Tujadili: Dunia ya machale!!!!!!!!

Tujadili: Dunia ya machale!!!!!!!!

Ujue Kaunga, mie huwa siamini kama ninamwamini mtu kwa sababu nimeamua kumwamini, huwa ninamwamini mtu sababu ame-earn trust yangu. Vile vile na mie huwa nahisi mtu ananiamini sababu nime-earn trust yake.

Hapa nina ushuhuda kabisa.
 
Kuishi kwa machale
Kuongea kwa machale
Kupenda kwa machale
Urafiki wa machale
Ushirika (biashara) wa machale
Undugu wa machale
Kanisani machale
Misikitini machale
Kazini machale
Kwenye familia machale
Kwenye ndoa machale​
Najua ni ngumu kumuamini kila mtu, lakini naona maisha ni magumu sana kwa kutomuamini mtu yoyote. Katika ndoa kila mtu anamtegea mwenzie, yaani hata kuufungua moyo wako kwa mpenzio unaogopa kwa kuhisi tu mwenzio atauexploit na kukuumiza. Where is the trust?

Kwenye masuala ya mali ndio kabisa, kila mtu anatoa ukweli nusu au hata pengine robo hii ni hatari sana kwa maoni yangu. Matokeo yake tunakuwa wapweke sana kwa kuwa tuna siri nyingi sana ambazo hatuzishei; licha ya upotevu wa mali unaotokea pindi mmiliki wa siri anapotangulia.

Labda swali la kujiuliza hapa, chanzo cha kuishi kimachale au kuangalia kila kitu kwa jicho la tatu if you may ni nini? Ni kujifunza kutoka kwa makosa ya wengine? je mazingira ya kutokea kwa hayo makosa ya wengine ni the same? Au waliokosea wanafanana na hawa wenzi wetu kwa kila kitu?

Wana jamvi kuna shida gani ukimuamini mtu?

Karibuni tujadili.
trusting makes you vulnerable and some people exploit this and hurt you 'very badly'. if i give you my
  1. heart, will you trample on it
  2. mwaliko nyumbani, utaniibia mke wangu
  3. money ya biashara, utanitapeli
etc
inakuwa vigumu kuamini watu because of this
 
Ujue Kaunga, mie huwa siamini kama ninamwamini mtu kwa sababu nimeamua kumwamini, huwa ninamwamini mtu sababu ame-earn trust yangu. Vile vile na mie huwa nahisi mtu ananiamini sababu nime-earn trust yake.

Hapa nina ushuhuda kabisa.
me too
 
yaani kuna hundred and one mifano ya hivyo kwa upande wa mali, lkn hata emotional machale ipo hasa kwa wababa. Usasikia wanaambizana "usimuoneshe mwanamke kuwa unampenda sana, atakusumbua" really? Matokeo yake anakuwa na mashaka na upendo wako kwake, n we both know nini kitatokea akimpata atakaye muonesha upendo.
uuwwwiiiiii, hii ilimkosti mtu...... anajuuutaaaa kusikiliza maneno ya watu.....
mada nzuri rafiki.
wengine machale yetu yapo mbali sana, lol! 100% trust
 
….unajua, kwa #AfyaYaAkili yako mwenyewe, jitahidi kujizuia mambo ….kwa "kiasi" au #KiwangoMaalum.
Ukiendekeza sana haya #Machale kiasi kwamba #UnashindwaKuReason, utajikuta unakuwa "Mtumwa"
wa fikra ndio inazaa hizo Paranoia!

#Machale sio lazima yakutoe raha, ….yapo kwa ajili ya kukusaidia kukusukuma mpaka mwisho wa mpaka kabla
mambo hajajafikia #ThePointOfNoReturn!

Kweli kabisa ukifanya kitu kwa kiasi uko mbeleni haitakuletea shida sana
 
kuna wengine inakuwa wameathirika kisaikolojia kutokana na maisha aliyopitia toka utoto ikiwemo kusalitiwa na watu wake wa karibu aliowaamini na kuweka maisha mikononi mwao.
 
Ujue Kaunga, mie huwa siamini kama ninamwamini mtu kwa sababu nimeamua kumwamini, huwa ninamwamini mtu sababu ame-earn trust yangu. Vile vile na mie huwa nahisi mtu ananiamini sababu nime-earn trust yake.

Hapa nina ushuhuda kabisa.

kweli kabisa kongosho , katika maisha ya kawaida ukiondoa wale walioathirika kisaikolojia huwa Trust ina erniwa either way.
 
uuwwwiiiiii, hii ilimkosti mtu...... anajuuutaaaa kusikiliza maneno ya watu.....
mada nzuri rafiki.
wengine machale yetu yapo mbali sana, lol! 100% trust
Umeona eeh, yaani mimi naona madhara zaidi ya kutomuamini kuliko kumuamini. Na come to think of it, nahisi mtu anayejiamini yuko more likely kuamini wengine kuliko aso jiamini au ajiaminiye kidogo.
 
Ujue Kaunga, mie huwa siamini kama ninamwamini mtu kwa sababu nimeamua kumwamini, huwa ninamwamini mtu sababu ame-earn trust yangu. Vile vile na mie huwa nahisi mtu ananiamini sababu nime-earn trust yake.

Hapa nina ushuhuda kabisa.

Kama hajakupa sababu ya kutomuamini hautamuamini kisa hajakupa sababu za kutosha za kumuamini?
 
Umeona eeh, yaani mimi naona madhara zaidi ya kutomuamini kuliko kumuamini. Na come to think of it, nahisi mtu anayejiamini yuko more likely kuamini wengine kuliko aso jiamini au ajiaminiye kidogo.
haya maisha ni matamu sana kujiwekea muda wa kumshuku mtu......
yaani nikikushuku tu unakaa pembeni ya maisha yangu. haijalishi wewe ni ndugu yangu au mpenzi. napenda kujiachia. sipendi kufanya kitu nikiwa nawaza NIKIONWA AU KUSHTUKIWA ITAKUWAJE....
nafurahia ninavyoweza kushi na kumsimulia mpenzi wangu upuuzi wangu na mambo yangu mazuri nikiwa nina uhakika wa either kupongezwa au kupewa ushauri bila kufikiriwa mpuuzi kwa jambo nililofanya.
machale machale machale...... hivi kwa nini niwe na mtu ambaye naishi naye kwa machale?
kwa nini niendelee kumtumia ndugu ambaye najua natakiwa kufanya naye kazi kwa machale?
hivi unajua unapojihusisha na watu kama hao unatumia muda wako mwingi sana kujilinda kuliko kufanya mambo ya maendeleo?
hata kama ni boss, ukiwa unaishi naye kwa machale utaishia kufanya yale yanayompendeza yeye tu badala ya kupanua wigo wa professional yako kwa kujaribu vitu vipya ambavyo vitaletea faida ofisi.
 
Kama hajakupa sababu ya kutomuamini hautamuamini kisa hajakupa sababu za kutosha za kumuamini?
ha haaaa, tupo tofauti....
kwangu mimi mpaka unipe sababu ya kutokukuamini, hapo utaona tu kimyaaaaaaa...........
tena wakati mwingine bila hata kuaga, lol!
 
Da! hii mada imenifanya nikumbuke mbali. ona sasa stress zimeshanirudia!
 
waoh, nimependa sana ulivyonyambulisha vizuri. Thanks buddy!

Sasa kuhusu kutomuamini mtu 100%, je kwa mwenzi wako wa ndoa ni % ngapi za kumuamini zinazotakiwa? Na kuna shida gani nikimuamini 100% hata kama akinidisappoint si ni tatizo lake na sio langu. Tunapokuwa na reservation na wapenzi wetu huoni kama inatufanya tuzidi kuwa far apart?

Muamini mwenzio kwa %66 = 2/3! Kama haujaona baya lolote kwake! Siku ukiona baya halitokusaprise sana! Ukimuamini kwa %100 unaweza hata kujinyonga ukigundua majanga yake! Also ukimuamini kwa 100% afu akuteme, ndio kabisaa unalo! Hapo ndio unaskia "chakula hakipiti!" so kumuamini kwa 100 ni tatizo lako coz athari zinakukuta wewe!
...
Hamtokua far apart coz you are reasonable man! Kutomuamini kwa asilimia zote inakua ndani ya akili yako tu! Hupaswi kumuonesha if hajaonesha kukusaliti!
What you do is only "kuprisume uwezekano!"
...
Mtu akijua unamuamini kwa zote hatoacha kukujaribu!
 
Kwenye mahusiano au ndoa hautakiwi kuishi kimachale mana kwa kufanya hvyo mnaweza kujikuta mna migogoro ambayo haieleweki

Ila kwenye maisha mengine uwezi kumwamini mtu mazima lazima uishi kimachale ukiangalia haswa walivyotendewa wengine na jinsi hali ya dunia ilivyo sasa maisha yamebadilika
 
yaani sidhani kama kuna siku atakuwa hana machale yule; na hivi..............

ahahahahhahahah sasa we ukisema umemshindwa mi si ndo atanitoa baru kabisa!?
umenifanya nikumbuke hadithi ya samson!
mwaya bora tujisalimishe tuu tumuulize direct!
The Boss lini unakuwa huna machale asee!
:A S 39:
 
Last edited by a moderator:
lakini hebu tuwaze hiv
HIV MTU KUWA TRUSTED KUNAANZA NA KUWA TRUSTFUL ENH?
LAKINI JE KUWA TRUSTFULL KUNAKUFANYA UKAWA TRUSTING?

kipi kinaanza na kumaliza hapo?
machale mpaka wake ni upi?
kipindi kipi na kwa nani natakiwa kuwa na machale?
machale yanaweza kubreshwaje?
na nikiwa sikuamini ndo unakuwa muaminifu au ndo unakuwa sio muaminifu kabisaa?
lakiiiini hiv kwanini nikuamini?
na kwanini niamini kuwa unaniamini?
kwanini niseme sina shaka na huyu aua na hiki?
kuamini kuliwahi kunipa faida na hasara wapi?
dah! Eiyer come zis way!
 
Last edited by a moderator:
Kuishi kwa machale
Kuongea kwa machale
Kupenda kwa machale
Urafiki wa machale
Ushirika (biashara) wa machale
Undugu wa machale
Kanisani machale
Misikitini machale
Kazini machale
Kwenye familia machale
Kwenye ndoa machale​
Najua ni ngumu kumuamini kila mtu, lakini naona maisha ni magumu sana kwa kutomuamini mtu yoyote. Katika ndoa kila mtu anamtegea mwenzie, yaani hata kuufungua moyo wako kwa mpenzio unaogopa kwa kuhisi tu mwenzio atauexploit na kukuumiza. Where is the trust?

Kwenye masuala ya mali ndio kabisa, kila mtu anatoa ukweli nusu au hata pengine robo hii ni hatari sana kwa maoni yangu. Matokeo yake tunakuwa wapweke sana kwa kuwa tuna siri nyingi sana ambazo hatuzishei; licha ya upotevu wa mali unaotokea pindi mmiliki wa siri anapotangulia.

Labda swali la kujiuliza hapa, chanzo cha kuishi kimachale au kuangalia kila kitu kwa jicho la tatu if you may ni nini? Ni kujifunza kutoka kwa makosa ya wengine? je mazingira ya kutokea kwa hayo makosa ya wengine ni the same? Au waliokosea wanafanana na hawa wenzi wetu kwa kila kitu?

Wana jamvi kuna shida gani ukimuamini mtu?

Karibuni tujadili.

Bandiko hili nimelisoma kwa machale sana !!
 
lakini hebu tuwaze hiv
HIV MTU KUWA TRUSTED KUNAANZA NA KUWA TRUSTFUL ENH?
LAKINI JE KUWA TRUSTFULL KUNAKUFANYA UKAWA TRUSTING?

kipi kinaanza na kumaliza hapo?
machale mpaka wake ni upi?
kipindi kipi na kwa nani natakiwa kuwa na machale?
machale yanaweza kubreshwaje?
na nikiwa sikuamini ndo unakuwa muaminifu au ndo unakuwa sio muaminifu kabisaa?
lakiiiini hiv kwanini nikuamini?
na kwanini niamini kuwa unaniamini?
kwanini niseme sina shaka na huyu aua na hiki?
kuamini kuliwahi kunipa faida na hasara wapi?
dah! Eiyer come zis way!

Duh maswali magumu haya, tumuite na EMT pia huenda akatusaidia.
Ila mimi nafikiri kama sijapewa sababu ya kutomtrust mtu basi sina sababu ya kutomtrust. Sasa kwa kiwango gani nitamtrust itategemea namtrust na kitu gani?
Mfano l want to do business with you, ninapaswa kutrack record yako of course baada ya wewe kunipa maelezo yako. Baada ya kujiridhisha then sina machaguo zaidi ya kukutrust with my money.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom