Ni kweli katiba mpya na bora inahitajika kulingana na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitekinolojia nchini na duniani kote. Inawezekana kabisa tangu 1977 nchi imepita kwenye changamoto nyingi za kiutawala, kiuongozi, kisiasa, kijamii na kiuchumi hivyo uwepo wa mahitaji mapya ya mwongozo wa kikatiba ili kujenga nchi yenye ustawi. Watanzania tulio wengi tunakubaliana na hili. Hata hivyo kuna hoja mbalimbali muhimu na ya msingi zinaibiliwa na zinahitaji tafakari kwa kina.
1. Je, ni wakati mwafaka sasa hivi kuanza mchakato huo ambao kimsingi hauko kwenye ilani ya uchaguzi ya ccm na hakuna bajeti yake au tunamtwika Rais jambo ambalo ni non starter kwa sasa na ambalo litamshughulisha na kumtoa kwenye malengo yaliyopo mbele yake na taifa.
2. Ndani ya chama cha mapinduzi vuguvugu hili likoje na kitaifa mapokeo ya wananchi yakoje? Je hoja hii ya manufaa kwa wanasiasa au jamii yote kwa ujumla?
3. Je, ikikubalika tuanze mchakato upya, tuanzie wapi kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba. Wapo wanaosema tuanze na rasimu ya warioba lakini hoja nyingine mbadala ni kwamba rasimu hii ilijadiliwa na kupitiwa na Bunge la katiba 2014 kwa akidi iliyokamilika na bunge kuandaa rasimu inayojulikana ya Sita je tuachane nayo hii ya Samwel Sita wakati mchakato ulikamilishwa kwa mujibu wa sheria hata km baadhi ya wajumbe walitoka nje na kususa lakini mchakato uliendelea hadi rasimu kukamilika. Hapa napo kuna mkanganyiko wa kisheria pia. Je hali hii irekebishwe kwa kupitia Bunge kwa kurekebisha sheria? Je kwa tamko la Rais hatakiuka sheria?
4. Je, turudi mezani na kuboresha rasimu ipi ya Sita au ya Warioba na pia kwa kuzingatia kipindi cha miaka aghrabu miaka 8 imepita je tujiulize mazingira hayajabadilika kweli kuhitaji mambo mapya kuingizwa? Au mchakato uanze upya kwa kuchukua maoni ya wananchi upya na kuachana na rasimu ya Warioba na ya Sita zenye migongano ya kimaudhui.
5. Je, hivi katiba ya sasa haifai moja kwa moja,wapo wanaoamini kuwa tunachohitaji sasa ni ustawi wa uchumi na kijamii kwanza kabla ya katiba mpya.Hoja ni kwamba katiba hii ni bora wakirejea kuwa imetuvusha kwenye matukio mbalimbali mf msiba wa juzi.Katiba mpya siyo mwarobaini wa changamoto zilizopo. Kundi lingine linasema katiba ya sasa ina matobo mengi mno na ina mifumo dhaifu inayokanyangwa. Wanarejea utawala uliopita kuwa ulikuwa mgumu na udhaifu wa Muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
a) Hoja nyingine ni kwamba wananchi wa kawaida hawahitaji mabadiliko ya katiba wanachohitaji ni kuwaondolea kero za maisha kiuchumi na kijamii. Hivyo hoja ya katiba mpya ni ya wanasiasa tena wanalenga uchaguzi wa 2025. Je hakuna njia nyingine ya kuboresha katiba au mifumo iliyopo kimkakati ili uchaguzi uwe wa haki badala ya kubeba hoja nzima ya katiba mf kuiangalia upya Tume ya uchaguzi na madaraka ya Rais kuhusiana na tume hiyo ili kuleta usawa na haki kwenye uchaguzi.
b) Hoja ya katiba mpya ni ya upinzani na wanaharaki pekee. Vipi ushiriki wa makundi mengine misimamo yao wakulima,wafugaji, wavuvi, viongozi wa dini, wafanyakazi nk.
c) Hoja ya hofu ni kuwa tukianza mchakato je hautaishia njiani tena na kupoteza raslimali kwa vile upande wa upinzani tayari baadhi wameanza na hoja zenye masharti kabla hata ya majadiliano kuwa wanataka rasimu ya warioba tu iheshimiwe na si vinginevyo(pre emptying discussion).
d) Je, kuanzisha mchakato huu kuna manufaa au hasara kwa sasa? Je, mazingira ya kisiasa yanaruhusu! Zipo hoja nyingi za kutafakari kwa umakini kwa pande zote ili huko mbeleni tusikwame