utapeleka hadi kwenye TV kuiuza kama Maisha Magic.
 
Kuna mdau aliwahi kusema kuhusu Pranks. Tanzania hakuna pranks na zinapendwa, wengi wamejazana kwenye channels za kenya na UG zenye pranks. Do public pranks utakuwa game changer in TZ. Tena ukiifanya vizuri utapeleka hadi kwenye TV kuiuza kama Maisha Magic.
Bongo watu watakutoa meno.. we huoni hata takwimu za watu wenye furaha tunashika nafasi za mwisho mwisho..😅
 
YouTube nako si lele mama kaza msuli ndugu.. unafikiri masaa 4000 ni mchezo😅

Kwanini usifanye masimulizi labda mfano makala za anga.. theory zake.. vifaa vyake.. gunduzi za anga.. swala zima linalohusiana na maswala ya anga mtu akitaka kupata information anawaza channel yako tu.. maana huko umemtafunia kwa lugha yake ya kiswahili yeye ni kumeza tu!.. ila hili litakuhitaji uwe na information za kutosha!
 
Anafanya pranks nyepesi nyepesi ambazo haziingilii serikali kwa namna yoyote ile. Yaani unafanya kituko au kitu cha tofauti mbele ya watu kuona reactions zao.
Ndiyo hivyo, assume unafanya kitu kitakachowafanya madada wawe wanakimbia hawakawii kukuitia polisi.
 
Sasa kama umeomba kibali cha kushoot maeneo hayo police gani atahangaika na wewe.
Ila kweli, sema polisi wa tanzania na wahusika kwa ujumla kuna vitu vya kawaida lakini kukupa kibari wanazngua. Ila you never know until you try kuanza kuwa na mashaka kabla ya kuanza ndiko kufail kwenyewe
 
Ila kweli, sema polisi wa tanzania na wahusika kwa ujumla kuna vitu vya kawaida lakini kukupa kibari wanazngua. Ila you never know until you try kuanza kuwa na mashaka kabla ya kuanza ndiko kufail kwenyewe

Naam, Kujaribu kwanza. Wenzetu wameweza na imekuwa-recognized kama vipindi vyengine vya entertainments, iweje kwetu ishindikane ilhali hakuna aliyejaribu.

Cha msingi ideas zisiwe za kuzua taharuki au kuingilia serikali kwa namna yoyote ile.
 
Mkuu kuna jamaa nimejuana naye hapa JF yeye channel yake ni hatari kabisa. Videos zake ni 1M+ views.

Huyu jamaa ni self taught video/movie producer na anashoot vidoe zake kwa simu tu .

Video zake nyingi ni maigizo katika sanaa ya mapigano.

The guy is original in his work. And people love it.

Hiyo ni moja.

Kuhusu kupiga pesa sasa hii ni issue nyingine kwasababu channel za burudani hazipati pesa nyingi kwa kila views 1000.

Ukirudi kwenye channel za let say finance and investing zenyewe $$$ per 1000 views ni kubwa kwasababu advertisers wanawalipa Google pesa nyingi kwa kila 1000 views. Simple as that.

Mkuu nikueleze tu kutegemea pesa ya Ads ni long time investment. Kama ukifikiria utatengeneza pesa ndani ya miezi muchache you will get disappointed. It takes huge effort + time.

Kama unataka utengeneze pesa kwa haraka kwa kutumia YouTube basi utumie channel yako kupata lead.

Unawez ukawa creative zaidi ukatengeneza product au service halafu unatumia audience yako kuwauzia product au service yako. Hii mbinu haitakufanya uwaze sana kuhusu pesa ya Ads ambayo kwa hakika hutoipata leo au kesho.

Cheers 🥂
 
KwaTanzania issue ya pranks, wizi mashughuli pia urembo wa wanawake namaanisha kuoaka make up, kutengeneza vipodozi mbalimbali nyumbani vinavyohusu sehemu mbalimbali za mwili,

nina black american friend amefaidika sana na kuweka youtube masuala ya urembo jinsi ya kutengeneza make up na hivyo nilivyotaja, step ndogo zimemfikisha pakubwa this year alikuwa posted na instagram account ya Fenty beauty inayomilikiwa na Rihanna na anaendelea kufanya makubwa......
 
Back
Top Bottom