Tujadili: Prenuptial/premarriage agreement/contract

Tujadili: Prenuptial/premarriage agreement/contract

Kaunga

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Posts
12,529
Reaction score
13,502
Mmekutana mmoja (Mke/mume) anazo za kutosha labda za kuzidi.
Mmoja anamwambia mwenzake wakubaliane, ikitokea wakaachana au mmoja akifa. Yaweza kuwa 'asiye nazo' ili amuhakikishie 'aliye nazo' kuwa hajampendea mali yake. Au mwenye nazo kwa maamuzi yake mwenyewe au kwa shinikizo la familia yake.

Sijui kama huu utaratibu tunao (watanzania), lkn kuna wakili mmoja wa mambo ya kodi NY anasema asilimia 60 ya wateja wake wana hayo makubaliano ya kabla ya ndoa.

Je utaratibu huo mnauonaje wana MMU?
 
kabla ya kufika mbali hizi agreements tanzania haziko enforceable coz zinapingana na policy ya family law..na law of marriage act..ya tz
 
kabla ya kufika mbali hizi agreements tanzania haziko enforceable coz zinapingana na policy ya family law..na law of marriage act..ya tz

Aah, sikujua hilo. Sasa unaepukaje pale mtu anakubali kuolewa nawe kwa mali ulizo nazo, na baada ya mwaka analeta visa ili muachane na mgawane mali pasu kwa pasu?

Halafu, l use to know (or l thought l knew) kwamba mali ulizochuma kabla ya ndoa ni za kwako. So kama ni kweli, si ni lazima uziorodheshe ili zijulikane? Is it not a sort of agreement?
 
hamuwezi gawana mali pasu kwa pasu coz legally speaking kuna joint acquired property na ile individual yani private so kama ulikua na lexus, nyumba 2 kabla ya kuoana then baada ya ndoa mkajenga nyumba nyingine ambayo inaonesha ni joint acquired propert hiyo ndo inagawanywa vinginevyo ni hamna kitu anakuja kama alivyoondoka..mfano wa joint acquied proerty labda wkt mnaoana baba mkwe aliwapa kiwanja wote wawili mkajenge nyumba then hapo ni pasu kwa pasu
 
i dun know what the law says in TZ but asking ur bf/gf to sign a prenup is risky. u're basically saying "i don't think the relationship is going to last" or "you are just with me because i'm rich". sisemi haina benefit lakini bado siko comfortable with it ki-vile. have faith that even if mta-break up then mtakuwa kama Guy na Madonna ambapo Guy hakuchua 1/2 ya mali za Madonna. it's hard kuimeza nikiambiwa ni-sign but that's just me maana sivutiwi na hela ya mwenza.

sorry for not being articulate enough and thx for controversial topic Kaunga
 
Last edited by a moderator:
hii kitu nzuri ila ina ubaya wake......ingawa kwa wabongo hawana hiyo...
 
Waislaam tunazo hizo kabla hamjaanza kuzifikiria, jamani Uislaam mzuri sana, na hata ndoa zetu zinaitwa "Aqd" kwa maana "contract".
 
Katika mazingira ya bongo hii kitu ni utata mkubwa.Hasa lile kabila lileee la kaskazini ni noma!
 
hii kitu nzuri ila ina ubaya wake......ingawa kwa wabongo hawana hiyo...

Fafanua BD, uzuri wake ni upi?
Mimi naona inabase kwenye kutokuaminiana zaidi, ingawa na binadamu tumekuwa crooked, imagine unaolewa na kibabu ambacho hata kiafya kinashauriwa kutoe manii mara moja kwa week, kisa mali zake; (kesi ya aipipi na dogo dogo wake).
 
Blaine, say Beyonce kakuzimikia nawe unampenda kwa dhati. Sasa ndugu zake na rafiki zake wanamwambia kuwa ni kwa sababu ya mali yake; utafanyaje nawe wampenda, si bora usign hiyo kitu ili kuwaassure wote, au utaamua kumuacha?
 
Last edited by a moderator:
Waislaam tunazo hizo kabla hamjaanza kuzifikiria, jamani Uislaam mzuri sana, na hata ndoa zetu zinaitwa "Aqd" kwa maana "contract".

Zomba si unaona na Serikali ya Tanzania kama alivyotuambia mkuu hapo juu inayo kitu kama hicho. Mali zako ulizochuma kabla ni zako, baada ndio zetu!
 
Basically, marriage is a contract

Kwa hiyo sioni kwa nini msiweke mtakacho kwenye contract hiyo
 
Kaunga nijuavyo mm ni kwamba mali alizo chuma mwenza b4 hamjaish ni zake na pia hata kama mtaisha for yrs kama mchumaji ni mmoja basi mnapotengana mahakama, haigawi pasu kwa pasu haya nimeyashuhudia. mchumaji hupewa asilimia kubwa zaid and hili limekuwa ni tatizo kwa wanawake wengi ambao hawafanyi kazi wakisubiria wanaume , inapotokea wanakwenda kufile divorce hawapati kama wanavyofikiri wao so to me its worth tuish pasi contract, na ikitokea mtu anasema tufuate formal procedures.
 
Last edited by a moderator:
Basically, marriage is a contract

Kwa hiyo sioni kwa nini msiweke mtakacho kwenye contract hiyo

Napigia mstari kwenye 'kuweka mtakacho'.

Kuna mdada mmoja alikubaliana na mchumba wake kwa maandishi kabla hajamuoa na kuwa mke no 3, kuwa nyumba atakayojenga huyo dada itabaki kuwa ya kwake na mume anatakiwa amsomeshe Mdogo wake wa kiume. Ni waislam so nafikiri alichosema zomba kinatendeka kwa waislamu, coz yule dada ni mtihimu wa darasa la 7 tu lkn she came up with those clauses. Nilimuadmire kwa kweli!
 
Last edited by a moderator:
Nadhani mwanzoni sikuelewa BUT through others contributions nimeelewa kitu...Kama alivosema Gaijin ndoa yenyewe hapo ilipo ni contract tosha na binafsi kama sheria hazizuii sioni ubaya kama mkiweka vipengele ya jinsi ya kugawana mali pindi ikitokea la kutokea...AGAIN...any contracts kwenye ndoa kwa maoni yangu naona ina-undermines its strength and longevity if not sustainability..kwa sababu kwa vyovyote inakuwa kama imejengwa kwenye 'materials' and not 'soul'
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin huoni kama hiyo couple wangekuwa na makubaliano kabla, ingesaidia?

Mf: mke anasema sawa nitakuwa mama wa nyumbani, lkn ukiniacha au ukinitesa nikalazimika kukuacha mali zote tutagawana pasu kwa pasu; ingepunguza udhulumati na poor judgement ya judge ambaye haoni reproductive activities (kumtunza mume na watoto) kama nayo ni kazi.
 
Last edited by a moderator:
SnowBall naelewa hasa hapo kwenye kupoteza maana ya mpaka kifo kiwatenganishe. Lkn ndoa nyingi siku hizi ziko kimaslahi zaidi, angalia idadi ya vijana wanaotafuta masuger mummies; au wadada wadogo wanaolewa na vibabu, is it because of love au materials?

Kuna hata same age, wenye mali wengi hawana Amani kuwa wanapendwa kweli au ni mali zao.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom