Tujadili: Prenuptial/premarriage agreement/contract

Tujadili: Prenuptial/premarriage agreement/contract

zinatumika na waislam wangapi pale ndoa inapofikia ukingoni? Hakuna wanawake wa kiislamu walioachika na waume zao kuchukua kila kitu pamoja na maisha ya ndoa ya miaka mingi na mke aliyedhulumiwa?

Waislaam tunazo hizo kabla hamjaanza kuzifikiria, jamani Uislaam mzuri sana, na hata ndoa zetu zinaitwa "Aqd" kwa maana "contract".
 
zinatumika na waislam wangapi pale ndoa inapofikia ukingoni? Hakuna wanawake wa kiislamu walioachika na waume zao kuchukua kila kitu pamoja na maisha ya ndoa ya miaka mingi na mke aliyedhulumiwa?

Ushasema "aliyedhulumiwa", sasa unachokitaka hapo ni nini zaidi? maana ya mikataba ni ikitokea kudhulumiwa unadai haki yako kutokana na mkataba, na Uislaam unaruhusu hiyo mikataba ya ndoa na hata ndoa yenyewe kwa maana kamili ni Mkataba, sasa kama mtu kakudhulumu na mkataba unao, hapo tatizo ni la aliyekudhulumu na si lako.

Kuhusu mali za mume na mke katika Uislaam ziko wazi kabisa na hakuna utata, uliza tukujuze, mwenye kudhulumu hudhulumu hata si lazima muwe na ndoa.
 
Waislaam tunazo hizo kabla hamjaanza kuzifikiria, jamani Uislaam mzuri sana, na hata ndoa zetu zinaitwa "Aqd" kwa maana "contract".

Unamaanisha nini unaposema "waislam tunazo hizo kabla hamjazifikiria"?
 
kuna wakili mmoja wa mambo ya kodi NY anasema asilimia 60 ya wateja wake wana hayo makubaliano ya kabla ya ndoa.
Tunaongelea Tanzania au tunaongelea wapi?

Wakili wa kodi wa New York anatuhusu nini wanandoa wa Tanzania?

Sweetie,sijaielewa thread!
Ni hivi hon;
Si unajua kuna watu tunaolewa na fulani kwa sababu ya pesa au mali zake. Baadhi ya nchi (nimeambiwa Tanzania ni tofauti) mkiachana mali zote mnagawana pasu kwa pasu, sasa mimi naolewa na wewe kwakuwa uliinherit madolari kutoka kwa baba Eiyer; lakini sikupendi kabisa huenda nampenda Asprin (asijidai lakini ni mfano tu, usiofanana na ukweli). So tunazaa mtoto mmoja, naanza visa ili say ukasirike unipige halafu nina file for divorce. With a good lawyer, mali tunaigawa na ninapata say custody ya mtoto then huyoo kwa ASA.

Sasa ili kuepuka yote hayo, say ndugu zako wanakushauri kuwa kabla ya kuoana nisign hiyo prenup agreement kuwa ikitokea ndoa isiwork, mali zako ulizorithi sintazigusa.

Au scenerio nyingine, mimi nakupenda sana, lakini wewe una machale kuwa huenda ninakupendea mali; hivyo ninakuambia just to prove it is you l want and not your money, lemme sign the prenup agreement.
 
Last edited by a moderator:
Unamaanisha nini unaposema "waislam tunazo hizo kabla hamjazifikiria"?

Nna maanisha nilichokisema, ndoa za Kikristo hazijampa mwanamke uwezo hata wa kujieleza mpaka miaka michache nyuma. Hata jina la kwao alikuwa hana ruksa ya kulitumia na inabidi abadili liwe la ukoo wa mumewe. Kudhalilishwa kwa hali ya juu. Lakini Aaaaahh, Uislaam miaka 1,400 nyuma ulituwekea wazi yote hayo na ndoa zikawa ni mkataba na si utumwa.
 
Naomba maandiko kutoka kwenye biblia yanayokubaliana na kauli yako hii.

Ukishindwa tafadhali futa kauli kuwa ukristo unamlazimisha mwanamke abadili ubini wake na bla bla zote ulizoandika hapo!
 
Naomba maandiko kutoka kwenye biblia yanayokubaliana na kauli yako hii.

Ukishindwa tafadhali futa kauli kuwa ukristo unamlazimisha mwanamke abadili ubini wake na bla bla zote ulizoandika hapo!

Biblia ipi?
 
nadhani mwanzoni sikuelewa but through others contributions nimeelewa kitu...kama alivosema gaijin ndoa yenyewe hapo ilipo ni contract tosha na binafsi kama sheria hazizuii sioni ubaya kama mkiweka vipengele ya jinsi ya kugawana mali pindi ikitokea la kutokea...again...any contracts kwenye ndoa kwa maoni yangu naona ina-undermines its strength and longevity if not sustainability..kwa sababu kwa vyovyote inakuwa kama imejengwa kwenye 'materials' and not 'soul'

thats right...!!
 
zomba ,nakusubiri hapa!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom